Hadithi: Mwekanadhiri na shetani

Hadithi: Mwekanadhiri na shetani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,170
Reaction score
829,116
SEHEMU YA KWANZA
Hapokale paliondokea mtu namkewe waliokua na ng'ombe jike ambae walimpenda sana. Wakamtafutia #FAHARI mzuri ili baadae ng'ombe wao awe #MBUGUMA. Basi mke akamwambia mumewe, ng'ombe wetu mara yakwanza akizaa ndama jike nitafanya #KARAMU niwakaribishe mabibi wote wamtaa huu, mume nae akamwambia mkewe ng'ombe wetu mara yakwanza akizaa ndama dume nitatoa pesa kumpa #SHETANI. Basi baada ya mwaka mmoja ng'ombe wao akazaa ndama dume, mke akamwambia mumewe unakumbuka ahadi ukiotoa..? Mume akajibu naikumbuka, mke akamwambia basi ahadi ile #NINADHIRI yapaswa uitimize usipo itimiza ng'ombe wetu wote watapatwa na miosi.

Mume akamwambia mkewe sasa shetani mwenyewe nitamuona wapi..? Katika kijiji kile kulikuwepo na mzee mmoja aliefanya makao yake nje kidogo ya mji, akiitwa #MTABIRI_WA_MALIMWENGU. mke akamwambia mumewe, mwendee mtabiri wa malimwengu huenda atakushauri namna ya kuitoa nadhiri hii.
Mume akakubali, siku iliofuata alifunga safari kummwendea mtabiri wamalimwengu.
 
Sehemu ya pili
Basi mke akamwambia mumewe mwendee mtabiri wa malimwengu huenda akakupa. msaada wa kuitoa NADHIRI hii. Siku iliofata mume akafunga safari hadi kwa mtabiri wa malimwengu, alimkuta, baada ya kukaribishwa vyema akapewa kigoda akaketi, yule mtabiri wa malimwengu akamuuliza akisema bwana #IMEJIDAWA asubuhi na mapema unashida gani..? Mweka NADHIRI akamjibu akisema, Mimi niliweka NADHIRI kwamba ng'ombe wangu mara yakwanza akizaa ndama dume nitatoa pesa nimpe shetani sasa kwabahati juzi ng'ombe wakazaa ndama dume napesa nilizo ahidi kumpa shetani ninazo, lakini shetani mwenyewe simjui je nifanyeje..?
Matabiri akamwambia nitakufundisha #AYA nawe utaisoma hadi uikariri moyoni kesho asubuhi nenda kwenye ule msitu mkubwa, ukifika katikati ya msitu panda juu ya mti mrefu kuzidi yote kusha mwite shetani kwasauti ya #KUPAZA akiitika mweleze shida yako nae atakukidhia.nawe utaisoma hadi uikariri moyoni kesho asubuhi nenda kwenye ule msitu mkubwa, ukifika katikati ya msitu panda juu ya mti mrefu kuzidi yote kusha mwite shetani kwasauti ya #KUPAZA akiitika mweleze shida yako nae atakukidhia.
Basi mweka NADHIRI akahifunza ile Aya hadi ikamkaa moyoni, siku ilofata akajilawa asubuhi sana akaenda hadi msitu, akauona mti mrefu akaukwea hadi juu, kisha amaanza kuisoma ile Aya kwautulivu sana, kisha akaita "SHETANIIII SHETANIII" akasikia sauti kwambali ikimwitika "UUUUU, UUUU!!!" Mweka NADHIRI akaiambia ile sauti "Niliweka NADHIRI kwamba ng'ombe wangu akizaa ndama dume nitatoa pesa kukupa wewe bahati ng'ombe wangu kazaa dume kwahiyo njoo uchukue pesa zako nilizo kuahidi. Ile sauti ikamjibu ikisema "NENDA KAMPE MKE WANGU MIMI SITUMII PESA" mweka NADHIRI akaiuliza ile sauti "MKEO ANAITWAJE NA ANAKAA WAPI.."? Lakini ile sauti haikujibu japo mweka NADHIRI aliuliza tenanatena,, basi mweka NADHIRI alirudi nyumbani akiwa kachoka kabisa asijue la kufanya.
Je mweka NADHIRI atampata wapi mke wa shetani..? Fatilia simulizi hii hadi ujue kilicho tokea.
 
Sehemu ya tatu
Baada ya MWEKANADHIRI kuambiwa naile sauti kua akampe mke wa shetani, MWEKANADHIRI alirudi hadi nyumbani kwake, na akamwelezea mkewe yalotokea kule msituni.
Mke akamwambia mumewe usichoke, mwendee tena mtabiri wa malimwengu ukamweleza yalotokea huko, basi MWEKANADHIRI asubuhi namapema alimwendea MTABIRI Kisha akamwelezea yalotokea najinsi shetani alivyomjibu kua aende akampe zile pesa huyo mke wa shetani.
Mtabiri akamwambia ndugu yangu usichoke wake washetani niwengi sana hapa mjini, tembea tembea mitaani, ukimkuta mwanamke asie mheshimu mumewe, basi huyo ndie mke washetani, MPE PESA HIZO UKIMWAMBIA ZIMETOKA KWAMUME WAKE SHETANI, akizipokea basi NADHIRI YAKO ITAKUA IMETOKA. Baada ya maelezo yale MWEKANADHIRI hakupoteza muda, sikuileile akaanza kutembea mitaani.
Baada ya kupita mitaa miwili tu alikutana na mwanamke alie VALIA LIBASI ZA ULIMBWENDE akitoka mlangoni kweke kuelekea mtaani, lakini kuzingitini mwamlabgo wake alisimama mwanaume mmoja alieonekana #MUUNGWANA akimuita kwasauti ya upendo "mke wangu mke wangu" heburudi maramoja kunakitu nimesahau nataka kukuagiza, lakini yule mwanamke hakurudi kumsikiliza mumewe badala yake alimnibu akisema "Nilikuwmo humo ndani hukuniambia lolote, maadamu nimeshatika sirudi nawala sisikii lamume wala nini" mpaka nitarudi safari yangu, yule mwanaume alihuzunika sana akarudi ndani. Basi mweka NADHIRI alipoona vule akamwendea jirani na nyumba alotoka mwanamke yule akamuuliza sifa za bibi yule, yule jira akamwambia, "Mwanake yule hamuheshimu mumewake tena humkaripia hadharani kama anakemea mtoto wake hivyo hana #NIDHAMU kwa mumewe,, mweka NADHIRI alipata maelezo yale alijisemea moyoni "huyu hasa ndie mke wa shetani anastahili kupewa pesa za shetani. Basi mweka NADHIRI akamkimbilia yule mwanamke ili ampe pesa za shetani, alipo mkaribia yule mwanamke akapaza sauti akisema "POKEA PESA ZITOKAZO KWA MUMEO SHETANI"je mwanamke yule alizipokea pesa za shetani.? Itaendelea...
 
Sehemu ya nne

Basi mweka NADHIRI alimfata yuma mwanamke, alipomkalibia alipaza sauti akimwambia "POKEA ZAWADI ITOKAYA KWA MUMEO SHETANI" yule mwanamke alikataa akiae "UNIPISHE MIMI, SINA MUME SHETANI, MUMEWANGU NIYULE PALE MLANGONI." Wapitanjia walipo sikia maneno yale walimwambia, hasa wewe unastahili kupewa pesa za shetani maana humtii mumeo. Maneno yale yalimfedhehesha yule mwanamke nae alirudi na kumuomba msamaha mumewe namume alimsamehe mkewe.

Basi mweka NADHIRI alichukia sana maana pesa zile hazikupokelewa, hivyo alirudi nyumbani nakumweleza mkewe kwamba yule mke wa shetani hakuzipokea zile pesa, mke akamwambia, usichoke mwendee tena MTABIRI WA MALIMWENGU, Huenda akakupa ushauri wanwisho kutimiza NADHIRI hii. Mweka NADHIRI alirudi tena kwa yule mtabiri alipofika alikaribishwa, mtabiri akamuuliza mweka NADHIRI, nae akamwambia mke wa shetani kazikataa zile pesa je nifanyeje..? Mtabiri akamwambia usichoke mwendee tena shetani ukamwambie mkewe kazikataa zile pesa, huenda akakupa ushauri wamwisho.
MWEKANADHIRI akarudi tena msituni akasoma ile Aya kisha akamwita shetani, nae akamuuliza kuna nini tena, mweka NADHIRI akamwambia mkeo amezikataa hizi pesa, shetani akamwambia nenda ukampe mwangu akizipokea basi NADHIRI yako irakua imekwisha, mweka NADHIRI akamuuliza mwanao anaitwaje na yupo wapi.? Lakini ilesauti haikumjibu tena japo mweka NADHIRI aliuliza. Basi alirudi nyumbani akamwambia mkewe aliojibiwa na shetani, mkwewe akamwambia arudi tena kwa mtabiri wa malimwengu, nae akaenda kisha akamwekezea talitokea msituni, mtabiri akamwambia, watoto washetani wapo wengi hapa mjuni, tembea mitaani ukikuta mtoto anae mjeuria mzazi wake huyo ndio mwana wa shetani mpe pesa hizo ukimwambua zimetoka kwa baba yake shetani, akizipokea basi NADHIRI yako imetoka. Basi mweka NADHIRI alitoka akaanza kuzunguuka mitaani, alipofika katika mtaa wa mvuleni wenye chuo cha wavulani alikuta #KUSANYILO kubwaa lawatu.
 
Back
Top Bottom