Hadithi: Kizuizi

Hadithi: Kizuizi

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Posts
4,421
Reaction score
1,792
HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA KWANZA

Majira ya saa tatu asubuhi waumini waliokuwa wanatarajia kuingia katika misa ya pili walikuwa wameanza kujongea katika kanisa katoliki parokia ya mtakatifu Francis maeneo ya National jijini Mwanza. Ibada ya kwanza ilikuwa inakaribia kumalizika, kipengele cha matangazo mbalimbali ndio kilikuwa kinaimalizia hiyo ibada iliyokuwa inaongozwa na paroko wa kanisa hilo. Hali ya hewa ilikuwa ya ubaridi na waumini walikuwa wamejikunyata kila mmoja kwa namna yake huku wakiyapokea matangazo hayo.

Mwanamama mfupi sana, nadhifu alikuwa mbele ya kipaza sauti akifuatisha mpangilio wa matangazo, aliyamaliza yale ya kawaida na sasa akayafikia mengine.

Matangazo ya ndoa yalikuwa yanasomwa.

"Bwana James Syaga wa parokia ya mtakatifu Kalolilwanga jijini Mwanza anatangaza kufunga ndoa na Bi. Emmy John wa parokia ya mtakatifu Joseph wilayani Kahama, hili ni tangazo lao la pili. Kwa yeyote mwenye kizuizi afikishe ofisini kwa paroko kabla ya tangazo la tatu" sauti ya mwanamama aliyekuwa anasoma matangazo ilisikika. Umri wake ulikuwa unafaa kuitwa bibi lakini alisoma kwa makini sana ukilinganisha na vijana ambao walikuwa na tatizo la kuchanganya herufi ‘r’ na ‘l’. Huyu hakukosea.

Kanisa zima lilikuwa kimya, vilio vya watoto na vikohozi vya hapa na pale pekee ndio viliweza kuvuruga utulivu kiasi fulani. Ndege waliokuwa wamejenga viota vyao katika kanisa hilo pia walikuwa wanaruka hapa na pale huku wakiimba nyimbo zao nzuri za kuvutia.

Mwanamama yule aliendelea kusoma matangazo mengine ya ndoa huku umakini ukiwa kwa hali ya juu kwa wale waliokuwa wanasikiliza, kwa wale wasiokuwa na ndoa wakawa wanajisikia aibu huku wenye ndoa wakijisikia fahari kuwa mfano kwa wengine.

Tofauti na vilio vya watoto, kuna watu wazima wawili walikuwa wananong'ona kwa tahadhari ili wasiweze kusikiwa na mtu mwingine kuwa na wao wanachangia kuvunja utaratibu ndani ya kanisa, hasahasa padri aliyekuwa anaongoza ibada hii ya misa. Maana hakuwa na dogo, akikugundua unanong’ona alikuwa anakusema hapohapo.

Wawili hawa mwanamke na mwanamume walikuwa katika mjadala mkubwa sana.
"Ni Jimmy huyohuyo...haiwezekani Bibiana haiwezekani" Mwanaume alikuwa akimwambia mwenzake wa kike aliyeitwa Bibiana.

"Wewe Deo, ndiye James huyo au watakuwa wamefanana majina?" Mwanamke ni kama hakuwa na uhakika bado.
"Ni yeye bwana, mi namfahamu hadi huyo msichana anayetaka kumuoa...anachofanya sio sahihi." Deo alimjibu Bibiana kwa manung’uniko makubwa sana.

"Kama ni yeye kweli, kesho naenda kwa Paroko, sikubali." alimaliza mazungumzo Bibiana huku uso wake ukitangaza chuki dhidi ya James Syaga.

Chuki aliyoijua yeye na nafsi yake.
Labda alitaka aolewe yeye? Labda ni chuki binafsi. Nani anayejua?
Deo akamuunga mkono.

****

Mazungumzo ya kunong'ona kati ya Bibiana na Deo ndani ya kanisa wakati matangazo ya ndoa yakiendelea yalimshtua kijana Joseph Boniphace ambaye alikuwa anaanza kupitiwa na usingizi baada ya kuwa amejikunyata kwa muda mrefu, mazungumzo hayo yalianza kama kero kwake, kwani yalikuwa yakimzuia kusinzia kwa amani, lakini kutajwatajwa jina la James na watu hawa kulichangia mshtuko wake wa pili. Kwa nini wanamtaja James?? Alijiuliza. Lazima kuna kitu hapa.

Kwa tabia ya kupenda kujua yasiyomuhusu alitumia fursa hiyo kujitendea haki. Aliukemea ule usingizi nao ukamtii. Akayaamuru masikio yake kuwa makini, nayo pia yakamtii. Akaifurahia hali ile. Akayafumba macho yake kama vile amesinzia kumbe yu macho!!

Tabia yake hii ya kupenda kujua mengi tena yasiyomuhusu ilimfanya apate umaarufu fulani usiokuwa na tija wala malipo, umaarufu wa kijinga katika vikundi vikundi alikuwa muongeaji mkuu, jambo gani limpite Jose asilijue? Skendo gani litapita mtoto huyu wa Boniphace pembeni na asilijue mwanzo hadi mwisho wake?? Kwa maisha yake hayo ya kujua kila kitu hatimaye akafupishwa jina lake kuwa Jose kwani kumuita Joseph ilionekana ni kupoteza muda lakini ili kumkumbuka mzazi aliyemzaa kijana huyu jina la Boniphace likafupishwa na kuwa B yaani Jose B.

Jose B licha ya kujifanya kujua mengi, hakuwa muongo kila mara alikuwa na taarifa za uhakika, kwa hali hiyo watoto wa mjini wakawa wanamuita’wa ukweli’ na hatimaye likaunganika jina tamu kutamka lililoyapendeza masikio ya kila mtu kusikia Joseph Boniphace akawa Jose B Waukweli.
Jina alilolipenda na kulitendea haki. Jose akawa Jose kweli.

