papag
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 1,137
- 1,608
Kwa uchungu mkubwa nimeona niongee kuhusu mkoa wangu wa Morogoro, kinachoendelea kinanihuzunisha sana, mauaji ya kusikitisha kila wakati, nimeona kijana mwingine tena kauawa, ni miaka mitatu sasa toka mtoto wangu mpendwa wa kwanza kwenye tumbo langu toka atolewe uhai wake.
Mlindwa wangu kila nikikumbuka nahisi naota mwenzenu, kijana wangu mpole mstaarabu, hakuwa na baya ma mtu, simu tu imechukua uhai wake, kinachoniuma zaidi,hukumu ndio imetolewa na huyo sijui jaji eti namuona jaji wa mchongo tu,wauaji wamekiri, na wamejieleza vizuri tu, cha ajabu hukumu imetolewa kifungo cha miaka 17, najiuliza aliyekamatwa na bangi, mbakaji hukumu yao miaka 30, ila muuaji ndio miaka 17?
Hivi huyu jaji ananichukuliaje mimi, Mungu anakuona popote ulipo we jaji, hata hiyo siku ya hukumu sikupewa taarifa wakati nilikuwa nauliza kila wakati lakini nilikuwa naambiwa nisubiri nitapewa taarifa, matokeo yake wamefanya uhuni tu mi nauita, ila wote waliohusika kupindisha haki mkono wa Mungu utawapitia acha niendelee kulia iko siku na wao watalia na kusaga meno.
nimetaka nakala ya hukumu nayo imekuwa tabu kuipata hivi hii nchi ni ya baadhi ya watu? tutegemee mauaji ya watu kwa hukumu hizi za kipumbavu yataisha? Tukimbilie wapi wakati wanaotoa haki baadhi yao ndio hao wanafiki wakubwa, Mungu anipe subra na uvumilivu, hakuna haki dunuani