mwana ally
JF-Expert Member
- Jan 30, 2014
- 363
- 119
Wakili wa Moyo-19
ILIPOISHIA:
Nimekuelewa.
Brenda alikata simu na kumgeukia shoga yake aliyekuwa na kimuhemuhe cha kutaka kujua Hans alikuwa akisemaje.
Vipi mzushi alikuwa akisemaje?
SASA ENDELEA...
Brenda alimweleza mazungumzo yote waliyozungumza na Hans.
Mmh! Anataka kuniambia nini?
Sijui, wewe ndiyo unajua mlizungumza nini katika ahadi ya penzi lenu.
Uhuu! Mage alishusha pumzi na kusema:
Brenda unanishauri nini? Mage alionekana kama ametahayari kusikia taarifa za Hans.
Kwa vile upo katika hatua nzuri za harusi, huu si muda wa kuzungumza na Hans unaweza kuharibu kila kitu ukakosa bara na pwani, Brenda alimtahadharisha rafiki yake.
Eti eeh, sijui Hans anataka kuniambia nini?
Achana naye.
Mmh! Sawa.
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, kila mmoja aliingia kwenye gari lake kurudi nyumbani.
***
Brenda alipofika nyumbani kwao alikwenda kuoga na kupata chakula kisha alijifungia chumbani kwake na kuwasha Ipad yake na kuanza kuchati na marafiki zake kwenye Twiter na Skype.
Akiwa anaendelea kuchati simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni aliipokea.
Haloo.
Haloo Brenda.
Abee, nani?
Brenda unaniuliza nani wakati tumetoka kuzungumza muda si mrefu.
Hans? Brenda aliuliza.
Ndiyo.
Unasemaje?
Brenda samahani sana.
Bila samahani.
Naomba unikutanishe leo na Mage.
Hans, si tumeisha ongea?
Hapana Brenda, kuna kitu cha muhimu sana nataka nizungumze naye kabla siku ya kesho.
Samahani Hans, nipo Bagamoyo sitarudi leo.
Naomba hata umpigie simu ili anisikilize hata kwa sekunde tano tu.
Hans kwanza samahani, hapa nipo na boy friend wangu, ana wivu sana naomba tuzungumze kesho, Brenda alidanganya.
Samahani, ila utakacho kisikia kesho usishangae najua Mage atafurahi.
Unataka kufanya nini Hans?
Nilitakiwa kumweleza Mage mwenyewe, kwa heri.
Hans alikata simu na kumfanya Brenda abakie na simu mkononi kama anatazama kitu cha kumshangaza. Alijikuta akijiuliza.
Hans anataka kufanya nini? Au anataka kujiua? Mmh! Ngoja nimweleze Mage maana sasa imekuwa kazi. Lakini kipi cha ajabu Mage akiolewa? Kwani alitaka akae vile mpaka lini? Hivi Hans ana shida na Mage au anataka kumvurugia maisha tu.
Brenda alijikuta akiwaza peke yake, wakati huo simu aliyopiga ilikuwa ikiita. Ilipokelewa upande wa pili.
Haloo shoga lete stori, Mage alipokea.
Mmh! Mtu wako ananisumbua sana.
Nani?
Hans.
Kakupigia tena? Mage alishtuka.
Ndiyo.
Brenda achana naye, kwa nini unamsikiliza?
Mage siwezi kumkatia simu kwa vile sina mgomvi naye.
Yaani hivi najiandaa kwenda kwa Colin, tulikuwa tuna chati tukaona haitoshi, tukaongea vilevile tukaona haitoshi, nimeamua kwenda kabisa kuonana naye uso kwa macho.
Duh!
Brenda, nimeamini Colin ananipenda sana.
Sasa ndiyo utulie.
Brenda, lazima nitulie Colin kaniahidi vitu vingi sana baada ya ndoa. Nina imani ndoto zangu nilizoziota kwa Hans zitakuwa mara kumi.
Basi ndiyo hivyo mtu wako, roho ya Mungu anatapatapa kama mfa maji.
Kwani alikuwa akisemaje?
Brenda alimweleza yote aliyoelezwa na Hans na alivyomdanganya, Mage baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema:
Kwani Hans anataka kuniambia nini? Mage aliuliza.
Akwambie nini! Yule mharibifu, huu si muda wa kumsikiliza, ukirogwa kumsikiliza tu ndoa huna.
Mmh! Nimekuelewa japo moyo unatamani kumsikiliza ili nijue anataka kusema nini?
La kusema hakosi, anaweza kukuvuruga akili na ndoa yako ukaiona chungu. Najua bado unampenda sana Hans, kama utampa nafasi narudia tena ndoa hakuna, Brenda alimtahadhalisha Mage.
Hata siku moja, labda siyo Mage mimi. Siwezi kuumizwa mara ya tatu, mbili zinatosha.
Basi ndiyo hivyo kuwa makini na Hans, kwa nini muda wote akae kimya, kusikia unataka kuolewa ndiyo ajifanye anakupenda sana.
Nimekuelewa basi wacha niwahi kwa mahabuba wangu.
Mambo si hayo.
Brenda alikata simu na kuendelea kuchati na mashoga zake.
***
Mlio wa simu ulimshtua Brenda aliyekuwa bado amelala. Alipoangalia ilikuwa namba ngeni, aliipokea.
Haloo.
Haloo, nazungumza na Brenda?
Ndiyo, nani mwenzangu?
Naitwa Ndubi rafiki mkubwa wa Hans.
Ndiyo Ndubi.
Kuna habari siyo nzuri.
Habari gani?
Hans amepata matatizo makubwa sana, nilijaribu kumpigia Mage simu yake haipatikani nikaona nikupigie wewe ili umjulishe.
Mmh! Matatizo gani?
Jana usiku wamevamiwa na majambazi nyumbani kwake. Mkewe na mwanaye wameuawa na yeye hatujui kama yupo hai.
Mungu wangu! Yupo wapi kwa sasa?
Yupo Hospitali ya Muhimbili, chumba cha wagonjwa mahututi.
Mungu wangu! Ngoja nimjulishe Mage.
Itakuwa vizuri.
Baada ya simu kukatwa, Brenda alimpigia simu Mage aliyekuwa bado yupo kwa mchumba wake Colin. Baada ya simu kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili.
Haloo Brenda mbona unaharibu pozi za watu, Mage alisema kwa utani.
Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.
Mungu wangu! Yupo wapi?
Muhimbili.
Nakuja sasa hivi twende.
Noo, tutakutana hospitali.
Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake na kuvaa bila kuoga.
Itaendelea..............
Fuatilia kwenye magazeti ya Risasi Jumatano & Jumamosi. Hii tamthiliya ipo kwenye episode kama sijakosea zaidi ya 40 sasa...Umeharibu uhondo wote, bora ungeimalizia
Sawa mkuu nimekuelewa; tukutane jioni tena muda huu majukumu nayo yamebana hapa.
Tupo pamoja.
Nitafanya hivyo, asante sana mkuuFuatilia kwenye magazeti ya Risasi Jumatano & Jumamosi. Hii tamthiliya ipo kwenye episode kama sijakosea zaidi ya 40 sasa...
Wakili wa Moyo - 20
ILIPOISHIA:
Brenda hakupoteza muda alimweleza taarifa aliyopokea asubuhi ile. Taarifa ile ilimshtua sana Mage.
Mungu wangu! Yupo wapi?
Muhimbili.
Nakuja sasa hivi twende.
Noo, tutakutana hospitali.
Mage alinyanyuka kitandani na kupitia nguo zake, akavaa bila kuoga.
SASA ENDELEA...
Hakutaka kumwamsha Colin aliyekuwa bado amepitiwa na usingizi. Alitoka hadi kwenye gari lake na kuondoka kuelekea Muhimbili kumuona Hans.
Njia nzima alijilaumu kukataa kusikiliza wito wa Hans kwa kuamini kuna kitu cha muhimu alitaka kumueleza.
Alijiuliza Hans alitaka kumweleza nini na kwa nini alilazimisha waonane usiku wa jana yake kisha asubuhi asikie habari kama zile za kushtusha!
Mungu wangu kama Hans atakuwa amekufa atakufa na kinyongo. Sikutakiwa kuwa katili kiasi kile. Japokuwa sikuwa tayari kurudiana naye lakini nilitakiwa kumsikiliza.
Mage alikuwa kwenye lindi la mawazo juu ya Hans kuwa katika hali ile. Alijikuta akitokwa na machozi kumlilia. Alijiuliza kama yeye ndiye angekuwa mke wa Hans na tukio lile likatokea ina maana angekufa yeye.
Kutokana na mawazo mengi alijikuta akiendesha gari pasipo kuwa na umakini. Alifunga breki mbele ya gari lililosimama baada ya taa nyekundu kuwaka katika makutano ya barabara za Ocean na Upanga.
Alikanyaga breki kwa nguvu zote huku akifumba macho na kuuma meno. Gari lilisota na kwenda kujigonga kidogo kwenye gari aina ya Land Cruser aliloendesha Mwarabu.
Kelele za breki zilifanya watu wote kugeuka kuangalia, askari wa barabarani alifika lakini Mwarabu hakutaka kesi kwa vile gari lake halikuharibika sehemu yoyote. Askari alimfuata Mage kumuuliza:
Vipi mbona hivyo?
Mage alishindwa kumjibu kwa vile presha ilikuwa juu na uso ulikuwa umejaa machozi. Askari hakutaka kumuhoji kitu, alimruhusu kuondoka. Mage aliondoa gari kuingia barabara ya Upanga kuelekea Muhimbili kumuona Hans.
Njia nzima Mage alikuwa akilia, alikumbuka maisha aliyoishi na Hans, mwanaume akiyempenda kuliko kitu chochote chini ya jua.
