Hajapewa talaka akamwoa!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Hebu tuchukulie kwamba, umeoa hivi karibuni, kama miezi sita tu iliyopita. Lakini unapokea taarifa za kuaminika kwamba, huyo mkeo ni mke wa mtu. Unaambiwa kwamba, aliolewa na kukorofishana na mumewe, lakini hawajaachana na ndoa yao ilifungwa Bomani kwa mujibu wa sheria za nchi.

Taarifa zenyewe zinaonekana ni za kuaminika kuhusu jambo hilo, ingawa hujaletewa taarifa rasmi.

Hebu niambie kama ni wewe ungechukua hatua gani?

Najua The Boss atakuja na swali hapa kwamba, Je, Mume mpya alikuwa anajua kuwa mkewe aliwahi kuolewa hapo nyuma?

Jibu ni kwamba, Alimweleza mumewe mpya kuwa aliwahi kuolewa na kuachika huko nyuma, lakini hakuweka wazi kuwa kuachana huko kulikuwa kwa kufuata taratibu au la, na mume mpya hakuwa mdadisi ili kujiridhisha, alichukulia powa tu akafunga ndoa, na maisha yakaendelea.

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
3,057
Points
1,500

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2009
3,057 1,500
Kwa kawaida kama kwenye ufungishaji wa ndoa serikalini, na ikiwa mwanamke aliwahi kuolewa, basi anatakiwa kuonyesha cheti cha ndoa.

Lakini hii huwa inatokea mara kwa mara, hata kigogo mmoja mheshimiwa mbunge wa kike aliwahi kuolewa na mume wa pili kwa sherehe kubwa lakini kumbe yule wa kwanza alikuwa hajatoa talaka.

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,240
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,240 2,000
Duh hiyo ndoa tayari ni batili! Ila muwage mnahakikisha wapendwa tena shukuru MUNGU huyo mume mwenza hakujakukuumbueni siku ya arusi
hakuna kitu kama ndoa batili
ndoa hasa ni maamuzi tu yenu wawili.....

hapo ndoa ni halali,isipokuwa legal procedures ndio batili,but ndoa ni halali..

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
hakuna kitu kama ndoa batili

ndoa hasa ni maamuzi tu yenu wawili.....

hapo ndoa ni halali,isipokuwa legal procedures ndio batili,but ndoa ni halali..
ninaiita batili kwa kuwa mmoja wa wanandoa hawa hakuwa muwazi kwa mwenzake ama sivyo angemweleza ukweli kuwa hajapewa talaka kisha mwenzie akakubali na kukubaliana wafunge ndoa hivyo hivyo ndo tungeidefine kama halali kwao but the fact kuwa mume hakujua hilo bado ni batili kisheria hata kiwao!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
hawakufunga ndoa kanisani wala kwa mkuu wa wilaya...
ilikuwa birthday ya mandela.....
kabla ya sherehe za birthday waliita ndugu na famillia na kufanya sherehe za kimila
na kujitangaza ni mke na mume.....
Kumbe! Hili nilikuwa silifahamu............

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
ninaiita batili kwa kuwa mmoja wa wanandoa hawa hakuwa muwazi kwa mwenzake ama sivyo angemweleza ukweli kuwa hajapewa talaka kisha mwenzie akakubali na kukubaliana wafunge ndoa hivyo hivyo ndo tungeidefine kama halali kwao but the fact kuwa mume hakujua hilo bado ni batili kisheria hata kiwao!
Unadhani huyo mume anatakiwa kuchukua hatua gani?

emrema

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
268
Points
0

emrema

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
268 0
Ndoa sio sheria wala kingine ni MOYO. Hapa hata kanisa linatatizika sana na kusababisha waumini wamkosee mungu kwa kwaombea wenzi wao wafe ili wajitoe. Waislamu walliona hili sawa kabisa kwa kuruhusu talaka.

Nasema hivi kama mioyo ya wawili hawa ipo tayari kuwa pamoja NDOA tayari, mengine ni maadhimisho tu.