Jose alijifanya amesinzia kabisa lakini masikio yake yalikuwa wazi yakisikiliza kwa makini minong'ono hiyo kama yalivyokuwa yameamurishwa. Machale yakamcheza kuwa hayo mazungumzo hayakuwa tu ya kimbea ambayo yanaweza kumuongezea umaarufu bali yangeweza kutumika pia kama biashara kwake.
Jose kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kupenda kujua kila kitu akawaza kuyatumia mazungumzo hayo ya siri kujipatia chochote kitu. Jose akawaza pesa!!

Japo hakuwa akimfahamu vyema huyo muhusika anayezungumziwa lakini aliamini akiweka jitihada atamfahamu.

Kizuizi!! Alijiuliza, wanataka kumwekea kizuizi gani? Alikosa majibu. Na hata kama angekuwa na jibu bado hakumjua muhusika.

Roho ilimuuma sana baada ya wawili hawa kukatisha maongezi yao. Aliumia kwa kuwa bado alikuwa hajapata stori iliyokamilika, lawama zake zilienda moja kwa moja kwa padri aliyeamuru waumini wasimame kwa ajili ya sala ya mwisho ya kufunga ibada. Jose B akahisi padri hakuwa ametenda haki.
Lakini alifurahi kwa kuwa alipata vitu vitatu, jina la James Syaga, pili majina ya waliokuwa wakimteta (Deo na Bibiana) na tatu KIZUIZI!!

"Hata hayo yanatosha!'' Alijisemea Jose B huku akiyakariri vyema majina hayo matatu kama vile anaenda kuweka majibu hayo katika mtihani darasani.

Sasa alitamani misa imalizike aanze kuitumia taarifa hiyo, alihofia kuwa maneno mengi ya kukariri aliyokuwa akiyataja padri kwa kutumia kinasa sauti yangeweza kumuathiri na kumsahaulisha yale majina. Hivyo kila padri alivyokuwa akiwaamrisha kusema maneno fulani. Deo alijibu kwa sauti ya chinichini, ‘Deo, James, Bibiana na Kizuizi’. Kwa mtindo huu hakuna lililompotea kichwani.

Jose B, alijiona mwenye bahati sana kuwa wa kwanza kupata habari. Nitazidi kuwa maarufu!!! Aliwaza.
Na pia nitapata pesa ikibidi.

***

Maandalizi ya harusi yalikuwa yamepamba moto, simu ya James Syaga ilikuwa bize kila mara, vikao vilikuwa vinaendelea jijini Dar es salaam. Marafiki wa James hawakutaka kumwangusha kila mmoja alishughulika ipasavyo, jambo zuri kila mmoja alikuwa vyema kiuchumi.

Milioni thelathini zilizuwa zimechangwa tayari katika vikao vitatu vya harusi. Na bado ahadi zilikuwa nyingi sana, na zilikuwa ahadi za uhakika. Kwani zilitolewa na watu wa uhakika.

Emmy John alikuwa amechukua likizo ya majuma mawili kazini, sasa alikuwa ni mtu wa kujifungia ndani tu akisubiri kwa hamu kubwa kutimiza ndoto yake, ndoto ya kuolewa huku akiwa na usichana wake (bikra), ahadi aliyowahi kuwahaidi wazazi wake tangu akiwa katika umri wa balehe. Na kubwa zaidi ndoto ya kuolewa na James, mwanaume wa maisha yake.

Emmy na James wote waliona kama siku hazisogei. Sasa tangazo la pili lilikuwa limepita, na lilikuwa limebaki tangazo moja waweze kuhalalishwa.

James Syaga na Emmy John kuwa mtu na mke wake.

Hiyo ndoto kila mtu aliyewafahamu wawili hawa alitamani itimie.

Na kwa nini isitimie? Pesa zilikuwepo. James alikuwa na biashara zake na Emmy alikuwa mfanyakazi, tena anayelipwa mshahara mkubwa.

Pande mbili za familia hazikuwa na vikwazo vyovyote juu ya ndoa hii. Familia ya Emmy ilimpenda sana James. Sasa nini cha kuzuia ndoto hii kutimia?? Hapakuwa na chochote!!!

Wakati kila upande ukiamini kuwa hakuna kitakachoharibika. Kinaibuka kizuizi katika tangazo la tatu na la mwisho, kizuizi kipo maili nyingi sana kutoka jiji la Dar es salaam, Kizuizi kipo jijini Mwanza.

Hakuna anayejua.

Je? Ni kizuizi kipi Bibiana na Deo wanataka kumwekea James Syaga?

Je? Jose B atafanikiwa KUKIGEUZA KIZUIZI biashara??

NINI KITATOKEA?

Usikose sehemu inayofuata. Huenda yakakukuta siku moja na wewe!!!!

ITAENDELEA
 
HADITHI: KIZUIZI
Sasa alitamani misa imalizike aanze kuitumia taarifa hiyo, alihofia kuwa maneno mengi ya kukariri aliyokuwa akiyataja padri kwa kutumia kinasa sauti yangeweza kumuathiri na kumsahaulisha yale majina. Hivyo kila padri alivyokuwa akiwaamrisha kusema maneno fulani. Deo alijibu kwa sauti ya chinichini, ‘Deo, James, Bibiana na Kizuizi'. Kwa mtindo huu hakuna lililompotea kichwani.
Hahahahaaaa, nimecheka kweli hapa! Huyu jamaa ni 'Jose B waukweli' kweli!
 
Tatizo mkuu sio kuendelea ila tatizo ni lini? Tunachoshwa na haya mambo ya kusubiri kwa ahadi hewa.
 
HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA PILI

Pande mbili za familia hazikuwa na vikwazo vyovyote juu ya ndoa hii. Familia ya Emmy ilimpenda sana James. Sasa nini cha kuzuia ndoto hii kutimia?? Hapakuwa na chochote!!!
Wakati kila upande ukiamini kuwa hakuna kitakachoharibika. Kinaibuka kizuizi katika tangazo la tatu na la mwisho, kizuizi kipo maili nyingi sana kutoka jiji la Dar es salaam, Kizuizi kipo jijini Mwanza.
Hakuna anayejua.

****

ENDELEA.........

Mzee Syaga Magayane alikuwa akiipokea mikono ya pongezi kutoka kwa wazee wenzake katika hali ya majivuno.

Ndiyo!! Lazima ajivune, kijana wake alikuwa ameamua kufunga ndoa. Raha iliyoje kupata mjukuu ukiwa na meno yako yote mdomoni???

Mzee Syaga akiwa amejihifadhi ndani ya suti maridadi ambayo wazee wachache wa umri wake waliweza kujikimu kuzivaa. Suti hiyo ilitoka jijini Dar es salaam, kwa mkamwana wake (Emmy). Japo alikuwa hajawahi kumuona lakini kwa asilimia zote alikuwa ameridhika mwanaye huyu kumuoa binti huyu ambaye alikuwa haishi kumpigia simu mara kwa mara.

"Laiti kama mama Jimmy angekuwepo…." Mzee Syaga aliwaambia wazee wanzake na kuwatia simanzi kwani alikuwa amewakumbusha msiba wa miezi kadhaa iliyopita, msiba wa mke wake mpenzi. Mama yake James.

Baadhi ya wazee walimgongagonga mgongoni ishara ya kumpooza. Akapoa!!!

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale idadi ya watu waliokuwa wamemzunguka walianza kupungua, mmoja baada ya mwingine.

Watano, wanne, watatu, wawili hatimaye mzee Syaga akabaki peke yake. Taratibu akaanza kujikongoja kurejea nyumbani kwake maeneo ya Nyakato Sokoni, hakutaka kupanda daladala kwani alipenda kuitumia fursa hiyo kufanya mazoezi ya viungo.

Alipofika shule ya msingi Gedeli ndipo alipogundua kuna mtu anaongozana naye muda mrefu sana tangu alipokuwa anatoka kanisani.

"Shikamoo mzee wangu!!!"

"Marahabaa mwanangu" alijibu kwa sauti iliyosikika barabara huku akipepesa macho kumtazama anayemsalimia. Sura ilikuwa ngeni.

"Mzee nimekuwa nakutazama muda mrefu kweli, kwanza pole kwa kutembea…"

"Hapana usijali usijali nafanya mazoezi" alijibu mzee Syaga. Huku akimtathmini yule kijana na mavazi yake ya heshima, shati iliyonyooshwa vyema na ikamkaa mwilini baada ya kuwa imechomekewa kwenye suruali yake ya kitambaa malidhawa.

"Ahaa!! Ok!! Naitwa Joseph Boniphace mzee wangu unanikumbuka??"

Mzee Syaga akafikiria kwa wakati kisha akakiri kutomkumbuka Joseph, Jose B akatabasamu kisha akajisogeza zaidi kwa mzee Syaga.

"Hata hivyo ni muda mrefu sana…anyway mimi rafiki yake na James, nimesikia anatajwa kanisani nikashtuka kweli ujue ni miaka hatujaonana!!" Jose B akaingiza kaujanja kake. Mzee Syaga akauvaa mkenge.

Kwanza akacheka sana kwa majivuno kisha akamshika mkono Jose kama anamsalimia hivi.

"Mwenzako ameamua kufunga ndoa kabisa, yaani nimefurahi kweli aisee…..amefanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi nimefarijika kwa kweli……" mzee Syaga hakuhitaji kumjua Jose zaidi akaanza kumwaga yake ya moyoni.

Jose akajisikia mshindi tena katika raundi ya kwanza. Mwisho wa mazungumzo mzee Syaga akampatia Jose B namba ya simu ya James.

Laiti kama angejua janja ya Jose B waukweli kamwe asingeitoa namba.

******

Gauni la harusi na shela yake vilikuwa vimekaa vyema katika kiwiliwili cha mwanadada Emmy, ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo mbele ya James.

James hakuijutia milioni moja na laki mbili aliyompatia Emmy kwa ajili ya kununua shela hiyo. Hakika ilikuwa imempendeza sana.

Hamu ya kumuoa Emmy ikazidi, wawili hawa wakawa wanatamaniana lakini wakajikaza na kuikumbuka ahadi.
Mpaka ndoa!!!

Wakiwa chumbani hapo, mara James alimsogelea Emmy akawa anamrekebisha gauni lake, katika kumrekebisha, kucha fupi za Jimmy zikakwangua shingo ya Emmy. Emmy akafanya malalamiko ya kimahaba, James akambembeleza naye pia kwa sauti ya kimahaba, mara wakajikuta wanatazamana usoni. Emmy akataka kuyakwepesha macho yake, James akawahi akamshika kidevu akamnyanyua wakawa wanatazamana, pumzi za Emmy zikaanza kupishana kwa nguvu, James akaligundua hilo, akazidi kumtazama Emmy. Emmy akausogeza mdomo wake ukakaribia kukutana na wa James. Hakuwa akijielewa ni nini anafanya lakini alihisi yupo katika hisia za ajabu sana.

James akaufungua kidogo mdomo wake ili aweze kumpokea Emmy, mara ghafla mlio mkali wa simu ya kichina ukawashtua, ilikuwa ni simu ya James. Emmy akajinasua kutoka katika mikono ya James huku akiona aibu.
James akailaani ile simu kwa kukatisha uhondo huo, kwa shingo upande akaitoa simu na kuitazama.
Ilikuwa namba mpya, hakusita kuipokea.

"James Syaga nazungumza hapa nani mwenzangu!!!" alihoji kwa ghadhabu kiasi fulani.

"Joseph hapa, Jose…" upande wa pili ukajibu kwa kutetereka kiasi fulani.

