Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
Haya ndugu zanguni baada ya siku nyingi kupotea nimerudi tena na Hadithi Mpya ya kusisismuwa JINI MAUTI
Watu walikusanyika kwa wingi katika maduka ya vitabu na vibanda vya magazeti kwa ajili ya kununua kitabu kimoja cha kusisimua, kitabu chenye historia ya kweli aliyoisimulia msichana mwenye miaka ishirini tu, Davina Patrick Mosenya ambaye katika kipindi hicho alikuwa hoi hospitalini.
Mara ya kwanza waliposikia simulizi ya maisha yake katika Kituo cha Redio cha Global kwenye Kipindi cha True Story, wengi waliumia, wengi walisikitika mno, wengine walilia huku wengi wakionekana kutokuamini kama msichana mdogo kama Davina angeweza kupitia maisha hayo.
Kitabu hicho kiliitwa Jini Mauti, kilikuwa na simulizi ya kweli yenye kutisha na kusisimua mno, watu walikinunua mno mitaani, walitaka kusoma kile alichokuwa amekisimulia msichana huyo redioni.
Watu waliokuwa katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam, wakawaagiza ndugu na marafiki zao wawanunulie kitabu hicho kilichoanza kushika hisia za watu kutokana na simulizi yake aliyoisimulia redioni kumsikitisha na kumtisha kila mtu.
Mitaani kukawa gumzo, siku hiyo ambayo kitabu hicho kilitolewa, idadi kubwa ya watu walikusanyika katika hayo maeneo maalumu ya kuuzia vitabu, kila mmoja alihitaji kopi yake huku wengine wakiwa tayari hata kutoa mara mbili ya gharama iliyokuwa ikiuzwa.
Vitabu vipi kaka?? alisikika jamaa mmoja, alikuwa mbele ya meza ya muuza magazeti.
Vitabu vipi??
Jini Mauti!?
Duuh! Unakuja kuviulizia sasa hivi! Mbona vishakwisha kitambo,? alisema muuza magazeti.
Yaani saa nne asubuhi nimechelewa??
Ndiyo! Watu wamewahi asubuhi na mapema kana kwamba wamekuja kupiga kura, vyote nimemaliza, hebu nenda Kariakoo au Ubungo unaweza kuvikuta vingine,? alisema muuza magazeti.
Kila kona, hakukuwa na Kitabu cha Jini Mauti kilichokuwa mezani, vyote vilikwisha huku watu wakivihitaji sana. Kila aliyekuwa na kopi ya kitabu hicho, alijifungia chumbani na kuanza kukisoma, hata kumuazima mtu mwingine hakutaka.
Msichana Davina alikuwa hoi kitandani, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa usioonekana katika mashine za hospitali. Kitandani pale, mwili wake ulivimba mno, macho yalikuwa makubwa na hata kupumua kwake alipumua kwa shida mno, huku wakati mwingine mwili wake ukionekana kuwa na magamba kama mti, magamba yaliyokuja na kupotea mara kwa mara.
Madaktari waliingia kwa zamu, kila aliyeingia mle chumbani, alimuonea huruma, alionekana kuwa msichana mdogo, mrembo ambaye hakustahili kupitia maisha aliyokuwa akipitia.
Vipi? Anaumwa nini?? aliuliza Dk. Migiro, alikuwa akimwangalia Davina machoni.
Hatujui, tumempima lakini hatukukuta ugonjwa wowote ule,? alijibu daktari mmoja.
Kweli??
Ndiyo!?
Hawakutaka kujiuliza sana, walijua kwamba ugonjwa aliokuwa akiumwa Davina haukuwa ugonjwa wa kawaida, alirogwa, ulikuwa ni uchawi ambao kwa namna moja au nyingine ndiyo uliomfanya kuwa kitandani hapo.
Wakati akiteseka kitandani, wakati akilia, kitabu chake kilikuwa kikifanya vizuri sokoni, historia ya maisha yake aliyokuwa ameiandika katika kitabu kile ilimsikitisha kila mtu aliyeisoma, na hata jina la kitabu kile, kilimsisimua kila mtu, walitaka kujua zaidi kilichotokea kwani kwenye redio alisema kwamba asingeweza kusimulia kila kitu ila kitabuni angeandika yote.
Juu ya kifua chake kitandani pale alikuwa na kitabu chake, kitabu kilichoandikwa kwa mkono wake, kitabu chenye mvuto hata kukiangalia kwa nje. Watu kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakiingia kumuona, na kila aliyeingia, kitu cha kwanza kabisa alitaka kukiona kitabu kile, kitabu kilichoweka rekodi ya kuuzwa zaidi ya nakala laki moja, tena ndani ya masaa matatu tu, yaani saa moja asubuhi mpaka saa tatu.
Davina! aliita mwanaume mmoja mara baada ya kuingia ndani ya chumba kile, alikuwa mwanaume nadhifu, alivalia miwani, alichomekea vizuri.
Abeee, aliitikia Davina kwa shida.
Vitabu vimekwisha mitaani! Tutoe kopi nyingine?? aliuliza mwanaume huyo.
Hakuna tatizo, ila naomba unisomee hiki kitabu, nimekiandika mimi mwenyewe lakini ninapenda kila wakati nikisome au mtu anisomee, nimepitia mambo mengi Geofrey, wengi wamekufa kwa ajili yangu, Mungu, ninaomba unisamehe, nisamehe kwa yote niliyoyafanya,? alisema Davina huku akianza kukuhoa madonge ya damu, kwa shida, akachukua shuka na kujifuta.
Kwa hiyo nianze kukusomea??
Ndiyo! Ila wakati unakisoma, jua kwamba kuna mambo mengi nilisimuliwa na mama yangu na mengine kuyaona mwenyewe.?
Je nini kitaendelea? Ukiweka (Like) Nitaendela kwa hara zaidi