holy holm
JF-Expert Member
- May 6, 2017
- 4,671
- 8,671
Habarini Wapendwa,
Hope mko njema licha hili janga linalo tukumba Mungu ni mwema sana.
Leo naomba kushare story ya Maisha yangu Mimi holy holm. Wiki chache zimepita nilileta humu thread ya jinsi nilivyoanza mahusiano ya kimapenzi na jimama na nilihaidi kuwaletea story nyingne ya maisha yangu, basi kwa hiari yangu sina budi kuwaletea.
Hii story ita base Katika Mji wa Musoma maana ndo nimeishi sana huku. Baadhi ya majina ya watu sitayataja hii ni kuwalindia heshima lakini ikibidi nitawaja. Tuweni tu wavumilivu maana story ni ndefu kidogo na nitakua naitoa vipande ili iweze kueleweka vizuri.
Nimezaliwa Musoma mjini nilikua naishi Kata ya Iringo mimi na familia yangu,tuko watoto sita.Kwa wanaoijua mitaa ya musoma enzi hizo ilikua sio mitaa salama sana kwa usalama hii ni kutokana na wimbi la makundi ya kihuni yaliyokua yameshamiri nahisi ni kuanzia 2010 mpka 2014 au 2015 kama sikosei mwenye kumbukumbu nzuri ataliweka sawa hilo. Binafsi yangu mimi sikua kwenye hayo makundi ila nilkua na marafiki ndani ya hayo makundi.
Tumelelewa kwenye maadili mema tu mimi na familia yangu ila wazazi wetu walikua wako busy sana na shughuli zao Baba alikua mwalimu na Mama alikua anauza nguo za mitumba (Nyasho) so muda mwingi tulikua tunabaki home wenyewe tu mpk jioni wazazi wakirudi.
Mwaka 2004 nilianza darasa la pili shule ya Musoma ambapo niliamishwa kutokana na maendeleo hayakua mazuri nikaamia Mwisenge primary tena nikahama kuja iringo (B) primary. Kwenye hii shule nilkutana na marafiki ambao tulikua tunaishi nao mji mmoja walikua ni jirani zangu.Kama mnavyojua kwa mlio kaa mtaa wa iringo enzi hizo kulikua na wahuni sana tena hasa kule kastamu milimani ulikua ukijichanganya angazao imekula kwako. Mimi na hao rafiki zangu tuliokua tunasoma nao nakumbuka tulkua na mtindo wa kukaa na hao wahuni japo wazazi walikua hawataki kukaa nao lkn haikuwa rahisi kutuzuia maana mda mwingi walikua kwenye shuguli zao.
Mara nyingi hao wahuni walikua wanatutuma tukawaitie mademu ambao walikua wanawataka wao muda mwingine wanatutuma bangi kwa mapusha wao kipindi hicho sisi hatuvuti sigara wala bangi tena walikua wanatukataza wao wenyewe. Kipindi hicho tulikua tumepanga nyumba ya vyumba viwili na sebule, chumba kimoja walilala wazazi na kingne alilala sista na wadogo zangu wawili wa kiume mimi na bro wangu tulikua tunalala kwa jirani kila mtu sehemu tofauti. Mimi nilikua na lala kwa na rafiki yangu tulikua tunasoma nae darasa moja. Kiukweli huyu rafiki tabia zake hazikua nzuri alikua na tabia ya wizi ambayo aliniambukiza kimtindo nikajikuta na mimi nishakua kezi.
Nakumbuka siku ya kwanza mimi kuiba japo tulikamatwa siku, tulikua tunaenda shule (darasa la pili tulikua tunaenda saa nne) njia tuliyopita kuliku na Mmama mmoja anakibanda chake anauza vitu bidhaa za dukani pamoja na matunda.Sasa bna huyo rafiki angu akanambia twende tuchukue hela hapo kibandani, kulikua na utulivu yaani kulionekana hakuna mtu hapo maana tulivyofika tuliita kama mara tatu kibandani, kibandani....kibandani...tulivyoona hakuna mtu anae kuja jamaa angu alinambia niangalie usalama wakati yeye muda huo alipanda kwenye hicho kibanda na kupitia kwenye kale katundu ambako wanapitishia bidhaa, moja kwa moja kwenye kopo la hela akakomba zote ile anatoka tu anataka kushuka yule mama cjui alitokea wapi akaanza kupiga yowe la wezi.
Tukiwa na uniforms zetu za shule tulikimbia vibaya mno kuelekea shuleni bahati nzuri watu hawakua wengi sana ( hiyo ndo nature ya iringo asubuhi watu sio wengi sana mtaani) tulikimbia mpka tukampotea yule Mama hatukuenda shule moja kwa moja tulipitia yale maeneo ya Afilux hotel kujua tulikua na shingap alizochukua kucheki zilikua ni sh 18000 na vijisenti me nilipewa buku 6000 yeye nae akachukua buku 6000 iliyobaki tukaingia kwanza kwenyee ka mgahawa kupoteza mawazo, tulikula siku hyo donati za kutosha baada ya hapo tukaenda pale stendi kwa wamachinga me nilinunua saa zile disco zilikua ni jero pamoja vile vikamera ambavyo ukichungulia unaona wanyama mbalimbali, Rafiki angu yeye alinunua karedio na vile vigemu fulani hivi ndo vilkua vina trend kipindi hicho.Baada kufanya hiyo shopping tulielekea shuleni sasa tukiwa hatuna wazo kama huko nyuma tumefanya msala.
Nitarudi kuendelea maana story ni ndefu ndugu zangu.
Au nasema uwongo ndugu zangu