"Nadhani sikufahamu!!!" alisema kwa utulivu Jimmy huku akijaribu kuizuia ghadhabu iliyokuwa inamuandama kwa kukatishwa alichokuwa anataka kufanya.

"Aaah!! Ndio lakini naitwa Jose….kaka kuna ishu nahitaji tuzungumze"

"Unaweza kuzungumza." Alijibu bila wasiwasi.

"Upo peke yako??"

"Tafadhali naomba uzungumze..suala la nipo peke yangu ama la hilo niachie mimi" alijibu kwa jazba.

"Ni biashara lakini…"

"Aisee…unaweza kwenda moja kwa moja kwenye pointi yako ya msingi??" alitoa karipio, hasira ilianza kumzidia.

"Una kizuizi katika ndoa yako..bila shaka haitafungwa kama hautafanya biashara na mimi"

"Nini???" alishtuka Jimmy.

"Kizuizi.." ilijibu kwa utulivu sauti ya pili.

"Ki…..kipi" aliuliza huku akikosa utulivu.

"Hicho unachouliza ndo biashara yenyewe niliyokwambia, biashara ya kizuizi"

"Kimewekwa katika kanisa gani??" sasa alikuwa amejiweka mbali na Emmy wakati anaendelea kuzungumza.

"Hata kulijua kanisa ni mojawapo ya hiyo biashara, kizuizi na kanisa vyote ni biashara."

"Ni nani wanaotaka kuniwekea"

"Kukutajia wabaya wako pia ni kigezo kimojawapo katika biashara hii, yaani kizuizi, kanisa na wabaya wako vyote ni biashara" ilijibu kwa utulivu sauti upande wa pili.

"Upo wapi wewe."

"Ukitaka kunijua nilipo maana yake umeingia rasmi katika biashara je upo tayari au"

"Nipo tayari."

"Tukutane Mwanza!!!" sauti ilimjibu huku ikijiamini kisha simu ikakatwa.

James Syaga akawa anatetemeka huku akijiuliza ilikuwaje akatokwa jasho jingi kiasi hicho. Wasiwasi ukatanda, hofu ikamtawala. Akazungumza machache na kumuaga Emmy.

Hofu ikatembea naye njia nzima. Akafikiria na kubashiri baadhi ya vizuizi vinavyomkabili. Akakiri kuwa vyote havikuwa na uwezo wa kuizuia ndoa yake isifungwe, na vichache vyenye uzito vilikuwa siri yake.

Sasa kulikoni hii simu kutoka huko inapotoka??

Tafurani.....

....Ni kizuizi gani Jimmy anataka kuwekewa??
....Je? Atayaweza masharti ya Jose B wa ukweli??
....Na ni biashara ipi Jose B anaitaka kwa James
....Bibiana aliapa ataenda kwa Paroko,
....NINI HATMA YA KIZUIZI HIKI????

ITAENDELEA..................
 
Rich Pol, njoo huku mizambwa amerudi tena
Kuna mtu anaitwa Jose B waukweli huku, wahiii
 
Last edited by a moderator:
HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA TATU

"Hicho unachouliza ndo biashara yenyewe niliyokwambia, biashara ya kizuizi"
"Kimewekwa katika kanisa gani??" sasa alikuwa amejiweka mbali na Emmy wakati anaendelea kuzungumza.
"Hata kulijua kanisa ni mojawapo ya hiyo biashara, kizuizi na kanisa vyote ni biashara."
"Ni nani wanaotaka kuniwekea"
"Kukutajia wabaya wako pia ni kigezo kimojawapo katika biashara hii, yaani kizuizi, kanisa na wabaya wako vyote ni biashara" ilijibu kwa utulivu sauti upande wa pili.
"Upo wapi wewe."
"Ukitaka kunijua nilipo maana yake umeingia rasmi katika biashara je upo tayari au"
"Nipo tayari."
"Tukutane Mwanza!!!" sauti ilimjibu huku ikijiamini kisha simu ikakatwa.
James Syaga akawa anatetemeka huku akijiuliza ilikuwaje akatokwa jasho jingi kiasi hicho. Wasiwasi ukatanda, hofu ikamtawala. Akazungumza machache na kumuaga Emmy.

*****

ENDELEA...............

Jose B waukweli alijikuta katika maisha yake anawaza jambo ambalo hapo kabla hakuwahi kuliwaza.

Utajiri!!! Na pesa zisizokuwa za jasho lake. Awali Jose B alikuwa akitumia tabia yake ya kujua mengi kutafutia sifa na umaarufu mtaani, ni yeye alikuwa wa kwanza kufahamu juu ya msiba mkubwa wa msanii maarufu wa filamu, ni yeye pia aliyeisambaza taarifa ya kuvishana pete ya msanii wa muziki Tanzania na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania. Haya yote yalimwezesha kupata sifa kemkem. Hili la sasa lilikuja kivingine.

Pesa.

Ile hofu iliyomkumba James wakati wanazungumza kwenye simu ilimtia jeuri. Akiwa katika moja ya chumba kimoja katika nyumba ya mzee Boniphace ambaye ni baba yake mzazi. Jose B alikuwa akikitazama kile chumba katika namna ya kukichoka, hakika ilikuwa lazima akichoke kwani kilikuwa hakina sealing board, hakikuwa na feni wala marumaru. Halafu kama hiyo haitoshi Jose alikuwa amezichoka karaha za kuishi na wazazi wake. Kila siku mama yake alimchukulia kama mtoto, alikuwa akimgombeza mbele ya wadogo zake bila kujali kuwa Jose alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu tayari.

Jose akaanza kufikiria juu ya kuhama, ili apate uhuru wa kutosha uhuru wa kujivinjari na mpenzi wake Diana.

Redio kubwa inayotumia santuri ‘CD' iliyokuwa inamilikiwa na rafiki yake ilimuingiza katika matamanio. Naye akatamani kuwa nayo.

