Hadithi: Sitosahau alichonifanyia daktari wa saratani ya matiti

Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI

TULIPOISHIA
Nilimtumia ujumbe “Mbona hutaki kupokea simu yangu, nisamehe mume wangu” nilimuita kimahaba hivyo. Kweli haikuchukua muda akapiga.

Nilipopokea simu nilimuita kwa hisia “Mume wangu” lakini cha kushangaza nilisikia nimejibiwa na sauti ya kike ikiniuliza

“Wewe nani???” niliishiwa nguvu

ENDELEA
“Mhh” ilibidi nigune kidogo nikasikilizia na kumuambia “Samahani labda nimekosea namba” nilikata simu kwa haraka nikaiangalia namba vizuri ili kujua kama ni ya kwake au nilikosea.

Nilipoiangalia ile namba niligundua ndiyo ile ile, nilikasirika, nilijaribu kujifosi kutokuumia lakini kadri dakika zilivyokuwa zinasogea ndivyo moyo wangu ulivyokuwa unauma na kujisikia vibaya zaidi na zaidi.

Nilijikuta namchukia kabisa Hemed, nikafuta namba yake na kuamua kukaa kwa amani.

Kiukweli sikujua penzi limeshaniingia sana, niliwaza siku nzima, pia nilijuta kumuambia mama yangu kuhusu yeye maana mimi nilikuwa nahitaji mume halafu yeye alionekana kuwa na wanawake tofauti tofauti.

Nilikumbuka kauli ambayo nilishawahi kuiona kwenye mtandao kwamba usimwamini mwanaume mwenye ndevu nyingi, na hilo ndilo lililonifanya nikahisi ni kweli.

Nikaanza kujitia moyo “Kwanza ni mkubwa kwangu, sikupaswa kuoana na mtu kama huyo…nitatafuta wa rika langu na hata wa dini yangu….Eeh Mungu niletee” nilisema huku nikipanga nguo zangu taratibu.

Ilipofika jioni ndipo niliona ujumbe kutoka kwa Hemed ukisema hivi “Hello mke wangu, leo mbona umenisusa hivi?” nilipoitazama namba ni ya kwake, nikaufuta ule ujumbe bila hata kumjibu halafu nikasonya lakini akanipandia hewani.

Niliitazama simu kwa muda mrefu bila kupokea lakini almashauri ya ubongo wangu ikaniambia nipokee ili nimuambie ukweli, nikapokea

“Hallo” nilisema

“Poa vipi mbona leo umekuwa kimya sana?” aliniuliza

“Embu niache bwana” nilisema

“Nikuache kivipi? Hivi nimekukosea au?”

“Hemed, niache na maisha yangu, sitaki mawazo ya haraka haraka tu hivi, nilipokuwa zangu bila mwanaume nilikuwa na furaha ya ajabu….naona stress zimeshaanza”

“Stress??? How???” aliniuliza

“Una mke wako, mimi sihitaji kuwa na wewe”

“Acha mambo yako, kila kitu si nilikueleza Pendo? Sina mwanamke, ila kuna mwanamke ambaye tumepanga kuoana, si nilikuambia haya tangu jana??” aliniuliza

“mimi sio mtoto”

“Nini sasa”

“Asubuhi nimekupigia, aliyepokea simu ni mke wako….ananifokea”

“Mke wangu? Simu yangu saa ngapi?” aliniuliza

“Saa mbili….mbona unakuwa muongo, embu angalia call logs za asubuhi acha kunidanganya bhana aah” nilisema na kukata simu kwa hasira nikaiweka pembeni na kujilaza kidogo kwenye kiti cha dukani

Baada ya dakika moja alinipigia, nikapokea, na nilipopokea tu alikuwa anacheka sana ndipo nikamuuliza “Vipi mbona unanicheka?”

“Hahahahaa…lazima nikucheke, sasa wewe hiyo simu amepokea nani? Huyo si ndio mdogo wangu nilikuambia anakaa na binti yangu mamy??” aliniambia

“Mmmh…” niliguna huku nikijikuta naelekea kumuamini “Hivi kwanini uwe muongo, simu mnashirikiana na mdogo wako?”

“Mara nyingi simu yangu ni ya kazi, nilikuwa bafuni kuna appointment nilikuwa nayo, nikamuambia kwamba akipiga mtu apokee”

“Khaa….sijui”

“Ndio, au kama vipi ngoja usiku nije nikuchukue tuende nyumbani kabisa ukamuone” alisema Dr Hemed

“Mh”

“Ndio hivyo…..namalizia jukumu hapa, halafu nakufuata ofisini kwako sawa?”

“Ok” nilisema.

