THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 388
- 552
Huu utakuwa ufafanuzi rahisi was kitu ama Muda.
Je inawezekana kwenda miaka ya mbele ama kurudi nyuma kwa akina Yesu na Yuda Eskaroti?
Sasa hapa utapata ufafanuzi wa time travel.
Ipo ama haipo utapata majibu.
Hebu anza na hii
Mtunzi: Jonas Rututuka
Mwandishi: Nelson Ntimba.
Time travel
MUDA
“MUDA NI NINI? Ama niulize wakati ni nini?. Watu huupima wakati kwa kutumia vitu mbali mbali. Wapo wanaopima muda kupitia kifaa maalum kiitwacho saa.
Lakini nayo saa hupimwa kwa kutumia kifaa kingine kama satilaiti ama kifaa chochote cha kuhisi mijongeo ya mawimbi na hata kifaa kingine cha kiumeme.Ajabu ni kwamba na vifaa hivyo vinaendelea kuitegemea saa ili viwe sahii.
Ningeliweza kuuliza maswali mengi kuhusu muda ama wakati ila kulingana na wakati tulio nao ambao unatuongoza hapa, Acha nizungumzie umuhimu wa kutokupoteza wakati. Je unajua siku nzima ina muda wa saa24?.Kati ya saa hizo saa 8 watu huzitumia kuwa shuleni,ama katika kazi, Na saa 8 nyingine hushauriwa na wataalam ziwe ni za kulala ama kupumzika wakati wa usiku.
Hivyo kila mtu ana saa 8 za ziadakwa ajiri ya mambo yake binafsi. Kumbe watu wote walio fanikiwa walitambua muda huo wa ziada na kuutumia vizuri.Hapo ndipo walipo fanikisha ndoto zao kuzitimiza.
Je unajua kuwa ukizitumia saa hizo vibaya kila siku unakuwa umepoteza saa 56 kwa wikinzima?
Ama umepoteza saa 224 kwa mwezi ?. Ama nisema utakuwa umepoteza saa 2688 kwa mwaka?
Na hii ina maana kuwa hapa shuleni ukiupuuza muda huo utakuwa umepoteza jumla ya saa10752 amabao ni sawa na mwaka mmoja kasoromwezi mmoja na saa 4 tu.
Ukitafakari hili kwa uzito . Utagundua upotevu wa muda tunao ufanya kwa kuendekeza mambo yasiyo ya muhimu. Hivyo basi wanafu……….”
Kabla kijana Nelson ajamalizia mazungumzo yake yalisikika makofi ya mkuu wa shule yakitokea nyuma ya mstari wa wanafunzi. Wanafunzi wote walihamaki na kugeuza vichwa vyao ili macho yao yahakiki kile ambacho masikio yao yalikuwa yakiwaletea.
Wapo walio anza kujikagua kama wana makosa yanayo onekana wazi. Wengine walianza kutawaliwa na wivu wakitamani mazunguzo yale wangeliyawasilisha wao. Wakati kila mwanafunzi akiwaza jambo lake akilini, Mkuu wa shule alipaaza sauti yake yenye muungulumo.
“Safi saafi sana kijana umenikosha kwa mazungumzo mazuri ya asubuhi kama hayo yenye kujenga. Tafadhali kijana huyu kuanzia leo namuweka kuwa mtunza muda wa shule mpaka pale atakapo maliza shule ndipo tutakapo mchagua mtu mwingine”
Mkuu wa shule alitua kidogo na kumeza mate kwa mbwembwe. Kisha akaendelea kuipaaza sauti yake yenye muungurumo.
“Tena akitoka hapa namaanisha baada ya masomo haje ofisini kwangu kuchukua zawadi yake”
Kijana Nelson hakuhamini kilicho tokea, alikuwa ameyaandaa mazungumzo yake kwa njia ya kawaida sana. Lakini alishangaa matokeo yake kuwa makubwa kiasi hicho. Muda wa masomo ulipo isha kama lilivyo semwa agizo la Mkuu wa shule aliingia ofisini kwake. Nelson alikuwa apotezi muda hata dakika chache.
Wapo walio mtania kwa kumuita mzungu kwa njinsi alivyo kuwa akiujali wakati. Aliingia kwenye ofisi ya Mkuu wa shule bila kubisha hodi. Mkuu wa shule alishutuka na kukimbilia mlango ili aufunge haraka. Hata hivyo Nelson alikuwa amesha zamisha kichwa chake na kuchungulia ofisini.
Alimuona mwanafunzi mwenzake akiwa amepiga magoti kama mtu aliye katika nyumba ya ibada akiomba msamaha kwa Muumba wake tena akijaribu kusisitiza kwa msisitizo mkubwa ulio ambatana na kilio cha uchungu.
Mwanafunzi mwenyewe alikuwa ni wa kike. Haraka Nelson alichomoa kichwa chake hata hivyo macho yake yalikuwa yamesha tuma taarifa hiyo kwenye ubongo nao ubongo ulikuwa ukilichakata jambo hilo. Ingawa alijaribu kuulazimisha ubongo wake usifanya kazi yake lakini ilishindikana.
Mkuu wa shule alitoka ofisini kwake na kumkuta Nelson karibu na mlango wa ofisi yake.
Mkuu wa shule alikuwa na wasiwasi na rangi yake ya ngozi ilionyesha matonetone ya jasho.
Alianza kumsifia Nelson huku macho yake yakienda kulia na kushoto chini na juu bila mpangilio.
Nelson alitambua kuwa hali haiko sawa.
Aliinamisha kichwa chake na kuanza kumsikiliza Mkuu wa shule,Kwani alihisi akimtazama usoni macho yake yatamhukum na kumshuku Mkuu wa shule.
Mkuu huyo hakuwa na lolote la maana zaidi ya kumumiminia tu sifa nyingi kijana Nelson. Baada ya sifa hizo Nelson alitoka ofisini na kuwakuta wanafunzi wakimsubiria agonge kengele ili waweze kwenda nyumbani.
Nelson alijilaum sana kwani mada hii aliyo iwasilisha kwa wanafunzi asubuhi aliiandaa miakamiwili iliyo pita. Ikiwa angeliitoa muda huo huenda angeliipata nafasi hiyo mapema. Hata hivyo alijisemea
“Hakuna kilicho haribika”
Kisha alikwenda kugonga kengele na wanafunzi wote walikusanyika mstarini.
Nelson aliendelea kusifiwa kwani hakuwahi kupoteza hata therusi ya sekunde.
Aliizoelea ratiba hiyo ya muda hivi kwamba wakati mwingine halinyanyuka bila kuitaza mpaka ilipo kengere na akiangalia saa yake anakuta muda umefika ama unapungua tu sekunde chache.
Wanafunzi hawakuwa na shida ya kubadili nyakati za saa zao.Wao walitumia kengele iliyo kuwa ikigogwa na Nelson. Naye akibadili ya kwake kupitia saa za wenzake. Mzunguko huo hakuna aliye wahi kuugundua kamwe,Maana walijua saa zao ziko sahii na zinawapimia wakati kwa njia waliyo ihitaji. Ili mradi walitimiza mambo yao kwa wakati ulio pagwa.
Ilikuwa siku ya jumatatu saa nne na nusu asubuhi,ndivyo saa ya Nelson ilivyo onyesha maana ilikuwa na mlio fulani ulio kuwa ukimkumbusha pale alipo pitiwa.Nelson alinyanyuka haraka na kukimbia ilipo kengere,Aliingonga kwa nguvu hata hivyo alishangaa itikio la wanafunzi halikuwa kama la siku zote.
Hakuna aliye shanngilia wala kutoka darasani kama siku nyingine wafanyavyo. Nelson alirudi darasani haraka akihofia labda mwalimu aliingia darasani mara tu baada ya yeye kutoka. Alifika darasani kitu kilicho mshangaza watu wote walikuwa kimya.
Tena wasio tikisa hata kope zao. Aliwatazama kwa muda mara akanyanyua mkono wake kutazama saa iliyo kuwa mikoni mwake mishale yake yote ilikuwa imesimama. Alijaribu kuipiga piga akihisi imeharibika.
Lakini ghafula alisikia mwanafunzi mmoja akisema
“Shetani amepita”
mwingine alicheka na kusema.
“Hapana Mungu alikuwa anatuhesabu”
Hapo minongono ya wanafunzi ilisikika kwa vurugu kama kawaida yao.
Nelson akiwa kwenye mshangao wa nini kimetokea aligeuka na kuitazama saa yake tena.
Ilikuwa ikiendelea kama kawaida yake kuhesabu wakati.
“Muda bado jamani kengele ya uji mbona inachelewa”
Aliongea mwanafunzi mwingine akimtazama Nelson aliyekuwa amepigwa na butwaa. Hata hivyo Nelson alitoka nje na kwenda kungonga kengere kwa mara ya pili.
Hapo wanafunzii wote walipaaza sauti zao za vigelele na kukimbilia sehemu ya uji. Nelson alionyesha kuchanganyikiwa kwani kila mara alikuwa akijiuliza ni nini kilitokea mpaka hali ikawa namna hiyo?. Hata hivyo hakupata majibu kabisa.
Ingawa jambo hilo lilimkumbusha jambo fulani lilowahi kutokea linalo fanana na hilo.Wakati huo Nelson alikuwa kijana mdogo alikuawa ameenda sokoni na mama yake kununua mahitaji. Wakiwa sokoni wananua vitu, ilitokea hali kama hiyo watu wote walikuwa kimya kwa ghafula.
Tena yule mama aliyekuwa anawauzia mchicha alionekana kama amepigwa shoti ya umeme. Na tukio hilo pia lilionekana kwa mama Nelson tena wakati huo alikuwa ameshika pesa mkononi.
Nelson alichua pesa hiyo na kumuwekea mama muuza mchicha mkoni mwake. Kisha aliuchukua mchicha na kuuweka kwenye kikapu chao.
Wakati akitaka kuwashutua alishangaa kuona wanaendeleza mazungumzo kana kwamba hakuna kilicho tukia. Miziki yote ya sokoni ilianza upya kuunguruma. Ila kutokana na umri wake kuwa mdogo hakuweza kujiuliza maswali mengi zaidi.