Jose B akamgeuza James mtaji, huku Kizuizi kikiwa ngao yake kuu.
Pesa nje nje!!! Akajisemeza na nafsi yake kisha akaachia tabasamu mwanana akajifunika shuka!!!

******

James alikuwa katika sintofahamu, alijiuliza ni nani huyo anayetaka kuingilia mipango yake ya kufunga ndoa. Alijiuliza tena ni nani anayetaka kumtia katika aibu, aliwafikiria rafiki zake waliotoa michango yao, walivyoacha majukumu yao mengine na kuamua kuisimamia shughuli yake iende sawa.

Leo hii anajitokeza mtu kumwekea kizuizi!! Hapana ilikuwa lazima achanganyikiwe.

James aliwaza mambo kadhaa ambayo yangeweza kuwa kizuizi cha yeye kufunga ndoa. Hakika vizuizi vilikuwa vingi sana lakini karibia vyote vilikuwa ni siri yake. Hakuna mtu alikuwa akivifahamu waziwazi, hata mzazi wake hakuwa akielewa siri za mwanaye.

"Ni nani huyu amefahamu siri zangu???" alijiuliza James bila kupata jawabu.

"Aliyepiga simu si -------- ni mtu mzima na akili zake, lazima kuna jambo hapa, sitakiwi kupuuzia." James alizidi kutilia mkazo suala hili. Huku akiwa makini katika usukani wa gari aliyokuwa anaendesha.
James alipofika nyumbani kwake alipiga simu ya Jose. Ikapokelewa upesi. Wakazungumza mengi huku Jose akisisitiza kuwa hayupo tayari kufanya biashara kwa njia ya simu.

"Hayupo tayari kufanya biashara kwenye simu????" alijiuliza James na kuzidi kupata mashaka juu ya uzito wa biashara hii iliyopo mbele yake. Kama haizungumziki kwenye simu basi ni jambo zito!!! Alikiri James.

Pesa ni kila kitu!! Baada ya kumaliza mazungumzo na Jose, alipiga namba fulani simu ikapokelewa na mwanadada. Baada ya mazungumzo ya dakika tatu James akapata nafasi katika ndege ya kusafiri siku inayofuata kuelekea jijini Mwanza. Safari hii ilikuwa ya siri sana hakumwambia mtu yeyote yule kama atasafiri. Kwani alitegemea kurejea siku hiyo hiyo. Ama kesho yake mapema.

"Nitakupigia simu kesho nikiwa Mwanza" James alimwambia Jose kisha wakaagana.

Jose B alijirusha rusha kwa furaha pale kitandani, furaha yake ilikatishwa na chaga za kitanda kile kufyatuka, Jose akajikuta anasalimiana na sakafu mbovu ya chumba kile. Huku akiwa amekasirika sana alikirekebisha kitanda na kuulaani umasikini kwa lugha zote alizozijua.

Usingizi ukampitia, mlio wa simu yake ukamshtua siku iliyofuata. Alikuwa ni James!!

"Nambie bro!! nipo Mwanza tayari, tuonane wapi kaka" Sauti ya James ilisikika ikinyenyekea. Jose akatabasamu.

"Poa nambie ulipo mi nakuja"

"Kamanga feri huku..unapajua"

"Mwanza ndo home kaka najua kila kona!" alijibu Jose kwa furaha.

"Poa basi nipo pande hizi ukifika karibu na haya mawemawe makubwa nibip"

"Shwari!!"

****

Majira ya saa sita mchana Jose alikuwa amekaa katika meza moja na James. Ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona.

Kule kujiamini kwa Jose wakati anatoka nyumbani kuliingia katika mgogoro baada ya jicho lake kumwona James. James alikuwa na hadhi ya juu sana, na mwonekano wake pekee ulitosha kuutangaza ukwasi wake. James alionekana kuwa kati ya watanzania wachache wanaofaidi matunda ya nchi hii.

"Yap!! Jose….ni biashara gani"

"Kizuizi"

"Kipi?"

"Nitangazie dau tuanze biashara!!"

"Wewe ndiye mwenye biashara kaka…anza!!" James alijibu bila kuwa na hofu yoyote.

Jose B akazungusha akili upesi upesi akaona akitaja pesa nyingi ataonekana mwenye tamaa sana, pia akahofia kutaja dau dogo kwani angeweza kuonekana mwongo na asiyejua biashara. Akaifikiria pesa ambayo kwake itakuwa faida zaidi.

"Milioni moja!!" akataja kwa uoga huku akijiuliza iwapo ni kubwa ama ndogo sana.

"Nitakupa milioni sita….tumalize

Biashara." James alimjibu Jose. Soda aliyokuwa anakunywa ikampalia. Jose hakutegemea kusikia dau likipanda maradufu kiasi hicho. Ilikuwa ndoto kusikia pesa kama hizo. Isitoshe tangu azaliwe hakuwahi hata kumiliki shilingi laki moja.

Jose akaamini ilikuwa siku ya muujiza kwake.

Milioni mbili ikawekwa mezani ikiwa ishara ya kuanza biashara, Jose alizikusanya huku akitetemeka. Hakuhesabu badala yake aliziweka kwa fujo katika mfuko wake.

Baada ya hapo Jose akageuka kasuku, akaanza kutiririka kila neno alilolifahamu. James akawa kimya anameza.

Akasimulia kuanzia mkasa wa kanisani, tangu lilipotangazwa tangazo la ndoa.

****

Bibiana alitamani sana kuwasiliana na paroko siku ile ile baada ya ibada lakini paroko akawa ametingwa na majukumu mengi hivyo akamwahidi kuwa amwone baada ya siku tatu yaani siku ya jumatano. Bibiana alipaona mbali sana lakini hakuwa na ujanja ilimlazimu kuvumilia.

Mawasiliano baina yake na Deo yaliendelea kwani lao lilikuwa moja.

Siku ya jumatano wakapanga waende wote kumwekea kizuizi James.

