Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Noma sana mzee, shusha mikeka kiongozi...
 
Ungejichanganya kwangu ningekufurahisha. Ungejua hujui
 
Kweli mkoani ndio maana wanaibiwa kiboya, huku Dar ile kwenda tu bafuni lazima mlango ufunge na kufuli...[emoji1787][emoji1787]

Yaani unaenda dukani unapiga stori na unaenda Ziwani unaacha nyumba wazi??[emoji848]
Mtaa ule ulikua umetulia sana unaweza kulala bila kufunga mlango wizi ulikua ni nadra sana kutokea lakin kuna mitaa mingine ni hatari sana acha mlango wazi uone [emoji23]
 
Inaendelea


Narudia tena katika mtu ambae alikua anipendi basi bonge alikua anipendi alinichafulia jna ila nilimpuuza tu maana roho yangu ilikua imetulia sasa baada ya kuwapiga tukio.Lakin yule Kaka ao bonge yeye yupo peace [emoji3577] sana nilikua nikikutana nae ananipa hi tunapiga story kidogo then kila mtu anafanya yake lakini bonge......

Maisha yaliendelea pale bro wang ( wadamu ) alirudi rasmi home maana alikua hakai na sisi sana, me na bro wangu hatunaga story kabisa yani ni buyu buyu kila mtu na mambo yake.

Mdogo wangu yule mwiz aisee dogo alikua ana majanga balaa yani shule alikua hafiki kabisa totally, nilimshauri hakushaurika nikaachana nae afanye anachoona ni sahihi kwake, Mzee na bro walikua hawajui kama dogo shule aendi ilikua 2018 hyo ndo yupo form 4.

Mzee alipokuja kufahamu aisee alimpiga sana dogo nusu kumuua....alimfunga kamba mikononi na miguu akachukua kisu akakiweka kwenye jiko la mkaa kilikua kikipata moto ana mchoma nacho mapajani, nilishindwa kuvumilia nilimzuia mzee asiendelee kufanya vile ikawa nikosa akanigeukia mimi lawama kama zote ziliniangukia lakini kunipiga ndo alikua hawez maana tungepigana.

Muda huo kipindi mzee tunabishana nae dogo cjui alifunguaje kamba akasepa kusiko julikana.Mzee pia alinifukuza na mimi nikasepa usiku huo huo nikaenda kwa rafiki angu mmoja hivi nikawa naishi nae.

Mzee alimtafuta dogo bila mafanikio me mwenyewe ckujua alikimbia wapi ilikua mwez wa tatu.Kwa vile nilikua na vipesa kidogo niliona nianze tena biashara ya ps maana kila kitu nilikua nacho ckua nashida sana.

Nilitafuta frame sehem moja hv nikalipia miezi mitatu 30k kwa mwez mmoja kuna msela wangu alikua ni muhitimu wa chuo cha Walimu alikua yupo tu kitaa hana ramani aliniomba awe ananipigia kazi nilikubali nikawa namuachia siku mbili hela anayopata anachukua yeye mimi siku tano hela ni zangu.

Niliamua kufanya hivyo maana me na yule rafiki angu ( tuliyepigana nae ) tuliji organized tukaanza kuchoma mawe ko nilikua busy sana.

Nakazi ya kuchoma mawe isikieni tu, hyo kazi ni ngumu jamani yaani ulikua ukilala usiku unatamani kusikuche lakin kwa vile nilikua natafuta pesa kwa hasira ilinibidi tu kuamka mapema kuwai kupanga magogo na kuni kwenye miamba.Hii kazi aina unafuu hata kidogo yaani asubui tunawai mlimani kukata miti magogo tulikua tunakod watu wa chain saw ndo wanatukatia sisi tunayasukuma kutoka mliman mpk chni alafu tunayabeba kwenye machela mpk kwenye mawe.

Nyundo yenyewe ya kupasulia mawe ilikua ni nzito kama ni legelege itakuangusha.Yaani ilikua ni asubui mpk jioni saa kumi niko kwenye mawe, hyo saa kumi nikishaoga saa kumi na moja naenda zoez la kwaya ( kama ni siku ya zoez ) nikitoka zoez naenda kwenye Ps kukaa jioni nachukua hela alafu naenda home kiwiz wizi nawapa madogo hela ya matumiz kisha nasepa napo kaa.

Life lilisonga hivo hivo kibishi yule dogo nilipata habar zake kuwa anaishi magetoni kwa wahuni flani alikua anasoma nao...siku moja nilimfuata hapo mageton, nilimwambia tu awe anasimamia pale Ps hela tutakua tunagawana alikubali ko alini save sana kusimamia Goli.

2018 ni mwaka ambao ulinipelekesha mpera pera sana, huku mawe huku ps, kwaya na bado mademu [emoji1787]....siku moja tulipokea taarifa ya msiba wa bibi yetu ko tulienda msibani na yule dogo kijijin tukakutana na Mzee pamoja na Mama yaani huo msiba ni kama ulituunganisha upya...mzee alisamehe akataka turud home lakin kwa upande wa Mama yeye alikataa kabisa kurud Musoma maana bado ana kesi na wale wanakikundi wake.Alibaki kijijin kuishi,tulivyomaliza kuzika tulirud home lakin dogo shule alikataa kata Mzee alimuacha afanye anachotaka.Aliendelea kusimamia Ps.

Mwezi wa tano huo kanisani kwetu kulikua na mahubir makubwa tu sasa cc tulichukua tenda ya kulinda Eneo la mkutano. tulikua watatu me jamaa wawili.Mahubir yalikua ni wiki tatu ko ilikua tunalipwa 80k kila mmoja pale mahubir ytakapoisha.

Hapo sasa ratiba ikawa tight kinoma, asubui kwenye mawe, jion kwenye mahubir na Ps usiku niko lindo.Mahubir aliisha salama nikawa bado naendelea na mawe yangu ( tulipanga tupate trip 20 za lori ambazo kwa wakat huo trip ya mawe ilikua 50k, lakin trip 20 hatukuzifisha )...kuna siku mdada mmoja hivi alikua anaduka kubwa tu kuna siku aliniomba niwe na lala dukani kwake maana mtu alie kuwa ana lala dukani alipata msiba.Nilishindwa kumkatlia ombi lake ila nilikua staki sema nilimuheshimu sana.


Hyo siku nimelala humo dukani Manzi yangu ( lizy ) alini text kuwa kafukuzwa kwao na hana pakulala nilimpgia simu akanielekeza mahali alipo nikamfuata, nilimchukua nikamleta pale dukani nilimuuliza kisa cha kufukuwa hakuwa na chamaana sana cha kunambia, nilijisemea tu hayanihusu nikamgonga tukalala kesho yake asubui nikamtoa mapema tu nikampleka kumpaki kwa rafiki angu ( yule ambae nilikua nalala kwake )...nilimpa 20k atumie kwa muda ule nikaahid kukutana nae mida.

Ngoja nikomee hapa nitarud kuendelea.

N.B. kuwa makin sana kusoma vizur unaweza kuchanganya ukadhani nmekupa chai [emoji23] pia huu mwaka 2018 pia ulikua una mambo mengi kweli nitajitahid nisiwachanganye.
 
Hatari sana mzee, unatema sana nondo aisee
 
sorry usingiz ulinipitia ngoja nianze niweke
4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…