Hadithi ya zawadi Teaser

Hadithi ya zawadi Teaser

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,475
Hey guys...

Well, kwa wale wapenzi mliokuwa mkiikubali hadithi ya zawadi napenda kuwataarifu kwamba karibu inaisha na hii ni sehemu ya muendelezo wake. Kwa ambao hamkuwahi kusoma mwanzo angalieni kwenye link https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/163697-zawadi.html

Saa tano, saa sita mpaka saa saba mwl. Samea hakuonekana. Binafsi sikuwa na wasiwasi wowote juu ya usalama wake kwasababu nilishazoea tabia yake ya kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine hata kulala nje. Nilijikuta nimelazimika kozea tabia zake zililokuwa zikinikwaza sana ili nipunguze kukereka nae mara kwa mara. Mwanzo nilichukizwa sana na vituko alivyokuwa akinifanyia na nilishindwa kabisa kuzuia hisia zangu mbele yake ila kadiri muda ulivyoenda nilijifunza taratibu. Japokuwa Wakati mwingine nilishindwa kuelewa mwanaume yule alikuwa akinichukulia vipi ama alisukumwa na chuki ya aina gani kunifanyia aliyokuwa akiyafanya bila huruma ila nilijifunza na kubobea kuwa sugu mbele yake. Alipochelewa kurudi nyumbani sikumuuliza alipotoka, aliponitolea maneno ya dharau na kejeli sikumjibu wala kulia, sana sana nilimtizama tu na kuendelea na kile nilichokuwa nikikifanya awali. "Bila shaka sasa hivi yuko mahali anafurahia hela zake na marafiki zake. Hmmmmm, ama kweli Zawadi nimepatikana." niliwaza huku nikitafuta mbu aliyekuwa akimzunguka mwanangu ili nimpige na nguo.

Mwanangu ndie aliyenipa faraja na furaha moyoni, kuna wakati niliamini Mwenyezi Mungu alinipa mtoto wa aina ile mwenye akili kuzidi umri wake , mjanja, mtundu na mwenye huruma na upendo uliotukuka juu yangu kwa makusudi ali awe mfariji wangu mkuu kwakuwa alijua uhitaji wangu kabla hata sijafika nilipokuwa nimefika kwa wakati ule. Isingekuwa Raheem hakika ningeshakumbwa na msongo wa mawazo na kuishia kufa kwa huzuni nisipate wa kuniokoa.

Finally saa nane na dakika tatu zilisikika hatua zikielekea kwenye dirisha la chumbani kisha mwl akaanza kuita "Zawadi, Zawadi! Nifungulie. Fanya haraka!" akaita na kuamrisha bila kutoa nafasi ya kujibiwa. Niliinuka kitandani haraka haraka na kuwahi mlangoni kuepuka kelele zaidi ili majirani wasije wakasikia, pia sikutaka amuamshe mtoto usiku ule mkali.Kwa namna ambayo nilikuwa nikijisikia wakati ule, nilishindwa kujua nimpokee kwa neno gani 'mume wangu kipenzi' kutoka kwenye vikao vyake vya ubia na Bar alipopendelea kuwekeza hela yake kila kukicha. Kati ya 'Habari, pole ama karibu' , hamna neno lililoweza kunitoka kwa urahisi hivyo nikasimama kimya pembeni ya mlango nikimsubiria mwl aingie ndani, kisha nikafunga mlango bila ya kusema neno.
"Mbona taa inawaka muda huu?!" aliuliza mwl bila ya salamu. "Mbu. Dawa imeisha hivyo nilikuwa naangalia mbu wasije wakamng'ata mtoto maana ni wengi sana." nilijibu swali lake japo niliona halina mashiko kwangu huku nikiwaza ni namna gani nitaweza kuondokana na aina ya maisha niliyokuwa nikiishi kwa wakati ule.

"Mbona hujapika?! Ina maana mmekula kiporo tu leo?!" mwl aliuliza akiwa jikoni baada ya kubadili nguo na kukorofishana na sufuria ."Ehhhh" nilimjibu kwa mkato. "Kwanini?!" , swali la mwl lilinikasirisha lakini nilijitahidi kutokuonyesha hisia zangu kisha nikamjbu kwa kumuuliza "kwani ulitaka kipikwe kitu gani?!Tunakula kile ambacho kipo." "Hela zako unazunguka nazo mfukoni tangu juzi huachi hata senti tano kazi kukesha bar alafu unakuja kuuliza habari ya chakula saa nane usiku ilhal hujui kwamba hata mafuta ya kupikia hamna." " Kama nilijua vile" alijisemea mwl na kukatisha nilichokuwa nawaza huku akichukua begi lake la laptop alilokuwa ameegemeza ukutani na kutoa kifurushi cha chips na mishkaki. "Dah!Poleni sana. Heri mimi naweza kula kuku, hahahah. Alafu, mama yangu anakuja kesho kutwa." maneno ya mwl. yaliambatana na kicheko cha kejeli wakati akielekea sebuleni na kifurushi chake. Owwkey" nilijisemea kichwani bila ya kumjibu mwl chochote maana nilijua fika alikuwa akijaribu kunichokoza ili niongee neno na kusababisha mvurugano usiku ule.

