maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,144
Juzi siku moja baada ya uzinduzi wa barabara ya juu kuna daladala ya kutokea Makumbusho kwenda Buguruni ilileta tafrani baada ya konda kumwambia dereva asipite flyover ili ajazie abiria pale kituo cha mafuta cha Oilcom iliyo pembeni ya flyover.
Dereva kama kawaida yao wanatumiaga akili za konda kuendesha gari nae akapita chini wakati abiria walikua wanahamu kupita juu maana wengi walikua hawajaizindua bado na hawakupenda kitendo hicho cha utovu wa nidhamu cha kuwanyima uroda wa flyover wakaanza kurusha maneno.
Kilichowauma abiria zaidi ni baada ya konda kukosa abiria pale sheli ndipo wakataharuki kulikua na sababu gani kuwanyima raha. Mzozo ulikua mkubwa mpaka daladala ikapark pembeni na kondakta kukunjwa shati huku dereva akisema yeye alimsikiliza konda ila nae alitamani kupita juu.
Kondakta huyo ilibidi awe mpole baada ya kuona gari zima limechachamaa na kulazimika kuomba radhi na kukiri hadharani kwamba hatorudia tena kufanya upuuzi wa aina hiyo na ndipo safari ikaendelea huku abiria wakiangalia kwa uchungu jinsi magari mengine yanavyopita juu ya flyover wakati wao wamenyimwa hiyo raha.