Palikuwa na mvuvi mmoja ambae ktk shughuli yake hiyo alijiwekea kanuni kwamba,endapo atakuwa baharini na ikatokea kuwa ametupa nyavu mara 3 na asipate kitu yaani zikatoka bila samaki basi siku hiyo atakuwa amefunga kazi na atarudi nyumbani akiwa mtupu.
Siku moja akiwa kazini kama kawaida akatupa nyavu mara ya kwanza kuvuta zikatoka kapa.Akatupa mara ya pili pia zikatoka hamna kitu,akajisemea moyoni bado ×1.
Mara ya tatu alipotupa kuvuta nyavu zikatoka na kichupa kidogo kazuri tu,akasema basi leo kazi imekwisha ,akakusanya nyavu zake na mtumbwi akauhifadhi kwa kazi ya kesho.
Akakichukua kile kichupa akakitikisa akasikia kuna kama kitu kina cheza mle ndani ya chupa.
Akahisi kuna uwezekano mle ndani mna mali hivyo pengine itakuwa ndio sababu ya kuuaga umasikini.
Akakifungua,alipokifungua ukatoka moshi mkubwa ulionyooka kuelekea mawinguni,kwa hofu akaanguka chini akazirai.
Alipozinduka akakuta jini refu limemsimamia akashangaa.Akamuuliza wewe nani?
Likamjibu Mimi ni jini akamtajia na ukoo wake akamwambia nilifungiwa ktk hii chupa kwa sababu nilimuasi mfalme wangu hivyo akaniadhibu kwa kunifungia chupani kisha akaitupa baharini.
Lile jini likamwambia nilikuwa nakusubiri uamke ili nikuue,mvuvi akapata ujasiri akamuuliza kwa nini uniue au ndio shukrani yako ya kukutoa humo chupani?
Likamjibu, sikiliza binadamu ni nimefungwa humo sasa ni mwaka wa150,miaka 50 ya kwanza nikaweka ahadi ya kuwa yeyote atakae nitoa humu ntamfanya kuwa tajiri kuliko kiumbe chochote,miaka 50 ikapita.
Nikaweka ahadi ingine nikasema moyoni yeyote atakae nitoa ktk miaka 50 hii mingine ntamfanya kuwa mfalme mkubwa duniani nayo ikapita asipatikane wa kunitoa.
Ndipo sasa nilipojiwekea ahadi kuwa kuanzia sasa yeyote atakae nitoa lazima nimuue,ndiposasa wewe ukaja kunitoa hivyo lazima nikuue.
Mvuvi akaomba sana akalia lakini halikumwelewa.
Mvuvi akajaribu ombi la mwisho akamwambia twende tukaulize kwa yeyote tutakaemkuta kama ni sawa haya unayotaka kunitendea, jini likakubali na makubaliano yalikuwa kuuliza kwa viumbe watatu tofauti.
Walikutana na viumbe viwili vya kwanza vyote vilisema kumwambia jini kuwa huyo ni halali yako kwa sababu binadamu hawana shukrani.
Kiumbe wa tatu alikuwa binadamu,jini akamkataa yule jaji akisema atakupendelea kwa sababu wewe ni binadamu mwenzake.Wakati wanabishana yule MTU akawasogelea akauliza kisa cha ubishani wao.
Mvuvi akamweleza kisa kizima,yule MTU akasema kwanza yeye haamini iliwezekana vipi lijini likubwa kama yeye likae ktk kichupa kidogo kama kile ikawa amekishika kile kichupa.
Jini likaonà kama vile huyu binadamu anaweza kutoa uamuzi utakaomsaidia yeye,akamwambia afungue kile kichupa amwonyeshe yule mtu akakifungua,jini likajigeuza moshi likaingia ndani ya chupa ile kuingia tu jamaa akaifunga ile chupa na mfuniko wake akampa mvuvi akamwambia haya irudishe ulipoitoa.
My take haya majini usipokuwa na mbinu ya kuyarudisha chupani yatakumaliza wewe.