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
Unadhani huyo mume anatakiwa kuchukua hatua gani?
mume yupi sasa?! Wa kwanza ana haki ya kushtaki kisheria na akalipwa fidia

Wa pili kama wana mapenzi ya kweli washughulikie talaka (wakiwakilisha uthibitisho wa ndoa ya kwanza kutokuwepo) kisha wabariki ndoa yao but si busara kuanza au kuendelea kuishi pamoja ilhali mke anahesabika kama mke wa mtu!

Wapate msaada wa kisheria

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
Ndoa sio sheria wala kingine ni MOYO. Hapa hata kanisa linatatizika sana na kusababisha waumini wamkosee mungu kwa kwaombea wenzi wao wafe ili wajitoe. Waislamu walliona hili sawa kabisa kwa kuruhusu talaka.

Nasema hivi kama mioyo ya wawili hawa ipo tayari kuwa pamoja NDOA tayari, mengine ni maadhimisho tu.
emrema umesema sawa bado talaka ni muhimu ili wawili hawa waishi hiyo NDOA yao bila kwayo bado ni wazinzi tu!

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,240
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,240 2,000
Ndoa sio sheria wala kingine ni MOYO. Hapa hata kanisa linatatizika sana na kusababisha waumini wamkosee mungu kwa kwaombea wenzi wao wafe ili wajitoe. Waislamu walliona hili sawa kabisa kwa kuruhusu talaka.

Nasema hivi kama mioyo ya wawili hawa ipo tayari kuwa pamoja NDOA tayari, mengine ni maadhimisho tu.
exactly
tena haya mambo ya kuzuia talaka
yanasababisha hata mauaji,wapo wanaume
wameshaua wake zao,ili wawe huru kuoa tena

First Born

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Messages
5,322
Points
1,250

First Born

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2011
5,322 1,250
sasa huyo mwanamke mbona ana tabia za uongo?
itafika mahali watagombana na huyo mzee mpya na kuja kuolewa na mwingine !!!!!!!!!!!!!!!!!!1

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,240
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,240 2,000
emrema umesema sawa bado talaka ni muhimu ili wawili hawa waishi hiyo NDOA yao bila kwayo bado ni wazinzi tu!
hakuna uzinzi hapo
nimetoa mfano wa mandela hapo juu

hivi wewe unajua vijijini hapa tanzania wengi hawafungi ndoa za dini wala serikali?

wanaiishi pamoja tu na kujitambulisha kwa watu kuwa ni mke na mume,basi

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Messages
10,476
Points
1,225

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined Jul 24, 2008
10,476 1,225
The Bosi hawa wawili hawako kijijini na ndio maana walifunga ndoa in the first place! Na mtoa mada ameileta hapa asaidiwe sio tumpuuze kwa habari za kufikirika! Hao wa kijijini wanarruhusiwa kumchukua mke wa mtu na kuishi naye tu kwa kuwa hakuna sheria wala kanisa?!

Tofautisha kuishi tu na mtu ambaye hakuwahi kumilikiwa kihalali whether through sheria za serikali, dini au traditions ambazo nazo pia zatambulika kama zitafuata taratibu zake

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,240
Points
2,000

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,240 2,000
The Bosi hawa wawili hawako kijijini na ndio maana walifunga ndoa in the first place! Na mtoa mada ameileta hapa asaidiwe sio tumpuuze kwa habari za kufikirika! Hao wa kijijini wanarruhusiwa kumchukua mke wa mtu na kuishi naye tu kwa kuwa hakuna sheria wala kanisa?!

Tofautisha kuishi tu na mtu ambaye hakuwahi kumilikiwa kihalali whether through sheria za serikali, dini au traditions ambazo nazo pia zatambulika kama zitafuata taratibu zake
ninachosema hapa ni hivi......
mwanamke alishasitisha ndoa yake zaidi ya miezi sita iliyopita
na sasa kaolewa tena.....hata kama legal procedures ni ndefu na kazikukamilika
huwezi kumuita muongo au mzinzi........
ndoa ya zamani imekufa na sasa kafunga ndoa mpya......ya halali na uwazi kwa kila mtu....

ndo maana waarabu,talaka ni maneno tu, mara tatu,na siku hizi hata sms tatu tu ni talaka tosha
hapa tatizo ni procedures za talaka, na sio uzinzi au uwongo

Forum statistics

Threads 1,352,855
Members 518,197
Posts 33,068,020
Top