chiqutitta
JF-Expert Member
- Nov 13, 2015
- 1,160
- 3,124
THE GIRLS IN ISLAND-11
“kuhusu swala la kutoroka na kuwaacha wenzangu huku ni swala gumu sana Shenaiza.” Niliongea huku nikiwaonea huruma wale marafiki zangu tuliowaacha.
“acha mawazo hasi Hijja, hata usalama wako hujaujua unawafikiria watu wengine ambao hawasakwi kama unavyosakwa wewe.” Aliiongea Shenaiza na kunifuata pale nilipo na kunishika mkono huku akinivuta. Sikua na jinsi zaidi ya kumfuata yeye kwakua mimi nilikua sijui njia.
Tulikimbia kwa muda wa nusu saa. Hapo Shenaiza alisimama kwenye mti mkubwa na kunifanya na mimi nisimame. Alinigeukia huku akitweta na kuniangalia usoni.
“unaniamini?” aliniuliza swali hilo baada tu ya kuniangalia.
“nafikiria kitu kama hicho.” Nilijibu huku nikiwa sina uhakika kama kweli nilikua ninamuamini.
“unatakiwa uniamini ili tuweze kufika mahala ambapo tutaweza kupata msaada.” Aliniambia hivyo huku akiwa katika hali iliyonifahamisha kuwa kulikua kuna haja kabisa ya kumuamini kiukweli.
“nakuamini.” Nilijibu kwa uhakika.
“kama unaniamini… unaweza kufumba macho yako?” aliniuliza tena
“naweza.” Nilijibu bila kusita.
“kama unaweza.. naomba ufumbe macho yako na usiongee chochote kwa muda huu.” Aliongea hayo maneno Shenaiza nami nikakubali kwa kutikisa kichwa. Baada ya hapo niliyafumba macho yangu na kutulia huku ngozi yangu ikiwa ni mlango pekee wa fahamu uliokuwa makini kuhisi kitu kitakachotokea au kunigusa.
Haikupita hata dakika moja. Nilianza kusikia muungurumo kama wa nyoka mkubwa aina ya anaconda. Kabla fikira zangu hazijanifikisha huko, nilianza kuona kitu kikiwa kinanizunguka pale nilipo. Sikuweza kuvumilia kufumba macho, nilifumbua na kumuona nyoka mkubwa wa rangi ya kijani akiwa ametuzunguka wote wawili. Nilitaka kupiga kelele, ila nilizuiliwa na Shenaiza ambaye alinifumba kwa mkono wake huku kidole chake akikiweka mdomoni mwake kama ishara ya kunikataza kupiga kelele.
Nilitulia huku moyo wangu ukiwa umekosa amani. Mwili mzima ulijaa vipele vya baridi lakini jasho likiwa linanitoka.
Yule nyoka alianza kupaa kimaajabu, nilishangaa na kuzidi kupatwa na uoga baada ya kuona tumefika juu sana huku tukiwa hatuna mahala pa kushikilia. Shenaiza aliniona jinsi nilivyokua Napata tabu. Alichokifanya ni kunipulizia unga amboa sikujua ulikua wa rangi gani kwakua alinishtukiza. Hapo nililala usingizi mzito na kuja kuamika nikiwa ndani ya pango lile la vito vya thamani.
‘umeamka… nadhani tunaweza kuendelea na safari.” Aliongea Shenaiza baada ya kuona nimerejewa na fahamu.
Sikujibu chochote, zaidi ya kuamka na kuendelea na safari. Tulitoka nje ya pango na kuanza safari ya kuelekea baharini.
Wakati tupo ufukweni nikimsubiria Shenaiza afanye maajabu yake ili tuondoke pale, nyuma yetu tulisikia mtu akipiga makofi. Tulipogeuka nyuma tulikutana uso kwa uso na malikia Trizza akiongozana na jeshi kubwa la wanawake majasiri wapatao arobaini.
Nilichoka huku moyo wangu ukipatwa na kiwewe cha ghafla, nilipomuangalia Shenaiza, alikua ameshika kichwa kuashiria kua hakua na njia nyengine zaidi ya kuingia mikononi mwa malikia. Hapo ndipo nilpogundua kuwa ule ndio utakua mwisho wa maisha yangu kutokana na kuhadithiwa kuwa kosa la kumsaliti malikia adhabu yake hua ni kutolewa kafara kwa majini..
usikose badae sehemu inayofuatia