Haki za wapagani ziheshimiwe

Haki za wapagani ziheshimiwe

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Kwa sababu sasa kuna kila dalili za Wakristo na Waislamu katika taifa letu kushindwa kuvumiliana na hivyo kuanza kuhatarisha hali ya usalama nadhani ni wakati muafaka kuwakumbusha waamini wadini hizo mbili kwamba katika nchi hii wapo wananchi wengi tu ambao ama hawakubaliani na imani hizo au mambo ya imani sio priority yao japo kwa sasa.

Na hapa nawatambua watoto wote bila kujali wamezaliwa katika familia yenye imani ipi,watoto hawana dini,bali wanafuata maelekezo au matendo ya wazazi na ndugu zao bila kuhoji au kuomba maelezo ya ziada,hivyo wakati mnajipiga vifua kutetea imani zenu kwa kusema,sisi waislamu au sisi wakristo mnaombwa kukumbushwa kwamba watoto wadogo ambao natambua huwa mnamaanisha wako katika imani zenu,wanakua hawajafikia uwezo wa kujitambua kwa hoja kwamba wanasimama wapi,hivyo naomba wasipelekwepelekwe tu.

Kundi lingine ni lile la wasio na dini haswa,hasa wakazi wengi wa vijijini,japo natambua kuna jitihada kubwa za imani zenu hizi mbili kujitanua mpaka huko,chonde chonde,msiwalazimishe kushiriki kwenye mambo ya ugomvi,hawa mambo yenu haya sio priority zao,wanamatatizo mengi tu yanayowakabili,msiwaongezee tatizo la kuhishi kwa hofu.

Kundi lingine ni la maliberals,hata kama mnawatambua kama wenzenu kutokana na majina yao,na kuingia kwenye nyumba zenu za ibada,nyie wenyewe wadini ndio mnapaswa kuamua kama ni wenzenu kweli au la?wezi,wazinzi,walevi,waongo n.k hata hawa hayo mambo yenu sio priority zao,japo kwa sasa.

Halafu kuna kundi la imani zingine,nying tu.najua mnatambua hili vizuri tu.

Naomba haya yazingatiwe na muendeshe harakati zenu bila kuwaingiza kwenye misukosuko isiyowahusu,nasema hivi huku nikitambua kwa dhati kabisa kwamba ni haki yenu kuendeleza hizo harakati zenu,na ninawatakia mafanikio kwa kila mnachokipigania.
 
Back
Top Bottom