Hadithi ya Mapenzi: Nakufahamu vizuri

Hadithi ya Mapenzi: Nakufahamu vizuri

Nzi Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
475
Reaction score
1,176
NAKUFAHAMU VIZURI
MTUNZI: KJM (0718274130)

SEHEMU YA KWANZA

Niliamka mapema kidogo kuliko kawaida yangu. Nikaingia bafuni na kuoga kisha nikarudi chumbani kwangu. Nikavaa nguo harakaharaka kisha nikatoka. Ni mtu ambaye kama hunijui ungedhani nawahi sehemu ya maana kidogo na yenye "dili" la uhakika. Ila haikua hivyo, niliamua tu kuwafurahisha majirani.

Nilipokua nakwenda wala sikuwa nikipajua. Ilikuwa ilimradi nitoke tu. Nikakaa kituoni kusubiri daladala nikiwa na begi langu lenye "laptop" ndani yake. Usafiri ulikuwa wa shida kidogo asubuhi hii, magari mengi yakigeuzia juu kwa juu baada ya kujaza mapema. Ukizingatia mimi nilikua nikiishi ndani kidogo, ilihitaji subira ya hali ya juu kupata gari kwa wakati ule ambao wengi walikua wakigombania kuwahi makazini mwao.

Mbali na mimi, na abiria wengi pale kituoni, pembeni yangu alikuepo dada mmoja mrefu mweupe, mwenye umbo lilichongoka vizuri. Macho yake yaliyokoleza wanja yalishabihiana sana na sura yake ya upole akikutazama. Mkono wa kulia alishika mkoba wake mdogo mweusi, na wa kushoto alikamata simu ya bei mbaya. Alivalia baibui jeusi lililombana kidogo kiasi cha kukupa uhuru wa kung'amua shepu yake. Manukato yake yalizagaa kituo kizima cha daladala. Baada ya kumthaminisha vizuri, niliona nimsalimie japo mwanzo sikufanya hivyo.

“Habari yako dada?”
Alinitazama, pasi na kujibu chochote. Nilijisikia vibaya sana, kwani abiria kadhaa walinigeukia kutazama nani aliyesalimia pasi na kupewa jibu. Nilifadhaika.
“Assalam alykum...” Nilisema tena kumuelekea yule dada, safari hii nikimtazama machoni.
“Waalykum Salaam..” Alijibu huku akitabasamu. Akanifanya nikashangaa zaidi.
“Unaonaje tukatembea tu hadi pale barabara kubwa ambapo magari ni ya uhakika? Unajua sio mbali kutokea hapa”. Niliona nitumie fursa ya lile tabasamu.

“Sawa, twende”. Alinijibu na kunifanya nishangae zaidi. Licha ya kumpa hilo wazo, lakini sikutegemea alikubali bila kusema chochote, nikijaribu kuangalia na alivyoanza na mimi. Ila nikaungana nae na kuondoka mdogo mdogo kuelekea barabara kuu ambapo ni mwendo za zaidi ya dakika 15 ukitembea kwa miguu.

“Adam, kwanini unapenda sana wanawake?” Aliniuliza swali hili hatua kumi tu toka tulipoanza safari. Nilikua sijaongea chochote, na nilipanga swali langu la kwanza liwe kuulizana majina, lakini yeye alionekana kunifahamu vizuri. Maswali kichwani mwangu yakawa mengi sana kuliko kawaida.

Ni kweli naitwa Adam, na ni kweli sifa ya kupenda wanawake ninayo, tena sana tu. Na hata yeye niliamua kumuongelesha kwa sababu hiyo. Ila cha kushangaza ni kuwa yeye simjui, kwanini mimi ananijua vizuri namna hiyo?.
“Hivi unanifahamu kumbe?” nilimuuliza kabla ya kumjibu swali lake.

“Adam Ahmad Ngudu, una miaka 29 tu na ni mtoto wa nne katika familia ya Marehemu Mzee Ahmad Ngudu, mtoto wa mke wake wa pili baada ya yule wa kwanza bi Maryam Suleiman Kijiko kufariki kwa ajali ya meli mwaka 1984, mtoto pekee wa kiume kwa mama yako. Hujafanikiwa kuoa, lakini una watoto wanne, Rukia, Kulthum, Safia na Latifa.

Mungu amekupa watoto wote wa kike ili aje akuonyeshe vizuri uchungu wa unayoyafanya ukifanyiwa wewe. Na naijua dhamira yako juu yangu, naijua vizuri tu, tena sana. Ila niseme tu, sitaki kuchezewa. Ukiamua kunipenda kweli, niko tayari”. Sikuwa na nguvu ya kusema chochote baada ya hapo. Nilihisi kama naanguka chini na sikujua tena kinachoendelea.

Itaendelea...

Mawasiliano: 0718274130

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAKUFAHAMU VIZURI

MTUNZI: KJM (0718274130)

SEHEMU YA PILI

“Pole sana, hapa upo nyumbani kwangu”. Ndio maneno niliyoyasikia mara baada ya kuzinduka. Sikujua nimefikaje hapo ambapo huyu dada anasema ni kwake. Nikakumbuka mara ya mwisho nilipoteza nguvu nikiwa njiani naelekea barabara kuu na huyu binti. Nikatizama saa yangu ya mkononi, ilisomeka saa 4:30 asubuhi. Nilishangaa!!. Nikakumbuka tena muda niliotoka nyumbani ilikua ni saa 12:38 asubuhi.

“Nimefikaje hapa kwako?” niliuliza huku nikijitahidi kukaa kitako.
“Ulipoanguka niliamua nisitishe kwenda kazini, nikakuleta hapa kwangu kwa msaada wa watu kadhaa pale karibu”. Alinijibu.

“Kwanini usinipeleke kwangu wakati unaonekana kunifahamu vizuri sana?” Niliuliza.
“Ningefanya hivyo ungekosa msaada, maana ningekupeleka na kuondoka, nisingeweza kukaa kwako muda mrefu hivi hadi uzinduke”. Alinijibu kwa utulivu kabisa na kunifanya nikose hoja.

“Ok, asante sana. Ila pamoja na wewe kunifahamu vizuri, mimi sijakufahamu bado”.
“Naitwa Lutfiya, mmoja kati ya watu ambao uliwatongoza zamani sana ingawa hukumbuki. Kipindi hicho nilikwambia naitwa Natasha. Tulikutana safarini wakati unaelekea Mbeya kwenye msiba wa mjomba wako Idrisa Fuad".

Nikajaribu kukumbuka baada ya maelezo haya, sikupata kumbukumbu yoyote nzuri. Ni kweli mjomba wangu alifariki kwa ajali na tukalazimika kumzika Mbeya, lakini sikumbuki kukutana na mtu aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Natasha. Niliinamisha kichwa zaidi ya dakika mbili nikitafakari lakini sikupata jibu.

“Usiwaze sana, huwezi kukumbuka chochote. Cha kufanya ni kunyanyuka hapo na ukaoge kisha nikusindikize nyumbani kwako, ili ikifika saa 8 Amina atakapokuja asikukose kama mlivyoahidiana”. Alinambia Lutfiya baada ya kuniona nimeinamia chini muda mrefu. Maelezo yake yalizidi kunipa ukakasi wa kutaka kujua yeye ni nani hasa anayeweza kufahamu hadi ahadi yangu na Amina na mambo yote yanayonihusu. Huyu ni mtu wa aina gani jamani?. Sikupata jibu, nilinyanyuka na kumuangalia vizuri, alikua akitabasamu.

“Pita hapo, nenda moja kwa moja kule ndio bafuni, kaoge nimekutayarishia kila kitu”. Sikuongeza neno nikaelekea bafuni. Nikiwa na mawazo lukuki kuhusu Lutfiya, nilihisi ni ndoto ndefu, haikuniingia akilini kabisa. Lakini ni ndoto gani hii isiyoisha? Nilishangaa!!.

Nikaingia bafuni na kufunga mlango, nikasaula na kuanza kujimwagia maji. Harufu ya yale maji ilinitisha kidogo. Yalinukia kama marashi. Nikafungua bomba kuangalia kama bomba la juu linatoa maji, lakini hayakutoka. Nikaangalia na bomba la chini, lakini nako hayakutoka. Nikajaribu tena kujimwagia kopo la pili mwilini, harufu ya marashi ilinikera zaidi. Nikaamua kuacha. Wakati navuta taulo nijifute kisha nivae nguo tayari kwa kuondoka, nikasikia sauti ya Lutfiya ikitokea mlango wa chooni na kusema “Adam, maji hayana tatizo hayo, nimeyaweka dawa tu ili usizimie tena mbele yangu”.

Itaendelea....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAKUFAHAMU VIZURI


MTUNZI : KJM (0718274130)


SEHEMU YA TATU


Nilijimwagia yote mwili mzima pasi na kupaka sabuni, nikajifuta na taulo na kuvaa nguo zangu kisha nikafungua mlango nikatoka.

Nilimkuta Lutfiya amesimama usawa wa mlango wa bafuni, ila akiwa tofauti kidogo na nilivyomuacha pale sebuleni wakati naingia bafuni. Safari hii alikua katika kivazi cha nguo nyepesi sana, iliyobana sana mwili wake na ilikuwa ikionyesha kila kitu katika mwili wake. Macho yangu yalipenya na kuona kifua chake kilivyo. Lahaulaaa...!! Moyo wangu ulienda mbio sana. Akanishika mkono na kunivutia chumbani huku akiwa haongei chochote. Nami nilipata kigugumizi nikawa naangalia tu mwisho wa hii ndoto yangu ndefu ya leo. Akafungua mlango wa moja kati ya vyumba vya ile nyumba, akanivutia ndani, kisha akaufunga na funguo.

“Baada ya kuoga ni kupaka mafuta, kuwa na amani” Aliniambia baada ya kunikalisha kitandani katika chumba kile nadhifu mno. Kisha akachukua kichupa kidogo cha mafuta ya nazi, akaanza kunipaka miguuni. Mikono yake laini ikagusa mwili wangu na kuanza kunisisimua vibaya sana. Muda huu alikua amechuchumaa chini, nilipata fursa ya kuziona kwa karibu zaidi nywele zake laini, zenye asili ya kiarabu. Aliziachia na zilionekana kutambaa hadi mgongoni. Hakika alivutia mno.

“Hivi unaishi na nani hapa?” Nilijikuta nikiuliza swali ambalo sikulitegemea. Nilishachanganyikiwa na bwana mkubwa ndani ya kaptura alishaanza kusumbua.

“Hapa naishi peke yangu kama unavyoishi wewe kule kwako”. Alinijibu na kuhamia kunipaka mafuta mkononi.

“Kwanini msichana mrembo kama wewe uishi peke yako jamani?”. Nilitupia swali jengine, safari hii nikishika nywele zake kwa mtindo wa kuzipapasa. Hakujibu swali langu, badala yake alinitazama sana katika mtindo kama wa kutaka niache ninachokifanya. Nikaamua kuacha kushika nywele zake.

“Umalaya utakukosesha vitu vingi sana Adam”. Aliniambia huku akisimama. Kisha akafungua mlango na kunielekeza kutoka. Nikatii na kutoka mle chumbani.

Nilisimama pale sebleni kwake nikimsubiri aje ili nitoke. Alikuja na kunipa ishara nikae katika sofa pale sebleni. Nikakaa.

“Adam, najua kuwa umefukuzwa kazi na najua jinsi kukosa kwako kazi kunavyomtesa mama yako. Najua unalazimika kutoka asubuhi ili mradi tu usionekane huna kazi kama ulivyozoeleka. Mama yako anakutegemea sana, na anapata sana tabu kwa kipindi hiki ambacho huna kazi. Najua jinsi gani unamsaidia. Na hilo ndilo jambo pekee linalofanya nitake kukusaidia. Nitakusaidia upate kazi tena, umsaidie mama yako. Ila msaada wangu nitautoa kwa sharti moja tu”. Aliweka nukta Lutfiya na kunifanya nisiwe na cha kusema zaidi ya kuuliza tu “Sharti gani hilo?”.


Itaendelea...


Mawasiliano: 0718274130


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAKUFAHAMU VIZURI
MTUNZI: KJM (0718274130)

SEHEMU YA NNE

“Sharti ni kunioa”. Aliongea kwa kujiamini Lutfiya na kunifanya nipigwe na butwaa. Sikuelewa kabisa kwa sababu haya mambo yalionekana kwenda kasi sana. Ni asubuhi hii hii ya leo tu nimekutana na Lutfiya, muda huu wa saa tano kabla asubuhi kuisha tayari anataka nimuoe, kivipi? Na ni nani haswa huyu Lutfiya? Lengo lake kwangu ni nini hasa? Kwanini pia ananifahamu vizuri namna hii?.
“Adam..” aliita Lutfiya baada ya ukimya wangu mrefu.

“Unawaza nini sasa? Mimi na Zubeda ambaye uliahidi kumuoa na ukafika hadi kwa wazazi wake, nani mzuri?, au kwakuwa hujui kuwa hata mimi nina maisha mazuri tu kuliko hata yule Zubeda? Tatizo lako ni nini? Au kwa kuwa Zubeda ana msambwanda?”. Lutfiya alizidi kuniacha katika wakati mgumu kwa maswali yake ya kila mara yanayoendelea kunifahamisha kuwa si mtu mgeni kwangu na pia si mtu wa kawaida.

“Naomba niende nyumbani, tutaongea siku nyingine”. Nilimsihi Lutfiya ambaye pasi na nilivyotarajia, alifungua mlango na kuniruhusu kutoka bila ya kuongea neno lolote.
Baada ya kutoka nje, nilishangaa kuona kuwa nyumba niliyokuwemo ni nyumba ya tatu tu kutoka nyumbani kwangu. Nyumba hii sikuwahi kuwajua wanaoishi hapa licha ya kuishi mtaa huu kwa muda mrefu kidogo.

Milango yake, wa mbele na wa nyuma ya nyumba hii muda wote ilikuwa imefungwa. Sikuwahi kumshuhudia mtu yeyote anayeingia wala kutoka katika nyumba ile hata siku moja. Wasiwasi juu ya Lutfiya uliongezeka maradufu. Nikatembea hatua za haraka na kurudi nyumbani kwangu.

Wakati naukaribia mlango, nikaingiza mkono wangu mfuko wa kulia wa suruali ambapo nakumbuka ndipo nilipoeka funguo zangu asubuhi wakati natoka. Sikuona funguo. Nikajaribu upande wa kushoto nako hakukuwa na funguo. Nikatulia kwa dakika moja na kuwaza wapi zitakuwepo funguo za nyumba yangu. Nikaamua kuelekea pale nilipoanguka na kuzimia leo asubuhi.

Nilipopiga hatua moja tu kutoka mlangoni, simu yangu iliyokuwa mfukoni ikaita. Nikaitoa na kutazama nani anayenipigia. Ilikuwa ni namba ngeni. Nikatulia kwa sekunde kadhaa kabla ya kuamua kupokea au Laa. Mara nyingi huwa sipokei namba ngeni, lakini kwa sababu nilituma maombi ya kazi kwenye taasisi kadhaa, nikahisi ni simu ya usaili. Nikapokea.

“Usiende huko, funguo zako umesahau hapa nyumbani kwangu”. Ilisema sauti ya kike ya upande wa pili na kukata simu.

Itaendelea..

Mawasiliano: 0718274130

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAKUFAHAMU VIZURI

MTUNZI : KJM (0718274130)

SEHEMU YA TANO

Kwakweli nilipigwa na butwaa ya hali ya juu sana. Nilijiuliza haswa Lutfiya ni mtu au ni kiumbe cha aina gani? Amejuaje kama mimi natafuta funguo? Na amejuaje kuwa naelekea pale nilipoanguka wakati nilikua sijapiga hata hatua tatu? Nani amemwambia uelekeo wangu na ninachowaza kichwani? Na namba yangu ameipata wapi? Nilijiuliza maswali mengi ambayo majibu yake sikuwa nayo.

Ila nikapiga moyo konde na kuamua kurudi moja kwa moja nyumbani kwa Lutfiya. Nilipofika nikagonga na kufungua mlango kabla ya kuitikiwa. Nikaingia ndani ambako sikumkuta sebleni kwake. Nikajaribu kuangaza angaza funguo zangu pale sebleni lakini sikuziona. Nikaelekea chumba ambacho Lutfiya aliniingiza baada ya kutoka kuoga. Nikagonga, nako sikuitikiwa. Nikaamua kuufungua mlango na kuingia ndani, sikukuta mtu.

Nako nikajaribu kutazama huku na huko, lakini sikuona funguo zangu. Nikajaribu kufungua vyumba viwili vingine vilivyobaki. Vilikua vimefungwa. Nikajaribu kwenda bafuni, huko nako sikukuta mtu!!. Nikaamua kutoa simu ili nipige ile namba aliyonipigia Lutfiya nimuulize yuko wapi?.

Nikaenda moja kwa moja kwenye "Call Logs" lakini sikuiona namba ile iliyonipigia mwishoni. Niliona namba nyingine za watu ambao niliwasiliana nao kabla ya yeye. Nikatazama tena kwa umakini, ni kweli haikuwepo.

Wakati naendelea kutafakari cha kufanya, simu yangu ikaingia ujumbe. Nikausoma. Ulitoka katika ile namba ya Lutfiya, na ulisomeka hivi "Nipo hapa nyumbani kwako, usinitafute huko".

Nilitoka mkuku mkuku kwenda nyumbani kwangu. Nilihisi kupata wazimu. Nikafika na kunyonga kitasa, mlango ulikuwa wazi na funguo zikining'inia mlangoni, nikazichomoa na kuingia ndani. Sikuona mtu sebleni kwangu. Nikapitiliza mpaka chumbani. Nako hakukuwa na mtu. Nikakaa kitandani nikiwa nimechoka na hizi purukushani. Nikasikia kama mtu anayeoga bafuni kwangu. Nikainuka na kuelekea bafuni, Lahaulaa.

Nilimkuta Amina akiwa anaoga, nilishangaa sana. Amina alinitazama vizuri machoni. Akafunga bomba la mvua na kuniuliza “Vipi mbona kama una wasiwasi Adam mpenzi? Hujapenda "suprise" yangu ya kufika kwako mapema kabla ya saa 8 kama tulivyoahidiana?”. Kwakweli nilipatwa na kigugumizi.

Itaendelea...

Mawasiliano ; 0718274130

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*NAKUFAHAMU VIZURI*

MTUNZI: KJM (0718274130)

SEHEMU YA 06

Nilikosa cha kumjibu Amina, nikabaki namuangalia tu. Nilishachoka na vituko vya Lutfiya. Wazo la haraka haraka nililokuwa nalo ni kuwa Lutfiya sio binaadamu wa kawaida, bali ni jini. Na mara kadhaa nilishasikia stori mbili tatu zinazowahusu majini na kero wanazowapa binaadamu, haswa wanapokuwa wanawataka kwa haja zao.

Lutfiya ameshanitamkia kuwa anataka ndoa, bila shaka huyu ni miongoni mwa majini mahaba ambao niliwahi kusikia habari zao. Ila kitu cha tofauti kuhusu Lutfiya, ni kwanini ajitokeze ana kwa ana? Stori zote za jini mahaba nilizozisikia ni kuwa huwa wanakuja usingizini tu.

Wanafanya mapenzi na binadamu kisha wanaondoka ukiwa usingizini bado. Ingawa athari wanazokuachia katika maisha yako ya kawaida ni kuwa hutatamani kuoa wala kuwa na mpenzi. Na hata ukiwa nae, mara nyingi jongoo hapandi mtungi mbele yake, hivyo utaishia kukimbiwa tu na wanawake.

Wakati niko katikati ya dimbwi hili la mawazo, huku nikiwa nimeganda pale mlango wa bafuni, nilihisi kushikwa begani. Nikanyanyua uso wangu na kuangalia mbele. Alikuwa amesimama Amina, binti wa kimanga mwenye sura ya mvuto sana. Alikuwa akitabasamu na kufanya vishimo vyake vya mashavuni maarufu kama dimpoz kuonekana vizuri. Kifua chake kilichosheheni matiti ya wastani yaliyosimama vizuri kilivutia sana.

Nadhani kila mwanaume duniani angetamani kuona kifua hiki. Amina alikuwa amelowa maji aliyokuwa amejimwagia hapo bafuni, kitu kilichofanya avutie zaidi. "Mheshimiwa spika" alianza kusumbua huko bungeni kwake. Nikasaula nguo zangu zote harakaharaka na kumkumbatia Amina kuelekea katika bomba la mvua pale bafuni.
“Ulijuaje kama nimekufuata ili nije nikuogeshe?” Aliniuliza Amina.

“Najua umenimis sana, najua una hamu na mimi”. Nilijibu tofauti kabisa na swali nililoulizwa. Kama tujuavyo, kichwa cha chini kikishasimama cha juu kinaacha kufanya kazi. Amina alinimwagia maji kisha kunipaka sabuni kwa mikono yake laini mno. Kisha akanisuuza na kunifuta maji na taulo kabla sijambeba na kuelekea nae chumbani ambako tulizama katika penzi zito sana. Tofauti na siku nyingine za nyuma, siku hii nilihisi utamu uliopitiliza kwa Amina.

“Leo mbona umekua mtamu namna hii baby?” Niliamua kumuuliza wakati huu amelalia kifua changu huku nikipapasa nywele zake.

“Leo nimetia ndimu badala ya Limao, kwahiyo ladha lazima iongezeke”. Alinijibu kwa mzaha Amina huku akicheka na kunifanya nami nicheke.
“Nafurahi sana ukiwepo hapa, maana lazima nitacheka tu”. Niliongeza.
“Mimi zaidi yako, mwezi mzima huu unanikwepa, tangu nikufumanie hutaki hata kunipa huduma mwenzio. Kwani nani aliyekwambia naweza kuachana na wewe sababu nimekufumania na Zuwena?

Watu wote humu duniani wanajua kuwa wewe unampenda Zuwena, ila wazazi wake tu ndio hawawezi kuruhusu mtoto wao aolewe na maskini kama wewe, na hapo ndipo tunapoitumia fursa ili angalau na sisi tunaweza kuwa mbadala wake”. Amina aliongea kwa hisia.

Ni kweli umepita mwezi mzima tangu anifumanie hapa nyumbani kwangu, nikiwa na mpenzi ninayempenda zaidi, Zuwena.

“Baada ya Zuwena, hakuna msichana anayeweza kuchukua nafasi yake isipokuwa wewe, nakupenda sana Amina”. Niliongea kwa hisia kidogo, sikujua ni kwanini leo. Sababu pamoja na uzuri wa Amina, yeye si miongoni mwa wanawake ninaowapenda zaidi. Hayupo hata tatu bora.
“Naomba uniahidi kitu Adam...” Aliongea Amina kwa sauti ya kunung'unika.
“Nambie tu mpenzi, sem chochote”. Nilijikuta nikijibu tu bila kujua athari ya majibu haya kwa Amina, binti aliyekuwa ananipenda sana.

“Utanioa?” Aliuliza swali gumu kidogo Amina, kwakuwa nilikuwa sitaki kumkosea ili niendelee kufaidi, nilijibu tu "Ndio nitakuoa".
Amina alifurahi sana, na kuanza kunibusu mashavuni, huku mkono mmoja akiupeleka kwa "Mheshimiwa spika" pale bungeni kwake. Nadhani lengo lake lilikuwa kutaka kufungua kikao kingine cha mchana baada ya mapumziko. Sikuwa na hiyana, nami nikaungana naye kwa kuanzia kwenye chuchu zake. Nilizitia mdomoni na kuanza kumung'unya kama pipi ya chocolate.

“Aaa..daa.m” nilisikia akiita kwa sauti ya chini sana Amina huku akizungusha zungusha kiuno chake.
Wakati tukiwa katika hali hii, nilihisi kama mlango unagongwa.
“Nasikia kama mtu anagonga, ngoja nikamtizame”.

Nilimwambia Amina ambaye aliitia kwa kichwa kuniruhusu. Nikaruka kutoka kitandani na kuelekea nyuma ya mlango, nikavuta bukta yangu iliyokuwa hapo nyuma ya mlango, nikavuta na singlendi yangu, kisha nikashika kitasa kabla ya kuzungusha ufunguo na kuvuta mlango.

“Adam”. Nilisikia sauti ikiniita ikitokea nyuma yangu kabla sijapiga hatua moja kutoka nje ya chumba.
“Unasemaje tena Amina?” niliuliza katika hali ya kukereka kidogo huku nikigeuka. Lakini tofauti na nilivyotarajia, kitandani nilimkuta amekaa Lutfiya, akiwa amevalia vizuri kama vile alivyokuwa asubuhi. Niliangaza chumba chote huku na huko, hakukuwa na Amina kabisa chumbani mle.

“Mpango wangu namba moja umekamilika, asante sana kwa penzi zito Adam, nenda kamfungulie Amina, akiondoka nitakuja tena tuendelee.. Lakini kumbuka ahadi yako uliyotoka kuniahidi punde tu kuhusu ndoa, bye”. Aliongea Lutfiya na kunifanya nikune macho yangu kuhakikisha ninachokiona. Nilipoangalia tena, hakukuwa na mtu pale chumbani.

Itaendelea..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom