Nyamayao
JF-Expert Member
- Jan 22, 2009
- 6,966
- 2,352
wapo katika ndoa kwa miaka 4 sasa, wamejaaliwa baby gal, mume alikaa muda mrefu sana bila ya kazi coz kule alikokuwa anafanya alipata matatizo akafukuzwa kazi, kapelekwa shule kwa pesa ya mkewe, katafutiwa kazi nzuri na mkewe walikuwa na maisha mazuri/maelewano na kila jema, mume kaanza kubadilika, leo akirudi ni kumpiga mke, kesho ni kutafuta sababu ili mradi wagombane, mke kavumilia yote mpaka majuzi mume alivyomwambia" mama anakuja kutoka kijijini but samahani sana kukutaarifu kuwa anakuja na mke mwenzio kutoka kijijini nina twins nae wana mwezi 1, mama kaonelea waje tutambuzane coz nae ni mke wa ndoa kama ulivyo wewe"...wamekuja hapo ndani hapakaliki mama mkwe ni visa na vituko anasema yule mjukuu wa kwanza siowa mwanae bali wake ni hao twins wachangaa, maneno ya kejeli kutok kwa mama mkwe hana raha, imekuwa kero, rafiki yangu ni kulia kulia tu, anasema ana mpango wa kuwaacha hapo ndani akaanze maisha mapya, nilikosa ushauri wa kumpa.
tumsaidie jamani.
tumsaidie jamani.
Last edited: