Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Mtunzi: R. Michaelray
JF member
Mapaa ya nyumba yanaonekana. Mchukua kamera ambaye yupo kwenye ndege anaendela kufanya kazi yake vyema. Moja kwa moja Picha inaonyesha Benki Fulani ambayo watu wapo katika misururu mirefu.
Ko! Ko! Ko! Ko! Ilikuwa ni sauti ya viatu vya mchuchumio vilivyowafanya watu wageuze shingo zao kuelekea kule sauti inapojia. Macho yao hayakuamini kile walichokuwa wamekiona. Alikuwa ni mwanamke mrembo aliyekuwa akiingia katika benki ile. Alivalia sketi fupi iliyoyashika vyema mapaja yake makubwa yaliyoshikiliwa na Hipsi za kawaida huku huko nyuma kukiwa na Mzigo haswa ambao kutokana na sketi kubana mistari ya chupi iliweza kujichora. Hakuna aliyejuta kumwangalia. Ilikiwa ni bahati sana kwa macho ya mwanaume yeyote kuona kiumbe Kama mwanamke huyu.
Mwondoko wake na mwili wake ulivyokuwa ukitingishika ulizidi kumfanya azidi kuvutia. Ilikuwa Kama anaamua vile kwani mwendo wake na sauti ya vile viatu alivyokuwa amevaa vilikuwa vinaendana haswa.
Moja kwa moja aliiingia kupitia Mlango ulioandikwa Only Staffs na kuacha gumzo huku nyuma. Kila mmoja alitamani angalau angeisikia hata sauti yake.
Nikiwa nimechelewa kutoka nyumbani. Nilitembea Kama mtu anaeikimbia hasara. Niliingia benki Kama kipofu, kwa kasi ile Kama ningejikwaa basi ningeweza kupata ajali mbaya Sana. Nikiwa katika mwendo ule ule ghafla nilishtukia nagongana na mtu laini. Na kila mmoja akiangusha vile alivyokuwa amebeba.
Alikuwa ni mrembo niliyegongana naye. Akiwa ameduwaa huku akiingalia simu yake ya IPhone iliyoanguka pale chini. Niliinama nakuichukua simu ile na kumkabidhi huku nami nikiendelea kuokota bahasha zangu zilizokuwa pale chini.
"Samahani Sana Mrembo"
Kmya.
Niliendelea.
"Sijui umeumia Dadaangu?"
Kimya kidogo.
"Usijali, ni mambo ya kawaida"
Aliongea huku akiendelea kuiwasha Simu yake iliyokuwa imezima.
Macho yangu yaligundua uzuri aliokuwa nao mrembo yule. Niliweza kubaini mwanya wa wastani na meno meupe pee yaliyojipangwa vyema. Jambo lililozidi kufanya azidi kuwa kisura.
"Sijui unaitwa nani mrembo"
Kmya.
"Sorry Kama nakusumbua"
Kimya kidogo huku akitoa kitu ndani ya mkoba wake mwekundu uliofanana na Sketi yake.
"Shika"
Akininyooshea kikadi.
"Tutaongea, hapa watu wengi wanatutizama si unaona"
Aliongea na Mimi nikimuonyesha ishara ya kukubali kile anachokiongea kwa kutingisha kichwa.
Tuliachana. Sikuamini kilichotokea, nilihisi nipo kwenye zile ndoto za bingwa Ali Nacha. Kukutana na mrembo yule ilikuwa Kama nimekutana na malaika. Sauti yake ilikuwa Tamu haswa masikioni. Sura yake ilikuwa inavutia machoni. Hakika alikuwa mwanamke wa ndoto kwa wanaume waliowengi.
Nilimaliza kilichonipeleka. Nikapanda Daladala kuelekea home. Nikiwa ndani ya daladala Mara anaingia mwanamke mmoja aliyevalia Surual nyepesi nyeusi akakaa karibu yangu. Alikuwa akinukia marashi yenye kuhamasisha ngono. Kutokana na kuwa alikuwa amevaa miwani nyeusi sikuweza kuona macho yake. Alitoka kwenye mkoba Simu kubwa na kuanza kubinya binya.
Kuna wakati alikuwa akicheka na pia kuna wakati alikuwa akisonya. Hii yote hakuna aliyekuwa akimfuatilia wala hakuna aliyejua anacheka nini.
Nilijikuta nikimsemesha;
" Natamani na Mimi nicheke"
Alinigeukia na kuniangalia bila kusema lolote. Nilijikuta nikijilaumu kwa kujipendekeza kwani nikiona Kama amenidharau.
Nikiwa karibu kufika nilitoa simu yangu nakupokea kwani ilikuwa ikiita.
"Hallo"
"Sauti ya upande wa pili"
"Sawa"
"Sauti ya upande wa pili"
"Nakuja nipo njiani"
Simu ikakatika.
"Ulisema unataka kucheka"
Nilishtushwa na sauti ya yule Dada.
"Hamna nilikuwa nakutania"
"Ahaaa"
Kimya kidogo
"Kwani unashukia wapi?"
"Kituo kinachofuata"
"Kwaremi"
"Ndio"
" Mi nashukia Madukani"
Alijibu akionyesha kuchangamka zaidi.
Katika maisha yangu sikupenda mrembo yeyote anipitie pembeni. Ilikuwa dhambi kubwa Sana kumuacha mrembo bila kumuangaisha. Ilikuwa lazima nifanye ya simba mwenda pole.
