Haipendezi, sherehe haina vileo

Haipendezi, sherehe haina vileo

ubuntuX

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
1,998
Reaction score
2,242
Nimepata kuhudhuria sherehe ya harusi ya jamaa yangu, licha ya kutoa mchango na kujitoa kwangu kote huko lakini sherehe haina bia wala k vant!

Kiukweli party ya harusi bila bia ni hamna kitu
Hii nimeifuatilia nijue sababu za msingi eti ni uislam unakataza, kama ni hivyo mnachangisha na kufanya sherehe usiku za nini?

Harusi na soda aifai kabisa, walau ata malta juisi lakini zote amna!

Hizi michango yetu mmepeleka wapi?
 
Kuna watu wanakusanya michango ya harusi na kuifanya mitaji ya kuanzia biashara na maisha. Unashangaa kamatim uchwara inajitutumua kuwa kima cha chini laki moja halafu mwisho wa siku mnanyweshwa soda kama watoto wa kipaimara.
 
Kwa hiyo unachanga pesa ili upewe bia?
 
Hizo mbona nzuri tu, cha msingi unaenda na chupa zako -Kvant, konyagi, Grants... wale wa dompo... Hata Jack Daniels zinaruhusiwa.
 
Kuna watu wanakusanya michango ya harusi na kuifanya mitaji ya kuanzia biashara na maisha. Unashangaa kamatim uchwara inajitutumua kuwa kima cha chini laki moja halafu mwisho wa siku mnanyweshwa soda kama watoto wa kipaimara.
Kwani kuna ubaya gani pesa inayobaki akafanyia mtaji wa biashara?
 
Aiseee. Si unaweza kununua bia zako kadhaa na kuhudhuria nazo. Na kunywa unavyotaka
 
Nimecheka sanaa huyo kajiongeza sana mnaenda na vizawadi vidogo alafu mnakula sanaa na kadi moja una watu kama wanne hahahaaaa kabana matumizi yasiyo na tija na kuyaelekeza katika mambo ya msingi hahahaaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Pambana na hali yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hela haibaki, inalazimishwa kubaki. Kama mtu anataka mtaji wa biashara aende NMB, CRDB, NBC au FINCA😛😛
Kwani unalazimishwa kuchangia shughuli?

Au roho ya kwanini inakusumbua?

Nyie ndo wale mkiona wenzenu wanatunzwa mahela kwenye sherehe roho zinawauma.
 
Hizo mbona nzuri tu, cha msingi unaenda na chupa zako -Kvant, konyagi, Grants... wale wa dompo... Hata Jack Daniels zinaruhusiwa.

Aiseee. Si unaweza kununua bia zako kadhaa na kuhudhuria nazo. Na kunywa unavyotaka
Sio kwamba hawana mpunga wa kuweka hivyo vinywaji ila kuna famila zingine swala la pombe ni marufuku sasa unapojinunulia uwende nazo unakuwa umewakosea.

-Ndumilakuwili-
 
Aisee dunia bhana, cha kushangaza wewe umetoka unanung'unika ila kuna mwingine (asiyetumia vileo) anaisifia kwelikweli hiyo hiyo sherehe.
 
Hizo mbona nzuri tu, cha msingi unaenda na chupa zako -Kvant, konyagi, Grants... wale wa dompo... Hata Jack Daniels zinaruhusiwa.
Kwenye sherehe za kiislam za ukumbini hata kuingia na Wine au pombe nyingine ukumbini hawaruhusu kabisa....na unakuta ni harusi ya usiku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom