Nzi Chuma
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 475
- 1,176
- Thread starter
- #21
@smart911 hebu nisaidie hii story Moderators wameuhamishia jukwaa gani? Maana naipata kwa kusearch.
Sent using Jamii Forums mobile app
@smart911 hebu nisaidie hii story Moderators wameuhamishia jukwaa gani? Maana naipata kwa kusearch.
@smart911 hebu nisaidie hii story Moderators wameuhamishia jukwaa gani? Maana naipata kwa kusearch.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tupe uzi huoNAKUFAHAMU VIZURI
MTUNZI: KJM-0718274130
SEHEMU YA NANE
★★★★★★★★★★★★
Nilikaa nilipoelekezwa, nikiwa sijui kikao hiki kinahusiana na nini haswa.
“Bwana Adam, mimi naitwa Saidi Alhuram, ni baba mzazi wa Lutfiya. Na hawa unaowaona hapa ni baba zake wadogo bi Lutfiya”. Alisema yule mzee ambaye alionekana kuwa na umri mkubwa kuliko wote pale kikaoni. Sikuwa na la kusema zaidi ya kuitikia tu na kumuashiria yule mzee aendelee.
“Dhumuni hasa lililotuleta ni hii kadhia ya leo, kitendo ulichofanya cha kumzini binti yetu. Ni kitendo ambacho hakijawafurahisha wazee wake wote Lutfiya. Ni kitendo kibaya mno. Kitendo ambacho kwetu sisi majini hatukikubali”. Aliongea yule mzee huku akinikazia sura. Alionyesha kuchukizwa. Maneno yake yalifanya nihitimishe na kujiridhisha kuwa Lutfiya hakuwa binadamu wa kawaida, bali ni jini. Hisia ambazo nilikuwa nazo tangu asubuhi ya siku hii nilipokutana na Lutfiya.
“Najua kuwa umefanya bila kujitambua, na hii yote ni kutokana na hila za mtoto wetu Lutfiya, lakini ndio ushazini tayari. Ni juu yako kuepuka zinaa kwa mtu yeyote, si lazima Lutfiya. Ila kwakuwa hii ni tabia yako, tupo hapa kuikomesha”. Aliongeza yule mzee na kumuangalia mzee mwingine ambaye alikuwa muda mwingi akiniangalia machoni. Ni kama alimpa ishara ya kuongea hivi.
“Lutfiya amefanya jambo hili juu ya mapenzi yake kwako, hajitambui huyu mtoto. Amefanya hivyo akitaka kutupa shinikizo la sisi kumuozesha kwako, na anajua kuwa si jambo rahisi sana”. Aliongea yule mzee aliyeachiwa kijiti.
Mpaka wakati huu nilikuwa sijawaelewa kabisa wazee wale. Nilibaki nikijilaumu mwenyewe tu kwa kujiingiza katika janga hili zito. Sikutegemea kama ningepitia wakati mgumu kama huu katika siku ile. Pamoja na wazee wale kutangulia kuongea, bado shauku yangu nilitamani kujua zaidi hatma yangu.
“Kwahiyo wazee, mimi mnaniambiaje? Nini mlichoamua juu yangu?”. Niliamua kuvunja ukimya.
“Tumeamua kukuozesha Lutfiya”. Alisema mzee Said.
“Sasa hivi?” Niliuliza kwa sauti, hamu ya kulijua jambo hili kiundani ilikuwa kubwa.
“Hapana”. Aliongea Mzee Said na kunifanya nishushe presha kidogo.
“Tutakuozesha binti yetu baada ya taratibu zote kukamilika, tunajua tusipowaozesha huenda Lutfiya akafanya jambo baya zaidi. Ni mwaka mzima sasa amekua akilitaja hili jambo tunamkatalia. Lakini leo asubuhi tulipofanya makosa ya kiulinzi juu yake ndipo alipoitumia nafasi hiyo kukutana na wewe na akafanya mliyoyafanya, ni tukio linaloonesha kuwa amedhamiria kweli hili jambo, tukiendelea kumuacha huenda akafanya makubwa zaidi”. Aliongeza Mzee Said na kunifanya nianze kupata picha kamili sasa. Ila nilijiuliza tu kama inawezekana kweli Lutfiya amenifuatilia mwaka mzima?.
“Kwahiyo ni taratibu gani ambazo zinatakiwa kukamilika ili uniozeshe?”. Niliuliza, kichwani nilikuwa sina nia ya kuoa, bali nilitaka tu kujua jambo hili kiundani ili nijue naliepuka vipi.
“Itabidi tuandae siku ya wewe kuja kwetu ujinini, upajue, uwaone na mama zake Lutfiya na ndugu wengine. Ni lazima pia tukuelekeze namna ya kufika huko, maana sisi tunaishi baharini”. Aliongea Mzee Said na kufanya nianze kutoka jasho jingi sana. Hali ya uoga ilianza kujirudia.
