Hadithi ya umslopagaas

Itakuwa ni kichaga mkuu..
teh teh teh teh.
 
Naaam, taratiibu naitafuna
 
Nipo nayo bado,sipo nyuma hata kidogo
 
SURA YA KUMI


Mbele, mbele tukaendelea mbio sana, tunavutwa na mkondo wenye nguvu hata halafu nilisikia sauti ya maji imepungua sana, nikafahamu ni kwa sababu iko nafasi zaidi na sauti imeenea.

Basi, nilijiinua pole pole na kwa uangalifu sana mpaka nikafanikiwa kupiga magoti, nikaunyosha mkono wangu juu, nisiweze kugusa kitu. Kisha, nilitwaa kafi nikaiinua juu, nisiguse kitu.

Tena, nililipeleka upande wa kuume na wa kushoto, lakini sikuweza kugusa kitu ila maji tu. Ndipo nilipokumbuka ya kuwa ipo taa na debe la mafuta katika mtumbwi, nikapapasa papasa huku na huko mpaka nikavipata, nikawasha kiberiti kwa uangalifu, nikaiwasha taa.

Nikatazama, nikamwona Bwana Good amelala chali anatazama juu tu, na Sir Henry amekiegemeza kichwa chake ubavuni mwa mtumbwi, na mkono wake umo majini akijaribu kuupima mwendo wa maji.


Lakini mwangaza ulipomwangazia Umslopogaas nilitaka kucheka. Nilisahau kusema ya kuwa tulichukua pande la nyama iliyopikwa, basi , tulipojitupa chini katika mtumbwi tusipigwe na mwamba wa juu, kichwa cha Umslopogaas kilifika karibu na ile nyama, na mara alipoizoea hali yetu aliona njaa.


Basi, hapo alilitwaa shoka lake akakata kipande cha nyama, na sasa anaila kwa raha. Alieleza baadaye, ya kuwa, katika kwenda safari ndefu, hupenda kushiba kwanza!

Wenzangu walipoona nimeiwasha taa, tulianza kufanya shauri juu ya hali zetu kadiri tulivyoweza.

Kwanza kwa shauri la Bwana Good tulizifunga kafi mbili pamoja, tukazisimamisha ka mlingoti katika omo la mtumbwi ili tupate habari mara ile ikiwa mwamba wa juu kama sehemu nyingi ni fupi kwa kimo tusije tukajigonga.

Ilikuwa dhahiri ya kuwa tumo katika mto unaopita chini ya ardhi unaochukua maji ya ziwa yanapozidi.

Mito ya namna hiyo ipo katika nchi nyingi, lakini nadhani wasafiri wachache wamepata bahati mbaya ya kusafiri ndani yake.


Kwa mwangaza wa taa yetu tuliweza kufahamu ya kuwa mto ni mpana, maana nuru ya taa haikuweza kufika mpaka mwisho wa kando zake.

Mara kwa mara mkondo wa maji ulituchukua karibu na ng’ambo hii au hii, tukaona ni mwamba ambao, kadiri tulivyoweza kuona, unafanya namna ya tao kiasi cha futi ishirini na tano ju yetu.

Ingawa mwamba ulikuwa juu hivyo, tuliona ni afandali tuweke mtu mmoja mbele katika mtumbwi ashike zamu, ana taa na podo tayari kuzia mtumbwi usisetwe kando ya mto, wala kupigwa na mwamba ukiwa mmoja unatokeza mahali.


Kwa kuwa Umslopogaas tayari amekula, yeye alishika zamu ya kwanza, hapo tulikula nyama kidogo tu, maana hatujui chakula chetu kitachukua muda gani.

Ndipo tulipochangamka kidogo, nikatoa shauri langu ya kuwa hali yetu si hali ya kukata tamaa kabisa, ila labda mto huu utoweke kabisa katikati ya dunia, kama walivyosema wale wenyeji.

Kama hautoweki, basi lazima utatokea mahali, labda upande wa pili wa milima, na kama ni hivyo, basi hatuna budi kujiokoa maisha yetu mpaka tufike huko.

Lakini Bwana Good alisema labda tutapatikana na hatari na vitisho vingi sana au labda mto huu utatambaa chini ya ardhi mpaka ukauke, na kama ni hivyo, basi ajali yetu itakuwa mbaya kabisa.


Basi, Sir Henry, ambaye siku zote ni mchangamshi, na kwa kweli yu kama nguzo yenye nguvu wakati wa shida, akasema, ‘’Basi, imetupasa tuamini kuwa mambo yatatokea vizuri, au kujitengeneza tuwe tayari ikiwa yatatokea vibaya.


Tumetoka katika shida nyingi pamoja, nami nadhani tutatoka katika shida hii pia.
Ilikuwa karibu saa sita tulipovutiwa chini ya ardhi, na mtu wa zamu ya kwanza aliwekwa saa nane, tukapatana ya kuwa kila zamu itakuwa kwa muda wa saa tano.

Umslopogaas na Bwana Good walishika zamu ya kwanza. Basi, ilipofika saa moja ya usiku, Sir Henry na mimi tulishika zamu, na wale wawili wengine walilala.

Kwa muda wa saa tatu mambo yalikwenda vizuri ndipo nilipoanza kuona joto linazidi. Kwanza sikufikiri neno lakini baada ya kupita nusu saa tena niliona joto linazidi sana, nikamwita Sir Henry, nikamuuliza kama na yeye anaona joto, au kama ni mimi tu ninayeona hivyo. Akajibu, ‘’Ndiyo, jasho linanitoka kwa wingi sana.’’
 
Basi, hapa wenzetu waliamka wanatweta kwa joto, tukaona ni lazima tuzivue nguo zetu, isipokuwa Umslopogaas aliyekuwa amevaa ngozi.


Joto likazidi mno, na jasho lilitutoka kama maji yanavyo miminika. Baada ya kupita nusu saa tena, ingawa tulikuwa tupu, tuliona shida kuvumilia joto kwa jinsi lilivyozidi.


Nikauchovya mkono wangu majini, nikautoa haraka, nikataka kupiga kelele, maana maji yalikuwa moto sana, karibu kuchemka.

Sir Henry akasema kuwa, labda tunapita juu ya mahali penye moto wa volcano chini yake, nami nadhani alisema kweli na hasa kwa sababu ya mambo yaliyotokea baadaye.


Sasa taabu yetu ilizidi hata nashindwa kuieleza, maana hatukutoka jasho tena kwa sababu jasho lote limekwisha kututoka, na sasa tumelala tu chini mtumbwini, tukauacha uchukuliwe na maji tukajiona kama kwamba tu makaa ya moto.


Ngozi yetu ilianza kupasuka, na damu ilipigana katika mishipa ya vichwa vyetu. Basi, mambo yaliendelea hivyo hivyo kwa muda, ndipo mto ulipopinda kidogo, nikamsikia Sir Henry anatoa sauti ya kushtuka, nikatazama mbele nikaona jambo la ajabu na la kufadhaisha kabisa.


Kadiri ya nusu ya maili mbele yetu, na kwa upande wa kushoto wa katikati ya mto, tuliona nguzo ya moto mweupe unabubujika katika mto na kupanda juu kadiri ya futi hamsini, ulikuwa ukiupiga mwamba wa juu na kutawanyika mpaka kuwa mkubwa sana, kadiri ya futi arobaini kuuzunguka, kisha ukarudishwa chini kama matao.


Nguzo hii ya moto ilionekana kama kwamba ni ua kubwa ajabu la moto linalotoa katika maji meusi ya mto.

Chini, nguzo ilifanana na kikonyo cha ua, kimenyoka vizuri, na unene wake ulipata futi moja au zaidi na matao ya juu yake yalifanana na majani ya ua kubwa la moto. Nani anayeweza kueleza jinsi lilivyokuwa zuri na lakutisha! Hakika mimi siwezi.


Ingawa tuko mbali kadiri ya yadi mia tano, moto huo uliliangaza pango zima kama kwamba ni mchana. Basi, tulipelekwa mbele kasi kuiendea nguzo hiyo ya moto, na moto ulimeka kwa ukali kuliko tanuru yoyote iliyowashwa na mwanadamu.


Sir Henry akalia, ‘’Peleka mtumbwi kuume, Quatermain… kuume!’’ na mara ile nilimwona ameanguka chini katika mtumbwi amezirai. Bwana Good naye alizirai pia. Walilala wale kama kwamba wamekwisha kufa.


Umslopogaas na mimi tu ndiyo tuliokuwa na fahamu zetu. Sasa tulikaribia zaidi, kadiri ya yadi hamsini tu, nikaona kichwa cha Yule Mzulu kinainamia mbele katika mikono yake. Yeye naye amekwisha zirai, na mimi nimebaki peke yangu.


Sikuweza kuvuta pumzi moto mkali ulikuwa umenikausha kabisa. Mwamba wote uliozunguka mto, pale moto ulipokuwapo, ulikuwa unameka wekundu na mti wa mtumbwi wetu ukataka kuungua.


Nikaona manyoya ya bata mmoja katika wale tuliowaua yanasinyaa na kuungua lakini sikukubali kushindwa.

Nilijua ya kuwa mimi nikishindwa, basi tutakuwa tumekwisha, maana tutapita katika mwendo wa yadi tatu au nne wa moto ule na kuangamia kwa maumivu makali kabisa.


Basi, nilitia kafi majini ili kuupinda mtumbwi wetu upite mbali na moto kadiri nilivyoweza, nikaizuia kwa nguvu. Macho yangu yalikuwa kama yanatoka kichwani, na ingawa niliyafumba, niliweza kuuona mwangaza mkali wa moto.


Sasa tulikuwa karibu kuukabili; ulinguruma kama moto wa jehanamu, na maji yaliyozunguka yalikuwa yanachemka kwa hasira sana.


Nukta tano zaidi zilipita. Basi, tumeupita nikasikia muungurumo wake nyuma yangu.
Ndipo na mimi pia nilipoanguka chini mtumbwini, nimezirai.

Nilipopata akili zangu tena, niliona upepo unaupepea uso wangu. Nikayafumbua macho yangu kwa shida, nikatazama juu.

Juu, juu sana, niliona mwangaza, ingawa giza lilinizunguka pande zote. Ndipo nilipopata fahamu, nikatazama.

Mtumbwi ungali unaelea katika mto, na katika mtumbwi, chini, wenzangu wamelala tupu. Nikawaza, ‘’Je, wamekwisha kufa nini? Je, niko peke yangu katika mahali hapa pa kutisha’’ Sikujua.

Ndipo nilipoanza kuona kiu imenishika. Niliuchovya mkono wangu majini, nikauvutia ndani tena kwa haraka sana na huku ninalia. Maana karibu ngozi yote ilikuwa.

Imebabuka. Lakini maji yalikuwa baridi sana, badaye nikayatwa nikanywa sana, nikajimiminia maji.

Mwili wangu ulikuwa kama kwamba unapapa maji kama kiambaza kinavyopapa mvua baada ya wakati wa jua kali lakini pale nilipoungua palinichoma mno.

Ndipo nilipowakumbuka wenzangu, nikajivuta karibu nao kwa shida nyingi, nikawanyunyuzia maji, nikafurahi sana, maana walianza kuamka kwanza Umslopogaas, halafu na wale wengine.

Kisha, na wao walikunywa maji mengi. Sasa walianza kuona baridi kinyume kabisa cha hali yetu ya karibuni tukaanza kuvaa kadiri tulivyoweza, maana tulikuwa tumeungua sana.


Tulipokuwa tukifanya hivyo, Bwana Good alionyesha namna ubavu wa kushoto wa mtumbwi ulivyoungua kwa moto.

Moto ule wa kutisha ulikuwa nini sijabata kujua, lakini nadhani haukosi uko ufa ardhini chini ya mto, na moto ule unatoka katikati ya dunia.

Mara tulipovaa nguo na kupata nguvu kidogo, tulianza kujaribu kutambua tuko wapi sasa. Nilisema ya kuwa niliweza kuona mwangaza kwa juu sana, na tulipoutazama, tulitambua kuwa ni mbingu.

tukatambua ya kuwa mto ulikuwa chini ya ardhi, na sasa umetokea tena, nao unapita katikati ya magenge marefu kadiri ya futi elfu mbili kwenda juu.

Juu sana tuliona mbingu ni nyeupe, lakini hapo tulipo ni nusu giza, kama katika chumba kilichofungwa milango na madirisha wakati wa mchana.
 
Naam mkuu shukran
 
Mkuu sura ya saba umeruka
 
Aisee, hatari sana
 
Shukurani mkuu
 
 
Daah, salute sana kwa Sir Henry, anaandika aisee uyu mzee.

Azidi kupumzika kwa amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…