Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Hapo zamani za kale aliishi mvuvi masikini ambaye kwa jina aliitwa Majuto. Majuto aliishi kwenye kijiji
kidogo pembeni mwa ziwa dogo pamoja na familia yake. Kwa miaka mingi sana watu wa kijiji hicho
walikuwa wakiishi wakitegemea ziwa hilo kwaajili ya samaki na maji kwa matumizi yao yote. Waliweza
kukamata samaki wakuwatosha wao na pia wachache ambao waliweza kuuza kwenye vijiji vya jirani ili
kujipatia mahitaji mengine.
Kila asubuhi Majuto aliamka mapema na kutayarisha ngalawa na ndoano yake na kwenda kuvua samaki
ili aweze kuipatia familia yake chakula. Ngalawa yake ilikuwa ni kubwa na imara sana yenye uwezo wa
kwenda umbali mrefu juu ya maji bila tatizo lolote. Lakini Majuto alikuwa sio mvuvi mzuri kwa kuwa
aliogopa sana maji na hakujua kuogelea. Kila siku aliwaza sana kabla ya kupanda ngalawa yake na
alifikiria itakuwaje kama ikizama au ikipata shida ya aina yeyote na akadumbukia kwenye maji. Ni kwa
sababu tu alikuwa hana njia nyingine ya kujipatia yeye na familia yake chakula ndio alilazimika kwenda
na kuvua samaki. Rafiki zake Majuto walijaribu kumfundisha jinsi ya kuogelea lakini kila alivyoweka tu
mguu wa kwanza ndani ya maji alihisi kama vile anazama na aliamua kukimbia. Kweli tatizo lake la
kuogopa maji lilikuwa ni kubwa na ni sugu.
Kila asubuhui Majuto alienda na ngalawa yake kuvua samaki lakini aliishia tu kutega ndoano yake
kandokando mwa ziwa ambapo hapakuwepo na samaki wengi. Alifanikiwa kumkamata samaki mmoja
mmoja tu na ndoano yake na mwisho wa siku alikuwa amekata jumla ya samaki watatu au wanne tu
wadogo. Hili jambo liliendelea kila siku, aliondoka asubuhi na mapema na alirudi jioni na samaki
wachache sana. Uwoga wake wa maji ulimsababisha asiweze kufanikiwa zaidi kama walivyo fanya
wavuvi wengine ambao waliweza kwenda umbali mrefu zaidi na kukamata samaki wengi zaidi
waliokuwa wakubwa.
Masikini Majuto siku zilivyopita uwonga wake haukupungua na alibakia kuwaza sana jinsi atakavyofanya
ili aweze kupata samaki wengi zaidi. Jamani jamani, nitafanya nini masikini mimi. Mbona wenzangu
wanafanikiwa na mimi nashindwa, alilalamika Majuto. Aliwaza sana mpaka ghalfa wazo lilimjia
nitaenda kumuomba mchawi anisaidie na kuniondolea shida zangu zote, alisema Majuto. Pamoja na
kuwa alishasikia kwa wazee wa kijijini na pia kwa watu wengi kuwa mchawi huyo aliyekuwa akiishi
milimani sio mtu mzuri, Majuto hakufikiri mara mbili. Hii ndio nafasi yangu kubwa ya kuweza
kubadilisha maisha yangu kabisa. Hao wanaosema kuwa hili sio jambo zuri hawapendi kuniona
nimefanikiwa, alisema Majuto.