Hadithi ya Uchawi wa Mama mkwe by Dr. Wansegamila

Hadithi ya Uchawi wa Mama mkwe by Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,995
Reaction score
8,273
LIPOISHIA
Baada ya dakika kama kumi hivi mimi nikiwa bado chini nimelala kwenye kapeti, mchawi yule nilimsikia akikoroma.

Nilishangaa sana mchawi kuja kwenye chumba cha watu na kuanza kukoroma kama vile alikuwa kwake. Mawazo yangu yakaenda kwa mume wangu kwamba amepelekwa wapi?
SONGA NAYO

Nilijaribu kuinuka pale nilipokuwa nimelazwa, nikashindwa. Na yule mchawi aliyeachwa anilinde akawa anaendelea kukoroma juu ya kitanda chetu.

Dakika kumi baadaye nilisikia kishindo nje ya nyumba. Nilijua kuwa lile kundi la wachawi walioondoka na mama mkwe wangu lilikuwa linarudi.

Moyo ulinienda mbio mithili ya mtu aliyemaliza kukimbia mbio fupi za mita mia moja. Niliona mlango wa chumba chetu ukifunguliwa.

Niliminya macho kujifanya nimelala fofofo.
Lakini niliyaachia kidogo ili kuona kama mume wangu amerudishwa au amekwenda kuliwa nyama na wachawi wale.

Nilifarijika baada ya kuona kundi lile la watu hao wabaya wakiwa wamembeba kama walivyokuwa wameondoka naye.

Walipomfikisha kitandani walishangaa kukuta mwenzao waliyemuacha akikoroma.
"Huyu mjinga kweli kweli. Tulimuacha amlinde mke wa baba Ajigale yeye akaamua kulala," alisema mama mkwe wangu.

"Muamshe. Muamshe kwa kumchapa na mkia wa taa," aliamuru mtu ambaye sikumjua kwa jina.
Mchawi mwingine alichukua mkia wa taa na kumchapa yule mchawi aliyekuwa akikoroma kwenye kitanda chetu. Hakushituka na wote mle ndani wakashituka.

"Huyu inawezekana alikuwa akimfukizia moshi huyu mke wa baba Ajigale ili asizinduke na matokeo yake naye fukizo limemkolea." "Ni kweli kabisa. Lete ugoro," alisema yule kiongozi wa wachawi.
Nilisikia kifuniko kikifunguliwa na baadaye alinusishwa yule mchawi aliyekuwa akikoroma.
"Chaa, chaa, chaa," alipiga chafya.

Baadaye aliketi kitandani na kuulizwa kulikoni alilala kitandani wakati aliachiwa kazi ya kunilinda!
"Huyu mama Ajigale alitaka kuzinduka. Nikaamua kuchukua dawa ya mafusho nikawa namfukizia moshi. Nilisahahu kujifunga kitambaa chenye dawa ya kuzuia mimi kuleweshwa, nikalewa.

Ndivyo ilivyokuwa," alijitetea.
"Lakini huyu mama Ajigale hakujua lolote?"
"Hakujua, nilipoona anajitingisha tu, nikamuwahi na mafusho."
"Umefanya kazi nzuri," alisifiwa.

Baadaye walimtoa pale kitandani na kumlaza mume wangu. Baada ya hapo walininyanyua pale chini ya zulia jekundu chumbani kwetu na kunilaza kando ya mume wangu.

Sikuthubutu kuonesha kuwa najitambua badala yake nilijitahidi kujilegeza kana kwamba nilipoteza fahamu kabisa.
"Isije ikawa ule moshi wa mafusho ulizidi. Tunaweza kumuacha akapata fahamu kesho saa tisa mchana, tutakuwa tumefanya kitu kibaya sana," mmoja wa wachawi alishauri.

Yule mkubwa wao akasema ni vema na mimi ninusishwe ugoro na kazi hiyo akapewa mama mkwe wangu kwa kuwa analala nyumba hiyo hiyo tofauti ni vyumba tu.

Walikubaliana. Kilifunguliwa kichupa chenye ugoro na kupewa mama mkwe.
"Sisi tunatoka. Utamnusisha mkweo baadaye na akianza kupiga chafya tu, toka atazinduka kivyake vyake," alisema yule mtu ambaye mimi namuita ni kiongozi wa wachawi.
"Sawa," akaitikia mama mkwe.

Giza nene lilitanda na baadaye mwanga ukaja kwa mbali na nikamuona mama mkwe akininusisha ule ugoro. Nilitamani nikatae lakini nguvu zilikuwa zimeniishia kabisa nikawa nashindwa kunyanyua mkono ili kupokea ule ugoro.

Alininusisha nikaanza kupiga chafya, haraka sana mama mkwe akakimbia kuelekea chumbani kwake.

Nilijaribu kuinua mkono, ukainuka, nikajaribu kuketi pale kitandani, nikafanikiwa. Niligeuza shingo kumuangalia mume wangu na hasa nilimuangalia kifuani kama bado alipumua au walimleta pale akiwa maiti.
Niligundua kuwa bado anapumua kwa sababu kifua chake kilikuwa kikitanuka na kushuka alipokuwa anavuta hewa.
"Baba Ajigale, baba Ajigale," nilimuita lakini hakuitika.

Niliwaza kwamba nimuendee mama mkwe nikamshurutishe aje amzindue?

Je, atapata fahamu au mpaka waje wale wachawi?

Fuatilia Jumanne ijayo.
 
ILIPOISHIA

Mara tu baada ya kumnusisha alipiga chafya mara tano au sita. Nilishukuru kwa kitendo kile maana nilikuwa nimeanza kuchanganyikiwa.

"Baba Ajigale, baba Ajigale, baba Ajigale," nilimuita, lakini hakuweza kuitikia.
Niliwaza kwamba nimuendee mama mkwe nikamshurutishe aje amzindue?
Songa nayo…

Nilipata akili haraka sana kwamba nikifanya hivyo mama mkwe atagundua kuwa nilikuwa naona kila kitu ambacho walikuwa wakikifanya na wachawi wenzake.
Akili ikaniambia nizidi kumnusisha ugoro uliokuwa juu ya godoro japokuwa ulikuwa ‘kiduchu' lakini nilijitahidi kuokoteza.

Baada ya kazi hiyo nilimnusisha tena akapiga chafya na kufumbua macho. Nilimuita, "Baba Ajigale." Akawa ananitazama bila kusema chochote.

Nilifungua mlango na kwenda jikoni kwenye friji, nilichukua soda na kurudi chumbani kwetu, wakati narudi mama mkwe naye akawa karibu kabisa na mlango wa chumba chetu.
Alikunja vidole vya mkono wake na kuachia kimoja akawa ananipa ishara kuwa nifunge mdomo wangu.

Nami sikumchelewesha nikamuambia kwa kunong'ona kuwa nimemnusisha ugoro nitamuambia kuwa umenipa wewe. Nikazama chumbani.

Nilipoingia chumbani, nilimuinua na kumketisha mume wangu kisha nikaanza kumnywesha ile soda.
Alikunywa kana kwamba alikuwa ametembea kwenye jua kali sana na alikuwa na kiu. Nilichukua shuka na kumfutafuta pua ambayo ilikuwa na chembechembe za ugoro. Alipiga chafya tena.

"Najisikia mchovu sana, kwani nilikuwa nafanya nini mpaka ukaamua kuninywesha soda?" aliuliza.
"Nimekuona unakosa nguvu, kila nikikuita huitiki , nikahisi kuwa inawezekana una sukari kidogo mwilini," nilimdanganya.

"Sawa, lakini mbona kuna harufu ya ugoro puani kwangu, kulikoni."
Kabla sijajibu swali hilo moyo ulipiga paa kwa sababu niliona nikimtajia sababu na aliyeleta ugoro kuwa ni mama yake na wachawi wenzake itakuwa balaa.
Nilifikiri sana, lakini sikupata jibu la haraka.

"Mbona hunijibu, imekuwaje kuna ugoro na kwa nini nimenusishwa?"
Nilijua kuwa mama mkwe kutokana na tabia yake ya ‘kubana' nyuma ya mlango wetu alikuwa anasikiliza mazungumzo yetu, hivyo nilipaza sauti ili asikie kule alipo:

"Ugoro nilikwenda kumuomba mama mkwe ambaye alinipa nikunusishe, alisema mtu akikosa nguvu akinusa ugoro anapiga chafya, kitendo ambacho kinachangamsha mapafu na kuyafanya yafanye kazi sawasawa, hivyo mtu kupata nguvu,"nilisema huku nikionesha kutokuwa na wasiwasi na maelezo yangu.

"Hebu nenda kaniletee maziwa yangu kwenye friji, au umekunywa?"
"Hapana, bado yapo."
"Hebu nenda kaniletee."
"Sawa."

Ile nafungua mlango tu, nikakutana na mama mkwe akiwa pembeni ya mlango. Akanong'ona, "Gonga."Alisema neno hilo huku akitoa tabasamu pana lililomuonesha mapengo yake ya meno ya mbele.

Nilitamani nicheke na hasira zote zilinitoka kutokana na mama mkwe huyo kunipa mkono wake na kunitaka nigonge kufurahishwa na nilivyomdanganya mume wangu.
Nilikwenda kwenye friji na kuchukua maziwa fresh yaliyokuwa yamekuwa baridi sana. Nilidhani ameondoka pale karibu na mlango wa chumbani kwetu.

Ajabu ni kwamba bado alikuwa amesimama palepale huku akitabasamu utafikiri alikuwa juha.

***
Kulikuwa kumepambazuka na majogoo yalikuwa yanawika kuashiria kuwa jua lipo mbioni kuchomoza. Niliinuka na kwenda bafuni kujisaidia na nilipotoka huko nilikwenda moja kwa moja kwenye meza ya chakula kumuandalia kifungua kinywa mume wangu kabla hajaenda kazini.

Naye alikwenda kuoga na akaingia chumbani kwetu. Mama mkwe hakuwa ameamka bila shaka kutokana na kazi nyingi za kichawi za usiku alizokuwa amezifanya.

Mume wangu alifika mezani na kukuta chai ipo tayari pamoja na mayai ya kuchemsha mawili na kipande cha mkate mweusi ambao anapenda kula.

Itaendelea wiki ijayo.
 
MAMA mkwe hakuwa ameamka bila shaka kutokana na kazi nyingi za kichawi za usiku alizokuwa amezifanya. Mume wangu alifika mezani na kukuta chai ipo tayari pamoja na mayai ya kuchemsha mawili na kipande cha mkate mweusi au kahawia (brown bread). SONGA NAYO.

Mume wangu baada ya kunywa chai alifika mezani hapo mtoto wetu Ajigale naye akapata kifungua kinywa baadaye alilalamika kuwa hali yake siyo nzuri.
"Umesema hali yako siyo nzuri, kwani unajisikiaje?"

"Ni kama vile usiku kucha nilikuwa nalima au kufanya mazoezi ya nguvu. Mwili wote unauma, sijui hii hali imenitokea kwa sababu gani?"
"Lakini…."

"Lakini nini? Bila shaka homa ya malaria inakunyemelea mwanangu," alidakia mama mkwe huku akinitupia jicho nami nikagundua kuwa bila shaka alidhani nitatoa siri ya walichokifanya usiku na wachawi wenzake.

"Malaria? Dozi nimemaliza wiki moja tu iliyopita?"
"Baba Ajigale, malaria huwa inajirudia na ndiyo maana madaktari hushauri kuwa ukimaliza dozi, rudi baada ya wiki moja kucheki tena damu."

"Mwili wote unauma, ni lazima itakuwa ni malaria," alisisitiza mume wangu.
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa akiwa na mtoto wetu, mume wangu aliomba apewe maji ambayo alisema atakunywa njiani.

"Nitakwenda kwanza shuleni kumuacha Ajigale kisha nitapitia ofisini ndipo niende hospitali kupima."
Alichukua begi lake na kwenda kwenye banda la gari akifuatana na mtoto Ajigale, muda mchache baadaye nikasikia mungurumo wa gari, nikaenda dirishani na kumuona akitoka kwa mwendo wa pole baada ya kufunguliwa geti na mtumishi wetu wa kiume.

Mama mkwe alipoona Ajigale na baba yake wameondoka alinijia nilipokuwa nimesimama huku akiwa ameshika mikono yake kiunoni, akaja karibu kabisa na uso wangu.
"Pale nilikukatiza kwa hasira. Ulitaka kumuambia mambo yangu ya kichawi ya usiku mumeo siyo?" alifoka mama mkwe huku akiwa na ndita usoni.

"Hapana mama, mimi nilitaka nimshauri kwenda kupima damu hospitali."
"Muongo mkubwa wewe, nakuambia kwa mara nyingine, ukitoa siri yangu nakufanya supu siku hiyohiyo wala sikutishi na kama unaona natania jaribu."

"Mama kwani ningetaka kumuambia mume wangu ningeshindwa? Sitaki tabia yako ya kunifokea kila siku kama mtoto mdogo," nami nilijitutumua kumpima kisha nilimeza mate na kukaa kimyaa baada ya kuona amepandisha hasira japokuwa sikuona kosa langu lakini nilijua kuwa alikuwa akijihami ili siri yake nisiitoe kwa mume wangu.

Tuliachana, yeye akaenda chumbani kwake nami nikaenda jikoni kufanya shughuli zangu za mapishi nikisaidiwa na msichana wa kazi.

"Mama kwani vipi? Mbona naona siku hizi hamuelewani na bibi?" aliniuliza msichana wa kazi.
"Shiiiiiiiii," nilimuambia huku nikiwa nimeweka vidole vyangu viwili kwenye mdomo wangu.
* * *
Ni saa kumi jioni alikuja jirani yangu, mama Kibela na kutokana na mvua badala ya kukaa kwenye kibaraza tuliamua kukaa sebuleni kuzungumza.
"Mama Ajigale nimekuja kukuambia jambo," alisema.
"Jambo gani?"

"Ni siri na nakuambia kwa sababu nakupenda. Unajua hapa kwako kuna wachawi wanakuja kila siku usiku?"

Baada ya swali hilo moyo ulinipiga ‘paa' na mara moja mama mkwe akatoka chumbani kwake na kujifanya kama anatoka nje kwenye kibaraza.
Nilijua kuwa naye moyo wake umempasuka kama ulivyopasuka wangu kwani alijua kuwa jambo lile nalijua mimi tu.

"Ehee, umejuaje kuwa kuna wachawi wanakuja hapa kwangu?"
"Sikiliza. Msiishi kitoto, hapa kwenu nimekuwa nikishuhudia wachawi wakija usiku na mara nyingine wanawachukua na kutokomea nanyi."
"Kweli mama Kibela?"

"Niongope jambo zito kama hilo? Ninachokisema ni kweli na niamini.Huwa wanatoka mbali kwa sababu huwa wanakuja na nyungo, ina maana wanasafiri na wakifika mmoja wenu anachukuliwa na kuwekwa katika chombo kisha huruka naye na kutoweka."
Wakati anasema hayo mama mkwe alikuwa nje, macho yetu yaligongana akawa amekunja uso kwa hasira.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia Jumanne ijayo
 
ILIPOISHIA
"Wachawi hao wanatoka wapi?" nilijifanya kumdadisi.
"Huwa wanatoka mbali kwa sababu huwa wanakuja na nyungo, ina maana wanasafiri na wakifika mmoja wenu anachukuliwa na kuwekwa katika chombo kisha huruka na kutoweka."

"Makubwa. Kama ni hivyo mbona watatuua!" Wakati nasema hayo mama mkwe alikuwa nje, macho yetu yaligongana akawa amekunja uso kwa hasira.

FUATILIA KWA KINA
Ni wazi kwamba kutokana na kukunja uso alikuwa anasikia yale aliyokuwa akinisimulia jirani yangu.
Alinieleza mengi sana na akasema yeye huwa anawaona wachawi kutokana na dawa alizopewa na babu yake.

Sikutaka kumdadisi kutokana na mama mkwe kuniangalia sana tena kama nilivyosema hapo juu, kunitupia jicho kali.
Nilijaribu kutumbukiza maneno mengine ili tuachane na ‘topiki' hiyo lakini mwenzangu akawa anaendelea kusimulia.

"Mama Ajigale haya ninayokuambia siyo masihara maana naona kama unadharau. Wachawi wale wanapofika huwa naona wanatoka na mtu humu ndani usiku. Kama Siyo wewe basi ni mumeo au mama mkwe wako. Lakini anakuwa hajitambui kwa sababu anabebwa kama maiti inavyotolewa ndani au mgonjwa mahututi."

"Habari hiyo naomba tuiache, inanitisha," nilisema huku nikimtupia mama mkwe jicho kiwogawoga.
"Sawa tuyaache. Lakini akifika mumeo muambie na kama atataka ushauri zaidi aje anione."
"Sawa," niliitikia, mama mkwe akasonya.

"Hee, mbona mama mkwe wako kasonya?" aliuliza kwa sauti ya chini.
"Achana naye. Tangu asubuhi ana mambo anadai hatujamtimizia," nami niliamua kumdanganya yule jirani yangu.

"Mnafanya vibaya. Wazee kama hawa hamtakiwi kuwasononesha kwa kuwanyima wanachokitaka, mtimizieni, kwani alitaka nini?"

"Wazee huwajui? Alikuwa akitaka apelekwe kwao lakini mwanaye amemkatalia. Ni hilo tu," nilizidi kumdanyanga lakini yote hayo tulikuwa tukiyasema polepole.
Kitendo cha kunong'onezana kilimshitua mama mkwe akaamua kuingia sebuleni na kukaa katika sofa lililokuwa kwenye kona.

Sikupenda kabisa macho yetu kugongana licha ya kuniangalia kwa macho ya kutisha. Tulianza kuongelea saluni gani nzuri ili kubadili mazungumzo lakini kwa sauti ya chini.

"Unamuogopa mama mkwe, wewe sema tu kwa sauti. Unataka nikupeleke saluni gani?"
"Mama nilitaka nimchukue mkweo anipeleke saluni ambayo amesuka nywele zake. Nimezipenda sana."
Mama mkwe alimuangalia kwa jicho baya na hakujibu chochote.

"Mh, mwaya, naona mama mkwe wako hataki utoke," alisema jirani yangu huku akimuangalia mama aliyekuwa bize kusuka mkeka wake ambao ulikuwa chini ya sofa wakati akiwa nje.
"Tunaongea tu. Nikuletee chai au soda ama maziwa?" nilimuuliza mgeni wangu.
"Niletee maziwa." Niliondoka na kwenda kumchukulia shoga yangu maziwa ambayo yalikuwa kwenye themosi.

"Lakini tusikae humu shoga bora tukae hapo nje kwenye kibaraza. Tuongee huku tukipunga upepo," alisema yule shoga yangu, hivyo kikao tukakihamisha na kwenda kukaa nje.

Kwa mara nyingine nilimtupia jicho mama mkwe, akawa anatikisa kichwa, nilijua kuwa alikuwa anadhani tuliamua kumkimbia baada ya yeye kukaa kwenye sofa pale sebuleni.
Mazungumzo yetu pale nje yalikuwa ni kuhusu saluni na mavazi huku kila mmoja akimsifu fundi wake wa nguo.

Mazungumzo hayo nadhani yalimfurahisha mama mkwe kwa sababu ile stori ya wachawi tuliiacha kabisa.

Baada ya mazungumzo marefu shoga yangu huyo aliaga akasema anakwenda kwake kuandaa chakula cha jioni.

"Si unajua mimi sina msichana wa kazi?"
"Haya shoga. Nitakupigia simu kesho kukueleza saa ngapi nikupeleke kule saluni."
"Usikose.

Si unajua Jumamosi mimi nina harusi ya wifi yangu? Leo Ijumaa, kesho inatakiwa twende asubuhi ili jioni tujiandae kwa sherehe ya ndoa."
"Sawa."

Wakati namtoa kwenye geti mume wangu naye akawa anaingia na gari lake akiwa na mtoto wetu Ajigale.
"Shemeji vipi, mimi naingia na wewe unatoka, au unanikimbia?"

Je, baada ya kuulizwa hivyo alijibuje? Fuatilia simulizi hii ya kusisimua Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 11


ILIPOISHIA.
Moyo ulinipiga, nikawa najiuliza ni nini mume wangu anataka kuzungumza na shoga yangu lakini sikupata jibu. Nilijiuliza sana kwa sababu hakuwahi kuniambia kama anawahitaji hawa majirani zetu hata siku moja, nilibaki nikiwa nimepigwa butwaa.

Mama mkwe naye alikuwa mtu wa wasiwasi baada ya kuona shoga yangu anarudi kwenye kisebule cha nje. Akawa anadhani kuwa inawezekana anataka kumueleza habari za wachawi kutuchezea usiku.
SONGA NAYO...

Haraka sana alichukuwa kigoda na kukiweka kwenye kona ya kisebule cha nje, akaketi. Mimi na jirani yangu tulikaa kwenye viti vya plastiki ambavyo huwa vinakaa pale sebuleni kila siku.

Mume wangu alikwenda kuegesha gari kwenye banda lake na mtoto wetu Ajigale alitoka garini mbio na akaingia ndani, nilimuelekeza kuwa chakula kipo kwenye ‘hotpoti' juu ya meza ya chakula na mchana wa siku hiyo nilikuwa nimeandalia pilau.

Baada ya kumuambia hivyo alitoka mbio kuingia ndani maana tulikuwa ‘tumemkuna' kwani pilau ndicho chakula anachokipenda sana.

Baada ya sekunde kadhaa mume wangu alifika pale kwenye kisebule. Kulikuwa na kitu ambacho hakikuwa na mtu, hivyo aliketi.
"Ndiyo jirani, kaka hajambo?"

"Hajambo, vipi leo nakuona kama vile umewahi sana."
"Ahhh leo nimeamka naumwa mwili wote kama vile nilikuwa nafanyishwa mazoezi."
"Umepima, isije ikawa malaria?"

"Nilipima. Mimi nilikuwa na wasiwasi sana. Unajua siku hizi ukijisikia homa yale mawazo ya malaria huna, unafikiria homa ya dengue."

Tulicheka wote watatu isipokuwa mama mkwe aliyekuwa ameketi kwenye kigoda akiwa bize kusuka mkeka wake.

"Unajua huu ugonjwa wa dengue ni gumzo sasa nchi nzima. Tumuombe Mungu atuepushie mbali. Sasa ulipopimwa wamegundua nini?" jirani aliendelea kudadisi.

"Hawajaona ugonjwa wowote wakasema labda ni uchovu wa kazi."
"Hapana shemeji yangu. Mimi nilikuja hapa kumjulisha mkeo jambo zito kidogo."
"Jambo zito, umenishitua, kuhusu nini tena shemeji?"

"Nilimwambia kuwa nyinyi katika nyumba yenu mnaishi kitoto kwa sababu huwa kuna wachawi wanakuja usiku na kuondoka na mtu mara kwa mara hapa kwenu."
"Unayoyasema shemeji ni kweli au unaota au unanitania?

"Shemeji tangu lini nawatanieni? Nasema hayo siriasi kwa sababu nawapenda."
"Wewe umejuaje au umeonaje?"

"Sikufichi shemeji mimi nyumbani kwetu baba yangu ni fundi sana wa mambo mengi ya kishirikina, yeye harogi lakini ana uwezo wa kukuzindika na kukufanya uweze kuona wachawi."
"Kweli shemeji?"