Kizuizi cha kumzuia asifunge ndoa na Emmy.

Ilikuwa siku ya jumanne, siku moja kabla ya kufika ile siku ambayo Bibiana alikuwa amepanga kumtembelea paroko kwa ajili ya kuweka pingamizi la James kufunga ndoa.

Alikuwa ametoka kuhemea mahitaji kadhaa katika soko maarufu la ‘Mwendesha'. Ulikuwa ni mchana tulivu sana kwani asubuhi ya siku hiyo kimvua cha rasharasha kilikuwa kimenyesha.

Alipofika nyumbani na kukitua kikapu chake, alipata ugeni wa ghafla. Walikuwa ni wanaume wawili waliopendezea katika suti zao, lakini walikuwa wameyaficha macho yao nyuma ya miwani. Mmoja alionekana kuwa mwenyeji kiasi eneo hilo huku mwingine akionekana kuwa mgeni.

"Bibiana Michael!!!" alisikia sauti ikimwita, akajiweka vyema kuwatazama wageni wake huku akiunda tabasamu la kuwakaribisha wageni.

Ghafla bila kutegemea alishangaa kukutanisha macho yake na mtutu wa bunduki, kabla hajafikiria kupiga kelele. Alikutana na macho makali kisha onyo!!!

Akakaa kimya!!!

"Nani yupo ndani??"

"Peke…peke yangu!!!"

Ishara ya kutangulia ndani ikamwongoza akaingia ndani.

Bibiana akaketi kwa uoga mkubwa, wale wanaume hawakuketi, jicho la bunduki likaendelea kumtazama binti yule.

"Bibiana…sina muda wa kupoteza. Unataka kumwambia nini paroko kuhusu ndoa yangu??"

Bibiana alikutana na macho makali ya James, alikuwa tofauti sana na yule James aliyemzoea miaka kadhaa nyuma. James huyu alitangaza ukatili waziwazi.

Wakati Bibiana akitoa macho bila kujua cha kujibu. James alitoa ishara ya ghafla. Na pale pale likafanyika tendo la kushtukiza.

Bibiana akalainika taratibu, akaanza kuliacha kochi alilokuwa amekalia, akasalimiana na vigaye vilivyochakaa vilivyokuwa ndani ya sebule yao bila kupenda. Akanyooka!!!!

Kimya kikatawala!!!!

Kimya kikuu.

********

****Jose B waukweli ameuza siri....

****James ana kwa ana na Bibiana ambaye anakijua kizuizi......

**** JE NINI KIMETOKEA????

*****Emmy hajui lolote kuhusu kizuizi...yupo jijini akiingojea ndoa.....

Usikose kufuatilia nini kimejificha hapa.

ITAENDELEA.............
 
Inaniuma sana!

Yaani kila kona imekuwa na VIZUIZI awali tulizoea Vizuizi vya askari barabarani katika ugaguzi au kutafuta magari yenye issue fulani,

Lakini sasa hata kwenye maisha kuna VIZUIZI.
 
mmmmhhhh mie nasubiri iishe yote ndo niisome kwa wakati mmoja, ikiisha naomba uni mention please ili nije kuisoma. Nice story though.
 
HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA TATU

“Hicho unachouliza ndo biashara yenyewe niliyokwambia, biashara ya kizuizi”
“Kimewekwa katika kanisa gani??” sasa alikuwa amejiweka mbali na Emmy wakati anaendelea kuzungumza.
“Hata kulijua kanisa ni mojawapo ya hiyo biashara, kizuizi na kanisa vyote ni biashara.”
“Ni nani wanaotaka kuniwekea”
“Kukutajia wabaya wako pia ni kigezo kimojawapo katika biashara hii, yaani kizuizi, kanisa na wabaya wako vyote ni biashara” ilijibu kwa utulivu sauti upande wa pili.
“Upo wapi wewe.”
“Ukitaka kunijua nilipo maana yake umeingia rasmi katika biashara je upo tayari au”
“Nipo tayari.”
“Tukutane Mwanza!!!” sauti ilimjibu huku ikijiamini kisha simu ikakatwa.
James Syaga akawa anatetemeka huku akijiuliza ilikuwaje akatokwa jasho jingi kiasi hicho. Wasiwasi ukatanda, hofu ikamtawala. Akazungumza machache na kumuaga Emmy.

*****

ENDELEA...............

Jose B waukweli alijikuta katika maisha yake anawaza jambo ambalo hapo kabla hakuwahi kuliwaza.

Utajiri!!! Na pesa zisizokuwa za jasho lake. Awali Jose B alikuwa akitumia tabia yake ya kujua mengi kutafutia sifa na umaarufu mtaani, ni yeye alikuwa wa kwanza kufahamu juu ya msiba mkubwa wa msanii maarufu wa filamu, ni yeye pia aliyeisambaza taarifa ya kuvishana pete ya msanii wa muziki Tanzania na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania. Haya yote yalimwezesha kupata sifa kemkem. Hili la sasa lilikuja kivingine.

Pesa.

Ile hofu iliyomkumba James wakati wanazungumza kwenye simu ilimtia jeuri. Akiwa katika moja ya chumba kimoja katika nyumba ya mzee Boniphace ambaye ni baba yake mzazi. Jose B alikuwa akikitazama kile chumba katika namna ya kukichoka, hakika ilikuwa lazima akichoke kwani kilikuwa hakina sealing board, hakikuwa na feni wala marumaru. Halafu kama hiyo haitoshi Jose alikuwa amezichoka karaha za kuishi na wazazi wake. Kila siku mama yake alimchukulia kama mtoto, alikuwa akimgombeza mbele ya wadogo zake bila kujali kuwa Jose alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu tayari.

Jose akaanza kufikiria juu ya kuhama, ili apate uhuru wa kutosha uhuru wa kujivinjari na mpenzi wake Diana.

