Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 13

UKURASA ULIOPITA TULIPO ISHIA.............

“Baba Calvin wako saivi amekuwa ni mwanaume haswa lakini kwa bahati mbaya huwezi hata kumsifia tena wala kumkumbatia, huwa kila nikilala nakumbuka usemi wako kwamba haipaswi mwanaume shupavu atoe machozi kwenye uso wake kwani ataonyesha udhaifu mkubwa sana mbele ya wale wanao mtegemea ikiwemo familia yake ambayo inamuangalia yeye kama kioo kwao na hilo nakuahidi kwamba huu uso wangu hautatoa machozi tena juu ya hilo jambo.

Nashukuru sana ulinipeleka kwa mtu sahihi sana kwenye maisha yangu, master Haru, kwangu yule ni zaidi ya mwalimu na kwangu ntamheshimu kama nilivyokuwa nakuheshimu wewe, atakuwa ni familia yangu kwa sasa.
Baba nakuahidi mbele ya uso wa dunia hii hautabaki hata mfupa ulio hai kwa yeyote aliye husika katika hili, kila mtu malipo yake yataendana na alicho kifanya, ila itabidi wafanyiwe kitu ambacho hata wenzao wakiona hawatakaa wakarudia kuichukua haki ya mtu mnyonge tena hapa duniani.
Mwanao naondoka leo na nitarudi tena kuwasalimia siku nikimaliza kazi hii nzito sana ambayo ipo mbele yangu, sayonora chichi to haha”. aliyaongea maneno hayo ya kijapani akimaanisha kwaheri baba na mama kisha akatoka mahali hapo bila kuangalia nyuma, akapanda gari lake na kupotea kwa kasi ya ajabu.
ENDELEA..........................

Alifika hotelini majira ya jioni kidogo na kupitiliza moja kwa moja chumbani kwake, akafika na kuwasha televisheni kabla hata hajaenda kuoga, akakutana uso kwa uso na taarifa moja ya kusisimua sana baada ya kumuona mtu ambae yeye huwa anamchukulia kama baba yake mdogo, hakuwa mwingine ni Juma wa kipindi cha nyuma leo tunamzungumzia Mr Fabian Decco akiwa anatangaza mbele ya uma kwamba mali zote za mzee Jackson Aron zipo chini yake baada ya mzee huyo kupoteza maisha na familia yake akiwa kwake Masaki.
Hiyo haikumshtua sana kwa sababu alifikiria kwamba labda itakuwa ameona ni muda mrefu sasa bila yeye kuonekana mbele yake ndiyo maana anataka kuzisimamia zile mali, kwahiyo Calvin alijua mr Decco alikuwa na maana nzuri tu ya kuendelea kuzilinda mali zao.

“mhhhhhhhh”aliguna baada ya kusikia akitangazwa mbele ya vyombo vya habari kwamba yeye amekufa, alishangaa imekuaje mpaka mzee huyo awe na ujasiri wa kumtangaza kwamba kafariki wakati hawajauona hata mwili wake, ni kama kichwani mwake kuna kitu alianza kuhisi kama hakipo sawa, akakumbuka tangu kwenye msiba wa wazazi wake kulikuwa na watu wenye suti nyeusi na miwani wakionekana kuwa walinzi wa mtu fulani, akifikiria tena alivyokuwa airport kuna watu walikuwa wanamfuatilia mpaka anafika nao Moscow katika nchi ya urusi, alifanikiwa kuwakwepa baada ya kwenda kununua sura ya bandia na kutotambulika mbele yao, hiyo ndiyo ilikuwa pona pona yake mpaka anafika airport kwa ajili ya kwenda kumtafuta mzee Haru ambae alielekezwa kumpata kwa namba maalumu nchini Japan. Akakumbuka vyema mpaka alivyoweza kuitoa ile sura bandia maeneo ya uwani pale airport na kufanikiwa kufika Japan akiwa salama kabisa.

“mbona haya mambo yananichanganya, inaonekana kuna kitu kimejificha hapa, huyu kwangu ni kama baba yangu sina imani kabisa kama anaweza kufanya kitu kibaya kwangu lakini kwa mtirirko wa haya matukio inanipa wasi wasi wa kumwamini moja kwa moja, hapa inanipasa kwanza nijue wale watu walitumwa na nani kunitafuta nadhani hapa nitakuwa nimepata sehemu nzuri sana ya kuanzia” Calvin alikuwa akiongea mwenyewe kisha akaondoka na kwenda kuoga.

