Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

Hadithi: Uchawi wa bilionea Bazoka

SEHEMU YA 23.

Bazoka akapokea simu na kuanza kuzungumza na Maganza na kuomba kuonana naye. Kwa Bazoka ilikuwa vigumu kwa sababu alikuwa na mambo yake mengi, akamwambia hivyo.
Kwa sababu Maganza hakuwa na haraka sana, akakubaliana naye ila akamwambia kesho yake ilikuwa ni lazima kufika hapo kwani alikuwa na mengi ya kumuuliza zaidi.
Baada ya kuzungumza, akakata simu, alitulia kwenye kiti chake na kuanza kumfikiria Bazoka. Moyo wake ukagawanyika, kulikuwa na upande ulimwambia inawezekana mwanaume huyo alihusika kwenye mauaji ya Bi. Semeni lakini upande mwingine ulimwambia hakuwa amehusika kwa lolote lile.
Alibaki akiwa katikati. Hakujua ni upande upi alitakiwa kukubaliana nao kwani ulimfanya kuchanganyikiwa kupita kawaida. Alitulia kwa dakika kadhaa, akainuka na kuelekea ofisini kwa bosi wake, Masumbuko na kuanza kuzungumza naye.
Alichomwambia ni kile alichokuwa amekutana nacho, jinsi maisha ya Bazoka yalivyokuwa na wasiwasi mkubwa, alivyokwenda kwa mke wake na kuzungumza naye, Masumbuko alibaki akimsikiliza mpaka alipomaliza.
“Kwa hiyo mke anasema hawakuwahi kutengana?” aliuliza.
“Ndiyo!”
“Na huko Magomeni hajui lolote lile kuhusu hilo?”
“Ndiyo!”
“Na ulipomuuliza kuhusu mume wake zaidi, labda kama alisafiri?”
“Aliniambia alisafiri na kwenda Uganda, alikaa huko kwa wiki mbili, hizo wiki ndizo ambazo alikuwa akiishi nyumbani kwa marehemu,” alimwambia.
“Mh!”
“Ndiyo hivyo bosi! Nadhani yeye ndiye aliyemuua Bi. Semeni!”
“Kwa nini umehisi hivyo?”
“Kutokana na hayo niliyokwambia. Swali linabaki moja tu, kwa nini alimuua?” alimwambia.
“Hapana. Maswali yanabaki mawili!”
“Na lipi jingine?”
“Kwa nini mwili wa marehemu ulikutwa umepigwa kitu kama kucha? Zile kucha za mnyama gani na aliingiaje kwake?” aliuliza maswali hayo yote.
“Mh! Nayo sijui! Ngoja nimalizane na Bazoka, nahisi naweza kupata majibu yote hayo!” alisema.
Alipomaliza, akainuka, akapiga saluti na kuondoka ofisini hapo. Moyo wake haukuwa umeridhika, maswali yote aliyokuwanayo yalikuwa ni muhimu sana na yeye kama mpelelezi ilikuwa ni lazima kupata majibu ya yote hayo.
Akaendelea na mambo yake, ilipofika usiku, akalala, na asubuhi jambo la kwanza lilikuwa ni kumtafuta Bazoka, alihitaji kuzungumza naye.
“Nakuja!” alisema Bazoka na kukata simu.
***
Bazoka alirudi nyumbani kwake akiwa amechoka, alipoingia tu, kwa jinsi alivyomwangalia mke wake, alihisi alikuwa na kitu moyoni mwake, alihitaji kufahamu kitu hicho.
Kwa miaka mingi waliyokuwa wameishi waliishi kwa furaha, kulikuwa na vitu vingi walivyopitia pamoja, walizoeana na alimfahamu sana hivyo alivyokuwa na huzuni, furaha na mambo mengine, alikuwa akiyafahamu yote.
Aisha alibadilika, hakuwa kama siku nyingine, alipomwangalia alihisi kabisa kulikuwa na tatizo, kabla ya kufanya kitu chochote kile, akamfuata na kusimama karibu naye.
“Kuna nini mpenzi?” alimuuliza huku akimwangalia karibu kabisa.
“Umefanya nini?” alimuuliza.
“Kufanya kitu gani?”
“Ulikuwa unatafutwa!”
“Na nani?”
“Polisi!”
“Polisi?” aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Ndiyo! Kuna mwanaume alikuja, alikuwa akikutafuta, aliniuliza baadhi ya maswali kuhusu wewe!” alimwambia.
“Maswali gani?”
“Safari yako ya Uganda, kuishi Magomeni na mambo mengine,” alimwambia.
Moyo wa Bazoka ukapiga paa! Hakuamini alichokisikia, kitendo cha polisi kufika mahali hapo na kumuuliza mkewe maswali kama hayo yalimfanya kukosa amani kabisa, furaha yote aliyokuwanayo ikatoweka. Ila hakutaka kuonyesha mshtuko wowote usoni mwake.
“Safari yangu ya Uganda? Kwamba imefanya nini?” alimuuliza.
“Sijui! Yeye aliniuliza tu. Hivi kuna nini mume wangu?” alimuuliza huku akimwangalia.
