Haki na wajibu ndio tunda la amani

Haki na wajibu ndio tunda la amani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,378
Truth and reconciliation... Ukweli na maridhiano huletwa na haki na wajibu baada ya hapo ndio hupata matokeo ya tunda la amani

Kuna kitu tunakilazimisha kifanyike hata kama hakiwezekani kabisa! Tumepanda magugupori lakini tunataka tuvune mahindi mtama na uwele

Tumefuga nguchiro na panyabuku lakini tunataka watotoe vifaranga vya kuku au bata
Kwa uchafu wetu tumeruhusu Chawa, kunguni na papasi waweke makazi ya kudumu viungani mwetu, lakini kwa uwendawazimu wa kiwango cha lami tunasema hawa ni sisimizi madu na mende.. Sijui tunatafuta kuvunja rekodi gani ya dunia

Zimebakia siku chache kuumaliza mwaka 2025.. Mwaka ambao hautasaulika kwenye historia ya Tanganyika.. Si kwa mema la hasha, si kwa furaha bali kwa uchungu huzuni na majonzi makubwa, kutokana na ukatili mkubwa uliopelekea kumwaga damu za maelfu ya watanganyika wasio na hatia ndani ya siku tano za giza kati ya October 29 na November 3

Baada ya yote hayo ya kunajisi uumbaji na ardhi, tukaanza kutangaziwa maridhiano na amani huku haki wajibu na ukweli vikitengwa pembeni kabisa! Hiki nacho kinaweza kuwa kituko cha aina yake

Tungeanza na UKWELI kwanza wa nini kilitokea ama kilisababisha yatokee yaliyotokea.. Ukweli huo ungefuatwa na takwimu sahihi na za wazi
Walikufa/uliwa wangapi
Walijeruhiwa wangapi
Walitibwa wangapi na kurusiwa

Wangapi bado wako kwenye matibabu

Wangapi walipata majeraha makubwa

Wangapi walipata ulemavu wa muda

Wangapi walipata ulemavu wa kudumu

Wangapi walipotea na kupatikana wakiwa hai

Wangapi walipotea na kupatikana wakiwa marehemu
Wangapi walipotea na hawakuwahi kupatikana

Baada ya ukweli huo tungefuata WAJIBU.. Nani awajibike kwenye nini kwa yaliyotokea.. Uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja na uwajibikaji wa pamoja

Kisha ingefuata HAKI.. haki kwa wote waliodhurika kwa namna moja ama nyingine! Hasa wahanga wa vifo, majeruhi na ulemavu. Bila kusahau familia zilizoathirika kutokana na hayo madhila
Baada ya yote hayo tungetafuta suluhu ya muda mfupi na ya kudumu kwenye meza ya maridhiano.. Hapa sasa amani ingepatikana bila hata ya kutumia nguvu yoyote!

Huu si mchakato wa siku mbili au tatu ni mchakato mrefu na mgumu lakini kwanza NIA NJEMA ingeoneshwa kwa vitendo kwa kutangaza mkeka huu wa kutafuta amani

Hii janja janja inayoendelea ya kutangaza amani huku mengine ya msingi Sana yakifumbiwa macho haitatufikisha popote na badala ya kudhani kwa kufanya hivyo tutafubaza harakati ni kujiongopea kulikopitiliza kwakuwa badala ya kufubaza ndio tutakuwa tunakomaza
1766640011682.jpg
 
 
Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
 
Nchi zote Duniani zilizotaka haki kabla ya Amani ziliishia kwenye machafukobna vita vya wenyewe kwa wenyewe,
Haki iko mbinguni tu tena siku yako ya hukumu.!!
 
TAKWIMU ZA WALIOUWAWA,WALIOPOTEZWA NA MIILI ILIYOPOTEZWA MBONA HAIWEKWI HADHARANI?
1766561720773.jpg
 
Duniani hakuna haki mkuu ni kuvumiliana tu neno HAKI ni pana sana kiasi kwamba haki kwako inaweza isiwe haki kwa mwingine

Chukulia haki za waislamu haziwezi kuwa haki kwa wakiristo and the vice versa

Hivyo hivyo katika democracy pia hakuna haki mbadala

Haki ipo kwa Muumba pekee kwani yeye ndio Alfa na Omega ndio jaji wa majaji akisema neno huwa na hakuna wa kumpinga

Dunia haina haki kwani hakuna sheria moja dunia nzima inayotawala HAKI, haki kwako inaweza isiwe haki kwa mwingine

KIKUBWA KUVUMILIANA NA KUPENDANA
 
Adhabu sio lazimu mtu akuchape fimbo, hata kuwa mtanzania ni adhabu tosha kabisa!, poleni nyote mlioumizwa na utawala huu.
 
 
Kutoka kwa Harakati Za Genz

Kilichotufikisha hapa ni hiyo AMANI mnayokomaa nayo.

Watu wanadai HAKI nyie mmeshupaza shingo kuitaka AMANI. Miaka yote mliyokuwa mnajivuania kuwa "Tanzania ni kisiwa cha AMANI" ni kwasababu watanzania waliamua kuwa WAVUMILIVU.

Walivumilia KUTEKWA na kupotezwa kwa ndugu na wapendwa wao. Huku kukiwa hakuna uwajibikaji kutoka kwa vyombo vinavyohusika.

Walivumilia UFISADI mnaofanya kila siku huku wao wakiishi maisha ya shida hata kupata huduma za MSINGI kwao imekuwa shida.

Walivumilia kupokwa kwa haki yao ya KUCHAGUA viongozi wao wanaowapenda na mkajichagua nyie kwa mtutu wa Bunduki ili muwatawale.

Kiufupi yote haya waliamua KUVUMILIA na sio kulinda AMANI. Mkiitaka AMANI ya kweli basi tendeni HAKI-kinyume na hapo ni sawa na kupaka rangi UPEPO.

WATANZANIA WA LEO SIO WALE.

#TUTAKUWEPO🫵😎
1766668915448.jpg
 
 
Brother katika story zako humu ulisema ushawahi kufanya kazi monchwari.sasa Jana nimepanda gari mwenge.dereva akaanza kupiga story za monchwari.moja anasema mule monchwari yeye ana lala vizuri tu na ule ubaridi.
Ila la pili anasema usiku alikuwa anasikia maiti zinajinyoosha yaani unasikia viungo vinalia kabisa.sasa hapa ndo kanichanganya.ipo hyo?
 
Truth and reconciliation... Ukweli na maridhiano huletwa na haki na wajibu baada ya hapo ndio hupata matokeo ya tunda la amani
Naunga mkono hoja, hii hoja ya haki na wajibu pia mimi nimeihubiri sana humu Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!

Na hapa Ili Haki Itendeke, Sio Tuu Itendeke, Bali ni Lazima Ionekane Imetendeka!, Kama Tumewashitaki Waandamanaji, Pia Tuwashitaki na Wauaji!

P
 
Brother katika story zako humu ulisema ushawahi kufanya kazi monchwari.sasa Jana nimepanda gari mwenge.dereva akaanza kupiga story za monchwari.moja anasema mule monchwari yeye ana lala vizuri tu na ule ubaridi.
Ila la pili anasema usiku alikuwa anasikia maiti zinajinyoosha yaani unasikia viungo vinalia kabisa.sasa hapa ndo kanichanganya.ipo hyo?
Mochwari kuna matukio live na halisi ya marehemu lakini vilevile kuna hallucinations za kawaida kutokanana na hofu na wore lakini pia kuna matukio ya wanga na wachawi
Sometimes huja kwa pamoja ama kwa kupokezana. Lakini pia bangi ukiipuliza na kuingia mule ndani unaweza ukadata maana bangi ina tabia ya kufungua jicho la tatu
 
Back
Top Bottom