Redio kubwa inayotumia santuri ‘CD’ iliyokuwa inamilikiwa na rafiki yake ilimuingiza katika matamanio. Naye akatamani kuwa nayo.

Jose B akamgeuza James mtaji, huku Kizuizi kikiwa ngao yake kuu.
Pesa nje nje!!! Akajisemeza na nafsi yake kisha akaachia tabasamu mwanana akajifunika shuka!!!

******

James alikuwa katika sintofahamu, alijiuliza ni nani huyo anayetaka kuingilia mipango yake ya kufunga ndoa. Alijiuliza tena ni nani anayetaka kumtia katika aibu, aliwafikiria rafiki zake waliotoa michango yao, walivyoacha majukumu yao mengine na kuamua kuisimamia shughuli yake iende sawa.

Leo hii anajitokeza mtu kumwekea kizuizi!! Hapana ilikuwa lazima achanganyikiwe.

James aliwaza mambo kadhaa ambayo yangeweza kuwa kizuizi cha yeye kufunga ndoa. Hakika vizuizi vilikuwa vingi sana lakini karibia vyote vilikuwa ni siri yake. Hakuna mtu alikuwa akivifahamu waziwazi, hata mzazi wake hakuwa akielewa siri za mwanaye.

“Ni nani huyu amefahamu siri zangu???” alijiuliza James bila kupata jawabu.

“Aliyepiga simu si -------- ni mtu mzima na akili zake, lazima kuna jambo hapa, sitakiwi kupuuzia.” James alizidi kutilia mkazo suala hili. Huku akiwa makini katika usukani wa gari aliyokuwa anaendesha.
James alipofika nyumbani kwake alipiga simu ya Jose. Ikapokelewa upesi. Wakazungumza mengi huku Jose akisisitiza kuwa hayupo tayari kufanya biashara kwa njia ya simu.

“Hayupo tayari kufanya biashara kwenye simu????” alijiuliza James na kuzidi kupata mashaka juu ya uzito wa biashara hii iliyopo mbele yake. Kama haizungumziki kwenye simu basi ni jambo zito!!! Alikiri James.

Pesa ni kila kitu!! Baada ya kumaliza mazungumzo na Jose, alipiga namba fulani simu ikapokelewa na mwanadada. Baada ya mazungumzo ya dakika tatu James akapata nafasi katika ndege ya kusafiri siku inayofuata kuelekea jijini Mwanza. Safari hii ilikuwa ya siri sana hakumwambia mtu yeyote yule kama atasafiri. Kwani alitegemea kurejea siku hiyo hiyo. Ama kesho yake mapema.

“Nitakupigia simu kesho nikiwa Mwanza” James alimwambia Jose kisha wakaagana.

Jose B alijirusha rusha kwa furaha pale kitandani, furaha yake ilikatishwa na chaga za kitanda kile kufyatuka, Jose akajikuta anasalimiana na sakafu mbovu ya chumba kile. Huku akiwa amekasirika sana alikirekebisha kitanda na kuulaani umasikini kwa lugha zote alizozijua.

Usingizi ukampitia, mlio wa simu yake ukamshtua siku iliyofuata. Alikuwa ni James!!

“Nambie bro!! nipo Mwanza tayari, tuonane wapi kaka” Sauti ya James ilisikika ikinyenyekea. Jose akatabasamu.

“Poa nambie ulipo mi nakuja”

“Kamanga feri huku..unapajua”

“Mwanza ndo home kaka najua kila kona!” alijibu Jose kwa furaha.

“Poa basi nipo pande hizi ukifika karibu na haya mawemawe makubwa nibip”

“Shwari!!”

****

Majira ya saa sita mchana Jose alikuwa amekaa katika meza moja na James. Ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona.

Kule kujiamini kwa Jose wakati anatoka nyumbani kuliingia katika mgogoro baada ya jicho lake kumwona James. James alikuwa na hadhi ya juu sana, na mwonekano wake pekee ulitosha kuutangaza ukwasi wake. James alionekana kuwa kati ya watanzania wachache wanaofaidi matunda ya nchi hii.

“Yap!! Jose….ni biashara gani”

“Kizuizi”

“Kipi?”

“Nitangazie dau tuanze biashara!!”

“Wewe ndiye mwenye biashara kaka…anza!!” James alijibu bila kuwa na hofu yoyote.

Jose B akazungusha akili upesi upesi akaona akitaja pesa nyingi ataonekana mwenye tamaa sana, pia akahofia kutaja dau dogo kwani angeweza kuonekana mwongo na asiyejua biashara. Akaifikiria pesa ambayo kwake itakuwa faida zaidi.

“Milioni moja!!” akataja kwa uoga huku akijiuliza iwapo ni kubwa ama ndogo sana.

“Nitakupa milioni sita….tumalize

Biashara.” James alimjibu Jose. Soda aliyokuwa anakunywa ikampalia. Jose hakutegemea kusikia dau likipanda maradufu kiasi hicho. Ilikuwa ndoto kusikia pesa kama hizo. Isitoshe tangu azaliwe hakuwahi hata kumiliki shilingi laki moja.

Jose akaamini ilikuwa siku ya muujiza kwake.

Milioni mbili ikawekwa mezani ikiwa ishara ya kuanza biashara, Jose alizikusanya huku akitetemeka. Hakuhesabu badala yake aliziweka kwa fujo katika mfuko wake.

Baada ya hapo Jose akageuka kasuku, akaanza kutiririka kila neno alilolifahamu. James akawa kimya anameza.

Akasimulia kuanzia mkasa wa kanisani, tangu lilipotangazwa tangazo la ndoa.

****

Bibiana alitamani sana kuwasiliana na paroko siku ile ile baada ya ibada lakini paroko akawa ametingwa na majukumu mengi hivyo akamwahidi kuwa amwone baada ya siku tatu yaani siku ya jumatano. Bibiana alipaona mbali sana lakini hakuwa na ujanja ilimlazimu kuvumilia.