"Sijui tutakutana lini tena"
Niliongea kwa kubahatisha.
"Tutakutana tuu!"
Kmya
"Andika namba zako"
Alinikabidhi simu wakati Daladala ikiwa imeshafika kituoni.
Kutokana na haraka ya kushuka niliamua kutoa wallet na kumtolea Kadi yenye namba ya simu. Nikamuaaga na kushuka.
**********
Shamila alifika nyumbani Mara baada ya kutoka Benki. Siku ya Leo alionekana mchangamfu Sana mwenye furaha. Mama yake aliweza kulibaini hilo.
Alishangazwa jinsi Shamila alivyokuwa akiongea kwa furaha huku akicheka Cheka. Haikuwa jambo la kawaida kwani Shamila tokea Baba yake alivyofariki akiwa chuoni alipoteza furaha yake. Hakuwa MTU mwenye tabasamu, nuru ya uso wake ilipotezwa na uchungu wa kifo cha Baba yake mzazi. Alikuwa akimtegemea kwa mambo mengi Sana. Japokuwa Familia yao bado ilikuwa na uwezo lakini bado Baba alikuwa nguzo muhimu.
Furaha ya Shamila ilimfanya mama yake ajisikie faraja. Kwani Shamila ndiye alikuwa mtoto wa pekee na ndio tumaini lake. Kumwona Shamila akifurahi ni jambo lililomnenepesha Mama huyu aliyefanana haswa na mtoto wake.
Jioni ilifika, kila Mara Shamila alikuwa akiiangalia simu yake Kuona Kama Mkaka aliyempa namba ya simu kuwa atampigia. Mpaka saa sita hakuna simu iliyokuwa ikiingia kwenye simu ya Shamila. Shamila alianza kukata tamaa huku machozi yakimlenga lenga.
Alishtushwa na mlio wa simu na kuichukua Mara moja. Ilikuwa namba ngeni, alishangilia kwa nguvu kwa kupiga makelele kwa furaha.
Alipokea, alichokisikia kilimkatisha Tamaa. Ilikuwa sauti ya mwanamke kutoka upande wa pili.
Moyo wake ukasinyaa, machozi yakaanza kutiririka kwenye mashavu yake laini. Mama aliingia kuona kilichomfanya Shamila ashangilie ni nini lakini alishangaa kumwona Mwanaye akilia.
"Una nini Mwanangu jaman"
Kimya
"Nambie basi, Mimi ndio Mama yako"
Kmya kidogo wakati Shamila anazidi kulia kwa kwikwi.
" Shida gani tena hii"
"Mama, we kalale usijali"
"Nilale ukiwa unalia Mwanangu"
Kmya
"Embu niambie una nini"
"sina kitu Mama"
" Mbona ulishangilia alafu sasa nakukuta unalia"
Kmya kidogo.
"Nimemkumbuka Baba"
"Baba!!!" Akihamaki
"Mmh! Mbona ulishangilia?"
Shamila alikosa jibu baada ya kujua amedanganya.
Mama akambembeleza mpaka usingizi ukawachukua wote pale pale kitandani.
*************
"Hapana, mimi ni Bwege"
Nilijitukana Mara baada ya kugundua nimefanya makosa ya kumpa namba yule mwanamke wa kwenye daladala namba za Msichana aliyenipa namba zake Benki.
Niliazimia ikifika asubuhi lazima nirudi kwenye ile Benki huenda nitapata pa kuanzia. Nilihisi kupoteza bahati ya kipekee.
Asubuhi ilifika, nikatoka kuelekea Benki.
Niliingia Benki kuelekea kwenye mapokezi ambapo wageni huandika majina yao na kuacha anuani zao.
Nikiwa ninaongea na mtu wa Mapokezi Mara anaingia Mtu mmoja upande wangu wa nyuma yangu kisha ananifunga machoni na mikono yake laini.
Sikujua alikuwa ni nani lakini harufu ya marashi na ulaini wa mikono vilitosha kunijulisha kuwa alikuwa ni mwanamke.
Aliniachia baada ya muda wa dakika moja. Niligeuka nyuma, sikuamini macho yangu. Mapigo ya moyo yalikimbia katika uwanda wa dura. Nilishusha pumzi Kama bata dume.
Nikabaki nimeduwaa nisipate cha kusema.
"Yaani wewe!"
Aliongea kisha akanikumbatia kwa nguvu. Nilihisi joto la aina yake, mtoto alikuwa mtamu haswa, maziwa yake madogo yaliyochongoka yaniweza kunichoma kifuani.
Sauti laini ilipenya masikioni mwangu ikisema;
" nimehangaika Jana mpenzi"
Nilikuwa Kama sijasikia vizuri, kuitwa mpenzi na mrembo yule.
Tuliondoka pale Benki na kuacha watu wakitutazama. Tulienda Hotel moja kwaajili ya mazungumzo.
Alijitambulisha anaitwa Shamila, na Mimi nikamwambia naitwa Michaelray.
Tukiwa tunaongea Mara sauti ya mwanamke ikasikika ikisema;
"Malaya wewe Jana ulifurahi kunipa namba ya Mkeo"
Ni sauti iliyowafanya watu waache kufanya shughuli zao na kumtazama aliyekuwa akiongea huku wakitaka kujua anayeambiwa.
Niligeuka na kumwona mwanamke tuliyekuwa nae Jana kwenye daladala akija nilipokuwa nimekaa na Shamila.
Itaendelea....