HADITHI : Ugonjwa unaoua

HADITHI : Ugonjwa unaoua

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,662
1. UGONJWA UNAOUA

Hadithi hii inamuhusu kijana Fredinho Piscus. Alikuwa miongoni mwa vijana walioishi katika Mtaa Complexo da Mare, moja ya mtaa wa kimasikini uliokuwa katika Jiji la Rio de Janeiro. Nyumba za huko zilikuwa zimebananabanana, watu walijenga hovyo huku usalama wa maisha ya watu katika mtaa huo ukiwa wa chini kabisa.

Mama yake aliuawa miaka ya nyuma mara baada ya kuwatapeli wauza madawa ya kulevya mzigo wao, kuanzia hapo, kijana huyo akaanza kuishi maisha ya kimasikini mpaka alipochukuliwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na uwezo kidogo.

Mbali na umasikini aliokuwa nao, Fredinho alikuwa na sura nzuri mno. Wasichana wa Kibrazil walimuonea wivu kwani kila walipomwangalia, alifanana sana na msichana. Watu wengi wakavutiwa naye, hata wale wageni walioambiwa kwamba Fredinho alikuwa mvulana, walibisha kwani aliokuwa na sura ya kisichana.

Kwa sababu watu walimwambia kwamba yeye ni msichana, mwisho wa siku akajikuta akiwa na marafiki wa kike kabisa. Kuna siku akafuatwa na kijana mmoja aliyemvutia uchochoroni na kumwambia kwamba alikuwa msichana, japokuwa alikataa katakata lakini kijana huyo alimwambia kwamba Mungu alijisahau, badala ya kumuewekea mbegu za kike, akamuwekea za kiume.

Uchochoroni hapo, kijana huyo akaanza kumlawiti Fredinho. Alisikia maumivu makali mno huku kijana yule akisisitiza kwamba Fredinho alikuwa msichana. Kuanzia siku hiyo, Fredinho akaanza kuuzoea mchezo huo, akawa hataki kabisa urafiki na wanaume.

Stori zilipozagaa mtaani, kutokana na uzuri wake, wanaume wanaanza kumfuata, hakuwakatalia, aliposifiwa tu kwamba ni mwanamke, akawa hana la kufanya.
Siku moja Fredinho akapigiwa simu na msichana aitwaye Sandra, huyu alikuwa ukuwadi mkubwa kabisa Jijini Rio De Janeiro. Msichana huyo akamwambia Fredinho kwamba kulikuwa na mwanaume wa Kimarekani aliyeitwa bwana Powell ambaye alitaka kumuona, walipoonana, mzee huyo akampenda Fredinho na mwisho wa siku kuanza kufanya naye ngono.

Bwana Powell alipotaka kurudi Marekani, hakutaka kumuacha Fredinho Brazil, akaondoka naye na kuanza naye maisha kama mke wake, walifanya mambo yote kama mke na mume wanavyofanya.

Ndani ya nyumba hiyo, kulikuwa na msichana anaitwa Cindy, huyu alikuwa mfanyakazi wa bwana Powell. Alipomuona Fredinho, akatokea kumpenda mno na hivyo kutaka kufanya naye mapenzi, hakujua kama kijana huyo hakuwa mwanaume rijali.

Alimtongoza sana Fredinho ila alimkatalia katakata. Siku moja msichana huyo akalazimisha, akamwambia kwamba akikataa, basi atabaki chumbani mpaka bwana Powell atakaporudi, Fredinho akawa mpole, akamwambia aondoke na kesho watafanya mapenzi kama anavyotaka.

Cindy anaondoka, Fredinho anabaki na mawazo, afanye nini ili amridhishe msichana huyo na wakati yeye si mwanaume rijali? Anachokifanya ni kununua kiungo cha kiume cha bandia na hicho ndicho anaanza kukitumia kwa msichana huyo kila anapotaka kuonana naye huku akiwa ameweka masharti ni lazima mapenzi wafanye usiku ili asijulikane, msichana huyo anaridhika pasipo kujua ni mambo gani yatatokea huko mbele.
 
Back
Top Bottom