"Kwa nini niseme uongo, kweli na ndiyo maana mimi huwa naona kuna kitu kinachofanyika hapa kwako. Tushukuru kwamba hukuweka ukuta na badala yake umezungushia seng'enge, hivyo kuwa rahisi kwangu kuona kinachofanyika hapa."

"Dahh kama ni hivyo tumo hatarini. Mumeo anayajua haya?"
"Yeye pia kazindikwa anaona wachawi, wakija hapa huwa aliye macho anamuamsha mwenzake, anajua kila kitu."

"Sasa mbona hajaniambia mambo ya hatari kama hayo?"
"Aliniambia kazi hiyo niifanye mimi kwa kumuambia mkeo maana yeye na wewe wote muda wenu wa kurudi kazini huwa mbaya."

Wakati shoga yangu akimuelezea mume wangu mambo hayo ya kilozi, mama alikuwa akinikodolea macho huku akiweka vidole vyake mdomoni, niligundua kuwa ananikataza kusema chochote kuhusiana na jambo hilo.

Anaelewa mimi pia najua kuwa wachawi huwa wanakuja nyumbani mwetu na yeye ndiye mwenyeji wao.

Anajua pia kuwa usiku uliopita ambao mume wangu analalamika kuwa anaugua mwili, yeye mama mkwe aliongoza wachawi wenzake kumchukua na kumpeleka wanakojua wao nami niliona.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba sijui walikwenda kumfanyia nini lakini kitu kimoja ambacho ni wazi kabisa ni kwamba kwa siku zote ambazo wanakuja wachawi, mume wangu hajimudu kunipa haki yangu ya kindoa.

"Sasa jirani kwanza nakushukuru kwa kutupa habari hiyo mbaya. Lakini haitoshi kutuambia tu, tueleze sasa tufanye nini kuondokana na hali hiyo?"

"Kwani jamani sikuwaambia? Kwamba baba yangu ni mtaalam wa kuzuia ushenzi huo mnaofanyiwa."
"Ina maana unaweza kutupeleka kwa baba yako ili akatuzindike na sisi pamoja na nyumba yetu?"

Je, nini kitatokea? Fuatilia Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 12


ILIPOISHIA
Hata hivyo, ukweli ni kwamba sijui walikwenda kumfanyia nini lakini kitu kimoja ambacho ni wazi kabisa ni kwamba kwa siku zote ambazo wanakuja wachawi, mume wangu hajimudu kunipa haki yangu ya kindoa.
"Sasa jirani kwanza nakushukuru kwa kutupa habari hiyo mbaya. Lakini haitoshi kutuambia tu, tueleze sasa tufanye nini kuondokana na hali hiyo?"

"Kwani jamani sikuwaambia? Kwamba baba yangu ni mtaalam wa kuzuia ushenzi huo mnaofanyiwa."
"Ina maana unaweza kutupeleka kwa baba yako ili akatuzindike na sisi pamoja na nyumba yetu?"
SONGA NAYO...

Maelezo ya yule jirani yetu yalimchanganya mume wangu lakini mimi sikuwa na presha kwa sababu nilikuwa najua zaidi ya maelezo yaliyotolewa. Tofauti ni kwamba mimi nilikuwa najua kuwa aliyekuwa akichukuliwa na kupelekwa kusikojulikana ni mume wangu.

Nilifarijika kwa sababu mama mkwe sasa ameshuhudia kuwa aliyesimulia au kutoa siri ya tukio hilo la usiku siyo mimi, hivyo mimi kumuona yule jirani yangu kuwa ni mwokozi wa roho yangu.
Tulikubalinana na yule jirani kuwa kesho atatupeleka kwa baba yake ambaye ni mtaalamu wa mambo ya ulozi.
***
Usiku wa siku hiyo ulikuwa wa balaa kubwa kama ilivyo ada wachawi walifika nyumbani kwetu saa nane au saa tisa za usiku wakiwa katika kikundi na kumchukua baba watoto wangu. Ni mama mkwe alikuwa akisimamia zoezi hilo. Mimi kama ilivyokuwa mwanzo nilijifanya nimelala fofofo.

Lakini baada ya majadiliano kati ya kundi lile la wachawi na mama mkwe iliamriwa kuwa asichukuliwe mume wangu na badala yake nichukuliwe mimi.

Niliogopa sana na kuamini kuwa sasa muda wangu wa kuishi hapa duniani umekwisha.
Niliamini hivyo kwa sababu nilikuwa sijui chochote kilichokuwa kimeamriwa nje ya nyumba baada ya kuondoka na mume wangu kwani baada ya dakika chache niliuona msafara ukirejea chumbani huku ukiwa umembeba mume wangu.

Nilijua kuwa kilichokuwa kimefanyika ni kubadilishana mimi na mume wangu lakini sikujua kabisa sababu ya wachawi wale kufanya hivyo na hicho ndicho kilichokuwa kikinitisha zaidi.
"Kwani huyu unataka tumchukue unataka akafanye nini?"
"Nataka naye tukamfundishe uchawi."

"Tukamfundishe uchawi, kwani huyu mkweo ni ndugu yenu?"
"Ni makubaliano kati yake na mumewe."
"Alikuambia?"

Mama mkwe alikaa kimya kwa muda bila shaka alikuwa akitafakari nini cha kujibu. Baada ya sekunde kadhaa alibadili jibu akawaeleza kuwa ni yeye aliyeamua hilo.
"Unajua kuna koo hazitaki kushiriki mambo ya ulozi."
"Najua."

"Kama unajua kwa nini unampangia mwanao jambo zito kama hili?" alikuwa akiulizwa na mtu mmoja ambaye alikuwa anaonekana kama ndiye kiongozi wao na nilijua hilo kutokana na mtu yule kuvaa shanga nyingi shingoni na kuonekana dhahiri kwamba alikuwa na amri za mara kwa mara kwa wale wachawi ambao walitekeleza kila alichowaambia.

Sijawaeleza kwamba wachawi hawa ambao walikuwa hawapungui kumi kila mmoja alikuwa amevaa nguo nyeusi na nyuso zao zilikuwa zimepakwa majivu na ilikuwa siyo rahisi kumtambua mtu kwa sura.
Sikuwa na la kufanya pale kwa sababu nilijisemea kimoyomoyo ‘hapa nikijifanya nakataa safari yao, basi wanaweza kunimaliza kwa kuniua moja kwa moja.'

Nilipakwa yale majivu kisha nikajikuta nikiinuliwa juu kwa juu kama maiti huku nikiwa nimefunikwa na nguo nyeusi.

Baada ya kutoka nje ya nyumba yetu niliiangalia ile nyumba ya jirani yangu nikagundua kuwa taa za ndani zilikuwa zinawaka, nikatambua kuwa walikuwa macho na waliona kila kilichoendelea pale. Lakini nadhani hawakuwa na uwezo au labda nao waliogopa kuingilia kati mambo haya ya kichawi.

Nililazwa nje ya nyumba yetu na mchawi mmoja akawa ananitambuka huku akisema maneno ambayo nilikuwa siyaelewi. Mchawi yule alifanya hivyo zaidi ya mara kumi.

Baadaye nilinyanyuliwa na kuwekwa kwenye chombo chao ambacho ni ungo mkubwa. Niliketishwa kisha kukawepo na mtu aliyekuwa amekaa nyuma yangu na kunishikilia nisianguke.
Nami kwa kuwa nilijua hatari ya kujionesha kuwa niliona kila kitu, nilijilegeza ili yule mtu aliyekuwa amepewa kazi ya kunishikilia aamini kuwa nilikuwa sijielewi.

Je, nini kiliendelea? Fuatilia wiki ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 13

ILIPOISHIA
Nililazwa nje ya nyumba yetu na mchawi mmoja akawa ananitambuka huku akisema maneno ambayo nilikuwa siyaelewi. Alifanya hivyo zaidi ya mara kumi.

Baadaye nilinyanyuliwa na kuwekwa kwenye chombo chao ambacho ni kama ungo mkubwa. Niliketishwa kisha kukawepo na mtu aliyekuwa amekaa nyuma yangu na kunishikilia nisianguke.
Nami kwa kuwa nilijua hatari ya kujionesha kuwa naona kila kitu, nilijilegeza ili yule mtu aliyekuwa amepewa kazi ya kunishikilia aamini kuwa nilikuwa sijielewi.
SONGA NAYO...

Nilipakatwa na wakati natafakari nini cha kufanya mama mkwe aliwaeleza wachawi wenzake kwamba kuna mama jirani amegundua njama zao.

"Yupo mama jirani hapa amegundua mchezo huu tunaoufanya," alisema mama mkwe.
"Ulijuaje kuwa amegundua?" kuna mchawi mwingine aliuliza, sikuweza kumuona kwa sura kwa sababu nilikuwa nimefumba macho kudanganya kwamba sijifahamu kutokana na dawa walizokuwa wamenipaka usoni.

Naamini dawa zile walizopaka kwenye sura yangu zilikuwa zikiaminiwa na wachawi wale kuwa zingenifanya nikose fahamu kwa sababu walifanya hivyo kwa mume wangu chumbani na tulimuacha akiwa hajitambui.

"Alikuja mchana na kuwaambia hawa (yaani mimi) na mwanangu (mume wangu)," alisema mama mkwe.
Baada ya kutamka maneno hayo, wachawi wale walipigwa na butwaa nami nikashushwa katika ungo ambao waliuandaa ili niruke nao.

Baadaye mchawi mwingine ambaye alionekana kana kwamba ndiye mwenye madaraka zaidi pale au kiongozi aliamuru turudi kwanza ndani.
"Hapa nje kufanya mashauri hayo siyo mahali pake, naomba turudi ndani ili tukayaongee haya," alisema kiongozi wa wachawi.

"Sawa, kwa hiyo tumrudishe mama Ajigale ndani siyo?" aliuliza mama mkwe.
"Ndiyo maana yake. Hujanielewa? Vijana fanyeni kazi yenu," alisisitiza yule kiongozi.
Nilijikuta nikinyanyuliwa juu kwa juu hadi chumbani kwetu.

Nilikuta mume wangu akiwa bado hajitambui na pembeni yake kulikuwa na mwanamke mwingine mchawi ambaye alikuwa akimlinda ili kuhakikisha kuwa hazinduki kabla mimi sijarejeshwa kutoka huko walikotaka kunipeleka.

Baada ya kuingizwa ndani nililazwa kando ya mume wangu na kundi kubwa la wachawi walikuwa wamekizunguka kitanda.

"Sasa tusimulie, huyo mama jirani alikuwa akiwaambia nini hawa wanao?" alisema huyo mchawi kiongozi ambaye jina lake zikuweza kulifahamu.

"Aliwasimulia kuwa kuna wachawi huwa wanafika hapa na kumchukua mtu, lakini aliwaahidi kuwa atawapeleka kwa baba yake ili akawape zindiko kwa hiyo naamini kesho atafanya hiyo kazi," mama mkwe alisema.

"Kama hivyo ndivyo naomba kitu kimoja, mtu mmoja aende sasa hivi kwenye nyumba ya mama huyo jirani akaone kama ana ubavu wa kutuzuia kufanya kazi yetu hususan kumchezea."
Aliamrishwa mtu mmoja kati ya wale wachawi waliokuwa wamezunguka kitanda kufuatana na mama mkwe wangu hadi kwa yule mama jirani yetu.

Walitoka na kwenda moja kwa moja kwa mama jirani. Sikuthubutu kufumbua macho ili kuona alikuwa amefuatana na nani lakini nilisikia wakitoka huku wakiwa wanashauriwa kutoacha usinga ambao hufanya kutengua zindiko lililowekwa katika nyumba wanayopania kufanya uchawi wao.