IKULU DAR ES SALAAM

Ndani ya Ikulu katika moja ya ofisi kubwa na nyeti zaidi hapa naizungumzia ofisi ya mkurugenzi wa usalama wa Taifa anaonekana mzee Kasisi Chacha mkurya huyu akiwa anamsubiria kijana wake mmoja kutoka nchini Cuba aweze kufika baada ya kumaliza miaka mitano akiwa kwenye mafunzo ya kikomando ili aje kuhakikisha nchi yake inanufaika ipasavyo na uimara wake kuhakikisha amani ya kutosha.

“Ester, victor anafika sangapi airport?” mzee huyu alimwuliza secretary wake huyu ambaye alikuwa ni mzuri na alivutia sana kila ukimtazama.

“nimeongea nae sio muda sana kaniambia baada ya masaa mawili atakuwa ashafika na anakuja moja kwa moja ofisini kuripoti” alijibu kwa heshima Ester.

“fine waweza kwenda”.

Dakika ya saba tangu masaa mawili yakatike tangu mzee huyu alipo muulizia kijana wake ambaye alikuwa akimsubiri kwa hamu kubwa sana.

“bosi”
mzee huyu alijitoa mawazoni na kunyanyua uso wake baada ya kushtuliwa na sauti ya mtu akimuita, alifurahi sana baada ya kumwona huyu bwana mdogo ambae alikuwa anampenda kama mwanae wa kumzaa kwa sababu kamlea mwenyewe baada ya kumuokota siku moja akiwa katika hali mbaya sana mtaani aliko kuwa anapigwa na wenzake wakati wakigombea chakula.

Kiufupi Victor alikuwa mtoto wa mtaani lakini maisha yake yalikuja kubadilika baada ya kusaidiwa siku ile majira ya usiku na mzee huyu akiwa anatokea kwenye majukumu yake ya kazi. Mzee huyu hakubahatika kuoa baada ya mkewe kufa akiwa na ujauzito wa Watoto wawili yaani mapacha wakati anajifungua, tangu siku hiyo mzee Kasisi Marwa hakuwaza kuoa tena wala kuwa na familia ikiwa ni kama kumuenzi marehemu mkewe kwa jinsi alivyo kuwa akimpenda.

Victor aliweza kupelekwa kwenye shule bora sana kisha baadae kwenda jeshini na kuunganishwa moja kwa moja kwenye mafunzo ya kikomando baadae mbayo yalimpeleka mpaka Cuba ili kuweza kuimarika zaidi.

Masikio yake yalisikia jina hilo la bosi likiitwa na moja ya watu ambao alikuwa anawapenda sana, akatabasamu

“mwanangu umerudi huku akimkumbatia Victor”

“ndio baba nimefanya kama ulivyo niagiza”

“safi na najivunia kuwa na mtoto kama wewe”

“asante sana bosi”

“hahahahaa naona ubaba umeuweka pembeni, haya kuna kesi kesi zilikuwa zinaendelea na sikuelewa zimeishaje ila kwa sasa kapumzike nikikuhitaji nitakuita”

“Sawa mkuu” kisha Victor akatoka kwa furaha isiyo elezeka baada ya kumkuta mzee huyo akiwa na afya njema kabisa kwani hakuna binadamu ambae alikuwa ana mheshimu kama mzee huyu na ndiye alikuwa familia yake ya pekee hapa duniani. Wakati anakatiza mapokezi alipokelewa na tabasamu zuri sana la mrembo Ester ambae alikuwa ashaanza kumpenda mwanaume huyu kwa mvuto alio kuwa nao.

“Victor” alishtuka akiwa anaitwa na mrembo huyo

“oooh mrembo unaniita kumbe, japo sijakujua hata kwa jina”

“naitwa Ester”

“sawa Ester nambie”

“samahani sana, nilikuwa naomba namba yako wikiendi kama ukiwa na muda tuonane”

“haikuwa shida kwa victor kuitoa namba ambayo atakuwa anaitumia Tanzania kwani wakati akiwa nje walikuwa wanawasiliana kwa code maalumu tu”

Alitabasamu sana mrembo huyu huku akimkonyeza Victor, mwanaume akatabasamu na kuondoka mahali hapo,

Bibie Ester akatamka “lazima uwe wangu Victor nakupenda”.

