Haki ya (za) mjane aliyeolewa tena

RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,966
2,019
Mwanamke akifiwa mumewe ana haki zipi katika mali za mumewe (au mali walizochuma na mumewe)? Yeye huwa ni msimazi tu wa mirathi au ana haki ya mgao kama mali zitagawanywa?
Je, kama akiolewa tena bado ana haki hizo?
Katika hili mume hakuacha wosia na ni Tz.
 
Roya Roy, kwanza tuanze na mjane kama mjane kabla hajaolewa tena manaake kama akiolewa tena huyo si mjane ni mwanandoa kama walivyo wengine. Mjane wa kike kama walivyowajane wengine anazo haki katika ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka,1971. Anayo haki ya kuendelea kutumia jina na mume wake(right to surname),anayohaki ya kuishi kwenye nyumba ya marehemu mume wake,kuiangalia na kuwatunza watoto na mali za marehemu kwa niaba yao,Vile vile yeye kama warithi wengine ana haki ya kupata mgao wa mali toka kwa mumewe kwa matumizi yake yeye(si kama mwangalizi wa familia) kwa kuwa katika hiyo mali ya mumewe yeye pia amechangia upatikanaji wake.Hapa watu watasema hapana hiyo haki ni ya wakati wa talaka tu,hapana hiyo ni termination right,kwa kuwa talaka inafanya ndoa iterminate na kifo pia vilevile.
Haki ya mjane huyu si asilimia 50 kwa hamsini,kwanza inategemea ushiriki wake katika kuchuma,na pia hata wosia aliouacha marehemu.Sehemu hii kwa kawaida huwa ina utata sana hasa pale marehemu ambapo hakumtaja kabisa mkewe kuwa mrithi lakini hata hivyo wosia huo huwa hauna nguvu kama haukushuhdiwa na watu wawili,na au haukusajiliwa.kikubwa na kushuhudiwa na mwenye kuandika awe wakati anaandika alikuwa na akili timamu.Hata hivyo kisheria unaweza kuchallenge wosia hasa kama hakukuwa na sababu za msingi za kukutenga.
Mjane huyu akiwa msimamizi wa mirathi cheo hicho si milele kinaisha pale akishamaliza kugawa mali zote na kukabidhi orodha ya ugawaji wake mahakamani(inventory).baada ya hapo akiolewa endapo alikuwa akiishi kwenye nyumba ya watoto anaondoka kwenye ile nyumba na kwenda kwa mumewe na kama ilikuwa ni nyumba alioirithi bado atakuwa na haki ya kuendelea kuishi kwenye hiyo nyumba.
Kwa leo ngoja tuishie hapa
 
.baada ya hapo akiolewa endapo alikuwa akiishi kwenye nyumba ya watoto anaondoka kwenye ile nyumba na kwenda kwa mumewe na kama ilikuwa ni nyumba alioirithi bado atakuwa na haki ya kuendelea kuishi kwenye hiyo nyumba.
Kwa leo ngoja tuishie hapa

Agustus,

Je akipata bwana- huyu mjane hana haki kuishi na mume wake mpya kwenye nyumba alioacha marehemu? Yaani mme mpya akahamia kwake? Na kama ni watoto wakalelewa wote na huyu bwana mpya?
 
Mjane...Mwanamke aliye fiwa...Je Mwanaume aliye fiwa anaitwa nani?
Malaya- Mwanamke....Mawaume wa tabia hiyo anaitwaje?....

Haya Ma thead ya mifumo dume Ya futwe...
 
akipata mume huyu mjane hana haki ya kuishi na huyo mume mpya kwenye nyumba ya marehemu,ambayo si yake,labda kama hiyo nyumba ya marehemu yeyey pia ni mrithi lakini kama si mrithi hawezifanya hivyo,japo jamii inayomzunguka inaweza kumvumilia na kumwacha aishi naye kama labda watoto bado wadogo anawalea lakini sio kisheria.
 
August..mas-ala lazima useme sheria unayotumia ni ipi? ya serikali? Kikabila au KIISLAM uislam ni mfumo kamili wa maisha so kila kitu kina jawabu lake.

Mke kuchukua Jina la Mumewe ni system za Kizungu...leo Mfano ROSE XYZ anaitwa ROSE SALUM,kesho mumewe akafariki, na akaja kuolewa na JOHN yawaje...PLEASE wanawake wabakie na MAJINA YA FAMILIA/KOO ZAO. HII NI DHULUMA INAFANYIWA WAO< LKN HAWAIONI..
 
Back
Top Bottom