Haki haitendeki, tumeamua kusimama na #FreeMaxenceMelo

Haki haitendeki, tumeamua kusimama na #FreeMaxenceMelo

Alafu lijamaa haliogopi, linatumia Real Name, alafu anajiingiza kwenye mtanange huu???
Jamaa ana moyo sana
 
Mungu ni wetu sote...atatupingania na mtetezi wetu atatoka ..asubhi itafika tu japokuwa itachelewa
 
9f5fab5c3b132c97d1c9982b88b157d5.jpg


66773578b3daada6cedd16cb8a31cb4b.jpg
 
Hii tabia ya ukandamizaji wa uhuru wa raia ndilo kaburi la serikali ya awamu hii
[HASHTAG]#free MaxenceMelo[/HASHTAG]
 
Kuna muda nataka kuongea mpaka nashindwa kabisa chuki niliyonayo dhidi ya Serikali kwa kitendo cha kumkamata ndugu yetu bila sababu za msingi.....

Nasikia maumivu utafikiri ni Mimi ......

Hii ni kwa sababu nililelewa na kukua katika misingi ya haki na Uhuru......

Naona kama nipo tayari kwa lolote kwa mtu anayetaka kupoka Haki na Uhuru wangu.....

Mungu anisamehe kama chuki yangu ni mbaya kwenye hili swala.......

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
Mkuu umenigusa sana, mimi mwenyewe nimejenga chuki isiyoelezeka dhidi ya watawala wa nchi yangu
 
Alafu lijamaa haliogopi, linatumia Real Name, alafu anajiingiza kwenye mtanange huu???
Jamaa ana moyo sana
Woga ni Dhambi,chanzo cha Magonjwa na Vifo.Tunataka uhuru wa kufikiri na si kufikirishwa kwa namna moja.Free Melo.
 
Mbegu inazidi kupandwa ila matunda yake yakikomaa sijui kama patapatikana mahala pa kuyala.
 
Una akili kama za Jesca, kama aliemshikila hayupo JF kwa nini anahitaji habari na majina ya watu wa JF asiende kuuliza mmiliki wa FB kama nia yake ni kushikilia wenye mitandao bila kufuatilia hiyo mitandao?!
Hahaaa umeujibu vzuri aisee#FreeMelo
 
Heshima kwenu Wakuu,

Tumefuatilia kwa karibu kutoka kwa Jopo la Mawakili Wasomi, ndugu jamaa na marafiki ambao, wamekuwa katika jitihada za Kisheria na kiungwana, kujua makosa ya Maxence na kumuwekea dhamana ili awe huru. Majibu tuliyopata yanaonyesha kile anachofanyiwa ndugu yetu hakina na wala hakifuati kifungu cha Sheria yoyote katika Sheria za nchi ya Tanzania.

Waliomshikilia wanaonekana kuongozwa kwa maelekezo na nguvu kubwa isiyomithilika wala kudhibitika hata kwa Katiba ya nchi. Mathalani leo ni siku ya pili Maxence ameshikiliwa bila kufikishwa mahakamani, alipaswa ahojiwe ndani ya saa nne (4) toka awekwe kizuizini lakini kahojiwa jana jioni karibu baada ya saa zaidi ya 28, hadi sasa mawakili wake hawajapewa hati ya mashtaka hivyo hawajui kashikiliwa kwa kosa gani na lini atafikishwa mahakamani. Na waliomshikilia wanajiapiza kuwa Mawakili hata waende mahakama kuu, Maxence hatapelekwa mahakamani mpaka wao wapende!

Na kama Maxence kashikiliwa kwa kosa linalohisiwa kwamba ni kwa kukataa kutoa taarifa za faragha za baadhi ya watumiaji wa JamiiForums.com, basi nayo itakuwa ni usiginaji wa Sheria maana kesi ya hilo suala tayari iko mahakamani na Maxence yuko nje kwa dhamana.

Kufuatia hayo yanayoendelea, katika hatua ya awali leo, wale wote tunaoguswa na kile anachokisimamia na kukipigania Maxence tunaombwa kuanzia sasa kuungana kwenye kampeni maalum kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Instagram, WhatsApp) inayoendeshwa chini ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]. Picha maalum kwa ajili ya kampeni imeambatanishwa hapo chini.

Wale mtakaotumia lugha za kigeni e.g Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, Kireno, n.k kumbukeni kunakili mashirika ya Kimataifa hasa yale yanayoshughulikia masuala ya habari, haki za waandishi wa habari, haki za binadamu na utawala bora.

Na pia kwa wale tunaolenga kufikisha masikitiko yetu kwa vyombo vya ndani, tumieni lugha ya staha kumueleza Rais Magufuli, Waziri Mwigulu Mchemba, IGP Mangu, Kamanda Sirro, na DCI Wambura.

Japo kwa maapizo ya waliomshikilia hakuna dalili, lakini iwapo kufikia saa saba (7) mchana wa leo, Maxence atakuwa bado hajafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka, tutafahamishana hatua inayofuata.

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]
View attachment 446473
Tunakupenda max brother......chochote kinachotokea tunakuombea MUNGU akulinde watu wabay wasikudhuru ila uwe salama salimini popote ulipo.
 
Back
Top Bottom