UNGANA NAMI MPAKA MWISHO WA KIGONGO HIKI langu jina naitwa FEBIANI THOMASI BABUYA, kurasa zangu napatikana kwa jina la Bux the story teller.

Hotelini kwa Calvin, baada ya kutoka kuoga akaenda kwenye kioo na kujitazama namna mwili wake ulivyo gawanyika vyema ukichochezwa na mazoezi makali ya takribani miaka miwili na miezi kadhaa. Akiwa ndani ya taulo lake akalifuata begi ambalo lilikuwa na nguo, akalifungua kwa password(nywila) na kisha kutoa nguo zote kwenye hilo begi, baada ya hapo akakutana na kioo kigumu ambacho kilimdai nywila ili kulifungua begi hilo upande wa Chini, akalifungua vyema na kutoa ala (kifaa kinacho tumika kuhifadhia upanga hususani katika nchi ya Japan). Calvin aliutoa upanga ulio kuwa una’gaa sana. Akiwa ameushika upanga huo aliokuwa amepewa kama zawadi na mwalimu wake master HARU baada ya kufanya vizuri kwenye mazoezi yake, mawazo yakampeleka mbali sana. Akiwa ndani ya Japan baada ya kumalizana na Dr Sanjey Prakash rasmi sasa aliitwa tena ofisini kwa mzee Haruto Hinata Haru ikiwa ni mara ya pili kuingia ndani ya ofisi hiyo na ni kwa mara ya tatu kumuona mzee huyu tangu siku ya kwanza afike ndani ya ngome hii.

“Calvin Jackson Aron Mavunde, kwa sasa una miaka ishirini na minne na umekua sana, umetimiza miaka miwili ukiwa hapa na kwa sasa umebakisha miezi sita pekee ili niweze kukuruhusu kuondoka hapa. Nakumbuka ulishawahi kuniuliza siku moja kwamba mimi ni nani, nilijuana vipi na baba yako na kwanini ananiamini sana mimi ndiyo maana akakuelekeza uje nikupatie msaada, najua una hamu sana ya kuyajua haya ila miezi sita iliyobaki ndiyo itakayo amua kama nikujibu haya maswali au nisikujibu. Ili uweze kujibiwa kuna kazi ndogo sana unapaswa uifanye ila pia ni kazi ngumu sana kwa mwanadamu wa kawaida kuifanya na usipokuwa makini unaweza ukashindwa, ukishindwa maana yake utakuwa umefeli mtihani, hiyo ni ishara ya kwamba sitakwambia chochote na sitakuruhusu uondoke na inawezekana nisije nikakuruhusu kuondoka tena kwahiyo unapaswa kuwa makini sana na akili yako inapaswa kufanya kazi kwa zaidi ya asilimia tisini kwa hii miezi sita ambayo imebakia, ukiilaza akili yako kidogo tu basi ujue ushafeli mtihani maana hautaweza kuufanya kwa usahihi, unaweza ukawa una haraka sana ya kuhitaji kuujua mtihani huo ila utaambiwa siku unamaliza miezi sita iliyo baki”.

Aliyaeleza kwa usahihi sana maelezo yake mzee huyu kitu ambacho kilimshangaza Calvin kwani hata salamu yake haikuitikiwa kabisa lakini aliamua kutokuwa mwongeaji kwa kuuliza maswali mengi bado maneno ya Akio yalikuwa yanazunguka kichwani mwake “na nikuonye tu siku ukikutana nae chunga sana kinywa chako kwa sababu ukiongea vibaya hata neno moja tu kwake litakugharimu maisha yako yote, yule ni mtu hatari sana”. Calvin akaamua kuitikia kwa heshima

“sawa master nimekuelewa”

“kwa sasa nitapenda zaidi ukiwa unaniita baba nadhani nitafurahi zaidi”

“sawa”

“nenda kajiandae usiku sana uwe macho rasmi unaanza mazoezi namimi mwenyewe”
Yalikuwa ni maongezi mafupi kati ya Calvin na master Haru ambaye hakuwa mtu wa kuongea ongea sana.

Majira ya saa tisa na nusu usiku pembezoni mwa mto Yamato, wanaonekana wanaume wawili na si wengine ni mzee Haru na Calvin wakiwa wote wameshika mapanga lakini mzee Hinata alikuwa ameshika panga feki huku Calvin akiwa amebeba upanga mkali sana unaong’aa gizani.

