FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,035
- 1,925
Mtunzi: Febiani Babuya
Mwandishi: Bux the story teller
Umri :Miaka 18+
Uurasa wa tatu
Sehemu iliyopita tulipoishia...
Aliamka asubuhi na mapema sana akarudi kwanza kwao, alitaka kuhakiki kama je kweli anafatiliwa, hakuenda na gari aliamua kuchukua boda boda na vitu vyote aliviacha hotelini. Alifika kwa tahadhari akafungua geti na kuingia ndani, alishtuka baada ya kuona mlango wa ndani umevunjwa. Alifika ndani na kukuta vitu vipo hovyo hovyo akajua kweli alikuwa sahihi kuondoka.
Akatoka haraka na kuzunguka nyuma ya nyumba ambako walizikwa wazazi wake, alipiga magoti akaingiza mkono mfukoni akatoa picha ya yule mtu aliyeiokota usiku ule wakati wazazi wake wanauawa, aliingalia kwa umakini sana na kutamka kauli moja tu baba na mama “NITARUDI”, kisha hakuzubaa tena mwanaume na tajiri huyu mtoto akaondoka kwa haraka sana.
Hakuwa na muda wa kupoteza alichukua vitu vyake kule hotelini, aliipeleka gari kwenye yard yao akafunga kila kitu kisha akaelekea airport, alifika akakata tiketi yake na kuambiwa ndege ilikuwa inaondoka masaa mawili mbele, ikambidi asubirie kwa muda, akiwa ameketi hapo alishtuka sana alicho kiona.
Endelea...
Alihisi kama kuna watu wanamwangalia sana akaamua kupotezea, ulifika muda wa kupanda ndege abiria wote walipanda na rasmi wakawa wanaiaga ardhi ya nchi ya Tanzania. Baada ya masaa mengi sana kupita takribani masaa 9 na dakika zake 7, hatimae walifanikiwa kuingia kwenye moja ya majiji makubwa sana na makubwa kibiashara ulimwenguni, si kwingine ni ndani ya jiji la Moscow Russia. Walifika salama na abiria wote walishuka na kwenda mapokezi kuchukua mizigo yao. Abiria mbali mbali wakaanza kutoka nje ya uwanja, hatujui ni kwanini Calvin alipita Russia badala ya kwenda Japan moja kwa moja. Je, ni nini kipo nyuma ya pazia?
Hadithi hii inaenda kukupa majibu ya kila kitu, ungana nami kwa majina naitwa Febiani Babuya lakini waweza kuniita Bux the story teller.
***************************
Calvin alihisi kama kuna watu wanamfatilia aligeuka na kuwaona wanaume wawili wakimwangalia kila hatua anayo piga, aliwakumbuka vyema ni wale aliowaona tangu akiwa airport ya Tanzania hiyo ikampa tahadhari ya kuwa makini kwenye kila hatua anayo piga. Calvin alitoka haraka na kuita taxi na kumuomba dereva atoe gari haraka sana, naye alifanya hivyo kwani kwake mteja ni mfalme na anapaswa kumsikiliza. Alitazama kwenye sight mirror na kuiona tax nyingine ikija upande wao akajua ni wale watu wanamfatilia, akamuomba dereva ampeleke kwenye duka kubwa la nguo lolote lililopo karibu.
“vipi hao watu wanakutafuta niwewe bro”, Aliuliza dereva tax yule.
“ndio“, akajibu Calvin kifupi.
“ kwani ni akina nani?"
"Siwajui ila wananifatilia tangu mbali sana" aliongeza Calvin.
Basi jamaa akampa wazo na kumwambia kama ni hivo ampeleke kwa mtu mmja akapate sura bandia ili asitambulike na kumuwezesha kuwatoka hao watu kirahisi kama atakuwa na pesa.
“Nipeleke pesa sio shida,” ikabidi gari igeuzwe haraka sana kuingia mkono wa kulia wa barabara huku nyuma wakifatiliwa na wale watu. Walifika hiyo sehemu Calvin almshukuru yule mtu akampa pesa yake na kumtaka aondoke haraka ili asije ingia matatizoni kwani alimuahidi kuchukua usafiri mwingine pindi akitoka ili asijulikane kirahisi. Akaingia ndani haraka sana, akafika ndani na kuwakuta watu wakiwa busy kuchora tatoo kwenye miili yao ikiwemo wanawake walio vaa nusu uchi, hakuwajali sana alienda kwa bwana mmja aliyekuwa busy na komputa yake mpakato, maana alielekezwa na dereva kwamba amtafute jamaa anaitwa Max X ndiye mwenye hilo eneo. Anacho taka yeye ni pesa tu hapo atamsaidia.
kweli alivyouliza tu jamaa alimwambia nifate, walipandisha ngazi mpaka juu, waliingia kwenye moja ya milango hapo juu, walimkuta mwanaume mmja ana upara unaong’aa sana huku amezungukwa na wanawake watatu wakimpa burudani. Yule jamaa aliyeongozana na Calvin aliita “Bosi” kuna mteja wako hapa. Max X aligeuka na kumtazama Calvin vizuri kisha akamuuliza anahitaji nini.
Calvin haraka akajibu nahitaji sura bandia ya haraka, haikuwa shida sana aliletewa sura nyingi sana kitu ambacho kilimfanya ashangae sana kwani hazikuwa na utofauti. Alitabasamu huku moyoni akimsifia mtu aliyezitengeneza sura hizo akiuhusudu uwezo wake. Baada ya kujiridhisha akachagua moja aliyoona inamfaa akaivaa pale pale kisha akalipia na biashara ikawa imeisha.
Huku nje wale jamaa walikuwa wanasubiri kama Calvin atatoka kwani walivyoona anaingia hapo walishuka kwenye tax na kujibanza sehemu kumsubiri atoke waunge nae, lakini ulipita muda kidogo bila mtu kuonekana.
“Mhhhh mbona kachelewa hivi kuna nini huko”
mmja wao aliuliza,
“tumfate ndani” mwingine aliongeza,
Wakaamua kuingia ndani wajue nini kinaendelea, lakini wakati wanapandisha walipishana na kijana mmja aliefanana mwonekano na Calvin hata nguo zake ila yeye alikuwa na sura tofauti kabisa, wakahisi watakuwa wamemfananisha tu wakapotezea na kuendelea kuingia ndani. Walifika ndani na kushangaa watu wakiwa busy kuchora tattoo, ni jamaa mmja tu ndiyo alikuwa anacheza na komputa mpakato, basi miongoni mwa wale wanaume alienda na kumuuliza "Bro kuna huduma naweza kupata hapa zaidi ya tattoo?" Jamaa akamjibu "Yes unapata sura mpya " Alishangaa na kuuliza "Ina maana hapa mna sura bandia?" Jamaa kamjibu "Ndio karibu", alitukana “shiiiiiiiiit”, akakimbilia kwa wenzake na kuwaambia yule mpuuzi katuchezea akili. Ndiye yule tuliyepishana nae anatoka nje, basi walikimbia mpaka nje lakini hawakukuta kitu, Calvin alikuwa ashaondoka muda sana bila kutambulika aliko elekea.
Ni ndani ya miongoni mwa jiji kubwa kabisa Japan liitwalo Osaka lenye idadi ya watu takribani 2.691 million, lenye kilomita za mraba 223, na ni miongoni mwa majiji ghali zaidi Japan na duniani kwa ujumla likiwa maarufu zaidi kwa vyakula vya ajabu vya kawaida na wenyeji wanaomaliza muda wao kula na kunywa. Ndani ya mji wa Sakai pembezoni kidogo mwa Osaka bay karibu kabisa na mto wa Yamato ambapo kuna bandari kubwa sana na miongoni mwa bandari muhimu zaidi nchini Japan, ni mji wenye wakazi sio chini ya 828,741 kwa takwimu.
Ndani ya jumba moja kubwa sana la kifahari ambalo limezungushiwa kwa uzio mkubwa na mrefu sana, ni jengo ambalo huwa linafunguliwa mara chache sana Kwa mwaka mzima kutokana na vitu vinavyo endelea humu ndani. Ni jumba linalomilikiwa na mzee mmja anae fahamika kwa jina la Hinata Haruto Haru, ambae kimwonekano ni kama kijana kutokana na mwili wake kutengenezwa kwa mazoezi ya hatari sana tangu akiwa kijana mdogo lakini kiuhalisia alikuwa ni mzee wa miaka 67. Kwenye jumba la mzee Haruto, Kunatumika kuwatengeneza majasusi hatari wa siri sana na maninja wanao tisha sana wanapomaliza mafunzo yao.
Mzee huyu anaonekana kwenye ofisi yake akiwa ameketi chini kikakamavu sana anafanya sala kwa kutumia hisia za hatari sana, alihisi kuna mtu anakuja toka mbali sana lakini ile mihemo ya sauti ya chini kabisa ya yule anayekuja alijua ni kijana wake. Akaamua kuendelea na sala mpaka yule kijana anafika alimuacha kwanza master wake amalize. Baada ya kumaliza aliita "Akio, nafkiri umepata taarifa za kifo cha rafiki yangu kutoka Tanzania Jackson Aron kwa kuuawa vibaya na watu wasiyojulikana." Akio akajibu ndiyo master kwani huyo mtu ni nani hasa kwako," Mzee Haruto alimkata jicho mpaka. Akio akajishtukia na kujua kwamba kakosea kuuliza, kisha akaambiwa utakuja kujua ila sijakuitia hicho.
Rafiki angu ni muda sana alikuwa ameniomba kwamba kama kuna tatizo lolote likitokea basi nimlinde na kumsaidia mtoto wake, hapo ntakuwa nimemtendea wema mkubwa sana hapa duniani. Sasa kwenye tukio la mauaji lililo tokea kwake nchini Tanzania maiti ya mwanae ajulikanae kama Calvin haikuwepo, hiyo inamaanisha kwamba alifanikiwa kutoroka, sasa nahitaji apatikane haraka sana popote pale. Utamtafuta Jackline kutoka Tanzania akwambie kinachoendelea, utakapopata majibu ndiyo utajua wapi pa kuanzia na nahitaji hili liishe haraka sana, kesho unatakiwa uende Tanzania kumchukua bwana mdogo aje hapa, picha zake hizo hapo, kisha Akio akaondoka. “Ntakuenzi kwa kumsaidia na kumtunza mwanao kama mwanangu Jackson”, alisisitiza master Haruto huku akijisemea mwenyewe.
Je, Akio atafanikiwa kumpata Calvin ambae wanajua yupo Tanzania na wakati huo alishaingia nchini Russia/Urusi? Na je Calvin ataweza kutimiza adhima yake ya kulipa kisasi angali hata WABAYA wake hawajui? Ukurasa wa tatu unafika tamati, tukutane kwenye kurasa zijazo hii ni ULIMWENGU WA WATU WABAYA, Mimi ni Bux the story teller, ungana nami mwanzo mpaka mwisho.
Chao.