Hadithi: Mwekanadhiri na shetani

Hadithi: Mwekanadhiri na shetani

(sehemu ya tano)
Ndipo akaambiwa pesa akampe mtoto wa shetani. Basi mweka NADHIRI alitoka akaanza kutembea mitaani, alipofika mtaa wa mvuleni wenye chuo cha wavulana alikuta kusanyiko kubwa, mweka NADHIRI akataka kujua kinachoendelea, akajisogeza pale kisha akamuuliza mmoja wa wakusanyikaji wale akamwambia, nikijana mmoja mwanafunzi, aliefanya #UDEDHULI kwa mwalimu wake, sasa alitaka kuadhibiwa lakini kawa jeuri na ameitwa mzazi wake lakini kijana huyu amekua kiburi anataka kumpiga baba yake, hivyo ndiohali ilikusanya watu wote hawa. Mweka NADHIRI alipopata maelezo yale aliamini kabisa huyu hasa ndio mtoto wa shetani.
#Alilipasua kundi la watu huku akipaza sauti akisema "NIPISHENI NIMUONE KIJANA HUYO ILI NIMPE ZAWADI ITOKAYO KWA BABAAKE SHETANI" watu waliokua mbele yake wakajitenga kando ilikumpisha, alipomkalibia kijana yule, mweka NADHIRI akapaza sauti huku akizitoa zile pesa akisema "POKEA PESA HIZI ZITOKAZO KWA BABA YAKO SHETENA" huku akiwa anamkabidhi zile pesa, lakini yule kijana alizikataa na kusema mimi siomwana wa shetani, baba yangu nihuyu hapa, watu waliokuwepo wakamwambia hakika unastahili kuwa mtoto wa shetani, maana humuadabikii mzazi wako. Basi yule kijana alifedheheka sana akangeukua baba yake, akamuomba #RADHI nae alimsamehe kisha baba akamwambia amuombe msamaha mwalimu wake kijana akafanya hivyo na ugomvi ukaisha.
Mweka NADHIRI alichukia sana akarudi nyumba hoi kabisa. Alipofika alimwelezea mkewe namkewe alimpa faraja, akamwambia usichoke mwendee tena mtabiri wa malimwengu huenda akakupa ushauri wamwisho kuitoa NADHIRI hii. MWEKANADHIRI akaenda tena kwa mtabiri.
Jee alipewa ushauri gani.?
Njo sehemu ya sita na yamwisho kujua kulicho tokea.
Sehemu ya sita ndio mwesho,,kesho...
 
Back
Top Bottom