Hadithi ya House girl

Hadithi ya House girl

Sweetcandle

Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
35
Reaction score
15
Sehemu ya 01;

...Naitwa Amina, ila wengi wamezoea kuniita "Mina wa Ukae" kutokana na kujulikana sana kujijini kwetu,nimezaliwa na kukulia Marangu Moshi,nimeishi na wazazi Wangu pamoja na mdogo Wang wa kiume Erick, maisha yetu yalikuwa ya chini na hali duni... Baba angu alikuwa mkulima mdogo na mama alijishughulisha na biashara ndogo ndogo ya kukaanga samaki,Mimi na erick tulikulia maisha hayo..nilifanikiwa kusoma mpaka darasa la saba tu,na baada ya hapo ndipo mambo yalipovurugika.......

......*****.....*****.......
Ilikuwa Jumamosi alfajiri...mida ya saa kumi na moja, nilimsikia mama akiniita kwa nguvu huku akisukuma mlango wa kutokea nnje uliokuwa nusu kuanguka katika nyumba yetu ya udongo akiashiria niamke..."aaarrghh mamaa".. nilijikuta nikihisi hasira za ghafla kutokana na kupenda sana usingiz Wa asubuh ukichangia na hali ya hewa ...nilijilazimisha kuamka nikitupa kiblangeti changu kilichochoka pembeni na kuamka kivivu..
"Maji hamna, nguo za baba ako chafu,mivyombo ya usiku michafu,.kikaangio cha samaki cheusi ...geuka uangalie huku nnje kulivyo kuchafu, halafu unalala tu...mwanamkeee!"..mama aliongea huku ameshika kiuno huku mimi nimejiegemeza ukutani...polepole nikarudi ndani na kutoa vyombo nnje,vyombo vilivyochoka vinatumika basi tu ....nikafagia uwanja uliokuwa mbele ya "kibanda chetu" na kubeba ndo kubwa kuelekea mferejini tulipokuwa tunateka maji..ni mbali kidogo na nyumban na kwa wakati huo tayari kulikuwa kunakucha....

Wakati naelekea kuchota maji kwa mbali nilimuona John (kaka aliekuwa akigombaniwa mtaani kutokana na umbile lake pamoja na kazi yake ya kukaanga viazi)...sio siri nilikuwa nampenda sana lakini hakuwah kunitongoza kwa kuwa hatukuwa na mazoea sana,nilisimama na kuishusha kanga yangu chini kidogo ya makalio na kuifunga staili ya mlegezo... nikadhamiria kupita mbele ya John makusudi huku nikitingisha makalio yangu ambayo kiukwel sikunyimwa..nilipewa ya kutosha, kifuani nilikuwa na chuchu ndogo zilizosimama sawasawa japo nilitaman niwe na maziwa makubwa ili niyatingishe vizuri... Nilifanikiwa kwa hilo, kiasi cha kusahau kumsalimia John kuhofia kupoteza step, nilipofika kwa mbele kidogo niligeuka kujua kama ameona lkn alikuwa bize na kibanda chake. ...nilijikuta nikifyonza na kuendelea na safari yangu huku nikimpangia nikirudi.....


..******** .......*****
House~gal ni stori yangu na si ya kwel, ni simulizi tu kwa ajili ya burudan na mafundisho ya hapa na pale ...nitakuwa nikiitoa kwa sehemu hapa hapa jf... Kama utaipenda unakaribishwa kusoma nasi kama itakupitia kushoto basi pita kama huoni. ..


Asanteni .

Sweet~candle
 
Umenikata stimu kabisa uliposema si ya kweli.., ni nzuri lakini nimekosa msisimko wa kuendelea kuisoma.
 
Huyo john si anatafutwa na yemi alade kumbe unae hlf umekaushaa.. lete stori hyo
 
Back
Top Bottom