Midekoo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2015
- 47,776
- 257,880
Sifa zote njema anastahiki Allah aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ahli zake, Sahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
“Basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu” (4: 3).
Katika aayah ya hapo juu imeweka baadhi ya vikwazo na masharti ya uke wenza na hivyo haifai kwa mtu kukiuka.
Ya kwanza: Mwanamme hawezi kuoa wake zaidi ya wanne.
Ya pili: Mwanamme anatakiwa atekeleze uadilfu baina ya wake zake. Na jambo hili ni wajibu kwake. Uadilifu unajumlisha makazi, chakula, mavazi, kuwatendea wema, kuwagawia muda sawa, na kadhalika. Na katika haya mume anabeba majukumu yote na ataulizwa Siku ya Kiyama kwa kutotekeleza kwa moja wapo ya tuliyo yataja. Kwa yule ambaye hana hakika ya kufanya uadilifu baina yao, Qur-aan inamwelekeza: “Hivyo oa mmoja tu”.
Haya yanatuelekeza kuwa wake wote wana haki sawa kabisa na hadhi kwa mume wao. Haifai kumpendelea mmoja juu ya mwengine. Na hii inamaanisha katika sheria ya Kiislamu, lau mume hatoweza kutoa msaada wa kutosha kwa yeyote miongoni mwa wake zake, huyo mke anaweza kwenda kwa Qadhi (au mahakama ya Kiislam) kushitaki na kudai talaka.