Hakijanyooka lakini wamejitahidi

Hakijanyooka lakini wamejitahidi

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,648
Reaction score
10,843
Hawa ni Askari Polisi wa Tanzania wakimhoji binti wa Nigeria mwendesha pikipiki. Ametokea Uganda na ameeleza kuwa angeenda kupumzika/ kulala Kibondo.

Japo Kizungu cha "makamanda" wetu hakijanyooka kivile, lakini mawasiliano yamefanikiwa. Kila mmoja ameweza kumwelewa mwenzake, na hilo ndilo lengo la lugha, mawasiliano.
 
Attachments

  • Nigerian_Girl’s_Encounter_With_The_Tanzanian_Police_#shorts(360p).mp4
    5.1 MB
Hawa ni Askari Polisi wa Tanzania wakimhoji binti wa Nigeria mwendesha pikipiki. Ametokea Uganda na ameeleza kuwa angeenda kupumzika/ kulala Kibondo.

Japo Kizungu cha "makamanda" wetu hakijanyooka kivile, lakini mawasiliano yamefanikiwa. Kila mmoja ameweza kumwelewa mwenzake, na hilo ndilo lengo la lugha, mawasiliano.
Ni kweli mkuu, kama kisingeeleweka asingekuwa anajibu! Makamanda kinawatosha kwa level yao! Hawa tujue wengi wao ni form failure yaani wanamzidi kidogo tu Mh. Musukuma! Kiingereza chao hakina tofauti na cha Mchina!
 
Sasa mtu ana zero kidato cha nne mnataka aongee fluent english ya nini?
 
Safi sana wameonesha ukarimu wa wa Tanzania😜🤪😝.
 
Guys D Mbili zinatosha , ile camera imekaa eneo gani maan inaonyesha eneo kubwa hadi tair ya mbele inaonekan,
 
Naam nadhani hata huyo Dada toka huko kwao alishafanya tafiti Watanzania wanazungumza lugha gani.
 
Naam nadhani hata huyo Dada toka huko kwao alishafanya tafiti Watanzania wanazungumza lugha gani.
Hata huko naijeria kuna maeneo ukienda hawajui kingereza zaidi ya kiausa na kiyoruba tu kwa hio ukimuongelesha ngeli ni mwendo wa lugha gongana
 
How many cc? Two fifty.

Wao: MIA HAMSINI

Dah inasikitisha sana. Hata mtoto wangu wa darasa la pili anajua two fifty ni mia mbili hamsini.
 
Back
Top Bottom