***
Ilipofika saa moja usiku nilitaka kufunga nikaona nimtafute nimuulize kama ananifuata au niondoke zangu, akanijibu

“Nakuja hapo soon….usiwe na wasiwasi”

“Saa ngapi?”

“Sasa hivi”

“Ok fanya haraka mimi sitaki kuchelewa nyumbani kama jana, au niache niondoke nije kesho mapema”

“No baby, unajua kabisa nia yangu kukuoa” alisema

“Mh…kunioa tena?”

“Ndio kwani sijakuambiaga?”

“Mh”

“Nakuja” alisema na kukata simu yake nikabaki nawaza huyu mwanaume anamaanisha au la, may be nilihisi yuko serious, nilikuwa nimeshampenda kidogo lakini niliona kabisa navyoelekea kutumbukia kwenye mapenzi na mtu ambaye hata hatujuani vizuri.

Nilisubiri dakika kama kumi na tano kweli alikuja yule kaka na siku ile alikuwa na gari yake, nikafunga duka na kupanda ndani ya gari na kuondoka kuelekea kwake nyumbani.

Tukiwa barabarani, kuna msichana alisimama katikati ya barabara akawa amenyoosha mikono kwa ishara ya kutaka kugongwa lakini Hemed alishika break na kushasha kioo akamchungulia yule msichana anacheka.

“Nitakugonga” alisema Hemed

“Ungenigonga uone kitakachokukuta” alisema binti huku akitabasamu na kuchungulia ndani ya gari. Ilionekana watu hawa wanafahamiana kwa kiasi kikubwa.

“Hahaha….vipi unafanya nini hapa?” Hemed aliuliza

“Nilikuwa nakusubiri wewe”

“Oh…basi sawa mi niko na mgeni nampeleka home” alisema Hemed

“Mh…” alisema yule msichana kisha akaniangalia na kuniambia “Mambo”

“Poa” nilijibu

“Basi, tutachat au?” aliuliza binti

“Hamna noma” alisema Hemed

Hemed aliendesha gari kwa mwendo wa taratibu, mimi sikumuuliza chochote, ila tulipofika getini kwenye nyumba aliyokuwa anaishi pia alikuja jirani mmoja wa kike, akampatia kitu fulani kwenye mfuko, na kumuuliza “Baadaye tutaonana au?”

Hemed akajibu “Kwa leo sidhani ila nitakuambia kwenye simu”

Niliweka mikono kifuani tu nashangaa mwanaume amezoeana sana na wanawake halafu wote ni wazuri nilijisikia vibaya ila sikutaka kumuonyesha kwamba nimekasirishwa. Alifungua geti kisha tukaingia ndani…..ITAENDELEA
 
Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Baada ya kuingia ndani ya geti tulishuka kwenye gari, kiukweli kulikuwa ni kuzuri kule ndani, kulikuwa na nyumba nzuri ya kisasa moja kubwa, pamoja na nyumba ambayo ilikuwa pembeni yenye milango miwili nje, ilionekana ni ya kupanga maana nje kulikuwa na wanawake wawili wakipika barazani huku wakipiga umbea na kucheka.

Wanawake wale, mmoja alionekana kuwa ni wa makamo kidogo huku yule mwingine akionekana binti mdogo aliyenizidi kidogo tu. Yule wa makamo nilikuwa kama namfahamu lakini kwa haraka haraka sikukumbuka niliwahi kumuona wapi kabla.

“Za jioni” nilisema huku nikiwatazama

“Salaaama” waliitika

“Hapa ndo kwangu karibu sana” alisema Dr Hemed, ni kweli ni pazuri, vumbi kulisikia ni bombani, kulikuwa kumependeza sana kulikuwa na mvuto wa ajabu chini kulikuwa na paving yenye rangi nyekundu iliyochanganyika na kijani kibichini.

Taa za kuwaka vizuri zilionekana vizuri kwenye nyumba iliyokuwa imepigwa rangi ya maziwa, nilifurahi sana kupaona licha ya kuwa na wasiwasi na pale

“Pazuri” nilimuambia lakini Hemed alikuwa ameweka umakini zaidi kwa wale wanawake na hata kuwafuata mimi akaniacha nikiwa nimesimama pale mwenyewe.

“Mmeshindaje nyie?” aliuliza

“Safi tu……” alisema yule mwanamke ambaye alionekana kuwa na umri mkubwa kidogo halafu yule mdogo aliinuka na kumfuata akamkumbatia Hemed kwa sekunde kadhaa wote wakawa wanacheka

“Unajua niko na mchumba wangu halafu unanikumbatia hivi ina maana unataka niachike au?” aliuliza

“Mmmmh kumbe mchumba?” alisema yule binti akiwa anamuachia, mimi ndo kwanza naangalia mbali, na kutabasamu kuihurumia nafsi yangu nikiiambia nimeingia cha kiume.

Hemed aliachana na wale wanawake akanifuata na kunivuta mkono akaniambia karibu ndani.

Niliingia lakini kiukweli moyoni sikuona kama yule mwanaume alikuwa ananifaa kabisa kwenye maisha ya ndoa, alikuwa ana mazoea mabaya na wanawake, halafu kingine ni kwamba alikuwa hata haoneshi kuwa tayari kuishi kama baba, na hata hayo yote yaliyotokea alikuwa haniambii samahani.

Tulipofika ndani tuliketi sebuleni, kulikuwa na sofa sio za chini ya milioni tano, za kisasa hasa, chini kulikuwa na zulia lililozunguka chumba cha sebule chote. Katikati kukawa na meza iliyochanganyika kioo na mbao halafu pembeni kukawa na kabati la vyombo kubwa sana.

Taa zenye mwanga hafifu zilikuwa zimezunguka kuta nne, zikiwa zinawaka mdogo mdogo, halafu juu kuna pangaboy lisilokuwa linazunguka.

Ukutani kulikuwa na TV nchi hamsini na tano huku chini yake kukiwa na case iliyobeba redio kubwa aina ya sea piano lakini kingine ni kwamba chumba kizima kilinukia vyakula tofauti tofauti. Nikavuta pumzi na kuketi sofani halafu nikamtazama machoni yeye anachezea ndevu zake mwenyewe halafu akanyoosha mkono na kuvuta rimoti zilizokuwa mezani akaanza kuwasha vifaa hivy vya umeme.

Vilivyowaka tu hivi, kulikuwa na channel iliyoitwa Clouds TV ndipo ilisikika nyimbo ya Harmonize iitwayo Nitaubeba.

Baada ya sauti ile kusikika, kuna msichana mdogo mdogo aliingia pale na kumfuata Hemed akamrukia
“Daddy…..” halafu akamlalia, alionekana binti mkubwa mkubwa miaka kama nane hivi

“What’s up” alisema Hemed

“I miss you daddy” alisema binti huyo

“I miss you….Nasra where’s Jacqueline?” aliuliza

“She’s is in the kitchen”

“Okay….” Alisema Hemed na kunitazama akasema “Huyu ndio binti yangu”

“Mmmmh mkubwa” nilisema

“Mh yah namshukuru Mungu anamjalia afya tele….. napambana kwa ajili yake” alisema wote tukatabasamu huku tukiendelea kuangalia TV taratibu.

Nilipoangalia saa niligundua ni saa mbili kasoro, nikamtazama na kusema “Ninataka kwenda nyumbani sasa”

“Hapana, tule kwanza…..hey” alisema huku akimgusa Nasra….Call Jacque for me” alisema

“Okay” binti alishuka mapajani na kwenda kumuita Jacqueline ambaye baadaye niligundua ni binti wa kazi.

Baada ya dakika mbili tu, Jacque aliingia pale sebuleni, alikuwa ni msichana mwenye sura nzuri sijapata kuona, Mungu alimjalia sana sikujua kama ni mtanzania au ni mwarabu au ni mtu gani but she looks so beautiful nilijikuta namkagua kuanzia juu kichwani mpaka chini.

Alikuwa na nywele ndefu zilizosambaa mgongoni mwake huku akiwa ana rangi nzuri mweupe pee…..alivaa gauni la blue lililomshika na kuonyesha umbo lake dhahiri lenye mvuto sana.

Gauni lilikuwa ni fupi sana lilikuwa katikati ya mapaja ndo limeishia tu, likionyesha uzuri aliokuwa nao nje na ndani, halafu aliponiona alishtuka kidogo

“Shikamoo”aliniamkia

“Marahaba” nilisema na kumgeukia Hemed ambaye alianza kumuongelesha

“Kwani chakula bado” aliuliza

“Tayari anko, nimeweka ukumbini mnaweza mkakaribia” alisema msichana yule

“Okay wewe hauli?”

