Hakika huyu anahitaji msaada ili naye apate elimu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Naitwa Yohana Benjamin, nimezaliwa mwaka 1993 Kigoma.
Nimesoma shule ya msingi Kabanga mazoezi, Kigoma wilaya ya Kasulu. Mimi nina ulemavu wa miguu, hata hivyo nimebahatika kumaliza na kufaulu vizuri mtihani wa darasa la saba (7) mwaka 2010.
Nilibahatika kupangiwa Shule ya Sekondari Mwadui , Shinyanga. Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Mwadui alinipokea vizuri sana lakini akawa na wasiwasi mkubwa sana juu ya mahitaji muhimu kwangu kutokana na aina ya ulemavu wangu. Kwa mfano, mazingira ya pale shule kama vile kupanga ngazi, au kwenda kujisaidia ndio ilikuwa changamoto kwa Mwl Mkuu wangu na mimi mwenyewe.

Ilifika mahali nikajipangia kula mlo mmoja wa jioni tuu, ili nisije kuhitaji kujisaidia mchana. Ikifika usiku nawaomba wenzangu wanisaidie kunisindikiza kwenye vichaka ndio nipate kujistiri.
Hali hii ilinisumbua mimi na mwl mkuu wangu, ikabidi nifanye uamuzi wa kwenda kuomba msaada kwa afisa elimu wa wilaya na hatimae afisa elimu mkoa, lakini kwa bahati mbaya wote walishindwa jinsi ya kuniwekea mazingira yakuniwezesha kuendelea na masomo. Nikarudi nyumbani.
Siku kata tamaa, nika amua kuja DSM kuonana na Idara ya Elimu Maalum, Wizara ya Elimu na Ufundi. Mungu si Athumani, nimemkuta Bwana Mwiga Afisa katika Idara hii, ndio amekubali kunipa barua nikajiunge na Shule ya Sekondari Pugu.Ndugu zangu mtakajaaliwa kuona taarifa hii, ninacho omba kwenu nisaidiwe kupata wheel chair inayonifaa kujisukuma kwenda darasani kutoka bweni na kwengineko.
Katika picha hii, kigari kinacho nisaidia nimebuni na kutengeneza mwenyewe baada ya kusaidiwa kuletewa vifaa kama mnavyoona. Najiendesha kwa kutumia mkono mmoja kuendesha usukani na mkono wa kulia ndio najisukumia chini.

Nina penda na kumudu masomo ya sayansi, hisabati na maarifa ya jamii. Malengo yangu ni kusoma hadi chuo kikuu. Nikiwezeshwa nitaweza.
Hapa DSM nimepokewa na ndugu yangu Bw. Robert Revocatus cm 0763 299960 au 0714 495951
mlemavu.jpg

mlemavu 2.jpg
 
hivi jamani kina Rostam,Chenge,LowasA na mkono hali kama hz wanaziona kweli????walau katika bajeti zao wangetoa hata asilimia 0.1 wakamsaidia kijana huyu bado ana usongo sana wa kusaka nondozzz kama serikali kweli inajali maisha ya watu tunaomba wamsaidie kijana huyu aendelee na shule na sidhani usafiri anaoutaka kama unagharimu kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko bajeti zao za chakula kwa siku!
 
Hao ulio wataja wamefuatwa au kufahamishwa kuwa kuna kijana/vijana kama huwa wanaitaji msaada au zinaanza lawama kwanza... lafu ufuatiliaji baadae!?
 
hizo sio lawama bali ni swali na suggestion!!any way nimeguswa sana na hali ya huyu mwenzetu

Hatimaye Yohana Benjamin, hapata Wheelchair

Wheelchair mdau aliyojitolea kumnunulia kijana mlemavu
Yohana Benjamin aliyeomba msaada tutani katika Globu ya Jamii majuzi

from Issa Michuzi blog said:
Mdau mwema huyu kaomba jina na bei ya wheelchair tuweke kapuni. Ndugu Michuzi kwanza nikushukru kwa kazi nzuri unayoifanya kwa faida ya jamii. Hongera sana. Pichani nimemkubidhi bwana Robert Revocatus Wheel Chair kwa ajili ya kijana Yohana Benjamin kama ulivyo onyesha umma kwenye Blog ya Jamii na TBC1 kwenye taarifa ya habari yao ya hapo jana.
Nimehakikishiwa kuwa kesho Robert atapelekwa Pugu Secondary ili akaendelee na masomo yake. Misaada zaidi itatakiwa ukizingatia hali yake na hali harisi ya shule zetu za umma. Kwa nyongeza tu nimekuja kujua kuwa Robert na Yohana ni watu wa Manyovu Kasulu waliohamia Kasangezi. Zaidi mnaweza kuwasiliana naye.

Asante sana kwa kazi nzuri.
 
tunamshukuru mungu kwa hilo na hawa waliotoa msaada
Hatimaye Yohana Benjamin, hapata Wheelchair

Wheelchair mdau aliyojitolea kumnunulia kijana mlemavu
Yohana Benjamin aliyeomba msaada tutani katika Globu ya Jamii majuzi

hongera ndugu nami nimeona mawasiliano yao nitachukua kwa ajili ya msaada zaidi kwa sababu ni mahitaji mengi ana hitajika kuwa nayo
 
ni kweli tuliojaaliwa uzima wa viungo vyetu vya mwili tuwasaidie hawa wenzetu walemavu
hongera ndugu nami nimeona mawasiliano yao nitachukua kwa ajili ya msaada zaidi kwa sababu ni mahitaji mengi ana hitajika kuwa nayo
 
Back
Top Bottom