- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
sidhani kama walikuja kama wana usalama,nahisi walimwendea kama watu wanaohitaji mazungumzo ya faragha na Dr. Ull. Ndio maana baadhi ya mabandiko yanaonyesha kuwa ni watu ambao alikua anawasiliana nao mara kwa mara wakijitambusha kama maafisa wa serikali. Hata ikija kufahamika kwamba Dr.ull kuna uzembe aliufanya,hauwezi kuhalalisha unyama aliofanyiwa.!!!
Hakuna haki inayofuatwa wala itakayokusaidia vyombo vya usalama viapofanya udhalimu. Hizo haki ulizoorodhesha zinauhusiano gani na Dr Ulimboka na yaliyomkuta? Hakukuwa na muda kwani aliposimama kutaka kuondoka alifuatwa akapigwa na kuburuzwa kuelekea kwenye gari ambalo halikua na number ambamo aliteswa na baada ya kupoteza fahamu na wao kuamini kwamba kafa alitupwa porini. Hayo mambo ya number sijui jina utamuuliza nani?Siyo kwamba ninahalalisha kilichotokea; mambo alifyofanyiwa Dr ulimboka ni ya kinyaman na ya aibu sana kwa taifa. Nilichofanya hapa ni kukumbusha tena kuwa tujitahidi kuwa makini tunapochukuliwa na watu tusiowafahamu kwa kisingizio kuwa ni wana usalama. Sheria za kutulinda katika mazingira hayo zipo kama ilivyobainishwa hapo.
Mkuu.... hapana. Mwanzisha mada ni mtu makini sana, labda wengine ni wageni hapa jamvini hamjamfahamu. Nadhani inatosha kujibu kwa staha kuwa Dr Ulimboka alitekwa na sio kama alikamatwa. Lakini bado kuna kitu cha kujifunza hapa.Huyu mleta Uzi ni mlevi aende zake kwa mama muuza akazimue badala ya kuleta utumbo hapa jamvini
JF ni darasa kubwa sana, miaka minne iliyopita, kuna mwanachama mmoja alitupa somo hapa kama ifuatavyo
(1) Je kuna yeyte kati yetu amewahi kufikiria ku-exercise rights zake mbele ya polisi?
(2) Ilikuwaje Dr. Ulimboka alikubali kukamatwa na polisi bila kuzingatia haki zake hizo? hasa zile tatu za kwanza? Inawezekana hakuwa anazijua; tujitahidi tujifunze mambo mengine yaliyok nje ya taaluma zetu, hasa sheria.
(3) Inawezekana alikuwa anazijua lakini hakuwa na nafasi ya kuzi-exercise kwa vile askari walimfuata wakiwa wamemshikia bunduki, lakini je iwapo askari wakikushikia bunduki mbele ya watu ukanyamaza unategemea mtakapokuwa peke yenu watakuwa na huruma kwako? Kwa marekani kuna kitu kinaitwa miranda rights, ambazo kwa Tanzania usipojibu swali la polisi utapata kipigo kikali sana hasa iwapo utakuwa peke yako pamoja na askari hao. Salama yako mbele ya askari wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa una shaidi mwingine independent.
Iwapo katika post hiyo umeona ni ulevi basi wewe binafsi una upungufu mkubwa sana wa akili, yaani akili yako haijakomaa kuweza kutambua mambo yanayojadiliwa na watu wengin. Katika kiswahili tuna methali inasema jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza; kwako wewe post hiyo inaonekana ni usiku wa kiza kikubwa sana, yaani huoni kitu. Kwa akili yako hiyo, nakushauri usiwe unachangia post usizozifahamu; kwa vile umejiunga juzi tu, basi tulia uwe unasoma na kufuatiliwa watu wenye wakili wanavyojadiliana mambo hadi akili yako itakapokomaa vya kutosha.Huyu mleta Uzi ni mlevi aende zake kwa mama muuza akazimue badala ya kuleta utumbo hapa jamvini
Mazingira ya kukamatwa kwake hayakuruhusu hayo uliyotaja yafuatwe. Lakini kilichotekea ni dhahiri kuwa alitekwa na watu wa usalama kwa nia ya kummaliza.