JICHO LA TATU
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 306
- 49
Habari zenu wajameni nina kaka yangu sasa yeye ana tatizo linamsumbua,Yeye alikuwa na uhusiano na binti mmoja wa kiarabu na akazaa naye mtoto wa kike ingawa katika mahusiano yao wao walipendana isipokuwa upande wa wazazi wa huyo binti wa kiarabu hawakua tayari kaka aishi na yule binti yaani kumuoa, kilichokuwa kinapingana ni utofauti wa dini.Sasa leo amepata habari kwamba binti katafutiwa mchumba na wazazi wake ambaye ni Mwarabu mwenzake hivyo anaolewa siku yoyote ndani ya wiki ijayo. Sasa hajui atafanya binti mwenyewe amechanganyikiwa c'z anampenda bro. Wote wawili hawaelewi wafanye nini tafadhali naombeni mawazo yenu katika hili.