Hadithi;The girls in island-12

chiqutitta

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,160
3,124
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
THE GIRLS IN ISLAND 12

Wakati tupo ufukweni nikimsubiria Shenaiza afanye maajabu yake ili tuondoke pale, nyuma yetu tulisikia mtu akipiga makofi. Tulipogeuka nyuma tulikutana uso kwa uso na malikia Trizza akiongozana na jeshi kubwa la wanawake majasiri wapatao arobaini.

Nilichoka huku moyo wangu ukipatwa na kiwewe cha ghafla, nilipomuangalia Shenaiza, alikua ameshika kichwa kuashiria kua hakua na njia nyengine zaidi ya kuingia mikononi mwa malikia. Hapo ndipo nilpogundua kuwa ule ndio utakua mwisho wa maisha yangu kutokana na kuhadithiwa kuwa kosa la kumsaliti malikia adhabu yake hua ni kutolewa kafara kwa majini..

Hatukupata hata muda wa kujadiliana juu ya tatizo hilo, tayari wale askari walitfikia na kutukamata. Walitufunga kamba wote nna kuanza kutupeleka puta mpaka kwa malikia. Malikia alitutazama kwa dharau na na kutuoa amri ya kurudi kwenye mji wake.

Tulipelekwa na kufika huko usiku. Waliammua kutufunga selo pamoja na Shenaiza na wao wakaondoka.

“hivi tutasalimika kweli?” nilimuuliza Shenaiza baada ya wale askari waliotukamata kuondoka na kutuacha peke yetu.

“kwa sasa hatuna njia yoyote,… labda tuangalie hiyo kesho nini kitatokea.” Aliongea Shenaiza na kuniangalia mimi ambaye wakati huo nilikua najuta kwa nini nilikubali kutoroka.

“nadhani huu ndio mwisho wa maisha yangu.” Niliongea huku nikionyesha kukata tamaa kabisa.

“wee huwezi kufa… niamini mimi. Nitayapigania maisha yako hata kama yatagharimu maisha yangu.” Aliongea Shenaiza maneno ya kishujaa.

“sawa… ila utawezaje kuyaokoa maisha yangu wakati umesema hatuwezi kutoroka hapa?” niliuliza swali huku sura yangu ikonyesha ni jinsi gani nilivyokua nina hofu na maisha yangu.

“usijali mpenzi wangu… acha hiyo kesho ifike.. nitakuambia unawezaje kuokoa maisha yako.”aliongea Sheaiza na kuniangalia kwa macho ya matumaini.

Siku ya pili ilifika huku mimi na Shenaiza hakuna hata mmoja wetu aliyepatwa na hata lepe la usingizi. Usiku kucha tulikua tunapanga na kupangua jinsi tutaavyoweza kujinasua katika uzio wa kifo.

Asubuhi walikuja wle maaskari wa kike waliojazia kutufuata pale tulipo na kutufungua kamba tulizofungwa.

Baada ya hapo, walinichukua mimi na kumuacha Shenaiza mule ndani. Moyoni nilijua kua ndio nilikua naenda kutolewa kafara. Nilitamani kulia ila nilijua hata kama nikifanya hivyo haitaweza kuwafanya wale wasichana wanionee huruma na kuniachia. Nilipelekwa mpaka kwa malikia na kukalishwa chini yake umabali wa mita kama tano hivi toka alipokaa.

“Hijja,.. unahangaika nini mpenzi wangu?” aliniuliza malikia kwa sauti ya kawaida kabisa. Tofauti na mawazo yangu niliyokuwa nayawaza baada ya kufika mbele ya malikia. Nilifikiria kuwa kama nikifika pale basi atanifokea na kuniadhibu hata kwa mijeledi.

“nahitaji kurudi nyumbani.” Niliongea kwa uwoga huku nikiwa nimeangalia chini.

“hilo lilikua ni swala la kuongea wewe na mimi tukiwa chumbani, na si kunitoroka. Ona sasa mpenzi wangu umelala kwenye chumba dhalili wakati hadhi yako ni kulala kwenye chumba changu.” Aliongea malikia na kuniangalia huku akitabasamu.

“naomba unisamehe,… sirudii tena.” Nilijikuta nimeongea maneno hayo na kumtazama malikia kwa sura ya upole huku macho yangu yakiwa yamelengwa lengwa na machozi.

“najua sio kosa lako, ni yule mshenzi ndio kakulaghai…. Sasa nitapambana nae.” Aliongea malikia na kubadiilika kutoka kwenye tabasamu hadi kwenye hasira.

“mfungueni.” Aliamuru malikia na wale walinzi walinifuata na kunifungua.

“sasa unaweza kwenda kuoga mpenzi wangu na ukajipunzishe ndani. Najua ni jinsi gani umechoka.” Aliongea malikia maneno yaliyonifanya nimshangae. Bila kusubirie arudie kuongea tena, nilinyanyuka na kwenda bwawani kuogelea. Baada ya hapo nilipatiwa nguo nyingine na wafanyakazi wa malikia na kwenda kulala chumbani kwake.

Alikuja chumbani mchana na kunikuta nimeshaamka. Tulikaa wote kitandani huku akinisihi nisirudie tena kitendo changu cha kutoroka kwa sababu ananipenda na hayupo tayari kuniona nipo mbali naye.

Kwakua sikua namuamini kwa kuhofia kubadilika na kuniua, niliamua kumpa dozi matata mchana huo kwakua nilishajua kua ndio silaha pekee niliyokua nayo ya kumtuliza kiumbe huyo.

Baada ya mechi hiyo kali kumalizika, wote tulilala na tukajikuta tumesahau ya nyuma na kuanza kupanga mipango ya harusi yetu. Niliamua kukubali ombi lake la kumuoa kwakua sikua na jinsi kwa kosa nililolitenda.

Kesho yake niliaga kwa malikia kua nilikua nahitaji kuonana na marafiki zangu.

“unahitaji kuonana na marafiki zako?” aliniuliza hilo swali malikia na kunifanya nidhani kuwa alikua anahitaji kunizuia.

“nipo tayari hata tuende wote au uwaite waje wao hapa kama huniamini tena.” Nilongea kwa kujihami.

“sio kwamba sikuamini mpenzi wangu, nakuamini tena sana, ila nasikitika tu kukuambia kuwa hakuna rafiki yako hata mmoja ambaye yupo hai mpaka sasa.” Aliongea malikia maneno yaliouchoma moyo wangu. Sikuamini kama malikia alikua anaweza kunipa taarifa zile kirahisi namna hiyo.

Ila upande mwengine nilijua kuwa kwa sababu hajui ni wapi tulipotoka kati yangu mimi na rafiki zangu hao ambao nilikua nawaona zaidi ya ndugu zangu kwa jinsi tulivyodumu katika urafiki toka tupo watoto kabisa tunaendesha magari ya mitete.

Bila hiyari yangu, machozi yalianza kunidondoka huku moyo ukikazana kunipa uchungu kila nilipokua nairudia kauli ya malikia ubongoni mwangu.

Mwili ulinisisimka ghafla huku nguvu nazo zikinipotea ana kujikuta nashindwa kusimama.

“kwanini malikia,.. kwanini?” nilijikuta naongea maneno hayo huku machozi mazito yakitiririka machoni na mengine yakizidi kutengeneza ukungu kwenye mboni za macho yangu.

“unanihukumu bila makosa mpenzi wangu… sio mimi!” aliongea malikia huku akinifuta machozi kwa kitambaa cha nguo yake.

“hata kama sio wewe,.. najua utakua umetoa oda ya wao kuuwawa… kama umewauwa kwa kosa langu la kutoroka, utakua hujafaya haki hata kidogo.” Niliendelea kulalamika huku nikilia kwa uchungu.

“sikiliza nikumbie,… marafiki zako walilewa na kufanya mapenzi sana kushinda uwezo wao, ndio sababu ya vifo vyao.” Aliongea malikia na kutoka nje.

Yale maneno niliyoambiwa na malikia sikuyaamini, niliamini kuwa yeye atakua ndio muhusika tu wa mauaji ya rafiki zangu. Nilinyanyuka na kumfuata nje alipokua amesimama.

“ziko wapi maiti za rafiki zangu?” nilimuuliza kwa jazba.

“huwa hatuhifadhi maiti sisi.. wapo katika shimo la kutupia maiti, kama unahitaji kupelekwa nipo tayari kukupeleka.” Aliongea malikia kwa ukali kidogo baada ya kuona nimeanza kumpandishia.

“nahitaji kwenda sasa hivi.” Niliongea na kumuangalia malikia ambaye hakujibu chochote zaidi ya kunipa ishara ya kukubali kunipeleka.

Tulitembe kwa muda wa masaa mawili na kufika eneo hilo lililokua na shimo kubwa sana lililokua na maiti nyingi zilizotupwa bila mpangilio.

Niliangaza sana na baadae nilifumba mdomo wangu kwa mkono baada ya kuzishuhudia maiti zote za rafiki zangu zikiwa zimezagaa eneo hilo. Nilipatwa na uchungu sana na kuanza kungua kiliio tena.

Nilimuomba malikia awatume vijana wake wazitoe zile maiti kwani nilikua nahitaji kuzizika na si kutupwa kama vile.

Malikia hakupinga hilo, alikubali kuwaita wafanyakazi wake .

baada ya kurudi, aliwaambia wafanyakazi wake wakazitoe zile maiti muda huo huo. Baada ya kuzitoa na kuzipanga mahala pa usalama. Niiliwaamuru wachimbe makaburi na kuwaelekeza jinsi ninavyotaka.

Niliwazika kila mmoja kwa imani yake ya dini. Kwakua mimi nilikua najua jinsi waislamu wanavyozika, wao niliwazika kwa kutanguliza na dua. Booker na Philipo niliwazika na kuwaombea walazwe mahala pema.

Nilitengeneza misalaba kama nionavyo wanavyoweka mbele ya makaburi yao. Haikuwa kazi rahisi kufnya hivyo. Ila msukumo wa kibinaadamu na mapenzi yangu juu yai ndio vilikua vitu vilivyonifanya nikubali kupoteza nguvu zangu na kuwazika kama binaadamu wa kawaida na hali ile ya mwanzo ya kutupwa. Machozi yangu yalinifanya niumwe kichwa huku sura yangu ikiwa haitamaniki kwa jinsi macho yalivyovimba kutoaka na kulia kwa muda mrefu. Hata sauti ilikata kutokana na kuitumia kama kipoozeo cha machungu yaliyokuwa moyoni wangu. Niliikumbuka sana siku niliyowapa ofa rafiki zangu kabla ya kuanza safari yetu ya kuchukua samaki tuliowatega siku mbili zilizopita kabla ya siku hiyo. Nililia zaidi nilipomkumbuka rafiki yangu Booker mzee wa totoz. Alikua mtu wa stori sana na mpenda utani. Hata kama nikiwa na hasira kiasi gani, basi nilimtumia Booker kama kuburudisho changu cha kuniondoa stress. Hakika ilikua zaidi ya uchungu ambao sikuwahi kuupata toka siku ya kuzaliwa kwangu.

Usikose sehemu inayofuatia hapo badae
 
thanks,imesikitisha ....
 
Back
Top Bottom