Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,809
- 140,807
MFALME ANA MASIKIO MAKUBWA KAMA YA PUNDA.
Zamani palikuwa na mfalme aliyekuwa na masikio kama ya punda. Siku zote alikuwa akifunga kilemba kichwani kuficha masikio yake. Nywele zake zilikuwa, zikawa ndefu sana.
Siku moja mfalme alimwita kinyozi mmoja hodari ili amnyoe. Kinyozi huyo aliambiwa asiseme atakachokiona. Kinyozi alikubali. Mfalme alivua kilemba. Kinyozi aliona mfalme ana masikio makubwa kama ya punda. Alipokuwa anamnyoa alijizuia sana asicheke.
Kinyozi alipomaliza kumnyoa mfalme, alikwenda nyumbani. Alijizuia sana asitoe siri hiyo hata kwa mke wake. Baadaye alishindwa kukaa kimya. Basi, kinyozi alifunga safari, akaenda msituni. Alipofika alichimba shimo dogo. Aliinamia kwenye shimo hilo akasema polepole; mfalme ana masikio makubwa kama ya punda. Kisha alifukia shimo hilo.
Baadaye mahali pale paliota mti. Ule mti ulikuwa, nao ukapata hamu ya kutoa siri ile. Basi kila upepo ulipovuma mti ulitoa sauti. Sauti ilisema; mfalme ana masikio makubwa kama ya punda. Mtu mmoja aliyekuwa anakata miti alisikia maneno hayo. Alipofika kijijini kwao aliwaeleza watu. Akasema; msituni kuna mti unasema maneno ya ajabu. Watu wengi wakaenda msituni kuusikiliza. upepo uliopovuma mti ukatoa sauti; mfalme ana masikio makubwa kama ya punda. Basi baada ya muda mfupi habari hiyo ilienea nchi nzima. Habari hiyo ilimfikia mfalme. Mfalme akasema; Loo! Kumbe dunia haina siri.
IKO SIKU SIRI YA JEURI YA BASHITE ITAJULIKANA
Mods sijakosea Jukwaa