Natasha Ismail
JF-Expert Member
- Jul 14, 2008
- 756
- 693
kaka ni hadith hii kumbuka.Sawa muendelezo mzuri ila nakumbuka alipewa million 1 lkn sikumbuki alitumia wapi na kwanini alikopa laki wakati alikuwa na million

usimkatalie kwanza,muulize kama anapesa zakututunza familia nzimaWe kivuruge kipi kinachokuchesha
Mmh napata hisia chafuuu na huu utekaji
Hatari sana mkuu chiloSEHEMU YA 24
Safari ya kuelekea Mkwajuni ilikuwa ikiendelea, kila mmoja alikuwa kimya ndani ya gari, Maganza alikuwa akiwaza ni kwa namna gani alishindwa kupakumbuka nyumbani kwa Bazoka huku yeye Bazoka akiwaza ni kitu gani kingetokea endapo angefika nyumbani kwake alipokuwa amepanga.
Hakuwa na mke huko na hakuwahi kuishi na mke, alihofu kwa kuwa angeonekana muongo na kumpa mwanya Maganza kugundua kilichokuwa kimetokea ama hata kuhisi tu kwa kidogo.
Ilikuwa ni lazima afanye jambo lakini tayari alikuwa amekwishachelewa, hivyo alitakiwa kukubaliana na kile ambacho kingekwenda kutokea huko.
Hawakuchukua dakika nyingi sana wakafika huko Kinondoni, wakateremka kutoka garini na kuingia ndani ya nyumba moja kubwa, ilizungushiwa ukuta na ndani yake kulikuwa na wapangaji wawili, wa tatu alikuwa Bazoka.
Wakawasalimia, Bazoka akachukua ufunguo na kuufungua mlango wa kuingia sebuleni. Sebule ilikuwa nzuri sana, ilivutia machoni mwa kila mtu aliyekuwa akiiangalia, ilipangwa vizuri na ilikuwa ni rahisi kusema ilikuwa moja ya sebule iliyokuwa imikilikiwa na mtu mwenye pesa.
“Hapa ndipo unapoishi?” alimuuliza huku akimwangalia.
“Ndiyo!”
“Na kule Mbezi?”
“Ndiyo nikulize wewe,” alisema Bazoka na kuanza hukucheka, akafungua friji na kutoa juisi, akammiminia Maganza na kunywa kidogo, aliporidhika, akamwambia angerudi, alitaka kuzungumza na wapangaji wenzake.
Moyo wa Bazoka ukapiga paa! Hakuamini kama mpelelezi huyo angechukua jukumu kama hilo. Aliwafahamu wapangaji wenzake vilivyo, hawakuwa kumuona mke wake wala mtoto wake hata siku moja, sasa endapo angekwenda kuwauliza ilikuwa ni lazima kumwambia hakuwa akiishi na familia yake.
Akatamani kumzuia lakini hilo lilishindikana, Maganza akasimama, akaliweka vizuri shati lake na kuanza kuusogelea mlango, akasimama katikati, halafu akamgeukia Bazoka.
“Usitoke! Nisubiri humuhumu ndani. Tena litakuwa vizuri nikienda na simu zako zote mbili,” alimwambia, hapohapo Bazoka huku akionekana kuogopa, akampa simu mwanaume huyo, akatoka nazo.
Maganza akatoka na kuelekea kwenye mlango wa chumba kimoja na kuugonga, mpango ukafunguliwa na msichana mmoja mrembo, alikuwa na weupe wa kununua dukani na nywele zake alizikata na kuweka brichi iliyoonekana kukolea hasa.
Akamwangalia mwanaume aliyekuwa akigonga mlango, kwa jinsi alivyoonekana tu alikuwa mtu hatari, mwili uliojengeka kimazoezi zaidi na kumwambia alitaka kuingia ndani.
“Wewe ni nani?” aliuliza msichana huyo.
“Polisi!” alimjibu na kumuonyesha kitambulisho chake, akaridhika naye na kuingia ndani.
Humo kulikuwa na wanaume wawili, walikuwa vifua wazi na hakujua walikuwa wakifanya nini muda huo ila kwenye meza kulikuwa na vipande kadhaa vya sigara na chupa za pombe zilizokuwa wazi.
Vijana hao wakamwangalia Maganza, walionekana kuogopa mno, kwa jinsi alivyokuwa amejitambulisha kwa msichana yule na kugundua alikuwa polisi, iliwatia hofu kwani mbali na kuwa na vipisi vya sigara pia walikuwa na misokoto ya bangi waliyokuwa wamevuta, waliizima lakini harufu iliendelea kutawala chumba hicho. Hakutaka kujali sana kuhusu bangi hizo, haikuwa kazi yake kukamata wavuta bangi.
“Unamfahamu mpangaji mwenzako?” alimuuliza msichana aliyemfungulia mlango.
“Yupi?”
“Huyo wa chumba cha kulia!”
“Ndiyo namfahamu!”
“Unaifahamu familia yake?” alimuuliza.
“Ndiyo! Ana mke na mtoto mmoja wa kiume.”
“Umeshawahi kuiona?”
“Ndiyo! Huwa ninaoshaga vyombo na mkewe na kushirikiana kwenye mambo ya usafi! Ila sasa hivi simuoni, nadhani kasafiri!” alimjibu.
“Sawa.”
Maganza hakutaka kukaa sana humo, akatoka na kuelekea chumba cha pili ambapo baada ya kufunguliwa mlango, akaingia na kuanza kuzungumza na mtu aliyekuwa akiishi humo.
Alichoambiwa chumba cha kwanza napo humo aliambiwa hivyohivyo kwamba kweli Bazoka alikuwa na mke na mtoto mmoja kitu kilichomfanya kuchanganyikiwa kweli, sasa akaanza kujiuliza kuhusu yule mwanamke aliyekutana naye Mbezi Beach.
Kama kweli yule alikuwa mke wa Bazoka na kumwambia kuwa hawakuwahi kuishi huko Magomeni, sasa kwa nini nyumbani pale, Kinondoni aliambiwa waliifahamu familia ya Bazoka?
Labda inawezekana alikuwa na wake wawili, kwa maana ya yule wa Mbezi Beach na Kinondoni, sasa kwa hakuwa akipakumbuka kule Mbezi Beach alipokuwa amekwenda? Nini kilitokea?
Kila kitu alichokuwa akijiuliza mahali hapo hakuwa na majibu nacho, alihisi kabisa kulikuwa na sehemu kulipokuwa na makosa lakini kubwa na baya zaidi ni kwamba hakupafahamu mahali kulipokuwa na kosa.
Akarudi chumbani kwa Bazoka, akamkuta mwanaume huyo amekaa kochini huku akiangalia televisheni. Moyo wa Bazoka ulikuwa na hofu nzito, alihisi tayari wapangaji wake walimchoma kwani hakuwa amewaambia lolote lile kwa kuwa ujio wa Maganza ulikuwa ni wa ghafla sana.
“Unaelekea wapi sasa hivi?” alimuuliza baada ya kuingia.
“Labda ofisini kwako nikachukue gari langu!” alimjibu.
“Oh! Kumbe uliacha gari ofisini. Twende ukalichukue!” alimwambia.
“Sawa,” alisema Bazoka, akainuka na kuanza kumfuata.
Wakaingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Bazoka alitamani kujua kilichokuwa kimetokea, alihitaji kufahamu alichowauliza wapangaji zake lakini kila alipotaka kufanya hivyo moyo wake ulisita.
Alimwangalia Maganza, alionekana kuwa na mawazo tele, hakuwa sawa kabisa. Tangu alipomfahamu mwanaume huyo hakuwahi hata siku moja kumuona akiwa na furaha, yaani kila siku alikuwa kama alivyokuwa.
Alijua masuala yake yalimsumbua sana, kuanzia kwa Yusufu aliyekuwa amemuua na mwili wake kuutupa msituni, kwa Bi. Semeni na hilo lililotokea alijua yalimchanganya sana.
Akaanza kufikiria suala lile kuelekea Mbezi Beach, mwanaume huyo alimfuatilia kwa karibu lakini mwisho wa siku walipofika huko, alimwambia hakukumbuka alipokuwa akiishi.
Hilo likampa nguvu Bazoka kwamba ule ulimwengu aliokuwa akiutumikia ndiyo uliokuwa ukifanya hayo yote. Alishukuru, alijiona kuwa salama kabisa, moyo wake ulikuwa na furaha kupita kawaida.
Walichukua dakika kama ishirini mpaka kufika kituo kikuu cha polisi, akateremka akachukua gari na kuondoka zake, sasa akafikiria kurudi zake ofisini kwani kulikuwa na kazi alizokuwa akitakiwa kumalizia.
Safari ya kurudi ofisini kwake iliyokuwa Posta jijini Dar es Salaam ikaanza, hakuchukua dakika nyingi kwani ilikuwa ni karibu na hapo kituoni, akafika na kuelekea ndani.
Alipofika mlangoni tu, mlinzi alishtuka kumuona, ni kama akawa haamini alichokuwa akikiona mbele yake. Alionekana kama kumuogopa fulani hivi mpaka Bazoka akaanza kuhisi kitu.
“Kuna nini?” alimuuliza huku akimwangalia.
“Ulitoka muda gani?” aliuliza mlinzi huku akimwangalia.
“Asubuhi! Kwani kuna nini?”
“Tangu asubuhi? Ila ulirudi!” alisema mlinzi.
“Nilirudi kivipi Abdu?”
Bazoka akapuuzia, akaanza kuelekea ndani. Kila mfanyakazi aliyekuwa akimuona alimshangaa, hakuamini kile alichokiona, Bazoka hakutaka kujali sana, akaanza kuelekea ofisini kwake, alipofika kwa sekretari wake, akapigwa na mshtuko.
“Bosi....” aliita kwa mshtuko.
“Unasemaje?”
“Umetoka muda gani?”
“Kivipi?”
“Ulikuwa ofisini!”
“Nilikuwa ofisini?”
“Ndiyo!”
“Muda gani?”
“Kama masaa mawili yaliyopita, na hukutoka maana nilikuwa hapahapa!” alimwambia.
“Hahaha! Angel unanitania.”
“Ndiyo ukweli!”
“Hapana! Nilivyokuaga asubuhi, sikurudi ndiyo narudi sasa hivi!” alimwambia.
“Ila ulirudi! Ukaingia ndani, ulionekana kuvurugwa!”
“Mimi?”
“Ndiyo!”
“Nahisi utakuwa unaota. Niletee kahawa,” alimwambia na kuelekea ofisini kwake.
Akaufungua mlango na kuingia ndani, akapigwa na mshtuko, macho yake yakatua kwa mtu aliyekalia kiti, alikuwa akiangalia dirishani, yaani alimpa mgongo, alivalia kama alivyovalia.
Hakujua alikuwa nani, akabaki akiwa amesimama huku akimwangalia. Kwa nini alikuwa ofisini humo? Alipewa ruhusa na nani na alikuwa nani? Akaanza kumsogelea, yule mtu ni kama alisikia hatua zake, akakizungusha kiti na kumgeukia Bazoka, wakaanza kuangaliana, Bazoka akashangaa, alimwangalia mwanaume yule, alikuwa akijiona yeye mwenyewe, yaani ni kama alikuwa akijiangalia kwenye kioo.
“Wewe ni nani?” alimuuliza huku akiwa ameshtuka.
“Naitwa Emmanuel Bazoka! Wewe ni nani?” alijibu mwanaume yule na kumuuliza, Bazoka akabaki akishangaa, majina aliyojitambulisha yalikuwa ya kwake.
“Unasema unaitwa nani?” aliuliza kwa mshangao.
“Inabidi uniambie wewe, nishakwambia jina langu!” alijibu mwanaume yule, yaani ni kama alikuwa pacha wake, alivyokuwa akiongea, sauti ilikuwa kama yake, jinsi alivyokuwa akitabasamu, cha ajabu hata nguo alizovaa zilikuwa kama zake.
Hapo ndipo akapata jibu ya yale aliyokuwa ameambiwa na wafanyakazi wake na wengine kumshangaa ilimaanisha mwanaume huyo aliingia ofisini kwake na kujifanya kwamba ni yeye, alitoka wapi na alikuwa akihitaji nini?
Hakuwahi kuwa na pacha yeyote yule, hakuwahi kuambiwa hivyo hata siku moja, alimwangalia vizuri, mwanaume yule alisimama na kuanza kumsogelea, alivyokuwa akitembea, naye alikuwa akichechemea kama yeye kutokana na kile kidonda cha mguuni.
“Wewe ni nani?” aliuliza mwanaume yule huku akimwangalia
“Bazoka!”
“Bazoka gani? Unamaanisha mimi ni wewe?”
“Hapana! Nahisi wewe ni mimi!” alijibu mwanaume yule, mara ghafla wakaanza kusikia mlango ukigongwa, alikuwa yule sekretari aliyemwambia ampelekee kahawa.
“Mfungulie huyo!” alisema yule mwanaume, akarudi kitini na kukaa, sasa naye akaanza kuangalia mlango, alihitaji kufahamu ni nani aliyekuwa akigonga, Bazoka akaufungua mlango na sekretari kuingia akiwa na birika ambalo ndani yake kulikuwa na kahawa.
Je, nini kitaendelea?
Niko apa
Hivi story haifai kusoma usiku kabisa basi tuSEHEMU YA 24

Hahahahah
shunie embu njoo huku ndugu yangu
Kwani ukinywa maji lita moja nani atakuuliza kwa mfano?Bro zama PM unachafua uzi bana .. au anzisheni thread mtongozane
Nakupenda sana shunieHahahahah
Mfyuu embu acha uoga wako,inatisha wapi sasaHivi story haifai kusoma usiku kabisa basi tu
Nyemo tantee
kwani unateseka na niniMnazingua sana anzisheni thread muitane huko ...