Bazoka hakujibu swali hilo kwa undani ila alichomwambia ni kwamba hapakuwa na tatizo lolote lile. Alifanya biashara zake kwa uangalifu mkubwa na alilipa kodi kama alivyotakiwa kulipa.
Baada ya kuzungumza mengi, wakala, wakaoga na kulala. Kichwa cha Bazoka kikaanza kumfikiria polisi huyo, alipomuuliza mkewe, sifa ambazo alikuwa akimwambia, zilikuwa zilezile alizokuwanazo Maganza.
Moyo wake ulikuwa na hasira mno lakini alitakiwa kulificha hilo, alijiamini alikuwa na ulinzi mkubwa lakini pia alikuwa na uhakika hapakuwa na mtu yeyote aliyefahamu kwamba ni yeye ndiye aliyemuua Bi. Semeni.
Siku iliyofuata akiwa ofisini akapigiwa simu na Maganza na kuambiwa aende ofisini kwake kwa lengo la kuzungumza naye. Hilo halikuwa tatizo, akaelekea huko.
Alipofika, akakaribishwa na kukaa kwenye kiti! Walizungumza machache na Maganza kumwambia kuhusu kile kilichotokea.
“Nilizungumza na mkeo!” alimwambia.
“Ulizungumza na mke wangu?”
“Ndiyo!”
“Lini?”
“Jana! Nilifanikiwa kufika nyumbani kwako na kuzungumza naye!” alimjibu.
“Inawezekanaje?”
“Kivipi?”
“Mke wangu alisafiri siku ile niliyozungumza na wewe, sasa iweje wewe ukazungumza naye, tena jana?” alimuuliza.
“Nilionana naye. Nilifika kwako Mbezi Beach na kuzungumza naye!”
“Kwangu Mbezi Beach?”
“Ndiyo!”
“Mimi mbona sikai Mbezi Beach?”
“Hahaha! Bazoka una maneno mengi sana! Unaishi wapi?”
“Kinondoni Mkwajuni!”
“Na nani?”
“NA familia yangu ila imesafiri tangu juzi!”
“Na kule Mbezi Beach?”
“Sijui lolote.”
“Na mwanamke niliyezungumza naye?”
“Nikuulize wewe uliyekwenda kuzungumza naye!”
“Una uhakika huishi Mbezi Beach?”
“Ndiyo!”
“Ngoja nifanye kitu! Twende nyumbani kwako! Nitakupeleka kwa usafiri wangu!” alimwambia.
Moyo wa Bazoka ukapiga paa! Kuhusu kwenda kwake lilikuwa jambo lisilowezekana kwani angeibua matatizo mengine zaidi. Akatamani kukataa lakini ilishindikana kabisa.
Wakatoka ofisini, wakaingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo, safari ya kuelekea nyumbani kwa Bazoka, Mbezi Beach ikaanza huku Bazoka akiwa pembeni na Maganza akiwa analiendesha hilo gari.
Njia nzima Bazoka alikuwa kimya, alikuwa akimwangalia tu MAganza alivyokuwa akiendesha gari. Safari iliendelea, alichokitaka Maganza ni kumuonyesha Bazoka nyumbani kwake na kuzungumza na mkewe tu.
Wakaendelea na safari walipofika Mbezi Afrikana, wakakata kulia na kuchukua njia iliyokuwa ikielekea Ramada. Walikwenda na kwenda, walipofika sehemu ya makutano, hapo Maganza akachanganyikiwa, hakujua akate kulia ama aelekee mbele.
“Nyumbani kwako ni njia ipi?” alimuuliza.
“Nyumbani kwangu ni Kinondoni! Sijajua huku unanipeleka wapi!” alimjibu.
Maganza akasimamisha gari kwa sekunde kadhaa, alikuwa akikumbuka kila kitu lakini cha ajabu baada ya kufika hapo, akasahau njia kabisa. Lilikuwa ni jambo lisilowezekana hata kidogo, alikaa hapo kwa dakika kadhaa, akakata kulia, wakaanza kuelekea mbele.
Walikwenda huko, alipatafuta nyumbani kwa Bazoka hakupaona, akahisi labda hapakuwa huko, akarudi nyuma, akaligeuza gari na kurudi walipotoka, walipofika njia ya kuelekea Ramada, wakaelekea huko.
Alipatafuta nyumbani kwa Bazoka lakini hakupapata na kubwa zaidi hakupakumbuka popote pale hata njia alizokuwa amepitia.
Alisumbuka huku na kule, aliona anachoma mafuta tu kwani kwa saa mbili zote alikuwa akihangaika kupapata nyumbani kwa Bazoka, hakukumbuka palikuwa ni wapi.
“Ni maajabu! Napakumbuka kabisa!” alimwambia Bazoka.
“Basi nipeleke!”
“Sipajui ni wapi! Hivi nilikuja huku ama kule...mbona nimepasahau kabisa?” aliuliza huku hata kwa kumwangalia usoni tu alionekana kuchanganyikiwa, hakupajua nyumbani kwa Bazoka mpaka alipoamua kurudi na Bazoka kumpeleka nyumbani kwake, Kinondoni Mkwajuni alipopanga baada ya kuhama Magomeni.
Maganza akachanganyikiwa mno.

Je, nini kitaendelea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom