Haki na wajibu ndio tunda la amani

Haki na wajibu ndio tunda la amani

Mochwari kuna matukio live na halisi ya marehemu lakini vilevile kuna hallucinations za kawaida kutokanana na hofu na wore lakini pia kuna matukio ya wanga na wachawi
Sometimes huja kwa pamoja ama kwa kupokezana. Lakini pia bangi ukiipuliza na kuingia mule ndani unaweza ukadata maana bangi ina tabia ya kufungua jicho la tatu
Sawaa Kwa uzoefu wako ushawahi kusikia viungo vya marehemu vikilia akijinyoosha.sasa huyo SI atakuwa mzima?
 
Sawaa Kwa uzoefu wako ushawahi kusikia viungo vya marehemu vikilia akijinyoosha.sasa huyo SI atakuwa mzima?
Kuona Mona kwa moja hapana! Ila mochwari kuna sauti nyingi na za ajabu.. Hasa kukiwa kimya na kwenye utulivu usiku
 
Truth and reconciliation...
Too bad. The topic for discussion starts and ends right there!
"Truth and reconciliation" by whom and with who?

Can there be "truth' from an illegitimate entity fighting tooth and nail to stay in power by all means necessary; including killing people?

Utaanzia wapi ku'reconcile' na kundi lisilokuwa na uhakika wa kubaki madarakani, madaraka ambayo waliyanyakuwa kwa kutumia nguvu?

Lakini nikiachana na hayo ya maridhiano; kwa mara ya kwanza naiona hiyo bendera iliyofunika hayo majeneza kwa jicho tofauti kabisa.

Bendera hii siyo nzuri kwa taifa letu.
Truth and reconciliation... Ukweli na maridhiano huletwa na haki na wajibu baada ya hapo ndio hupata matokeo ya tunda la amani

Kuna kitu tunakilazimisha kifanyike hata kama hakiwezekani kabisa! Tumepanda magugupori lakini tunataka tuvune mahindi mtama na uwele

Tumefuga nguchiro na panyabuku lakini tunataka watotoe vifaranga vya kuku au bata
Kwa uchafu wetu tumeruhusu Chawa, kunguni na papasi waweke makazi ya kudumu viungani mwetu, lakini kwa uwendawazimu wa kiwango cha lami tunasema hawa ni sisimizi madu na mende.. Sijui tunatafuta kuvunja rekodi gani ya dunia

Zimebakia siku chache kuumaliza mwaka 2025.. Mwaka ambao hautasaulika kwenye historia ya Tanganyika.. Si kwa mema la hasha, si kwa furaha bali kwa uchungu huzuni na majonzi makubwa, kutokana na ukatili mkubwa uliopelekea kumwaga damu za maelfu ya watanganyika wasio na hatia ndani ya siku tano za giza kati ya October 29 na November 3

Baada ya yote hayo ya kunajisi uumbaji na ardhi, tukaanza kutangaziwa maridhiano na amani huku haki wajibu na ukweli vikitengwa pembeni kabisa! Hiki nacho kinaweza kuwa kituko cha aina yake

Tungeanza na UKWELI kwanza wa nini kilitokea ama kilisababisha yatokee yaliyotokea.. Ukweli huo ungefuatwa na takwimu sahihi na za wazi
Walikufa/uliwa wangapi
Walijeruhiwa wangapi
Walitibwa wangapi na kurusiwa

Wangapi bado wako kwenye matibabu

Wangapi walipata majeraha makubwa

Wangapi walipata ulemavu wa muda

Wangapi walipata ulemavu wa kudumu

Wangapi walipotea na kupatikana wakiwa hai

Wangapi walipotea na kupatikana wakiwa marehemu
Wangapi walipotea na hawakuwahi kupatikana

Baada ya ukweli huo tungefuata WAJIBU.. Nani awajibike kwenye nini kwa yaliyotokea.. Uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja na uwajibikaji wa pamoja

Kisha ingefuata HAKI.. haki kwa wote waliodhurika kwa namna moja ama nyingine! Hasa wahanga wa vifo, majeruhi na ulemavu. Bila kusahau familia zilizoathirika kutokana na hayo madhila
Baada ya yote hayo tungetafuta suluhu ya muda mfupi na ya kudumu kwenye meza ya maridhiano.. Hapa sasa amani ingepatikana bila hata ya kutumia nguvu yoyote!

Huu si mchakato wa siku mbili au tatu ni mchakato mrefu na mgumu lakini kwanza NIA NJEMA ingeoneshwa kwa vitendo kwa kutangaza mkeka huu wa kutafuta amani

Hii janja janja inayoendelea ya kutangaza amani huku mengine ya msingi Sana yakifumbiwa macho haitatufikisha popote na badala ya kudhani kwa kufanya hivyo tutafubaza harakati ni kujiongopea kulikopitiliza kwakuwa badala ya kufubaza ndio tutakuwa tunakomazaView attachment 3520598
Bendera hii ni MBAYA
 
Chukulia haki za waislamu haziwezi kuwa haki kwa wakiristo and the vice versa
Wananchi kuchagua viongozi kwa uhuru bila kusumbuliwa nako ni kumnyima haki mwislamu au mkristo?
Hivi akili zenu huwa mnazipeleka wapi mnapoandika upuuzi namna hii?
 
Mshana Jr rekebishwa kichwa cha habari kama sijakosea
Haki na Wajibu ndio tunda la Amani? Nadhani Amani ni tunda la Haki na Wajibu.
 
Mshana Jr rekebishwa kichwa cha habari kama sijakosea
Haki na Wajibu ndio tunda la Amani? Nadhani Amani ni tunda la Haki na Wajibu.
Unaweza kuwa sawa lakini kwa muktadha wa hili andiko nimefafanua kwa mtazamo yakinifu kwenye maudhui
Kwasasa watawala waliojipa madaraka feki hawaongelei kabisa haki na wajibu bali amani ndio wanaipambania sana
 
Haki na wajibu sahihi 100%

Mfano tukiamka watanzania wote tukasema tudai haki , tutaikosa .?

Kinachotokea ni sisi wenye nchi kwakuwa tushazoea kutibu ugonjwa kwa painkillers .


.
 
Kwahiyo ili uone akili ya mtu hadi aungane na hoja yako akipinga hana akili

That's dictatorship!!!
Ni wapi nimeandika hivyo?
Huwezi kuweka mawazo yako kuwasilisha ninachofikiri mimi. Huku ndiko ninakokuita kukosa akili unakozidi kudhihirisha hapa.
 
Back
Top Bottom