“Nitakula baadaye kidogo” alisema huku akigeuka na kuanza kutembea, nilipomtazama alivyokuwa amejaliwa umbo na kubeba mzigo nyuma hakika nilijua kabisa Hemed hawezi kumsamehe. Nikatulia kimya kama nimemwagiliwa maji

“Huyo ndiyo aliongea na wewe kwenye simu”

“Mh…..hvi Hemed…..huyu….am mh au basi” nilishindwa kusema chochote kabisa

“Tukale chakula basi” alisema

“Okay ila nakula kidogo tu niondoke nyumbani nimechelewa sana”

“Haya powa”

JE UNAHISI HEMEDI ANAFAA KUWA MUME WA PENDO? JE HEMEDI NA JACQUE HAMNA KINACHOENDELEA?? ITAENDELEA

Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
UKURASA WA KUMI NA MBILI
TULIPOISHIA
“Mh…..hvi Hemed…..huyu….am mh au basi” nilishindwa kusema chochote kabisa

“Tukale chakula basi” alisema

“Okay ila nakula kidogo tu niondoke nyumbani nimechelewa sana”

“Haya powa”

ENDELEA
Tulinyanyuka pale kwenye kochi, akanipeleka ukumbini huku akiwa amemshika mkono mtoto wake Nasra tukaenda kula chakula cha usiku kwa pamoja.
Pale tulikula vizuri kulikuwa na mchanganyiko wa vyakula kama saba, siwezi kukataa mate yalinijaa kulinukia kulikuwa na wali, nyama ya ng’ombe, kuku, maziwa, mboga za majani, kulikuwa vitu vingine vingine like wow. Nikapagawa.

Tulinawa, kila mmoja akajipakulia chake tukaanza kula taratibu huku tukipiga story mbili tatu

“Kwa hiyo sasa umeshaamini sina mke?” aliniuliza

“Ah mmh ni kweli nimeshakuamini kwamba huna mke lakini mh” nilisema

“Mh nini?” aliniuliza

“Hamna” kiukweli sikuweza kumuambia chochote kuhusiana na tabia zake nilizoziona lakini kiukweli nilikuwa nimeshamtilia mashaka makubwa, wanawake walikuwa sana karibu naye, nilimuhisi vibaya na vile alivyokuwa anajua kujibiringita kitandani wakati wa tendo ndo kabisa nikajua yule ni chakula cha wengi.

“Sema tu usiogope kabisa”

“Huyo ni mdogo wako uliyekuwa umemuuliza kuhusiana na chakula?”

“Oh Jacque?” aliniuliza

“Yes”

“No, huyo ni househelp, alitafutwa na mama Nasra, ana asili ya Ethiopia”

“Mmmmmmh really akakutafutia msichana kama huyo?”

Hemed alitabasamu halafu akaniuliza “Kwani ana shida gani?”

“Actually she’s very beautiful sidhani kama umeweza kumsamehe wewe mwanaume huuh”

“Hahahahaa….hapana siko hivyo naheshimu kazi yake, najiheshimu kama baba nikifanya hivyo nitapoteza vingi sana”

“Really??” nilimuuliza

“Yeah” mara ghafla nikasikia sauti ya Jacque inamuita nje ya ukumbi “Vipi Jacque”

“Nakuomba mara moja”

“Njoo huku tuinjoy chakula, meet my fiancée” alisema

“Mh, basi ukimaliza tutaongea”

“Okay”

Tuliongea mambo mengi sana, lakini baada ya muda mfupi Nasra aliondoka pale tulipokuwa halafu akaenda zake huko ndani sisi akatuacha tunamalizia kula.

Ghafla Nasra alirudi akikimbia huku akiita “Dady….daddy” tukabaki tunashangaa

“Whata is the matter young lady?” aliuliza mtaalamu akamshika akaanza kumpapasa nywele

“Aunt Jacque is Crying” alisema Nasra baba akashtuka

“Crying???” aliuliza kwa mshangao

“Yes”

“What’s the problem…..” alisema na kuinuka akamshika binti yake “Let’s go” alisema wote wakiondoka na kuelekea alipokuwa Jacque

Nilibaki nikijiuliza mengi nilijua labda ana matatizo yake binafsi lakini kiukweli walikaa sana nasikia wakiongea kwa sauti ndogo kabisa huko ndani sikuelewa tatizo ni nini

Kwa kuwa sipendi kuingilia masuala ya familia za watu, nilitulia, nikasubiri kama dakika kumi nikanawa na kuamua nisimame niondoke zangu kuelekea nyumbani maana muda ulikuwa umeenda

Niliita
“Doctor, nataka niondoke sasa” ndipo Hemed akatoka na kuniambia,

“Sorry for this, ngoja nikupe nauli huyu ana matatizo” alisema na kufungua wallet akanipa shilingi elfu kumi na kuniaga niondoke.

Niliondoka nikiwa na doubt kwamba tatizo limekuwaje kubwa hadi akashindwa kunisindikiza kama alivyokuwa ameahidi. Niliondoka zangu
JE KWANINI JACQUE ALILIA? USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
 
Back
Top Bottom