Watu hao wawili walifika katika nyumba ya jirani yetu na walikuta bado taa zikiwa zinawaka nje na ndani.
"Anza wewe mwenye usinga kwenda kuingia ndani," ulikuwa ni ushauri wa mama mkwe.
Yule kijana aliyepewa kazi hiyo alimuangalia mama mkwe na kumtupia swali.
"Nikiingia ndani, nifanye nini?"

"Wewe ingia tu, si tunaangalia kama nyumba hii ni nyepesi au nzito?"
"Hilo ni jambo gumu. Kama nyumba ni nzito itakuwaje?"
"Kama ni nzito tutarudi kwa kiongozi wetu pale nyumbani kwa mwanangu halafu atajua cha kufanya."
***
Mle ndani wale wachawi waliobaki na kiongozi wao kazi yao ilikuwa kuchezacheza huku wakiimba kwa sauti ya chini sana.

Mmoja ambaye naamini ndiye alikuwa kiongozi wao alikuwa akitia uvumba kwenye chetezo ambayo walikuja nayo na moshi ukatanda chumba kizima.

Itaendelea wiki ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 14


ILIPOISHIA
Muda mfupi baadaye nilisikia sauti kali kama ya radi, nilipigwa na butwaa na kujiuliza kama nje kuna mvua au ni nini, sikuwa na jibu.
Baada ya dakika kadhaa kupita na wachawi wakiendelea kucheza ngoma za kichawi kwa kutumia manyanya, aliingia mama mkwe huku akitweta kama mtu aliyekuwa akikimbizwa.
SONGA NAYO...

Mama mkwe alianza kueleza yale niliyoyaeleza juu kwamba walifika katika nyumba ya jirani yetu na walikuta bado taa zikiwa zinawaka nje na ndani ya nyumba.
Akasema walibishana na kujiuliza nini watafanya mle ndani, "Nikiingia ndani, nifanye nini?"
"Wewe ingia tu, si tunaangalia kama nyumba hii ni nyepesi au nzito?"
"Hilo ni jambo gumu. Kama nyumba ni nzito itakuwaje?"

"Kama ni nzito tutarudi kwa kiongozi wetu pale nyumbani kwa mwanangu halafu atajua la kufanya," nimemuambia na ndiyo maana nimerudi.

"Sasa nyumba ni nzito ya huyo jirani ina maana ina zindiko?" alihoji kiongozi wa wachawi.
"Ndiyo maana yake kwa sababu yule kijana ameingia ndani, lakini ameshindwa kutoka, kwa maana nyingine ameganda, hawezi kunyanyua mguu."

Wachawi wote mle chumbani waliachana na mimi na mume wangu na kumzunguka mama mkwe ambaye alisimulia mengi na hasa jinsi alivyotumia usinga ili kumuokoa kijana aliyekuwa amefuatana naye lakini ikashindikana.

"Kilichobaki sasa ni sisi kwenda kwenye nyumba hiyo jirani ili kuangalia jinsi ya kumuokoa mwenzetu."
"Lakini nani ana zana za kumnasua mchawi akinasa?" aliuliza mama mkwe.
Mtu mmoja alisema yeye anao unga mweusi ambao ni mchanganyiko wa mkaa wa mifupa ya sokwe mtu na mafuta ya simba dume na ya nyani ambayo huwekwa kwenye tunguri.

Watu wengine wawili na mama mkwe pia yule mwenye dawa walikwenda nyumba jirani kwenda kumuokoa mwenzao aliyenaswa ndani ya nyumba lakini baada ya dakika thelathini walirudi wakiwa hawana mlengwa.

"Imeshindikana, ile nyumba ni hatari," alisema yule mwenye tunguri huku mama mkwe akitetemeka.
"Mama mbona unatetemeka sana?" alihoji kiongozi wa wachawi.

"Natetemeka kwa sababu yule mwenzetu kama itashindikana kumnasua na akakaa pale mpaka kesho asubuhi, nitaumbuka, kwa kuwa yule mama mwenye nyumba ile anajua wachawi huwa wanafika hapa, basi gogo litaniangukia."

Iliamriwa kuwa kiongozi wao aende kwake akachukue dawa ambayo waliamini kuwa ni bora kuliko ile ya usinga ili waweze kwenda kumnasua mwenzao.
Kitendo kile kilinifurahisha kwa sababu badala ya kunichukua mimi ili wanipeleke huko walikotaka kunipeleka sasa kazi iligeuka, ikawa ni kazi ya kumnasua mwenzao.

Walitoka chumbani kwetu na kusimama sebuleni lakini kila lililokuwa likizungumzwa nilikuwa nalisikia.
Chumbani kwangu kulikuwa na saa ya ukutani niliiangalia nikaona inasomeka kuwa ni saa tisa na nusu usiku na nilijaribu kumtingisha mume wangu, ikawa ni kazi bure kwani alikuwa amelala fofofo kutokana na dawa alizopakwa na wachawi.

"Jamani kaeni tu kwenye hizo sofa tumsubiri kiongozi," nilitambua sauti hiyo kuwa ni ya mama mkwe, alikuwa akiwakaribisha wachawi wenzake kama vile wapo pale kihalali kwa mambo halali.
Kimyaa kilitawala kwa dakika kadhaa na nikawa natamani nishuke nikawachungulie lakini moyo uliniambia nisifanye hivyo kwa usalama wangu.

Jogoo alisikika akiwika na jimbi langu (jogoo wangu) naye alidakia na kuwika, hali hiyo ilinifanya niinue kichwa na kuangalia tena saa, ikawa inasomeka kuwa imetimia saa kumi na dakika tano.

"Hii hali inatisha sana, unasikia majogoo wanawika, hiyo inaashiria kuwa kunakucha na watu wataanza kutoka mitaani hasa wale wanaokwenda kuchukua bidhaa sokoni," alisikika mama mkwe akizungumza.
"Sasa tufanye nini? Inatakiwa akili ya ziada kuamua cha kufanya," hiyo ilikuwa sauti ya mwanaume ambaye sikumjua kwa jina.

"Au hapa tulipo kuna mtu ambaye ana dawa ya kumfanya mtu asionekane?" alikuwa ni mama mkwe akiwatupia swali wenzake.

"Hilo ungelikumbuka wakati mkuu anakwenda nyumbani kwake kwa sababu kama hiyo dawa ipo, tungeitumia kama tutashindwa kumng'atua kwa leo pale aliponasa mwenzetu," alidakia mwanamke mwingine ambaye pia sikumfahamu kwa jina wala kumtambua kwa sauti yake.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 15

ILIPOISHIA
"Hilo ungelikumbuka wakati mkuu anakwenda nyumbani kwake kwa sababu kama hiyo dawa ipo, tungeitumia kama tutashindwa kumng'atua kwa leo pale aliponasa mwenzetu," alidakia mwanamke mwingine ambaye pia sikumfahamu kwa jina wala kumtambua.
Wakati wakiwaza hayo yule kiongozi mkuu wa wachawi akawa ameingia na tunguri zake nne zenye shanga.
SONGA NAYO...

Walijitahidi kufanya shughuli zao za kishirikina kwa kujifanya kurusha ‘kombora' lao la kichawi huku wakisema kwamba likitua kwenye nyumba ile ya jirani, litasambaratisha dawa zilizomfanya mwenzao anase.

Nilisikia wakibishana wengine wakidai yule mkuu wao kakosea kuchanganya unga wa dawa walizotumia kutengeneza kombora hilo.

Kwa kuwa kikao chao walikuwa wakifanyia kwenye sebule yetu, nilisikia wakisema dawa walizotia kwenye pembe ya nyati hazikutimia.
Sikujua ni dawa gani walizotia kwenye ile pembe lakini nilisikia mtu akiambiwa apulize kuelekea kwenye ile nyumba ya jirani.

"Nimepuliza limekwenda lakini sasa itabidi watu waende kumalizia kule kule kwenye nyumba," alisema yule mtu aliyekuwa akionekana kama kiongozi wao.
Baadaye alitumwa mama mkwe na kijana mwingine kwenda kwenye ile nyumba ya jirani ili kumalizia dawa nyingine za kumnasua.

Wachawi wengine wote walikaa kwenye kochi pale sebuleni kana kwamba walikuwa ni wageni wetu rasmi ambao walisubiri chakula au hotuba ya kukaribishwa na mwenye nyumba.

Walikuwa wakinong'ona maneno ambayo mimi nilikuwa siyasikii lakini nahisi walikuwa wakijadili ugumu au kazi waliyonayo ya kumnasua mwenzao ambaye alinasa kwenye nyumba ya jirani.
Nilijitahidi kumtingisha mume wangu ili kuona kama ataamka lakini ilishindikana kwani alikuwa akiendelea kukoroma kutokana na dawa walizomnusisha.Wakati naendelea kumtingisha mume wangu huku nikiwaza

nini cha kufanya ili kumzindua nilisikia kishindo cha mlango wa barazani kufunguliwa.
Nilijikusanya pale kitandani na nikaenda kuchungulia nikashuhudia mama mkwe akiwa na yule kijana wakiwa wamesimama mbele ya wachawi wenzao.
"Imeshindikana," alisema mama mkwe.

"Inamaana ile dawa haikufanya kazi?" alihoji yule kiongozi wao.
"Ndiyo maana yake. Tumejitahidi kupuliza ile pembe nyingine kwa kupitia dirishani, ameshindwa kunasuka. Alikuwa akisema miguu imeganda kama vile imepakwa supagluu."
Wakati wanazungumza hayo muda nao ulikuwa siyo rafiki yao kwani majogoo yalianza kuwika kuashiria kuwa kunakucha.

"Sasa jamani tumeshaumbuka, tufanye nini?" alihoji mama mkwe.
"Hakuna cha kufanya, tungoje jua lichomoze tuone mwenye nyumba atafanya nini," alisema kiongozi wa wachawi.

Akaongeza: "Cha kufanya kila mmoja arudi nyumbani lakini ni muhimu kuwahi eneo la tukio ili kuhakikisha tunamlinda mwenzetu."

"Tutamlindaje wakati amenasa na tumejaribu kumnasua tumeshindwa?" alihoji mwingine.
"Kumnasua kweli tumeshindwa lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa tupo pale kwa sababu siku hizi kuna mtindo mbaya sana wa kuua watu," akasema yule kiongozi.

"Umesema kweli, wote tuwe pale," akadakia mama mmoja ambaye sikumfahamu.
"Unajua tukiwa wote pale tutazuia watu wasimpige au kumchoma moto. Ni hatari sana kama tutamuacha peke yake," alisisitiza yule mchawi kiongozi.

"Lakini mimi sitaweza kwenda pale, nitakuwa nimeumbuka sana," ilikuwa ni sauti ya mama mkwe.
"Sawa, wewe usiende lakini hutaeleweka vibaya?" alihoji kiongozi wao.
"Hapana. Nikiamka tu nitajifanya nina malaria."

Wote walikubaliana kwamba asubuhi wawe eneo la tukio na watu wakijazana basi nao wawe kama mashuhuda lengo kuu ni kuzuia mauaji kwa mwenzao.
"Nenda chumbani kampake dawa ya kumzindua yule baba mwenye nyumba," aliamuru kiongozi wa wachawi.

Haraka sana nilifumba macho huku nikiyafunua kidogo, kwa kuwa kulikuwa na giza hakuweza kuona kuwa naona.
Nilimuona yule mchawi akifungua kibuyu kidogo na kumpaka mume wangu dawa sehemu ya pua.

Itaendelea wiki ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 16
ILIPOISHIA
Asubuhi nyumba ya jirani ilikuwa imejaa watu ambao walikuwa wakipiga kelele.
"Mchawi, mchawi kanasa ndani." Umati ulikuwa mkubwa sana na kelele zikawa nyingi, mume wangu aliamka.

