Wapendwa wanaJF, Heshima mbele!
Nimekuwa nikitafakari kuhusu haki za marehemu. Hivi marehemu anakuwa hana haki tena ya kuwa na siri? Mtakubaliana nami kwamba siku hizi kuna utaratibu wa kusoma wasifu wa marehemu wakati wa maziko. Kati ya vitu vinavyotajwa ni pamoja na umri, elimu, kazi alizowahi kufanya, idadi ya watoto na pengine idadi ya wake (wives), chanzo cha kifo, n.k.
Mfano: Watu wengi katika uhai wao hawapendi kutaja umri wao (mimi simo). Inakuwaje basi mtu aliyekuwa anaficha umri wake atajiwe tarehe au mwaka wake wa kuzaliwa anapokuwa marehemu?
Mbaya ni kwamba hakuna Chama cha Marehemu (kifupi CCM? Kibunango usinipige viboko) kinachoweza kutetea maslahi yao na wala hawawezi kuandamana kutoa kilio chao.
Mi nadhani habari yoyote ambayo mtu aliifanya siri yake, basi ibaki kuwa siri milele. Mnalionaje hili wanaJF?