"Mamii, mamii, aomba nyonyo" aliita mwanangu Raheem akiwa nusu usingizini huku akijisogeza kuwa karibu nami. Nikamvuta karibu na kumlaza kwenye mkono wangu wa kulia, mwanangu akapata alichokuwa akihitaji na kurudi kulala. Mimi nikafunga macho na kusali huku nikitamani usingizi unipitie lakini haikuwa bahati yangu. Yaani sikuweza kulala mpaka mishale ya saa tisa na nusu baada ya kutoonyesha kuvutiwa na maongezi ya mwl aliyokuwa akitaka kuanzisha huku akijifanya ni mwanaume aliyejaa upendo tele juu yangu. Mwisho akakasirika na kuanza kujiongelesha maneno ambayo niliamua kuyapuuza kuepuka shari na mwishowe akajilalia zake bila mafanikio ya kunifanya nianzishe malumbano.


Siku mbili za amani, wiki nzima iliyojaa vituk,hivyo ndivyo maisha yetu yalivyokuwa. Ni kama mwalimu alikuwa akichukia kuniona nina amani na furaha yake ilitokana na kusononeka kwangu maana wakati mwingine alijaribu kwa hali na mali kuniudhi. Hata nilipojitahidi kutokumridhisha kwa kuniona na huzuni bado hakuacha kujaribu, alikuwa anakusudia kweli kweli. Wakati mwingine niliona kabisa kwamba alikuwa akinichukia kutoka moyoni, upendo alionionyesha pindi alipojisikia kufanya hivyo niliona ni wa kuigiza ama kujilazimisha. Sana sana alikuwa mzuri kwangu pale alipotaka tendo la ndoa, na hilo kwake halikuhitaji mjadala kamwe. Hata kama nilikuwa ni mgonjwa ama nimechoka kiasi gani, hakuwa tayari kuelewa na kulazimisha kwangu isiwe kulileta ugomvi kati yetu mara kwa mara, ugomvi ambao ulizua maneno ya kejeli, dharau na masimango. Siku moja alidirika hata kuniambia maumbile yangu hayakuwa na mvuto tena kwake kwasababu yamebadilika na kuwa mapana sana baada ya kupata alichokitaka. Uzuri sikutilia maneno yake maanani kwasababu nilijua alikuwa akijaribu kunikera baada ya kutimiza haja yake hivyo sikumjibu chochote.

Taratibu alianza kunitoka moyoni. Sikujali alipochelewa wala alipolala nje. Uwepo wako ulinikosesha amani na furaha muda mwingi maana hakuwa akiniacha nipumue hata kidogo.


Siku ambayo sitoisahau maishani mwangu ni siku moja ya ijumaa, siku ambayo mwl alinieleza kwamba kesho yake kungekuwa na kikao hivyo angeomba nisiende popote. Nilipohoji kilihusiana na nini hakuona tabu kunijulisha, "kuna watu watakuja hapa, mashekhe, ili tumalizane na huu ugomvi. Nimeamua kwamba nataka tuachane na wao watakuwa mashahidi nikikupa talaka, nilitaka hata mama yako awepo ila nimempigia sana simu hapatikani." Moyoni nilijisemea "ahhh na iwe tu." kisha nikamjibu "Owwkey. Ila hayo maswala ya kukalishana vikao unajua ni namna gani sipendi, we kama umeshafanya maamuzi yako wala sipingani na wewe. Lakini hayo maswala ya vikao ningeshukuru kama yasingekuwepo"
Hakuongeza neno, akaenda kuoga kisha akala. Alipoingia chumbani alinikuta nimeshapanda kitandani tayari. Akaanza kuniuliza kuhusu sh. 25,000 niliyokuwa nimemuomba miezi miwili nyuma kwaajili ya kumtumia bibi yangu aliyekuwa mgonjwa huku nikimuahidi kuirudisha mama atakapopata maana ndie aliyenituma kumuomba mwalimu. Baada ya kumjibu kwamba angepata siku chache mbele alianza kuongea na kulalamika kwamba aliitaka hela yake kwa wakati ule na sio baadae, kesho wala kesho kutwa. Kuepusha shari nilimwambia mimi nalala na kama nae anaweza ni vizuri akalala tukaendelea na maongezi siku iliyofuata.