Je, nini kitatokea? Songa nayo:

Baada ya mume wangu kuamka, alifikicha macho kutoa matongotongo machoni kisha akasimama na kujinyoosha mwili.

"Mhhhh… Mama Ajigale, mwili unauma sana," alisema.
"Pole sana, kwani ulifanya kazi gani?"
"Hakuna, vipi mbona kuna kelele huko nje?"
"Nasikia kuna mchawi kanasa katika nyumba ya huyo shoga yangu."
"Shoga yako yupi?"

"Yule aliyekuja hapa nyumbani na kusema atatupeleka kwa baba yake akatufanyie zindiko."
"Acha utani, kwake ameshikwa mchawi?"
"Siyo ameshikwa. Amenasa!"
"Unatania?"

"Husikii kelele huko nje? Njoo hapa dirishani uone."
"Kwani hapo dirishani huyo mchawi aliyenasa anaonekana?"
"Hapana …uje uone watu walivyojazana nje ya madirisha."
Mume wangu alifika dirishani.

"Kwa kuwa yule mama mwenye nyumba ni rafiki yako nenda kamuone," aliniambia, bila ajizi nilijitanda kitenge changu na kwenda kujionea japokuwa picha nzima nilikuwa naijua kutokana na kusikia waliyokuwa wakiyafanya wachawi usiku hapa nyumbani kwangu.
Nilifika pale na yule shoga yangu aliponiona aliniita pembeni akaanza kunisumulia:
"Unajua mama Ajigale, kama nilivyokuambia jana kuwa nyumbani kwako kuna wachawi wanakuja kila siku usiku huku wengine wakitumia ungo."

"Nakumbuka uliniambia hivyo tena mbele ya mume wangu, huyo aliyenaswa ni nani?" Nilianza kumpeleleza.

"Shoga namjua basi? Labda wewe ukimuona unaweza kumfahamu."
Jirani yangu huyo alinipenyeza licha ya kuwepo watu wengi, walimpisha kwa kuwa walikuwa wanajua kuwa yeye ndiye mama mwenye nyumba, huku nami nikijitahidi kumfuata.
Tulifika ndani ya nyumba na kumkuta mchawi akiwa bado ameganda katikati ya sebule huku watu wakiwa wamejazana kwenye madirisha ili waweze kumuona, alikuwa amevaa kaniki kiunoni.
"Ua, mchawi huyo, ua, mmwagie mafuta ya taa, achomwe moto," yalikuwa ni maneno ya watu waliokuwa wamefurika nje ya nyumba hiyo.

Niliingiwa na hofu kubwa hasa niliposikia watu wengine wakisema mchawi yule achomwe moto.
Lakini hata mume wa rafiki yangu niliona ana wasiwasi baada ya kusikia maneno hayo kwani alianza kuhangaika kupigia simu watu ambao mimi sikuwajua.

"Jamani njooni haraka wasije kumdhuru huyu mchawi," alisikika akisema.
Nilimuaga shoga yangu nikachomoka kasi kuelekea nyumbani kwangu, njiani nikakutana na mume wangu ambaye alikuwa amevaa bukta, fulana na makubazi miguuni.
"Ehee, huyo aliyenaswa unamfahamu?" simjui, yupo tu pale sebuleni anang'aang'aa macho."
"Sasa wenye nyumba wanasemaje?"

"Baba mwenye nyumba nimemuona akihangaika kupiga simu kwa watu ambao siwajui, anawaambia waje kumnasua mchawi."
"Amepiga simu polisi?"
"Sijui."

"Lakini akishafika huyo mtu akamnasua, huyo mchawi atapita wapi? Ni wazi atauawa palepale nje ya nyumba yake ni vema akaita kwanza polisi."
"Hilo naona hajakumbuka, amepaniki, ni vema ukawahi kumpa ushauri huo."
"Hapana turudi sote tukatoe ushauri kwa pamoja."

Nilikubaliana na mume wangu hivyo nikageuza njia na kuanza kuelekea tena kwa jirani yetu.
Tulipofika watu ndiyo walizidi, bahati nzuri tulikuta kuna waandishi wa habari wa Gazeti la Uwazi ambao baada ya kutuona walitukabili.

"Mama samahani, mimi ni Chande Abdallah na huyu ni bosi wangu Makongoro Oging' waandishi wa gazeti la Uwazi, tumeambiwa wewe ulikuwa ndani, unamfahamu huyo mchawi aliyenaswa?"
"Kaka mimi huyo aliyenaswa kweli nimemuona lakini simfahamu kwa jina wala sijawahi kumuona hapa mtaani."

"Lakini watu wanasema wewe na mama mwenye nyumba ni marafiki, je, umeonana naye na mmeshauriana nini?"

Je, kilifuatia nini? Usikose kusoma kisa hiki cha kusisimua Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE - 17

ILIPOISHIA
Bahati nzuri tulikuta kuna waandishi wa Gazeti la Uwazi ambao baada ya kutuona walitukabili.
Mama samahani, mimi naitwa Chande Abdallah na huyu ni bosi wangu Makongoro Oging, waandishi wa Gazeti la Uwazi, tumeambiwa wewe ulikuwa ndani, unamfahamu huyo mchawi aliyenaswa?"
Kaka huyo mchawi aliyenaswa kweli nimemuona lakini simfahamu kwa jina wala kwa sura, sijawahi kumuona hapa mtaani."

"Lakini watu wanasema wewe na mama mwenye nyumba ni marafiki, je, umeonana naye na mmeshauriana nini?"
SASA SONGA NAYO..
"
Tumeshauriana kwamba waitwe polisi."
"Polisi wataweza kumnasua mchawi aliyenaswa?" alizidi kunidadisi Chande na nikagundua kuwa sikumalizia kile nilichokuwa nataka kumfahamisha.

"Ahhh…. Kweli, ni kwamba nimeshauri waitwe polisi kwa usalama wa huyu mchawi kwani kama itatokea akanasuliwa kisha kutolewa nje ya nyumba, ni wazi watu wenye hasira kali watamgombania na kumtoa uhai," nilijibu na Chande akawa anaandika kwenye kijitabu chake.
Niliwaacha waandishi hao na kwenda kwa mama mwenye nyumba ambaye alikuwa na mumewe nami na mume wangu.

Mume wangu alipewa jukumu la kuita polisi naye akapiga namba 112 na polisi wakaitikia.
"Polisi naini, naini hapa, tukusaidie nini?" Simu ilisikika kwa sababu aliweka spika ili tusikie wote tuliokuwa tumemzunguka.

"Hapa Mtaa wa Pwiriri, kuna mchawi amenaswa."
"Sawa, sasa mnataka msaada gani kwa sababu sisi polisi hatuwezi kumnasua!"
"Hapana msaada wetu ni kwamba tunataka mje kulinda usalama wake na wa mali pia kwa kuwa watu wanatishia kumlipua kwa mafuta ya taa. Sasa wakifanya hivyo akiwa ndani ni wazi kwamba vitu vingi pamoja na nyumba vitatekelea, tafadhalini njooni," alizidi kuomba mume wangu.
"Nimekuelewa, tunakuja," alisema polisi huyo na kukata simu.

Nje ya nyumba fujo zilizidi na wakati tunatafakari nini cha kufanya, aliingia mtu mmoja ambaye alikuwa ni mzee wa makamo.
"Baba karibu sana. Umekuja na teksi?" alihoji mwenye nyumba.
"Ndiyo," alijibu mzee huyo.
"Sawa. Shilingi ngapi anataka?"
"Nimeshamlipa," alijibu mzee.

"Jirani zangu huyu ni baba yangu mzazi na ndiye aliyenitengenezea nyumba hii ili wachawi wasiingie," akatutambulisha.

"Shikamoo baba," tulijishitukia mimi na mume wangu tukimuamkia kwa pamoja kama vile kuna mtu alituamuru kufanya hivyo.

"Mzee hawa ni jirani zangu, baba na mama Ajigale, tunaishi nao vizuri. Ilikuwa tuwalete kwako Jumapili ijayo ili kuwazindikia nyumba yao," alisema baba mwenye nyumba.
"Bado hamjachelewa, walete tu. Tumalize kwanza hili lililonileta," akasema.
"Hapana baba tusubiri kwanza polisi. Si unaona jinsi fujo zilivyotanda hapo nje?"

Kabla hajajibu lolote tulisikia ving'ora vikilia nikajua kwamba hao ni polisi wanakuja. Hata hivyo, nilishanga kusikia ving'ora vya magari mawili nikajiuliza kwa nini wamekuja na magari mawili kana kwamba kuna fujo tayari zimefumuka.

Nilichungulia dirishani nikaona kumbe walikuwa wameongozana na gari la Kikosi cha Zima Moto.
Watu waliokuwa wamejazana mlangoni akiwemo mama mkwe wangu walipisha na kuweka njia bila hata kuamrishwa baada ya kumuona mkaguzi wa polisi yaani Inspekta Kijo akija ndani pamoja na maofisa wengine wa polisi.

Aliingia akiwa na askari sita wote wakiwa na silaha za kivita, Semi Machine Gun (SMG).
"Nani mhusika mkuu hapa," alisema Inspekta Kijo.
"Ni mimi hapa, hawa ni jirani zangu na huyu ni mke wangu," alijibu baba mwenye nyumba.
"Huyu ndiye mchawi aliyenasa hapa?"
"Ndiyo."

"Ina maana hawezi kujisogeza kabisa?" aliuliza swali yule inspekta wa polisi, swali ambalo halikuwa na jibu kwa sababu alimuona na kama angeweza kujisogeza tusingesema alinasa.
"Sasa mtamnasuaje?" aliuliza tena.

"Yupo mtu wa kumnasua, huyu baba yangu, tulikuwa tunawangoja nyinyi mje kwa usalama wa huyu mchawi. Tulifikiri kama tungemnasua bila nyinyi kuwepo, watu wenye hasira wangeweza kumuua."

Itaendelea wiki ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -18

ILIPOISHIA
Mzee wa baba mwenye nyumba alichukuwa dawa nyeusi na kuichanganya kwenye maji kisha kummwagia yule mchawi aliyenasa ndani miguuni mara tatu, akamsukuma na akapepesuka, ikawa tayari amemnasua.

‘Ua mchawi huyoooo, chinja, piga maweee," zilikuwa ni kelele za wananchi waliokuwa wamejazana nje ya nyumba.
SONGA NAYO...

Polisi wanne wenye silaha ilibidi watoke nje na kuwatawanya watu wenye hasira. Hata hivyo, bado watu walikuwa wabishi kuondoka ndipo askari mmoja akalipua bomu la machozi.
Moshi ulifumuka na kujaa nje lakini mwingine uliingia ndani na kutufanya nasi kububujikwa na machozi kutokana na muwasho wa moshi huo ulipoingia machoni.

Wakati watu wanakimbia huku na huko kutona na woga wa kishindo cha mlio wa bunduki na moshi wenye pilipili, polisi walitumia mwanya huo kumtoa ndani mchawi na kumuingiza katika gari lao, ‘Difenda'.
Walimchukuwa na mzee wa baba mwenye nyumba ile na mmiliki wa nyumba na mkewe. Mimi nilishauriwa na mume wangu nimsindikize jirani yangu kwa kuwa ni shoga yangu.

Tulifika polisi na kukuta makamanda na askari wengine wa vyeo vya chini wakitusubiri kwa kuwa habari ile ilisambaa kwa kasi kubwa mji mzima. Wote tuliingizwa katika chumba kimoja pale polisi na tukaketi kwenye viti. Yule mchawi aliambiwa asimame, akaanza kuhojiwa.