“Tutamtuma mwakilishi wetu kesho kuja kukupa maelekezo kamili, tafadhali nakuomba uwepo hapa nyumbani kesho saa 4:00 asubuhi. Sisi tunaondoka”. Alimalizia Mzee Said na kuniacha na butwaa. Kisha wote wakasimama na kushikana mikono. Nilipepesa macho na sikuwaona tena. Nilijaribu kupiga kelele. Lakini nilijishangaa sana, sauti haikuwa ikitoka. Nikaamua kurudi kitandani na kuendelea na usingizi wangu. Lakini sikuweza kulala. Usingizi ulipaa. Nilitingwa na mawazo mazito mno. Nilianza kujutia vitendo vyangu vyote vya kimalaya nilivyovifanya huko nyuma. Saa chache za usiku huu zilizobaki, niliziona zaidi ya siku nzima. Nilibaki macho mpaka saa 12 asubuhi ambapo niliamua kutoka nje.
Nilienda moja kwa moja kwa muuza uji ambaye alikuwa akikaa nyumba kama tano kutoka nilipo. Mara nyingi nilikuwa nikipata uji asubuhi maeneo hayo, nilipenda sana uji wa ngano.
Zahara, dada aliyekuwa akiuza uji pale, alishanizoea sana. Alinipachika jina la "Fundi", hakumaanisha vingine bali ni fundi wa wanawake, mtaalamu wa kutengeneza wanawake.
“Karibu sana Fundi, nishakuwekea uji kabla hujafika, nilivyokuona tu nikasema ngoja nikutilie kabisa”. Alisema Zahara mara baada ya mimi kukaa pale na kumsalimia.
“Asante sana bi Zahara”. Niliitikia wakati napokea kikombe kikubwa cha nusu lita cha uji wa ngano.
“Jana nilishangaa kidogo, nilikuona ukiingia katika ile nyumba pale”. Alisema Zahara na kunifanya nishtuke kidogo.
“Kumbe uliniona? Enhee nambie, ina nini ile nyumba?”. Niliuliza kwa shauku.
“Nyumba ile ilikuwa ikiishi watu ambao walisemekana ni majini, baada ya wao kuondoka, hakuna aliyeweza kuishi ile nyumba, kila mtu alishindwa, ina vituko balaa..” Niliendelea kumsikiliza Zahara kwa umakini.
“Jana nilipokuona umeingia nimeshangaa sana, nikahisi labda na wewe ni mmojawapo kwakweli...” Aliongeza Zahara, bado nilikuwa nimeduwaa nikimsikiliza.
“Hebu nambie, ulienda kufanya nini mle ndani? Na ulipata wapi funguo za kuingia mle?”. Zahara aliuliza maswali ambayo sikuwa na majibu yake.
Itaendelea...
Sent using Jamii Forums mobile app




Huu wino balaa*NAKUFAHAMU VIZURI*
*MTUNZI: KJM-0718274130*
*SEHEMU YA TISA*
Sikuwa na majibu ya maana ya kumjibu Zahara, nilikatisha maongezi kwa kubadilisha mada. Nilimaliza kupata kikombe cha uji na kufikiria nini cha kufanya baada ya pale. Ahadi ya wale wazazi wa Lutfiya ilikuwa waje nyumbani saa 4 asubuhi. Nilifikiria kuwakimbia. Sikutaka wanikute nyumbani kwangu muda huo. Niliamua kutokomea na kwenda mbali zaidi. Lakini wakati sijafanya maamuzi ya wapi hasa pa kwenda, wazo jingine likanijia kichwani. Nikaamua kuelekea huko nilikofikiria. Nilikabidhi kikombe cha uji kwa Zahara kikiwa kitupu, nikamlipa na kuelekea nyumbani kwangu. Kwakuwa nilikua sijaoga, nikaingia bafuni na kuoga haraka haraka, kisha nikaingia chumbani kwangu, nikavaa na kutoka. Saa ya mkononi ilisomeka saa moja na robo asubuhi. "Bado mapema sana" nilijisemea moyoni na kupanda daladala nikiwa na begi langu (lenye vitu muhimu ikiwemo laptop) mgongoni.
Nilikuwa naelekea kwa babu yangu Mzee Mbogo-Para. Mtaalamu sana wa sayansi ya giza. Japo ni muda mrefu nilikuwa sijaonana nae wala kuwasiliana nae, niliamua kwenda moja kwa moja kijijini kwake pasi na kuwasiliana nae. Lengo ni kwenda kumueleza yanayonisibu na kuona jinsi gani atakavyonisaidia.
Mzee Mbogo-Para alikuwa akiishi mbali kidogo, ilinihitaji kupanda daladala za kuelekea mjini, huko ndipo ningepata gari za kuelekea kijijini kwa Mzee Mbogo-Para, safari ya zaidi ya masaa mawili hadi kufika sehemu ambayo ningepanda bodaboda na kunipandisha vilima na kushusha makorongo kwa zaidi ya nusu saa ndipo ningefika nyumbani kwa babu yangu huyu. Pamoja na kuyajua hayo yote, niliamua kwenda kwake kwakuwa sikuwa na namna ya kufanya. Mjini mambo yalishavurugika!!.
Baada ya kufika mjini nikatafuta gari zinazoelekea kijijini kwa babu. Zilikuwa za shida kidogo, hivyo nililazimika kusubiri. Tulikuwa tumesimama kituoni na abiria wengine ambao niliwatambua wanasubiri gari ninayoisubiri mimi. Nikapiga jicho la kitalii na kukutana uso kwa uso na dada mmoja mrembo akiwa amesimama sio mbali na nilipo. Kama ilivyokuwa kawaida yangu, tayari moyo wangu ulishaanza kwenda mbio. Nikaamua kumsogelea nikiamini huenda ningepata chochote.
“Za saa hizi dada..”. Nilimsalimia baada ya kufika alipokuwa amesimama.
“Nzuri tu, za kwako Adam?” Alijibu huku akiniangalia vizuri usoni, alikuwa anatabasamu. Nilishangaa kunijua jina langu. Akili yangu haraka haraka nikajua huyu atakuwa Lutfiya, ndiye mwenye tabia hizi. Nikaishiwa nguvu.
“Hapana, mimi sio Lutfiya, ni mdogo wake, naelekea huko unakoelekea wewe kuna jambo”. Alisema yule dada baada ya kuona nimekaa kimya nikiwaza. Sikuongeza neno lolote, nikaamua kuondoka na kusogea nilipokuwa mwanzo. Gari ilifika na nikapanda. Ila cha ajabu sikumuona yule dada mle ndani ya gari. Nikajiuliza maswali machache kichwani mwangu bila majibu. Ila nikaamua kupuuza.
Nikiwa njiani nilipitiwa na usingizi mzito, wala sikujua yanayoendelea. Hii ilitokana na kutolala karibu usiku mzima. Nilikuwa nimechoka sana.
“Kaka..tumefika” nilishtuka kutoka usingizini, konda alikuwa akinitikisa ili niamke. Niliangaza huku na huko na kugundua kweli nilishafika kijijini Mtakuja, kijiji cha babu yangu Mzee Mbogo-Para. Nilishuka, nikasimama na kupiga myayo mfululizo. Konda alikuwa amenisimamia pembeni akiniangalia kwa makini.
“Vipi bro, mbona kama tunashangaana?” nilimtupia swali konda nikianza kupiga hatua kuelekea zilipo bodaboda.
“Heshimu kazi za watu blazaa.. Heshima kitu cha bure bloo... Mimi nimetumwa hela kaka.. Wee vipi? Mi nkushangaeee?? weee vipi.. ?? Nitie changu nikisongeshe mbele kwa mbele..” Konda aling'aka kwa sauti ya juu. Nilikuwa nimesahau kuwa sijalipa nauli. Japo maneno ya konda huyu yalinichoma, lakini sikuamua kusema chochote zaidi ya kutoa pesa yake mfukoni na kumlipa. Alinipatia "change" yangu na kuiweka mfukoni. Nikasogea kwenye bodaboda na kupanda moja ya bodaboda ya kijana pale kituoni.
“Mbogo-Para” nilimwambia yule kijana baada ya kupanda.
“Elfu kumi bro..” alisema yule bodaboda huku akigeuka kunitazama.
“Fanya saba”. Nilimsihi.
“Utanipa nane, nitakusaidia...” aliongeza bodaboda na kupiga 'starter' kuanza safari. Mimi sikuongeza neno lolote, nilifikiria tu kufika salama. Njiani nikajiwa tena na mawazo ya yule binti niliyekutana nae pale kituoni. Aliniambia anakwenda ninapokwenda mimi. Anaenda kwa ajili ya 'jambo'. Ni jambo gani hilo? Na kwanini hakupanda gari ilipokuja? Nilijiuliza maswali mengi sana juu yake. Lakini nikajipa moyo kuwa leo ndio mwisho wao hawa majini. Babu yangu anakwenda kumaliza kila kitu. Bodaboda ilitembea dakika 33 na kunifikisha katika kiunga cha Mzee Mbogo-Para ndani ndani ya kijiji kile cha Mtakuja. Nikampa boda boda stahiki yake na kuniacha nikielekea mlango wa kijumba kile kidogo cha udongo kilichoezekwa kwa makuti ya kumba.
“Hodii..” nilibisha katika mlango ule wa kijumba cha makuti. Mlango wake ulikuwa wa makuti pia.
“Karibuu.." Sauti ambayo sikuifahamu, iliitikia huko ndani. Nikafungua mlango na kuingia katika kisebule cha kijumba kile ambacho kilikuwa katikati ya vyumba viwili.
“Karibu Adam, umefika muda muafaka sana, ni saa nne kasoro dakika tatu..” alinikaribisha Mzee Mbogo-Para, pembeni yake walikuwepo wale wazee watano wazazi wa Lutfiya, na pia alikuwepo yule binti ambaye nilikutana nae pale kituoni.
Itaendeleaa...
Sent using Jamii Forums mobile app