Lahaula, maoni yangu yalikuwa kama mafuta ya taa ama petrol juu ya moto maana aliacha nguo alizokuwa akipanga na kunifata nilipokuwa nimelala.
"Unasema nini wewe?! Mi naulizia hela yangu unaniambia habari ya kulala?Hela niliyoitolea jasho mwenyewe!Pumbavu!!!" alifoka huku akinipiga vibao kwenye shavu langu la kulia. Nikajaribu kuzuia machozi yasinitoke huku nikifunika shavu langu kwa mikono. Akanishika mikono yote miwili pamoja kwa mkono wake mmoja na kunipiga kwa mwingine. Kama bado hiyo haikutosha akanikaba shingoni na kuendelea wakati huo huo akigomba, "Nitakupiga mpaka niipate hiyo hela. Sikuachi mpaka niipate nakwambia." Machozi yalinitiririka kama maji ya uvuguvugu juu ya uso wangu, moyo uliniuma kuliko ambavyo niliwahi kuumia maishani mwangu lakini nilijizuia nisipambane nae kwa matumaini kwamba angeniacha baada ya kuona sipambani nae lakini haikuwa hivyo. Hata nilipomuomba aache kunipiga hakuacha wala kuguswa na kilio changu, ndio kwanza aliongeza nguvu kana kwamba alikuwa akimpiga kibaka aliyemkwapulia simu Posta ama Kariakoo. Alinipiga tena na tena bila kujali chochote kisha akaniamuru nimpigie mama yangu simu usiku ule na kumwambia kuhusu kurudisha zile fedha tulizoazima, nilipokataa kutii amri yake na kumjibu kwamba ningefanya hivyo kesho yake alinipiga tena. Mara hii alitumia mkono mmoja kunikandamiza pembeni kidogo ya nyonga na kunisababishia maumivu makali huku akinipiga vibao kwa mkono mwingine.
Nilipoamua kutoa simu yangu chini ya mto nilipokuwa nimeiweka pindi nataka kulala ndipo aliponiachia. Nikainuka kitandani huku nikitetemeka kwa hasira na uso ukiwa umeanza kunivimba kwa kasi.


kisukari Yericko Nyerere Jestina Ngwanakilala Avemaria Masanilo Matola First Born Shantel One and Only Change_it Tonny Elia Rejao Ninaweza Maketa Che Kalizozele ibraton lutamyo samito mbongopopo vngenge Blaki Womani LOOOK lodikasaji zamboni ndyoko Mamaya mtoto wa mfugaj BlackBerry MwanajamiiOne King'asti klorokwini Dio Al-Mende Gagurito Tusker Bariiiidi Pasco VoiceOfReason Kanigini kasopa WomanOfSubstance FirstLady1 divalicious bryleen Kweli Husninyo Bayo Matope MESTOD na wengine woooote ambao nimeshindwa kuwa-tag, MKO TAYARI KUNUNUA KITABU AU NIWEKE MAKARATASI YANGU CHINI YA GODORO???!
 
Last edited by a moderator:
Dah mama mchungaji ulitukomeshajeeee!!!

Watu tulikuwa tushaizoea mara huyooo ukadisappear! Hope hujambo
 
Yaani wewe wifi wewe! Basi tu wewe ni familia. Ndio sijui ukatufanyaje sasa? Hebu leta kitabu, kwenye library yangu nina section ya swahili books. Mwanakijiji, Fadhili Mtanga, Nyambari Angwine na wengineo. Nitafurahi kukuongeza
 
Dah mama mchungaji ulitukomeshajeeee!!!

Watu tulikuwa tushaizoea mara huyooo ukadisappear! Hope hujambo

Niliona fursa kipenzi Avemaria , si unajua tena mjini hatuishi kwa mawe. Andaa vihela kidunchuu tu kwaajili ya kupata uhondo kamili.
 
Last edited by a moderator:
Yaani wewe wifi wewe! Basi tu wewe ni familia. Ndio sijui ukatufanyaje sasa? Hebu leta kitabu, kwenye library yangu nina section ya swahili books. Mwanakijiji, Fadhili Mtanga, Nyambari Angwine na wengineo. Nitafurahi kukuongeza

Inabidi unisamehe tu wifi, siunajua tena wakati mwingine mambo yanaingiliana hata kaka yako anashindwa kurekebisha!!Heheheh

Ngoja nifanye niongezeke hapo kwenye shelf maana ni kama umeniongezea fuel na MESTOD kaniongezea speed. Asanteni, endeleeni kunipa moyo bana nikamilishe fasta.
 
Last edited by a moderator:
Niliona fursa kipenzi Avemaria , si unajua tena mjini hatuishi kwa mawe. Andaa vihela kidunchuu tu kwaajili ya kupata uhondo kamili.

Dah haya bhana. Hongera sana!

Nini shida mama, ntavunjia kibubu kwa Zawadi so we mlete tu.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
oooh@Lizzy asante sana sikujua kama watu mnakuwa na vipaji mbalimbali
 
Hadithi za humu zinanikomesha kitu kimoja, inaanza inanoga hafu inapotea kabla haijaisha. Bora ulete tu kitabu mama.
 
Bonge la hadithi ambayo ukiisoma hata mara ya kwanza lazima usisimke asante sana Lizzy
 
Back
Top Bottom