"Wewe mchawi unaitwa nani?" alihoji afisa mmoja wa polisi huku akiandika kwenye jalada.
"Naitwa Pimbi Msafiri,"
"Unaishi wapi?"
" Nangose."

"Dini yako?"
"Mpagani."
"Hebu eleza ulifikafikaje katika nyumba uliyokutwa na ilikuwaje ukakutwa ndani katika nyumba ya watu?"
"Mimi nilialikwa na wachawi wenzangu pale Kijiji cha Nangose na wakaniambia kuwa tuna safari ya mbali. Tuliambiwa tutasafiri kwa ungo. Wakasema mwenyeji wetu huko ni bibi wa Ajigale.

"Mimi sikumjua huyo bibi na hakika nilikuwa kama bendera fuata upepo…"
Yule askari polisi alitugeukia sisi.
"Jamani ile nyumba ndiyo anayoishi bibi wa Ajigale?" akauliza askari.
"Hapana. Hiyo nyumba ni ya huyu mama jirani yangu," alisema shoga yangu huku akinyoosha mkono kuelekeza kwangu. "Na huyu ndiye mama Ajigale."

"Sasa wewe mchawi mbona unataka kunichanganya? Nakuuliza uliingiaje pale uliponasa, unasema mambo ya nyumba nyingine, ohoo, usinichezee," alifoka.
"Hapana afande, nakuja hukohuko. Nimeanza mwanzo ili unielewe."
"Endelea."

"Lengo la safari ilikuwa kwenda kufanya uchawi katika nyumba ya akina Ajigale. Sasa tuliondoka kwa ungo kutoka Nangose na baada ya kufika kwa bibi wa Ajigale, alitoa mashitaka kuwa mama wa nyumba niliyoingia alitangaza kuwa huwa anatuona kila tunapofika pale usiku."
"Kwani huwa mnafika mara kwa mara?"
"Ndiyo, huwa tunafika mara nyingi."

"Mkifika huwa mnafanya nini?"
"Hakuna cha maana tunachokifanya. Huwa tunamchukuwa mwenye nyumba na kwenda naye makaburini."
"Makaburini kufanya nini?"

"Si ndiyo uchawi wenyewe? Tunakwenda kumchezea maana kwa kufanya hivyo mama yake yaani bibi wa Ajigale hufurahi."
"Anafurahia kitendo hicho cha kumchukuwa mwanaye?"
"Ndiyo na anasema anataka amfundishe uchawi ili akifa arithi mkoba wake wa kichawi."
"Akitataa je?"

"Hawezi kukataa, atapumbazwa kwanza kwa dawa za kichawi kabla ya kuambiwa uamuzi wa mama yake, angezidi kukataa, hakungekuwa na namna nyingine zaidi ya kumfanya kitoweo."
"Mlikuwa hamumuogopi mkewe wakati mnamchukua?"
"Mkewe tulikuwa tunamtia dawa ya usingizi, kwa hiyo tukimchukuwa mumewe alikuwa haoni na hata mumewe alikuwa hajui kinachoendelea."

Aliposema hayo niliishiwa nguvu kwa kuona hatari ambayo mume wangu anataka kufanyiwa na mama yake, kwamba angekataa uchawi, angeliwa nyama yake? Hilo lilinitisha zaidi.
Lakini mchawi yule hakujua kuwa mimi nilikuwa sipumbaziki na dawa zao, nilikuwa naona kila kitu kama nilivyosimulia hapo mwanzo.

"Sasa ikawaje mkaenda nyumba ya jirani?"

Je, kilifuatia nini pale polisi? Usikose simulizi hii ya kusisimua Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -19
Mwandishi Elvan Stambuli
ILIPOISHIA
"Mkewe tulikuwa tunamtia dawa ya usingizi, kwa hiyo tukimchukuwa mumewe alikuwa haoni na hata mumewe alikuwa hajui kinachoendelea."

Aliposema hayo niliishiwa nguvu kwa kuona hatari ambayo mume wangu anataka kufanyiwa na mama yake, kwamba angekataa uchawi, angeliwa nyama yake. Hilo lilinitisha zaidi.
Lakini mchawi yule hakujua kuwa mimi nilikuwa sipumbaziki na dawa zao, nilikuwa naona kila kitu kama nilivyosimulia hapo mwanzo.
"Sasa ikawaje mkaenda nyumba ya jirani?"
SONGA NAYO...

"Ilikuwa tunakwenda kuwanyamazisha kwa sababu Bibi wa Ajigale (mama mkwe wangu), alisema kesho yake wangekwenda kwa mzee wao ili awape dawa ya zindiko la nyumba ya Baba Ajigale kitu ambacho bibi hakupenda. Nilitumwa nikawamalize."

Maneno hayo yalimtia hasira mume wa shoga yangu na nilikuwa namuona dhahiri alikuwa akitetemeka pale alipokuwa ameketi. Naamini ingekuwa pale siyo kituo cha polisi, angemrukia na makubwa yangetokea.

Jibu lile lilimfanya polisi aliyekuwa akichukuwa maelezo ageuze shingo na kutuangalia kama vile ni mtu aliyekuwa anasema kimoyomoyo ‘mngemalizwa nyie'. Akaendelea kumhoji:
"Ukawamalize kwa kutumia silaha gani?"

"Tulikuwa na mabomu ya kichawi, alikuwa ameyachukuwa Bibi wa Ajigale."
"Mlilipua hilo bomu?"

"Hapana, huwa ni la kutegea mlango wa chumbani na mimi ndiye ilikuwa nikifika mlango wao wa chumbani, bibi anikabidhi kisha nimalize kazi. Lakini kabla hata sijakaribia mlango wa chumba, nikiwa sebuleni nikanasa. Nilijikuta siwezi kusogeza mguu wala kurudi nilipotoka. Hayo ndiyo maelezo yangu."
Yule afande aliyekuwa akimhoji alimpa kusaini kila karatasi aliyoandika maelezo yake naye alifanya hivyo huku akitetemeka.

Polisi aligeuka na kutuangalia kwa mara nyingine. Alisimama na kujinyoosha kisha alimuita askari mmoja ambaye hakuwa na cheo chochote, wenyewe huwaita praiveti akamuamuru amchukue yule mchawi Pimbi Msafiri akamfungie mahabusu.

"Sasa mzee njoo nawe nipate maelezo yako. Jamani huyo bibi anayetajwa mnamjua?" aliuliza yule Inspekta wa polisi.
"Ni mama mkwe wake huyu mama," yule baba mwenye nyumba jirani yangu akajibu huku akinyoosha kidole kuelekeza kwangu.

"Duh, mama mpo salama hapo kwenu kweli?"
Niliona aibu sikujibu swali hilo kwa sababu ukweli ni kwamba mimi pia nazozana mara kwa mara na mama mkwe wangu kutokana na tabia yake ya kishirikina na hasa alipogundua kuwa kuna mpango wa kwenda kwa mzee wa jirani yangu akatupe dawa ya zindiko ili tuizindike nyumba yetu baada ya wao kugundua kuwa wachawi walikuwa na kawaida ya kuja usiku kutuwangia.

Baba mwenye nyumba baada ya kuhojiwa jina lake na kabila pamoja na dini yake, mahojiano na polisi yalikuwa hivi:"Mzee uliamua uwapeleke jirani zako kwa baba yako akafanye zindiko kwenye nyumba yao, kwa nini ulivutika kufanya hivyo?"

"Nilivutika kwa sababu niliona jirani zangu wanateswa na wachawi kila siku usiku."
"Wewe ulikuwa ukiwaona hao wachawi?""Ndiyo. Nilikuwa nawaona na mara nyingi tulikuwa tunaamshana na mke wangu na kushuhudia vituko vyao bila wao kutuona. Tulipoona wamezidisha vituko tukawa tunaacha taa zetu bila kuzima ili waingiwe na woga, lakini wakawa hawajali."
"Ukafanyaje?"

"Nilimtuma mke wangu huyu akawaambie na alipowaambia mama mkwe wake huyu mama alikuwepo ndipo usiku wa leo walipoamua kutuangamiza kama mchawi Pimbi alivyokueleza. Hawakujua kuwa nyumba yetu imezindikwa na siyo rahisi mchawi kuingia na kuleta madhara. Hayo ndiyo maelezo yangu."

Mzee huyo alisainishwa na polisi maelezo hayo. Yule askari alisema tusubiri kidogo kwani anakwenda kwa mkuu wa kituo kumpa taarifa na kupata maelekezo yatakayofuata. Hakuchelewa alirudi akasema:
"Tumekubaliana kwamba bibi naye akakamatwe, ahojiwe. Hivyo, mzee kaingie kwenye gari ‘difenda' la polisi ukatuoneshe nyumba tukamtie mbaroni."

Je, nini kitaendelea? Fuatilia mkasa huu wa kusisimua wiki ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -20
ILIPOISHIA
Mzee huyo alisainishwa na polisi maelezo hayo. Yule askari alisema tusubiri kidogo kwani anakwenda kwa mkuu wa kituo kumpa taarifa na kupata maelekezo yatakayofuata. Hakuchelewa alirudi, akasema:"
TUMEKUBALIANA kwamba bibi naye akakamatwe, ahojiwe. Hivyo, mzee kaingie kwenye gari ‘difenda' la polisi ukatuoneshe nyumba tukamtie mbaroni."

Mzee mwenye nyumba aliingia kwenye gari lakini mimi pia kwa kuwa majirani walisema ndiye ninayeishi naye niliambiwa niwemo kwenye msafara.
"Lakini mume wangu ambaye ndiye mama yake yupo nyumbani, nendeni tu mtamkuta," nilijitetea kukwepa kwenda kumkamata mama mkwe wangu.
"Hapana mama, mambo ya wanaume huyajui, tunaweza kufika pale tukakuta huyo mumeo hayupo," alisema askari polisi.

"Mama twende tu, tutarudi wote."
"Basi kama ni hivyo tuondoke na mkeo," nikashauri.
"Sawa, twendeni kwani gari hili lina nafasi kubwa."
Mwendo wa gari haukuwa mrefu kwa sababu dereva aliwasha king'ora, hivyo magari barabarani yakawa yanatupisha.

Tulifika nyumbani tukamkuta mume wangu akiwa ameketi nje ya nyumba na mama mkwe alikuwa ndani.
Mume wangu macho yalimtoka kutokana na kusikia king'ora cha gari la polisi likiwa na askari wawili likisimama mbele ya nyumba yetu.
"Mzee habari za hapa?" askari kiongozi wa msafara alimsalimia mume wangu.
"Nzuri jamani, kuna nini?"
"Tumekuja kumchukuwa mama yako."
"Mama?"

"Ndiyo anahusika na…?"
"Anahusika na nini wakati tukio linatokea alikuwa hapa nyumbani?"
"Hapana. Ametajwa na yule mchawi aliyenasa ambaye tunamshikilia kituoni."
"Mchawi?"

"Kwani mzee huna habari kwamba hapo kwa jirani yako kuna mchawi leo usiku amenaswa?"
"Najua na mke wangu nimemuagiza amsindikize shoga yake."
"Yupo kwenye gari na shoga yake. Alijaribu kukataa tusije naye lakini nimemlazimisha na tunaye kwenye gari pamoja na majirani zako."

"Ahaa, mke wangu shuka basi tujadili kabla mama hajachukuliwa," akasema.
"Mzee huo siyo utaratibu, lakini muite na mzungumze," alielekeza yule askari.
Nilishuka na kumfuata mume wangu. Tuliingia ndani na kumkuta mama mkwe akiwa ametoa macho kama vile amekabwa.

"Ehee huko polisi mambo yalikuwa vipi?" aliniuliza mume wangu kwa kunong'ona ili askari aliyekuwa nje ya nyumba yetu asiweze kutusikia.
"Yule mchawi kamtaja. Kasema walikuwa na mama mkwe lakini yeye ndiye aliyeingia ndani na mama akabaki nje," nami nilimnong'oneza.
"Hakuna njia, inabidi tumsindikize."

Tulitoka nje tukiwa na mama, kama ilivyo ada, watu wakajaa tele nje ya nyumba yetu wakitaka kujua kwa nini polisi wamefika tena kwa king'ora.Watu walizungumza mengi, wengine wakisema mama mkwe ndiye aliyesababisha yule mchawi anase, wengine wakawa wanasema naye aliingia ndani lakini kwa kuwa ni ‘mzima' kishirikina, alichomoka na kumuacha yule mchawi kijana akiwa ameng'ang'ana sakafuni.

Lakini wapo waliopatia na kusema kwamba mama mkwe wangu alimsindikiza yule mchawi kuwamaliza wale majirani huku wengine wakimtoa kabisa na kuona kuwa yeye alikwenda kuwaonesha nyumba tu ili mchawi amalize kazi kwa wale jirani.

Mazungumzo hayo watu walikuwa wakiyasema kwa sauti na sisi wote tulikuwa tukiyasikia waziwazi na kumuongezea hofu mama mkwe wangu ambaye alikuwa hajui hasa atakachofanywa polisi.
Nilimuangalia nikamuona anatetemeka kama vile alikuwa anaumwa malaria kali kwani hata kanga ilikuwa inamshinda kuifunga ikawa inaanguka, uzuri ni kwamba ndani alikuwa na gauni refu.
Ilibidi kila wakati nimfuate na kumfunga vizuri kanga yake iliyokuwa ikianguka wakati tunakwenda kupanda gari la polisi.

Kabla sijapanda gari nilimuuliza mume wangu kama mtoto wetu Ajigale alikuwa ndani au la kwa sababu alitakiwa aende shule, akasema alimkodishia teksi na tayari ameshafika shuleni kwa sababu aliwasiliana na mwalimu wake wa darasa akamjuza.

Mama mkwe aliingizwa kwenye gari nami nikamfuata lakini mume wangu alikuwa akitufuata kwa nyuma akiwa kwenye gari lake.Kama tulivyokuja nyumbani, safari ya kurejea polisi ilikuwa fupi tulifika na kukuta watu kibao wakiwa wanangoja ili wajue kitakachoendelea.

Je, nini kitafuata? Fuatilia mkasa huu wa kusisimua Jumanne ijayo
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -21

Mama mkwe aliingizwa kwenye gari nami nikamfuata lakini mume wangu alikuwa akitufuata kwa nyuma akiwa kwenye gari lake.
Kama tulivyokuja nyumbani, safari ya kurejea polisi ilikuwa fupi tulifika na kukuta watu kibao wakiwa wanangoja ili wajue kinachoendelea.
SONGA NAYO...

Nje ya kituo cha polisi walikuwepo watu wengi mno kuliko wale tuliowaacha, habari zilishazagaa kwamba kuna mchawi amenasa kwenye nyumba moja na amepelekwa polisi.
Gazeti la Uwazi nalo likawa limetoa habari kuhusiana na mkasa huo ukurasa wa mbele. Lilikuwa limeandika kwa wino uliokolezwa ‘Mchawi anaswa laivu'.

Bila shaka toleo lile lilikuwa maalum kutokana na habari yenyewe jinsi ilivyosisimua, nadhani bodi ya uhariri ikaona itoe habari ile ikisindikizwa na picha kibao zilizoenea ukurasa wote wa kwanza.
Naamini gazeti hilo lilichangia kufanya watu kujaa pale kituo cha polisi.

Mara baada ya gari la polisi kuingia kituoni, watu walilisogelea ili kumuona mchawi, hawakujua kuwa alikwisha ingizwa selo.

"Yupo wapi, yupo wapi," zilikuwa ni kelele za watu waliotaka kushuhudia.
Baadhi ya watu walidhani mchawi aliyenasa ni mama mkwe, lakini wengine wakawa wanabisha na kusema kwamba aliyenaswa ni mwanaume.

Gazeti ndilo lililokuwa likiaminiwa kwa hiyo niliona baadhi ya watu wakikusanyana kwenye makundi na kusoma mstari kwa mstari habari iliyoandikwa na Makongoro Oging' na Chande Abdallah kwenye kurasa za gazetini.

Tuliingia ndani ya chumba cha mahojiano na mama mkwe alianza kuhojiwa.
Baada ya kuulizwa jina lake na umri akaambiwa aanze kusimulia mkasa wa usiku uliosababisha yule mchawi anase kwenye nyumba ya watu.

"Ni kweli huyu mchawi alikuja nyumbani na wenzake na akataka afanye dawa kwenye nyumba ya huyu jirani, (akinyoosha kidole kuelekea kwa mwenye nyumba."
Polisi aliandika na baada ya kuona yupo kimya anasita kuendelea akamhoji:
"Ehee, ikawaje bibi?"

"Baadaye tulipofika kwenye nyumba, nilimuambia aingie yeye kwa sababu ndiye aliyekuwa na dawa za kutia ndani ya nyumba ile."
"Kwani dawa zile zilikuwa za nini?"
"Dawa za kudhuru."

"Kudhuru nini au nani?"
"Dawa za kudhuru watu."

"Kwa nini mlitaka mdhuru watu ambao hawajawakosea?"
"Ilikuwa ni amri ya mkuu wa wachawi."
"Mkuu wa wachawi? Ni nani huyo?"
"Anaitwa mzee Ngwamba."

"Mzee Ngwamba anaishi wapi?"
"Anaishi Kijiji cha Mabatani."

"Kwa hiyo wewe hujui sababu ya mzee Ngwamba kuamuru watu waliokuwa katika nyumba jirani kuwekewa dawa ya kuwadhuru?"
"Najua."
"Tueleze basi."

"Ni kwamba huyu bwana (alinyoosha mkono kumuelekeza askari aliyekuwa akihoji kwa baba mwenye nyumba ya jirani), alikuja pale nyumbani na mkewe, akawakuta mwanangu na mkwe wangu, akasema kuna wachawi wanakuja pale nyumbani kila siku."
"Ehee, baada ya kusema hivyo?"

"Huyu baba akasema baba yake anajua dawa ya kinga au zindiko la nyumba, hivyo alimuahidi kwamba leo angewapeleka."

"Kwa hiyo mzee Ngwamba alijuaje hayo?"
"Ni mimi nilimuambia."
"Na aliposikia hilo akasemaje?"

"Ndipo akaamuru kuwa wakawekewe dawa ili wamalizwe wasiweze kuwapeleka hawa kwa baba yake."
"Wewe mbona hujanasa, uliingia ndani ukatoka salama?"
"Hapana, mimi sikuingia, niliishia nje aliingia yule kijana tu, kazi yangu ilikuwa kuonesha nyumba ya hawa jirani."

"Baada ya hapo ikawaje?"
"Alipoingia ndani tu, akaniambia kuwa hawezi kunyanyua mguu kwenda mbele wala kurudi nyuma, kuona hivyo nilirudi nyumbani kumuambia mzee Ngwamba."

"Mzee Ngwamba baada ya kupata taarifa hizo alifanya nini?"
"Alitoa dawa akasema tukammwagie yule aliyenasa, tulikwenda lakini hakunasuka."
"Ehee, ikawaje?"

"Zilifanywa kila mbinu kwa kutumia dawa mbalimbali ili kumnasua lakini zote ziligonga mwamba ndipo wakaamua kuwa aachwe tu maana ilishindikana kumtoa."
"Asubuhi mambo yakawaje?"

"Nilimsikia mama mkwe wangu huyo hapo akimuamsha mwanangu na kumfahamisha kuwa kuna mchawi kanaswa, kachungulia dirishani na nikawa nasikia kelele nyingi za watu nikajua mambo yameharibika."

Mama mkwe kaamua kusema ukweli, hakuficha kitu, je nini kiliendelea?

Fuatilia mkasa huu wa kusisimua Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -22

"Alitoa dawa akasema tukammwagie yule aliyenasa, tulikwenda lakini hakunasuka."
"Ehee, ikawaje?""Zilifanywa kila mbinu kwa kutumia dawa mbalimbali ili kumnasua lakini zote ziligonga mwamba ndipo wakasema aachwe tu maana imeshindikana kumtoa."
"Asubuhi mambo yakawaje?"

"Nilimsikia mama mkwe wangu huyo hapo akimuamsha mwanangu na kumfahamisha kuwa kuna mchawi kanaswa, wakachungulia dirishani na nikawa nasikia kelele nyingi za watu nikajua mambo yameharibika."
SONGA NANYO...

Maelezo mengi ya mama mkwe yalikuwa yakishabihiana na ya yule mchawi aliyenaswa. Lakini polisi walitaka kujua zaidi kuhusu lengo lake la kualika wachawi kuja nyumbani kwa mtoto wake.

"Sikuwa na lengo lingine isipokuwa nilitaka afundishwe uchawi ili nikifa aweze kurithi mikoba yangu," alisema mama mkwe hali iliyomfanya mwanaye, yaani jirani yangu kutokwa na jasho japokuwa kulikuwa hakuna joto pale ndani ya kituo cha polisi.

"Mama ina maana ulikuwa unataka unifundishe uchawi mama!" alidakia jirani yangu.
"Usiingilie mahojiano mzee. Elewa kwamba hapa ni polisi au niwatoe nje ya kituo?"
"Hapana. Nimeshangaa kumsikia mama anasema hayo aliyoyasema wakati mimi sijui chochote kuhusu hilo. Kama hivyo ndivyo mbona hakuniambia lolote baada ya tukio na kabla?"
"Mzee tuliza mori," alisisitiza polisi.

"Au niwatimue wote?"
Nilitamani nimnyamazishe yule jirani yangu kwa kuona kuwa tukitimuliwa, hatutajua mengi zaidi kuhusu kundi lile la wachawi.

"Sasa kwa nini mwanao hujamjulisha kuhusu ujuzi wa uchawi uliotaka arithi?"
"Ndiyo maana walikuwa wakija nyumbani wachawi wenzangu ili kumchukuwa na kujaribu kumpumbaza akili ili baadaye nikimuambia asipinge."

"Kwa hiyo ulijua kuwa ukimuambia angengataa?"
"Najua kabisa kuwa kama ningemuambia akiwa na akili zake timamu angekataa. Mara nyingi tuna uzoefu ni watu wachache sana ambao wakiambiwa watapewa uchawi wanakubali. Hawa wasomi huwa hawakubali na zaidi huwa wakali. Hawataki kabisa kusikia habari hiyo."

"Sisi polisi tuliambiwa mlitaka kuwaua jirani zenu hawa (huku akiwageukia wale jirani zetu) na ndiyo maana mkaenda kuingia ndani ya nyumba yao japokuwa wewe hukuingia. Hamkuona kuwa hilo lilikuwa kosa kubwa la kuua na kuingia nyumba ya watu?"

"Ni kweli mwenzangu aliingia ndani ya nyumba na akanasa kama mlivyomuona, mimi nilikaa nje, sikuingia, ilikuwa bahati yangu.""Kwani mnapofanya uchawi, mnapata faida gani?
Swali hilo mama mkwe hakujibu, alimuangalia yule polisi kisha akainamisha kichwa chini.
"Sasa itabidi tuwapeleke mahakamani, mama unasemaje?"

"Unataka nifungwe? Utapata faida gani? Acha kuwa na roho hiyo mwanangu!"
"Achana na faida, kwani wewe ulipokuwa ukifanya mambo haya ya ulozi ulikuwa unapata faida gani?"
Yule polisi aliyekuwa akimhoji mama mkwe aliandika mambo fulani kwenye jadala ambalo alikuwa analitumia kunakili mahojiano.

Alimuangalia mama mkwe kisha mwanaye na akanyanyua mkono wa simu ya mezani. Nilikuwa karibu naye nikaona anabonyeza namba moja, mbili nne kisha akaiweka sehemu ya kusikilizia sikioni.
"Mwambie Koplo Beti aje ofisini kwangu." Jibu la upande wa pili sikulisikia lakini yeye akajibu.
"Ndiyo, aje amchukue huyu bibi, mwambie achukue ufunguo wa mahabusu."

Nilijua kuwa huyo Koplo Beti alikuwa anakuja kwa ajili ya kazi moja; kumchukua mama mkwe na kwenda kumtupa mahabusu.Mama ni mama, nilimuona mume wangu akitetemeka baada ya yeye kujua kuwa mama yake anakuja kuchukuliwa na kwenda kufungiwa mahabusu.

Moyoni nilikuwa na furaha sana kuona sheria inaanza kufuata mkondo wake. Nilikuwa nawaza kama wangefanikiwa kumfanya mume wangu mchawi na kumrithisha mikoba ya kichawi mambo yangekuwaje.
Niliamini kuwa lile litakuwa fundisho kwake na wote ambao watasikia habari ile kupitia vyombo vya habari.
Wakati nawaza hayo, yule Koplo Beti akawa amefika.

Je, nini kilijiri? Fuatilia mkasa huu Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -23

Wakati nawaza hayo, yule Koplo Beti akawa ameshafika.
"Jambo afande?" akasalimia huku akipiga guu chini na kutoa saluti kwa mkuu wake wa kazi.
"Mchukue huyu bibi, kamfungie lokapu mpaka nitakapotoa maelekezo mengine."
"Haya bibi inuka, songa mbele," aliamuru yule askari wa kike.
Mama mkwe kwanza alionekana dhahiri kwamba alikuwa akishindwa kuinuka bila shaka kutokana na wasiwasi wa kwenda kufungiwa selo.
SONGA NAYO...

Mama mkwe na yule mchawi aliyenasa kwenye nyumba ya jirani wakawa wameshafungiwa lokapu.
Mume wangu alijitahidi kuomba kwa kamanda wa polisi ili mama yake asiwekwe ndani na badala yake amuwekee dhamana alishindwa.

"Unajua mzee, hatumuweki ndani huyu bibi ili kumkomoa, tunamuweka tukiwa na maana yetu," alisema yule kamanda wa polisi."Nakuomba sana kamanda, kwa nini asiende kulala nyumbani na kesho nikamleta?" alizidi kuomba mume wangu.

"Sisi jeshi la polisi hatufanyi kazi kwa kubabaisha. Ni kwamba, kutokana na tukio analohusishwa nalo kuna taarifa za kintelejensia watu wenye hasira kali wanamsubiri ili wampige. Wanaweza kuchoma moto nyumba yako na ukapata hasara mara mbili.

Kuuawa kwa mama yako na kupoteza mali kwa kuchomwa nyumba na vitu vyako. Hatuwezi kujua. Wanaweza kujichukulia sheria mkononi usiku mkiwa mmelala."
"Sasa ina maana nimuache hapa polisi siyo?"

"Ndiyo maana yake. Elewa tukimuachia na balaa likazuka huko kwako, wakubwa wetu watatuona hatukutumia ujuzi wetu wa miaka mingi katika kazi hii, naomba sana usituponze na usijiponze pia."
"Ukimpa dhamana sitampeleka nyumbani, nitamhamishia kwa mtu mwingine, naomba sana."

"Mzee unasema tu, huko nje umechungulia? Kuna watu kibao wanasubiri kuwaona hawa. Wapo wenye magari na waendesha bodaboda. Watakufuatilia kwa nyuma kwa hiyo usitake kuhamishia tatizo hili katika nyumba ya mtu mwingine," alisema yule kamanda huku akifunika jalada la kesi hiyo, akainuka na kuliweka kabatini.

Tuliangaliana na mume wangu baada ya jibu la kamanda, akilini mwangu nilijisemea kwamba anachosema kiongozi huyo ni kweli kabisa, kwani nje ya kituo cha polisi kulikuwa na umati wa watu waliokuwa wakiimba; "Tunataka watolewe, wachawi hao, tuwaue."

Nilitishika sana kusikia maneno hayo ambayo yaliashiria kuwa watu walikuwa na hasira kubwa kwa mama mkwe na yule kijana mchawi aliyenasa ndani ya nyumba ya jirani.
Yule kamanda aliondoka ofisini kwake baada ya kulifungia jadala la maelezo ya mama mkwe na yule mchawi mwenzake na alituacha tukiwa mle ndani.

"Baba Ajigale unasikia huko nje, tutafakari sana kuhusu huyu mama, wanaweza kumuua hawa," nilimshauri mume wangu."Ni kweli mke wangu, nadhani tukubaliane na haya wanayosema polisi, tusing'ang'anie kumtoa."

Hakukuwa na njia nyingine isipokuwa kumsubiri kamanda ili tumuage na tuondoke. Wakati nawaza hili na lile yule kamanda aliingia akiwa na karatasi ambayo nilikuwa sijajua ilikuwa ya nini.
"Mzee, na nyinyi mlioingiliwa ndani na wachawi, mnaweza kwenda na RB ya kesi yenu hii hapa," alisema huku akimpa jirani yetu ile karatasi.

"Tafadhali tueleze utaratibu wa kesho," mume wangu alitaka ufafanuzi.
"Kesho tunatarajia kulipeleka jalada ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka na kama litarudi tutaona watafunguliwa mashitaka gani. Cha muhimu ni kwamba jioni mleteeni chakula bi mkubwa," alishauri yule askari kamanda wa polisi.

Tuliondoka wote wanne, yaani mimi na mume wangu na jirani na mkewe hadi nyumbani. Tulijisikia aibu kutokana na kitendo cha mkwe wetu kwenda kwa jirani na kutaka kuwaangamiza.
* * *
Kulipopambazuka tulijiandaa kumpelekea bibi chai. Nilichemsha chai na maandazi na kuweka kapuni. Tulipofika polisi tulikuta mkusanyiko mkubwa wa askari, walipotuona wote waligeuza shingo zao kutuangalia.

"Mmekuja, jamani njooni ofisini kwangu," alisema yule kamanda wa jana.
Tulipokwenda akatuambia kuwa asubuhi alipokwenda kuwaangalia watuhumiwa waliokuwa lokapu, alikuta mama mkwe amefariki dunia.

Usikose kufuatili simulizi hii ya kusisimua Jumanne ijayo.
 
UCHAWI WA MAMA MKWE -23

Wakati nawaza hayo, yule Koplo Beti akawa ameshafika.
"Jambo afande?" akasalimia huku akipiga guu chini na kutoa saluti kwa mkuu wake wa kazi.
"Mchukue huyu bibi, kamfungie lokapu mpaka nitakapotoa maelekezo mengine."
"Haya bibi inuka, songa mbele," aliamuru yule askari wa kike.
Mama mkwe kwanza alionekana dhahiri kwamba alikuwa akishindwa kuinuka bila shaka kutokana na wasiwasi wa kwenda kufungiwa selo.
SONGA NAYO...

Mama mkwe na yule mchawi aliyenasa kwenye nyumba ya jirani wakawa wameshafungiwa lokapu.
Mume wangu alijitahidi kuomba kwa kamanda wa polisi ili mama yake asiwekwe ndani na badala yake amuwekee dhamana alishindwa.

"Unajua mzee, hatumuweki ndani huyu bibi ili kumkomoa, tunamuweka tukiwa na maana yetu," alisema yule kamanda wa polisi."Nakuomba sana kamanda, kwa nini asiende kulala nyumbani na kesho nikamleta?" alizidi kuomba mume wangu.

"Sisi jeshi la polisi hatufanyi kazi kwa kubabaisha. Ni kwamba, kutokana na tukio analohusishwa nalo kuna taarifa za kintelejensia watu wenye hasira kali wanamsubiri ili wampige. Wanaweza kuchoma moto nyumba yako na ukapata hasara mara mbili.

Kuuawa kwa mama yako na kupoteza mali kwa kuchomwa nyumba na vitu vyako. Hatuwezi kujua. Wanaweza kujichukulia sheria mkononi usiku mkiwa mmelala."
"Sasa ina maana nimuache hapa polisi siyo?"

"Ndiyo maana yake. Elewa tukimuachia na balaa likazuka huko kwako, wakubwa wetu watatuona hatukutumia ujuzi wetu wa miaka mingi katika kazi hii, naomba sana usituponze na usijiponze pia."
"Ukimpa dhamana sitampeleka nyumbani, nitamhamishia kwa mtu mwingine, naomba sana."

"Mzee unasema tu, huko nje umechungulia? Kuna watu kibao wanasubiri kuwaona hawa. Wapo wenye magari na waendesha bodaboda. Watakufuatilia kwa nyuma kwa hiyo usitake kuhamishia tatizo hili katika nyumba ya mtu mwingine," alisema yule kamanda huku akifunika jalada la kesi hiyo, akainuka na kuliweka kabatini.

Tuliangaliana na mume wangu baada ya jibu la kamanda, akilini mwangu nilijisemea kwamba anachosema kiongozi huyo ni kweli kabisa, kwani nje ya kituo cha polisi kulikuwa na umati wa watu waliokuwa wakiimba; "Tunataka watolewe, wachawi hao, tuwaue."

Nilitishika sana kusikia maneno hayo ambayo yaliashiria kuwa watu walikuwa na hasira kubwa kwa mama mkwe na yule kijana mchawi aliyenasa ndani ya nyumba ya jirani.
Yule kamanda aliondoka ofisini kwake baada ya kulifungia jadala la maelezo ya mama mkwe na yule mchawi mwenzake na alituacha tukiwa mle ndani.

"Baba Ajigale unasikia huko nje, tutafakari sana kuhusu huyu mama, wanaweza kumuua hawa," nilimshauri mume wangu."Ni kweli mke wangu, nadhani tukubaliane na haya wanayosema polisi, tusing'ang'anie kumtoa."

Hakukuwa na njia nyingine isipokuwa kumsubiri kamanda ili tumuage na tuondoke. Wakati nawaza hili na lile yule kamanda aliingia akiwa na karatasi ambayo nilikuwa sijajua ilikuwa ya nini.
"Mzee, na nyinyi mlioingiliwa ndani na wachawi, mnaweza kwenda na RB ya kesi yenu hii hapa," alisema huku akimpa jirani yetu ile karatasi.

"Tafadhali tueleze utaratibu wa kesho," mume wangu alitaka ufafanuzi.
"Kesho tunatarajia kulipeleka jalada ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka na kama litarudi tutaona watafunguliwa mashitaka gani. Cha muhimu ni kwamba jioni mleteeni chakula bi mkubwa," alishauri yule askari kamanda wa polisi.

Tuliondoka wote wanne, yaani mimi na mume wangu na jirani na mkewe hadi nyumbani. Tulijisikia aibu kutokana na kitendo cha mkwe wetu kwenda kwa jirani na kutaka kuwaangamiza.
* * *
Kulipopambazuka tulijiandaa kumpelekea bibi chai. Nilichemsha chai na maandazi na kuweka kapuni. Tulipofika polisi tulikuta mkusanyiko mkubwa wa askari, walipotuona wote waligeuza shingo zao kutuangalia.

"Mmekuja, jamani njooni ofisini kwangu," alisema yule kamanda wa jana.
Tulipokwenda akatuambia kuwa asubuhi alipokwenda kuwaangalia watuhumiwa waliokuwa lokapu, alikuta mama mkwe amefariki dunia.

Usikose kufuatili simulizi hii ya kusisimua Jumanne ijayo.
Mwendelezo vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwendelezo jamani!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom