chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,576
- 28,497
Heshima kwenu wana MMU.
Nimeadimika sana hapa Jamvini ingawa huwa napitia kuzisoma post za wadau mara kwa mara.
Wakuu nisiwachoshe sana, niingie kwenye mada iliyonileta hapa.
Nina mpenzi wangu ambaye tupo naye kwenye mahusiano takriban miaka miwili sasa, tumekuwa tukishirikiana katika hali na pale tunapokwazana huwa tunafikia muafaka na kuondoa tofauti zetu.
Mpenzi wangu huyu bado yupo Chuo Jijini Dar akichukua masomo ya Usimamizi wa biashara na akaunti na mimi kwa sasa nipo nje ya Jiji kwa majukumu yangu ya kikazi.
Huyu binti nilishamuahidi kuanzisha naye familia Mungu akijalia.
Kuna wakati mawasiliano yetu yanakuwa hafifu sana lakini mara nyingi hili jambo halileti tatizo kwani tunaaminiana.
Wiki kama mbili hivi zilizopita amepata eneo la kufanya mazoezi kwa vitendo (field) katika ofisi fulani ya uhasibu Jijini Dar.
Jana tumewasiliana kaniambia kuna jamaa hapo ofisini kwao anapofanyia field kuna Principal accountant ametokea kumtongoza na anaendelea kumsumbua sana licha ya yeye kumuambia tiyari ana mpenzi ambaye ni mimi.
Wakuu huyu mpenzi wangu amekosa raha kabisa katika eneo hiki analolifanyia field work.
Nilimuuliza jina lake akanitajia, pia nilimuambia anipatie namba ya huyo Jamaa niwasiliane naye na nimuambie aache kumsumbua mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu aliniambia jamaa akimpigia simu huwa hapokei simu yake na anazifuta namba zake, ila kaniambia akishazipata atakapopiga tena au ataziomba kwa wenzake atanipatia, yupo na wenzake sita katika eneo hilo lakini yeye ndiye anasumbuliwa sana.
Mpenzi wangu ni wa kawaida, siyo wa kuwatisha wanaume kiviile lakini kuna kitu fulani ndani yake nimekipenda na nisingependa kukipoteza kamwe ndiyo maana nataka awe mwenzi wangu.
Wana MMU naombeni ushauri wenu juu ya hili Jambo, na nitakapozipata hizo namba nifanyeje maana nisingependa kumpoteza mpenzi wangu, pia vilevile nisije nikaharibu matokeo yake ya field work baada ya kuongea na huyo Principal accountant wao akapoteza marks,..
Natanguliza shukrani wakuu,..