******************************
Mzee Haru anaanza “kuna mazoezi mawili tu unayopaswa kufundishwa, zoezi la kwanza unapaswa ujue vyema sana namna ya kuutumia upanga na kwa spidi kubwa sana ambayo ni wanadamu wachache sana wanayo, wote tumeshika mapanga ambayo ni halisi kabisa kwahiyo unavyo pigana hesabia kwamba mimi haunijui na upo vitani kwahiyo ukicheza vibaya unakufa” sijajua kwanini mzee huyu aliamua kumtishia Calvin kwa kumwambia kwamba ana upanga halisi wakati haikuwa kweli. Basi mapambano yalianza vyema, Calvin alikuwa ameshaiva sana kwenye mapigano ya kila aina lakini kwenye upanga alikuwa kama kijana mdogo sana. Alishtuka na kuogopa baada ya upanga huo kupitishwa kwenye shingo yake akakaa chini kwa uoga akijua ndo anakufa hivyo, lakini alishangaa kutoiona alama yoyote ile ya damu alivyo mtazama mzee huyu alikuwa akicheka tu, akajua lile panga ni la mbao lakini limetengenezwa kwa namna ambayo ni ngumu sana mtu kulitambua. Basi alinyanyuka huku akiwa anajicheka kwa kufanywa mjinga, na rasmi mazoezi magumu ya kutumia upanga yakawa yameanzia hapo.

Miezi mitatu na nusu baadae majira ya saa tisa kamili usiku juu ya mti mmoja pembezoni mwa mto huo wa Yamato wanaonekana wale wale wanaume wawili wakiwa wanapigana vilivyo kwa kutumia panga ambazo zilikuwa na makali sana, haikuisha hata dakika moja walikuwa na mpambano mzito sana ambao ulipelekea matawi ya miti yote kudondoka chini.

“kuhusu kutumia upanga sasa umeiva vyema kama nilivyokuwa nahitaji na nakuomba tu usikae ukalitumia panga wala kutembea nalo sehemu nyingi unazo enda kwani siku utakayo amua kuutumia upanga wako inawezekana ukawa mtu hatari sana kitu ambacho kitapelekea kuleta taharuki kubwa miongoni mwa watu mbali mbali, kwahiyo hii italeta kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wanao kuzunguka. Leo nakupa huu upanga kama zawadi ya pekee, huu ni upanga ambao nimekuwa nikiutumia Kwa zaidi ya miaka thelathini sasa na kuulinda sana kwa miaka yangu yote na kwa nguvu zangu zote, huu upanga ni hazina kubwa sana ndani ya nchi ya Japan kwahiyo unapaswa uutumie vyema ikiwemo na kuulinda kama unavyo yalinda macho yako.

Chamwisho huu upanga utumie pale itakapo kubidi ila tu usiutumie vibaya kwa kuwadhuru watu wasio kuwa na hatia yoyote ile hiyo itapelekea nikuue kwa mikono yangu mwenyewe kitu ambacho hakitakiwi kutokea kwa sababu mimi ndiye ninaye takiwa kukulinda kwa namna yoyote ile. Je Calvin atapewa mtihani gani na unadhani atafanikiwa Kutoka kwenye ngome hii?

Ukurasa huu unafika tamati, tukutane na Kalamu ya professor kwenye kurasa zijazo.

ULIMWENGU WA WATU WABAYA

mimi ni Bux the story teller.....ChaoView attachment 2280884
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 14

UKURASA ULIOPITA TULIPO ISHIA.............

“kuhusu kutumia upanga sasa umeiva vyema kama nilivyokuwa nahitaji na nakuomba tu usikae ukalitumia panga wala kutembea nalo sehemu nyingi unazo enda kwani siku utakayo amua kuutumia upanga wako inawezekana ukawa mtu hatari sana kitu ambacho kitapelekea kuleta taharuki kubwa miongoni mwa watu mbali mbali, kwahiyo hii italeta kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wanao kuzunguka. Leo nakupa huu upanga kama zawadi ya pekee, huu ni upanga ambao nimekuwa nikiutumia Kwa zaidi ya miaka thelathini sasa na kuulinda sana kwa miaka yangu yote na kwa nguvu zangu zote, huu upanga ni hazina kubwa sana ndani ya nchi ya Japan kwahiyo unapaswa uutumie vyema ikiwemo na kuulinda kama unavyo yalinda macho yako.
Chamwisho huu upanga utumie pale itakapo kubidi ila tu usiutumie vibaya kwa kuwadhuru watu wasio kuwa na hatia yoyote ile hiyo itapelekea nikuue kwa mikono yangu mwenyewe kitu ambacho hakitakiwi kutokea kwa sababu mimi ndiye ninaye takiwa kukulinda kwa namna yoyote ile.

ENDELEA...................

Baada ya siku mbili kupita Calvin alipelekwa kwenye moja ya vyumba ambavyo vilikuwa na ukimya mkubwa mno kiasi kwamba huwezi kusikia kitu chochote kile.
“zoezi la mwisho kwa hii miezi miwili na nusu iliyobakia ni hisia, una hiyo milango yako mikubwa ya fahamu mitano lakini usisahau hisia ndo kitu cha mhimu zaidi kwako, hayo maskio yako yanatakiwa yawe yanafanya kazi kuanzia umbali wa mita mia moja ili kuweza kusikia kitu chochote ambacho kinaendelea kwa umbali huo” aliongea master na mara moja utekelezaji ulianzia hapo, mazoezi haya yanahitaji utulivu mkubwa sana kuanzia mapigo ya moyo na namna mtu unavyokuwa unapumua, kwa kufuata maelekezo Calvin alikuwa anayafanya vyema sana kitu ambacho kilimpatia furaha sana master Haru .

Tarehe 12 mwezi wa 3 mwaka 2015 ikiwa imepita takribani miaka miwili na zaidi ya miezi 6, ndiyo siku rasmi ambayo YOUNG BILLIONAIRE Calvin Jackson alikuwa anakamilisha mafunzo yake ndani ya nchi ya Japan.

“kwa sasa naweza nikasema umekuwa miongoni mwa wanaume wa shoka sana lakini ili niweze kuliamini na kulithibitisha hilo bado una kazi moja ya kuifanya, nadhani unakumbuka vyema nilikuahidi ili niweze kukujibu maswali yako na kukuruhusu kuondoka kuna mtihani wa kuufanya, una dakika tatu tu pekee za kuufanya, unapaswa ufanikiwe kunipiga ngumi moja tu kwenye mwili wangu, hicho kitu ni rahisi sana kukitaja lakini utekelezaji wake ni mgumu sana, haya sitaki maelezo mengi kazi ni kwako kama uondoke au ubaki ila ukumbuke tu ukishindwa nafasi ya kuondoka tena itajitokeza baada ya miaka mingine miwili ijayo” ni maneno rahisi sana yalitoka kinywani mwa mzee huyu lakini yalikuwa ni magumu mno kwenye suala la kuyatekeleza.

Calvin alizikunja ngumi zake vizuri kisha akamwendea kwa spidi ambayo ilimfanya mzee huyu akubali kwamba bwanamdogo alikuwa ameiva haswa, Calvin alirusha ngumi nzito zaidi ya kumi na mbili kwa sekunde nane pekee lakini hakubahatika hata kumgusa mzee huyu, kabla hajarudi nyumba alirusha mateke kwa mkupuo kisha akiwa hewani akizunguka na double kick kwa kasi ya ajabu sana lakini alishangaa kumwona mzee huyu amesimama nyuma yake akiwa anamwangalia mikono yake iko nyuma, wakati anamwangalia mzee huyu alionyesha kusikitika tu na kuangalia upande wa saa, ilikuwa imebakia dakika moja tu pekee, Calvin jasho lilimtoka kwa maana alikuwa na sekunde sitini pekee za kumsaidia na kujitetea ili aweze kutoka nje ya kambi hiyo. Mzee haruto alimkumbusha tena “kuna muda unapaswa kutumia zaidi akili kuliko nguvu” kisha akapotea mzee huyu na kusimama upande wa pili Calvin aliogopa hii hakuwahi kuiona kabla alicho amua kukifanya ni kujaribu bahati yake kwa kutumia hisia, basi akayafumba vyema macho yake halafu alimfuata mzee huyo kwa kasi sana akatishia kama anarusha ngumi maeneo ya kichwani kisha akasimama ghafla, wakati ule mzee Haruto alikuwa amepotea ili kuikwepa ngumi ile lakini raundi hii alikuwa na bahati mbaya, kwani wakati anakwepa ngumi ya kwanza Calvin alikuwa tayari amesimama na kuzitumia vyema hisia zake, kwa mbali alisikia kama kuna upepo unapita karibu yake kwa kasi sana, alijibetua kwa teke moja safi sana ambalo lilimrudisha mzee Haruto kama hatua kumi nyuma. Ilikuwa ni mara ya kwanza kupigwa na binadamu na kusogezwa umbali mrefu kiasi hicho, alitabasmu na kuangalia saa ilikuwa sekunde ya hamsini na tisa dakika ya pili.

Alitamka “now you free to go (sasa uko huru kwenda) na nitakujibu maswali yako kuhusu mimi na baba yako”.

Bux the story teller

"Ni zaidi ya miaka thelathini iliyopita katika nchi ya Malaysia ndani ya jiji la QuaraRumpa, ni miongoni mwa majiji mazuri sana na majiji pendwa yaliyojengwa kwa ubora mkubwa sana hapa ulimwenguni. Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka kwahiyo ni muda ambao watu mbali mbali kutoka sehemu mbali mbali duniani huwa wanasafiri sehemu tofauti tofauti ulimwenguni kuweza kufurahia sikukuu za kufungia mwaka pamoja na likizo mbali mbali. Ni muda ambao nilikuwa kwenye mapenzi mazito sana na mwanamke mmoja ambae nilimpenda sana na ndiye alie nipatia mtoto wa pekee ambaye nae nimeishia kumpoteza, nilipewa likizo ya miezi sita baada ya kumaliza mafunzo yangu ya ukomando, basi niliichagua nchi ile ambayo nilikuwa naipenda sana kutoka moyoni.

Nakumbuka ilikuwa ni wikiendi majira ya usiku nilitoka na mpenzi wangu tukaenda hotelini kuweza kupata chakula cha usiku lakini kwa bahati mbaya sana baada ya kushuka kwenye tax niliyokuwa nimepanda nilidondosha waleti yenye pesa, kadi za bank na kila kitu kwenye ile tax bila hata kujua, tulifika hotelini na kuagiza chakula cha gharama sana kwa sababu sikuwa na shida kabisa ya pesa, tulivyo maliza kula chakula akaja mhudumu kudai malipo yake, lahaula ile naingiza mkono mfukoni nilishtuka sana sioni kitu chochote, hakuna alie weza kuniamini mle ndani wote walijua mimi ni mhuni na sikutaka nijitambulishe kama mimi ni komando kwa sababu nilikuwa ni mtu wa siri sana.
Mhudumu aliamua kuwaita walinzi ili wanikamate kwani walishahisi mimi ni mwizi, lakini kabla ya hilo kutokea kuna kijana mmoja alikuwa amekaa kwa muda kidogo na maeneo yale akiwa kavaa suti huku ameshika begi yake nyeusi, nilimuona tangu naingia mle ndani ila sikuwa hata na mpango nae kwani uwepo wake pale ulikuwa haunihusu kwa lolote, na kwa mwonekano wake haikuhitaji hata kujielezea kwamba ni mtu mwenye pesa za kutosha. Alinyanyuka taratibu kusogea upande ule ambao nilikuwa nimekaa na sikujua alikuwa na lengo gani.

Alivyofika pale hakutaka mambo mengi, aliwakataza watu wasifanye chochote kama tatizo ni pesa basi atalipa yeye pamoja na gharama za usumbufu, alikuwa kijana mpole na smati sana nilivutiwa naye, lakini niliipenda kauli yake moja “hata kama mnamdai mtu kiasi gani, mnapaswa kuelewa na kuuthamini utu wa mtu kwanza, sina imani kama mtu huyu alikurupuka kuja hapa lazima alijipanga lakini inawezekana kuna shida imetokea ndio maana akafikia kukosa pesa, mlipaswa kumsikiliza kwanza” kisha akalipa pesa milioni kumi taslimu akidai zingine ni za usumbufu, baada ya hapo akanipa pole na kuanza kuondoka, kwanza nilibaki nimeduwaa tu nisielewe cha kufanya.

Mimi ni komando nimezunguka sehemu nyingi sana duniani na nimekutana na watu wa kila aina lakini sikuwahi kufikiria kwamba watu wema wa namna hii bado wapo duniani wakiendelea kuishi. Kwenye maisha yako unapaswa kumheshimu sana mwanadamu ambaye anakusaidia wakati una uhitaji mkubwa sana wa hicho kitu na ulikuwa huna namna ya kukipata alafu mtu huyo anakusaidia na hana hata shida na hiyo asante yako, mwalimu wangu jeshini aliwahi kuniambia siku moja kwamba mtu anae kusaidia shilingi miatano ukiwa una uhitaji nayo ni mtu muhimu na wa thamani zaidi kuliko mtu anae kuja kukupa milioni mia moja ukiwa hauna shida na hiyo pesa, siku ile nililithibitisha hilo kwani nina pesa nyingi sana lakini siku ile nilikuwa nahitaji pesa ya kawaida tu ili nilipie bili lakini sikuwa nayo kwa muda ule, wanadamu wa hivi wamebaki wachache mno ukizingatia na kiwango alicho kitoa pale angeweza hata kununulia gari ndogo au kwenda kufurahi nchi yoyote ile, siku ukimpata mtu wa aina hii haupaswi kumpoteza kwa namna yoyote ile hata Kama ni kwa gharama ni wachache mno kwenye hiki kizazi.

Basi haraka sana nilimkimbilia kabla hajaingia kwenye gari ili niweze angalau kumfahamu hata jina

“hey bro” nilimuita akageuka

“oooh ni wewe mr nilijua unaendelea kula ndiyo maana sikutaka kukusumbua”

“no kula nishamaliza, hivi wewe ni nani na umetoka wapi?”

“Jackson Aron, natokea Tanzania” alinijibu kifupi

“daaah aisee nafikiri nchi yako inastahili heshima kubwa sana, mtu hata hunijui lakini umeamua kunisaidia kwa kunitolea pesa nyingi kiasi kile alafu ajabu hutaki hata asante yangu nimeshidwa hata kukuelewa ndugu yangu”

Alitabasamu kijana yule kisha akanijibu “pesa ni muhimu sana lakini pesa ni watu, pesa inatengenezwa na watu, pesa inatumiwa na watu hiyo inamaanisha bila pesa mtu unaweza ukaishi hata kama ni kwa shida lakini pesa haiwezi kuwepo bila watu. Hiyo inatukumbusha kwamba ubinadamu na utu ndio msingi mkubwa wa haya maisha mafupi tunayo yaishi kila siku kwa sababu kuna siku sitakuwa na pesa ila nitasaidiwa na kuzikwa na watu, na unapaswa uishi ukielewa kwamba ukipata nafasi ya kumsaidia mtu usisubiri malipo wala asante kutoka kwake ila tu kupitia msaada wako nayeye ataenda kusaidia wengine nao wengine watasaidia wengine, na hivyo ndivyo mimi ninavyoishi na nilivyo lelewa na wazazi wangu kwahiyo usijali kabisa kwa kilicho tokea pale japo unapaswa tu kuwa makini na siku nyingine”.

*********************************

Tangu nianze kuyaishi maisha yangu yote kwenye dunia hii iliyo jaa dhuluma na dharau, baba yako mzee Jackson ndiye binadamu wa kwanza kunihakikishia kwamba hata kuwe na watu wabaya kiasi gani ila kwenye hilo kundi watu wema huwa wanakuwepo japokuwa ni wachache mno, yule ndiye mwanadamu wa kwanza mimi kunivutia kwa maelezo yake hapa duniani.

Tangu siku ile sikuhitaji kumpoteza miongoni mwa wanadamu wachache sana ambao walikuwa ni bora sana kuwahi kuishi kwenye uso wa dunia hii, nilimuomba tukakae sehemu bahati nzuri hakuwa mbishi akakubali, niliamua kumuelezea uhalisia wa maisha yangu, nilimwamini na kumpatia siri zangu haraka kwa sababu maelezo yake yalikuwa yapo tofauti na wanadamu wengine. Nayeye aliniweka wazi kwamba yupo pale kibiashara aliagizwa na baba yake Aron Mavunde,alikuwa na mkutano na tajiri mmoja kwenye lile jiji ameshamaliza na kesho yake alikuwa anatarajia kurudi nchini Tanzania.

Basi kuanzia siku ile tulikuwa watu wa karibu sana kiasi kwamba tulianza kutembeleana kuna muda alikuwa anakuja Japan na nilifanikiwa kumuunganisha na matajiri wengi sana ndani ya Osaka kwa sababu alikuwa anapenda sana biashara lakini hata yeye pia aliweza kuniheshimisha kwenye familia yao, ilikuwa ni kama familia yangu pia na babu yako mzee Mavunde, alikuwa ananiita mimi ni pacha wa baba yako. Nilikuwa mpweke sana lakini nilivyo ipata familia ile maisha yangu yalikuja kuwa ya furaha kubwa sana.

Unaweza ukajiuliza kwamba ni kwanini nilikuwa karibu na familia yako alafu wewe haukuwahi hata kunifahamu. Baada ya kuimarisha urafiki mkubwa baina yangu na baba yako, nilikuja baadae kuhisi kwamba kuna watu wananifuatilia kwa sababu nilikuwa jasusi, baadae nilifikiria sana ninaweza kuiingiza familia ile matatizoni, niliamua kuanza kuishi kwa siri sana na sikuhitaji kuwa karibu sana na familia ile, nilimuita baba yako kwa siri nikamweleza kila kitu na akanielewa. Tangu hapo nilikuwa nakuja Tanzania kwa siri sana na mara nyingi nilikuwa nikitumia sura bandia kila napokuja, pale kwenu nilikuwa ninakuja kama mfanyabiashara na usingeweza kunijua kwani nilikuwa kila nikija nadadilisha sura ila wewe nakujua tangu mama yako ana mimba yako na mpaka siku unazaliwa nilikuwa kwenu.

Nimekuwa nikiishi hivyo kwa siri sana kwani nchi nyingi sana zinanihitaji ili zinitumie kwa mambo yao kwa sababu ya uwezo nilio nao, bahati mbaya sana kwao siwezi kuruhusu hicho kitu kitokee kamwe ni bora nife, hata siku baba yako anauawa ilitakiwa nije nikuchukue haraka sana lakini nilichelewa kupata taarifa mapema na ndiyo sababu hukuona msaada wowote wa haraka, hata hivyo baba yako alitumia akili kubwa sana kukuelekeza kwangu kabla hajafa sababu kubwa alijua hakuna mwanadamu aliye hai ambaye anaweza kukugusa hata kucha yako tu unapokuwa kwenye mikono yangu, hii nyumba yangu ni miongoni mwa sehemu chache sana duniani zenye ulinzi mkubwa sana , siku nimemtuma Akio akufuate Tanzania kabla hajafika airport ndio muda ulio nipigia simu ikawa rahisi sana kukupata, ukiachana na hilo nilifurahi kwa ujasiri wako wa kuweza kufika mpaka japani pekeako bila msaada wowote.

Kule Tanzania kuna binti yangu ambae naye sitaki atambulike kabisa ndio maana huwa tunaonana mara chache sana, binti huyu ni mtaalamu sana wa mambo ya mitandao, nilimpeleka Tanzania kwa sababu najua kule ni salama kwake kwahiyo nikaamua awe anasoma chuo kule, alikuwa anasoma chuo kama tu sehemu ya kutoa upweke kwa sababu alichokuwa anakisoma tayari alikuwa anakijua sana miaka mingi hivyo niliamua kumuachisha kabisa masomo. Jina lake anaitwa Yevada, hili ni jina ambalo nilihitaji awe analitumia kwa sababu za kiusalama ila pia ana jina lake la shule hilo sitakutajia ila kama ukibahatika kukutana nae atakueleza mwenyewe, ni binti mzuri sana na kama utafanikiwa kuwa nae karibu basi jukumu la kumlinda ni juu yako na uhakikishe hakutwi na tatizo lolote lile, code zake za kumpata ni T9M79, akikuuliza nani mjibu M45Haru atajua umeagizwa namimi, kwenye suala la kuonana mtajuana wenyewe ila hakikisha anakuwa salama huyo binti.

Nini kimejificha nyuma ya hili? iweje mzee huyu Haru adai kwamba ana mtoto wa kike ambae yupo Tanzania ingali sisi tunajua kwamba alikuwa na mtoto mmoja wa kiume ambae alifariki? Je Calvin atafanikiwa kumpata Yevada?.. .......

Kwa Leo natundika Daruga katika ukurasa wa 14 sina la ziada tena tukutane wakati ujao kwenye kalamu ya professor.

Chao

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
FB_IMG_1656868568665.jpg
 
Imefika patamu sana, shukrani mkuu endelea kubaki kwenye kutimiza ahadi Yako hivi si ulisema kimoja Kwa siku eee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom