Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 481
Jambo wote JF,
Msichoke kusoma! Nahitaji msaada!
Ndugu naombeni msaada wenu. Wakati fulani huko miaka ya nyuma, niliwahi kuoa mdada mmoja mkenya. Tuliishi kwa miaka 7.
Katika ndoa yetu ambayo haikuwahi kuwa na baraka za Paroko tulibahatika kupata mabinti 2. Wa kwanza alizaliwa 1990 na wa pili 1995. Tulikorofishana naye 1996. Kipato changu hakikuwa kinatosha. Nilikuwa najilipia shule na wakati huo huo kuhudumia familia. aliondoka na kurudi kwao kwa madai hakuzoea shida. Wakati huo nilikuwa naishi Dar. Aliondoka na watoto wote. Yule wa kwanza alipofika darasa la 7 akaleta ukorofi (kwa madai ya mama yake) ikabidi niende kwao Nairobi na kwa kuongea na binti ilibidi niondoke naye na kumtafutia shule huku.
Alipata shule na sasa yuko high school. Shida sasa! Huyu mdogo naye kamaliza 8, hakupata alama za kutosha kujiunga na form 1. Mama yake kanipigia simu kuwa mtoto hakufanya vizuri. Tukakubaliana atafute shule huko na mimi nitafute atakayefanikiwa basi aende shule.
Taarifa hizi ni tangu 28th Dec 10. Nilihangaika kwa kweli, sijui yeye kama alikuwa anahangaika! Last week nikapata shule fulani ya kanisa katoliki. Nikamwambia, kwanza hakutaka aende lakini baada ya kuhimiza sana akasema hana muda wa kumpeleka. Ikabidi nikatize safari yangu na kwenda NRB kumchukua.
Nikampeleka shuleni na kwa bahati akafanya vizuri. Wale masista wa pale wakanambia nikalipe ada na ikifika J2 nihakikishe nampeleka mtoto shule. Nilikiwa njiani nikamjulisha huyu mama kuwa mtoto anatakiwa shule jumapili. Akaanza oooh ni mapema sana na mimi nilikuwa na mipango ya shule, mara sijui huyu mtoto kakulia kwenye maadili ya kiislamu umempeleka shule ya kikristu. Nilikasirika na kukata simu.
Binti alikubali kusoma pale. Kesho yake nikampigia simu kuwa naenda kulipa ada akanung'unika sana mwisho akanambia sawa nenda kalipe. Nikaenda kulipa shs 1,438,000/= acha mahitaji mengine. Kumbe huku nyuma akampigia simu mtoto aombe kwenda kuchukua baadhi ya vitu vyake. Kwa nia njema kabisa nikamkubalia.
Kufika jioni akanipigia simu kuwa amepata shule huko kenya na ada ni shs 55,000/= kwa muhula. Kwanza niliduwaa halafu nikamuuliza zile ambazo nimeshalipa inakuwaje? Alichonambia hiyo itabidi iwe hasara. Nikamwambia kuwa hayo ni masihara.
Nilimtaka ahakikishe kuwa leo Jumamosi tarehe 22/1/11 kuwa mtoto anakuwa hapa kwangu ili nimpeleke shule Kesho. Niandikapo ujumbe huu SIJAONA HATA ALAMA YA HUYU BINTI YANGU KUJA. Na mbaya zaidi hata simu zao hazipatikani.
Nifanyeje jamani, shida sio hasara ila ile munkari alokuwa naye ya kusoma hapa kwetu Tanzania na ndoto alizokuwa nazo kwa kipindi kifupi nilichokaa nacho ndo kinanitesa.
Jamani nisaidieni ushauri.