Haki ya abiria inakuwa wapi hapa kisheria?

Haki ya abiria inakuwa wapi hapa kisheria?

Gaston Mbilinyi

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2010
Posts
296
Reaction score
51
WanaJF,

Jana nilikuwa nasafiri kwa daladala tokea Mzumbe kwenda Morogoro(M). Njiani tukasimamishwa na trafik ambaye alimchukua kondakta wa daladala hiyo wakawa na mjadala kwa takribani nusu saa mbali na lilipokuwapo gari. Abiria tulipoomba kuwa ama tupelekwe tuendako na wenye gari wafikishwe katika vyombo sheria iwapo yako makosa yaliyofanywa kisheria au tuambiwe gari mbovu ili turudishiwe nauli ili tupande gari lingine. Trafik waliokuwapo hapo wakawa wakali kwa madai kuwa tunawaingilia kazi na wanaweza kutufikisha kituo cha Polisi na baadae kufikishwa mahakamani.

Kwa majibu hayo ya trafik ilibidi abiria tuwe wapole, lakini swala hilo lilinipa cha kufikiri na hatimaye sijapata jibu na ndio maana nikaona niombe msaada wenu wanaJF ili mnielimishe kama siku nyingine nifanyeje ikitokea hali kama hiyo maana naona kama haki yetu abiria ilikuwa inadhurumiwa tu. NISAIDIENI!
 
Na mgeendelea kupiga kelele wangewashuti viuani ninyi abiria woooote maana vitu vyenye ncha kali wanavyo na wako juu ya sheria
 
Hao siku hızı wanatisha mkuu!risasi wanazimimina tu kama wanacheza vile ni bora abiria mlifyata mapema yangekuwa mengine sahizi Chezea Mw ...ma ww
 
kama ni kweli, walimhoji kwa muda huo uliosema, basi hamkutendewa haki. na vilevile kama kweli mlipouliza mustakabali wenu mlitishiwa basi mlionewa saana. ila siku hizi kuna utandawazi na makamanda wote wa polisi wametoa namba zao za simu .ni vyema khali kama hiyo inapotokea mkaomba msaada zaidi kwa wakubwa wao. polisi wao wanahaki ya kutekeleza wajibu wao bila bughudha, khali kadharika abiria pia tunahaki zetu. hivyo askari naye anatakiwa awe mwepesi wa maamuzi.
 
Ni kweli tatizo na hawa wakuu wao wanawatetea unless kama issue imegusa hisia ya watu wengi kwa kuwa hawa police inasemekana huwa wanapeleka kiwango flani kwa makamanda wao na hata kama hawapeleki lakini nao makamanda kuna sehemu huwa wanawaingilia kiutendaji hawa staff wao hivyo kwa mantinki hiyo ikitokea wana matatizo wanawakingia kifua kwa kusema tunalifanyia kazi
 
Askari ikuwa wajibu wake awaeleze kwanini anawachelewesha na hiyo ndiyo inayotakiwa kujenga mahusiano mazuri na jamii. Askari anayeongea kwa kificho na kondakita ni wale watafuta rushwa .ambao wanachafua hazi ya jeshi la polisi.
 
poleni sana,polisi wamekuwa kama wahuni wasio jua kutekeleza majukumu yao kwa weledi
 
Ni kweli tatizo na hawa wakuu wao wanawatetea unless kama issue imegusa hisia ya watu wengi kwa kuwa hawa police inasemekana huwa wanapeleka kiwango flani kwa makamanda wao na hata kama hawapeleki lakini nao makamanda kuna sehemu huwa wanawaingilia kiutendaji hawa staff wao hivyo kwa mantinki hiyo ikitokea wana matatizo wanawakingia kifua kwa kusema tunalifanyia kazi
jibu alilokupa lina maana mbili, moja anatekeleza , mbili amekuacha kiaina. polisi si mali ya mtu, unyama unyamani. usichoke tunza kumbukumbu zako za mawasiliano, mpigie mkuu wake zaidi na mueleze hatua zako za mwanzo. mkuu amini usiamini jambo lako litatatuliwa kwa haraka.
 
Tupo pamoja mkuu just nilikuwa naonyesha jinsi hawa watu wanavyolindana though ukifuatilia ikatokea hawatekelezi si unakimbilia kwa DC ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na kuwa kuwa ni mwanasiasa anapenda sifa lazima issue itabebwa kisiasa na kama kuna ukweli lazima huyo mkuu wa police atapewa makavu live
 
Askari ikuwa wajibu wake awaeleze kwanini anawachelewesha na hiyo ndiyo inayotakiwa kujenga mahusiano mazuri na jamii. Askari anayeongea kwa kificho na kondakita ni wale watafuta rushwa .ambao wanachafua hazi ya jeshi la polisi.

Nimekugongea like hapo kwenye maandishi meusi, na ndio maana hawa jamaa huwa wanaongea na makondakta. Kwanini inapotokea ajali anaekamatwa ni dereva na si kondakta?jibu hapa ni kwamba traffic police wanatakiwa waongee na madereva na si makondakta kwa kuwa dereva ndio ana dhamana ya usalama wa gari husika.
 
Back
Top Bottom