Opera Min
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 901
- 657
"Kwa sasa Simba inaendelea na semina ya ueledi kwa wanachama wake kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka mfumo wa uanachama kwenda mfumo wa hisa"
Akifafanua kwa mifano amesema Simba iliyotimiza miaka 81 mwaka huu ina idadi ya wanachama wapatao zaidi ya Elfu Nane ambao wanatakiwa kulipa ada ya shilingi Shilingi Elfu Moja kwa Mwezi sawa na Shilingi Elfu kumi na mbili kwa mwaka lakini wengi wao hawalipi ada.Aliongeza kwa kusema hata kwenye klabu ya yanga,vyama vya Siasa hali ni hiyo hiyo wanachama ni wagumu kilipa ada
Akiongelea faida ya mfumo wa hisa amefafanua Simba itanufaika kwa mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50,ambapo Asilimia Tisa itarudishwa kwa wanachama hai,Asilimia Moja kwa waasisi wa klabu na Asilimia Arobaini itabaki klabuni kwa ajili ya uendeshaji wa timu.
Hata hivyo Alipingwa na kukosolewa vikali na bwana Issa Masoud mdau wa Simba na Mtaalam wa mambo ya fedha aliyebobea kwenye maswala ya hisa kwamba mfumo wa hisa ni mgumu kwa klabu kwani unahitaji kuibadilisha Simba iendeshwe kimfumo wa kampuni,Bwana Issa alisema kunahitajika juhudi ya kuwashirikisha wanachama wajadiliane na kukubaliana upi mfumo bora utumike kuiendesha klabu na sio kuwadikteti wanachama wakubali tu kuipeleka Simba kwenye mfumo ambao mbeleni unaweza ukaleta Matatizo makubwa.
Akijibu swali lililoulizwa na moja ya mtazamaji wa kipindi hicho "kwa nini kila mwaka Manara anajigamba kuchukua ubingwa lakini wanaangukia pua?" Manara alijibu kwa kumshutumu vikali aliyekuwa Rais wa TFF Jamali Mlinzi kuwadhulumu Ubingwa na kuwapangia Ratiba ngumu na Waamuzi wa hovyo kwa lengo la kuwakwamisha Simba.Malinzi kwa sasa yuko Rumande akishikiliwa kwa kesi ya Matumizi mabaya ya Ofisi.