Waliishi maisha ya mapenzi kama njiwa, kila mmoja alimpenda mwenzake penzi la glasi halikuwa na kificho kila mmoja aliamini anapendwa na mwenzake.
Alikumbuka ahadi ya Hans alipomwambia kumuacha yeye ni sawa na roho kuachana na mwili. Alimhakikisha yeye ndiye mwanamke wa maisha yake.
Baada ya Hans kuozwa kwa shinikizo la wazazi, walikubaliana avumilie ili baadaye amuache mwanamke wa kulazimishwa ikiwa pamoja na kutozaa naye.
Lakini Hans alionekana kugeuka pale alipopata mtoto ndani ya ndoa yake, tofauti na walivyokubaliana kutozaa na yule mwanamke na kwenda kinyume na kumfanya naye akubali kuolewa na Colin.
Alijiuliza nani aliyefanya kitendo kile, alijikuta akitengeneza mawazo ya kijinga kuwaza labda mpango ule kaufanya Colin kutokana na wasiwasi wa kurudiana na Hans.
Nikigundua Colin kama ndiye aliyemuua mpenzi wangu, nitamchukia mpaka kufa na nitakuwa shahidi namba moja kuhakikisha na yeye ananyongwa, Mage aliwaza.
Alipofika Muhimbili alisimamisha gari na kuelekea kwenye wadi ya wagonjwa mahututi. Nje ya wadi aliikuta familia ya Hans, hakuna aliyemjali japokuwa alionekana amevimba macho kutokana na kumlilia Hans.
Alipojaribu kuingia wadini alikatazwa na kuamua kusimama pembeni peke yake, baada ya muda shoga yake Brenda alifika na kwenda aliposimama.
Vipi shoga?
Yaani mama Hans kanifukuza kama mbwa!
Kwa nini?
Hata sijui wakati anafahamu mimi na mwanaye tulikuwa vipi.
Kwa hiyo hujui hali ya Hans?
Sijui chochote.
Mara simu ya Mage iliita alipoangalia ilikuwa ikitoka kwa Colin, aliitazama na kukunja uso bila kuipokea. Brenda aliyekuwa akimtazama usoni, alimuuliza.
Simu ya nani?
Achana nayo, alijibu kwa mkato.
Mmh!
Baada ya muda simu iliita tena, Brenda alishtuka kuona jina la Colin bila kupokelewa.
Shoga mbona hupokei?
Achana naye.
Ha! Wewe si ulikuwa kwa Colin na umeondokaje?
Sijamuaga nimemuchana bado amelala.
Unajua unachokifanya unaiweka ndoa yako njia panda.
Kwani asiponioa nitapungukiwa nini? Mage alijibu huku akiibinua midomo.
Mage, usipoteze muda wa Colin, kuamini unampenda kumbe upo naye kivuli tu.
Brenda mwenye uamuzi wa kumpenda ninao mimi.
Kwa hiyo Colin si chaguo lako?
Brenda huu si wakati wa kuzungumzia Colin zaidi ya kujua hali ya Hans ndiye aliyetuleta hapa.
Mmh! Sawa.
***
Colin baada ya kushtuka usingizini alijua mpenzi wake yupo msalani au bafuni, lakini muda ulikatika bila kuonekana. Alikwenda msalani kumtafuta huku akimwita bila kupata jibu. Alitoka hadi nje na kumuuliza mlinzi.
John umemuona shemeji yako?
Ametoka asubuhi sana, hakukuaga?
Ameniacha nimelala.
Tena alionekana kama analia nilijua mmegombana.
Hata sielewi kitu.
Colin alimpigia simu mchumba wake, lakini iliita bila kupokelewa. Alirudia zaidi ya mara tatu, vilevile haikupokelewa. Alijiuliza Mage amepatwa na nini, wasiwasi wake labda kwao kumetokea tatizo.
Aliingia ndani na kuvaa pensi na fulana, chini alivaa ndala na kuingia kwenye gari kuelekea Kigamboni kwa kina Mage ili ajue amepatwa na nini.
Alikimbiza gari, kutokana na foleni aliamua gari lake kulipaki Posta ya zamani na kuchukua bodaboda ili awahi kufika. Baada ya kuvuka alichukua nyingine iliyo mpeleka nyumbani kwao Mage.
Alimlipa dereva na kuingia ndani ya geti, alipofika sebuleni alimkuta msichana wa kazi akifanya usafi.
Habari Sofi?
Nzuri shemu, shikamoo.
Marahaba, vipi Mage yupo?
Sijamuona toka asubuhi.
Mama?
Yupo chumbani kwake.
Kaniitie.
Colin alibakia sebuleni kumsubiri mama Mage, baada ya muda alitokea na kushangaa kumuona Colin katika hali ile.
Vipi baba, kwema?
Kwema, sijui hapa.
Hapa hatujambo, mwenzio yupo wapi? mama Mage alimuulizia mwanaye baada ya kumuona Colin peke yake.
Itaendelea..........