Haka kaugonjwa vipi

3ZOV

JF-Expert Member
Dec 28, 2020
6,249
6,979
Habari za jumapili ndugu zangu na wikiendi kwa ujumla

Nije kwenye mada,

Nasumbuliwa na mafua wiki sasa mchana naweza nikashinda vizuri na nikaendelea na kazi zangu vizuri tu ila ikifika usiku wakati wa kulala Hali inabdalika Sana inatokea Hali mpaka pua moja inaziba napumua kwa shida Sana
Sasa kuna kipindi nilikuwa ikifika wakati wa kulala natafuna tangawizi basi Hali inakuwa shwari
Baadae nikanunua citrozen nikawa nakunywa ila hizi dawa sasa nikinywa asubuhi basi kutwa nzima mwili unakuwa hauna nguvu, mdomo unakuwa mchungu na njaa kali Sana nikaacha kuzitumia hizi dawa
Nimerudi kwenye matuminzi ya tangawizi na mazoezi kidogo basi usiku usingiz unakuwa mzuri
 
Kula Mali mao fanya mazoezi. Sio kila mafua Ni korona hofu nayo unakusumbua.

Vaa barakoa usije ambukiza wenzako.
 
Wahi hospitali, sio kwaajili yako, wewe unaonekana haujali ndio maana umeacha week ipite unapiga soga JF. Ila nenda kwaajili ya kuwaokoa uwapendao na wanaokutegemea.
Mkuu nilienda hospitali nikapewa citrozen nikapona kabisa after two weeks mafua yamerudi tena
Nikaamua kutumia tamgawizi na mazoezi kidogo nikapata unafuu
Hali ilioko sasa hivi sina uwezo wa kunusa na ladha ya chakula imepotea kabisa
 
Kula Mali mao fanya mazoezi. Sio kila mafua Ni korona hofu nayo unakusumbua.

Vaa barakoa usije ambukiza wenzako.
Kwa maeneo ya kazi alikuja mteja ana mafua na jirani yangu pia alikuwa na mafua sasa baada ya kuyapata mimi nikachukulia Hali ya kawaida tu
Ila nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Mkuu nilienda hospitali nikapewa citrozen nikapona kabisa after two weeks mafua yamerudi tena
Nikaamua kutumia tamgawizi na mazoezi kidogo nikapata unafuu
Hali ilioko sasa hivi sina uwezo wa kunusa na ladha ya chakula imepotea kabisa
Uwezo wa kunusa kupotea,kupotea kwa ladha ya chukula ni moja za dalili zinazoonyesha kwa wagonjwa waliopona covid-19 aka corona..
 
Mkuu nilienda hospitali nikapewa citrozen nikapona kabisa after two weeks mafua yamerudi tena
Nikaamua kutumia tamgawizi na mazoezi kidogo nikapata unafuu
Hali ilioko sasa hivi sina uwezo wa kunusa na ladha ya chakula imepotea kabisa
Hio ni Corona mkuu, moja ya dalili ya Corona ni kukosa uwezo wa kunusa na ladha ya chakula, tafadhali wahi anza kupiga nyungu (Majani ya mlimao, majani ya mpera, majani ya mchai chai, majani ya muembe).

Na tumia dawa ya kunywa (Chukua asali kwenye chupa ya Mil500, changanya na tangawizi ya kutwanga, pilipili manga ya unga kijiko kimoja, habasoda kijiko kimoja, mdalasini kijiko kimoja = changanya vizuri then iweke kwenye jua, halafu uwe unakunywa kijiko kimoja asubuhi kabla ya kupiga mswaki unakaa kama baada ya saa moja ndio unapiga mswaki then unakunywa chai. Halafu usiku kabla ya kulala unapiga kijiko kimoja).

Halafu wanya mazoezi sana ya kukimbia.

Na kama kuna watu unaishi nao, hawajaugua bado, basi na wao watumie pia, huwezi kujua lini na wao hali zitabadilika.

Mimi nimepoteza ndugu 5 kati ya 9 waliougua kwa gonjwa hili ndani ya siku 6 tu, na dalili zilianza kwa kukosa harufu ya kunusa, ladha ya chakula, mafua, kifua kwa mbali, mwili kuchoka haraka. Baada ya kujua hio dawa ya asali, waliobakia 4 imewasaidia na baadhi wameanza kupata harufu na kusikia ladha ya chakula na hali zao zimeanza kuimarika, mmoja ndio bado ana hali mbaya.

Tumia hizo dawa, utanishukuru baadae mkuu.
 
Pole sana ,Inasikitisha sana!
 
Habari za jumapili ndugu zangu na wikiendi kwa ujumla

Nije kwenye mada,

Nasumbuliwa na mafua wiki sasa mchana naweza nikashinda vizuri na nikaendelea na kazi zangu vizuri tu ila ikifika usiku wakati wa kulala Hali inabdalika Sana inatokea Hali mpaka pua moja inaziba napumua kwa shida Sana
Sasa kuna kipindi nilikuwa ikifika wakati wa kulala natafuna tangawizi basi Hali inakuwa shwari
Baadae nikanunua citrozen nikawa nakunywa ila hizi dawa sasa nikinywa asubuhi basi kutwa nzima mwili unakuwa hauna nguvu, mdomo unakuwa mchungu na njaa kali Sana nikaacha kuzitumia hizi dawa
Nimerudi kwenye matuminzi ya tangawizi na mazoezi kidogo basi usiku usingiz unakuwa mzuri
Duuuuh ya nini ospitali wakati dawa umeshaijua
 
Kula Mali mao fanya mazoezi. Sio kila mafua Ni korona hofu nayo unakusumbua.

Vaa barakoa usije ambukiza wenzako.

Mkuu yaani sisi watz ni kama mtoa mada mmoja alisema ni Certfied Fools ,yaani katika hali kamaa hii tuliyonayo dunia nzima na vyombo vya habari kila siku vinatoa tahadhari ya ugonjwa wa Uviko19 na jinsi ya kujilinda ,utakuta jitu lina mafua na kikohozi tele lipo ndani ya daladala halina barakoa wala kitambaa linapiga michafya tu na kukooa bila hata kujifunika...Mpaka unajiuliza huyu mtu brain inafanya kazi kweli? Hata kama yeye hajijali basi hajali wengine kwa kuvaa barakoa ili asiwarushie ma virus wenzake.
 
Back
Top Bottom