Mawasiliano baina yake na Deo yaliendelea kwani lao lilikuwa moja.

Siku ya jumatano wakapanga waende wote kumwekea kizuizi James.

Kizuizi cha kumzuia asifunge ndoa na Emmy.

Ilikuwa siku ya jumanne, siku moja kabla ya kufika ile siku ambayo Bibiana alikuwa amepanga kumtembelea paroko kwa ajili ya kuweka pingamizi la James kufunga ndoa.

Alikuwa ametoka kuhemea mahitaji kadhaa katika soko maarufu la ‘Mwendesha’. Ulikuwa ni mchana tulivu sana kwani asubuhi ya siku hiyo kimvua cha rasharasha kilikuwa kimenyesha.

Alipofika nyumbani na kukitua kikapu chake, alipata ugeni wa ghafla. Walikuwa ni wanaume wawili waliopendezea katika suti zao, lakini walikuwa wameyaficha macho yao nyuma ya miwani. Mmoja alionekana kuwa mwenyeji kiasi eneo hilo huku mwingine akionekana kuwa mgeni.

“Bibiana Michael!!!” alisikia sauti ikimwita, akajiweka vyema kuwatazama wageni wake huku akiunda tabasamu la kuwakaribisha wageni.

Ghafla bila kutegemea alishangaa kukutanisha macho yake na mtutu wa bunduki, kabla hajafikiria kupiga kelele. Alikutana na macho makali kisha onyo!!!

Akakaa kimya!!!

“Nani yupo ndani??”

“Peke…peke yangu!!!”

Ishara ya kutangulia ndani ikamwongoza akaingia ndani.

Bibiana akaketi kwa uoga mkubwa, wale wanaume hawakuketi, jicho la bunduki likaendelea kumtazama binti yule.

“Bibiana…sina muda wa kupoteza. Unataka kumwambia nini paroko kuhusu ndoa yangu??”

Bibiana alikutana na macho makali ya James, alikuwa tofauti sana na yule James aliyemzoea miaka kadhaa nyuma. James huyu alitangaza ukatili waziwazi.

Wakati Bibiana akitoa macho bila kujua cha kujibu. James alitoa ishara ya ghafla. Na pale pale likafanyika tendo la kushtukiza.

Bibiana akalainika taratibu, akaanza kuliacha kochi alilokuwa amekalia, akasalimiana na vigaye vilivyochakaa vilivyokuwa ndani ya sebule yao bila kupenda. Akanyooka!!!!

Kimya kikatawala!!!!

Kimya kikuu.

********

****Jose B waukweli ameuza siri....

****James ana kwa ana na Bibiana ambaye anakijua kizuizi......

**** JE NINI KIMETOKEA????

*****Emmy hajui lolote kuhusu kizuizi...yupo jijini akiingojea ndoa.....

Usikose kufuatilia nini kimejificha hapa.

ITAENDELEA.............

mizambwa umetisha sana kaka
 
mmmmhhhh mie nasubiri iishe yote ndo niisome kwa wakati mmoja, ikiisha naomba uni mention please ili nije kuisoma. Nice story though.

Angalia kwani nitaweza kuwa nimekusahau kukukumbusha ukisubiri ifike mwisho. Kwani Mungu akipenda inategemewa kuwa hewani kwa zaidi ya mwezi mmoja. Ni kisa kirefu juu ya KIZUIZI.

Endelea kutiririka kila inapotoka.
 
mizambwa, inaniuma sana
Uko juu! Wapi Mommadou Keita....

Angalia kwani nitaweza kuwa nimekusahau kukukumbusha ukisubiri ifike mwisho. Kwani Mungu akipenda inategemewa kuwa hewani kwa zaidi ya mwezi mmoja. Ni kisa kirefu juu ya KIZUIZI.

Endelea kutiririka kila inapotoka.
 
Last edited by a moderator:

HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA NNE

"Bibiana…sina muda wa kupoteza. Unataka kumwambia nini paroko kuhusu ndoa yangu??"
Bibiana alikutana na macho makali ya James, alikuwa tofauti sana na yule James aliyemzoa miaka kadhaa nyuma. James huyu alitangaza ukatili waziwazi.
Wakati Bibiana akitoa macho bila kujua cha kujibu. James alitoa ishara ya ghafla. Na pale pale likafanyika tendo la ghafla.
Bibiana akalainika taratibu, akaanza kuliacha kochi alilokuwa amekalia, akasalimiana na vigaye vilivyokuwa ndani ya sebule yao bila kupenda. Akanyooka!!!!
Kimya kikatawala!!!!

****************

ENDELEA.........

Bibiana alikuwa ametishika haswaa na ujio wa ghafla wa James nyumbani kwake. Mwanzoni alidhani kuwa ilikuwa ni kwa nia njema lakini baada ya kushuhudia jicho la bunduki akatambua kuwa hapakuwa na amani tena.

Kabla hajaelewa kwanini afuatwe na bunduki nyumbani kwake, nyumba ya kimasikini isiyokuwa na chochote cha kuweza kupora. Bibiana alijikuta ameelekezwa kwenda ndani, James asiyekuwa na huruma hata chembe usoni alimuuliza ni kitu gani alitaka kushtaki kwa paroko ili kuzuia ndoa yake isifungwe. Bibiana alijikuta anatetemeka badala ya kujibu kile alichokuwa anaulizwa.

Hofu yake haikumsaidia lolote, alitakiwa ajibu ni siri gani alitaka kuipeleka kwa paroko. Neno moja alilotamka Bibiana lilitosha kumshawishi James aliyekuwa ameikamata vyema bastola yake aliyokuwa anaimiliki kihalali kabisa, kuminya kiwambo cha kuzuia sauti kisha akafyatua risasi iliyopenya vyema katika mbavu za Bibiana ikimweka katika ladha yenye ubaridi unaofurahisha kisha maumivu makali ya kushangaza na mwisho kuzitenganisha.

Lile neno alilotamka Bibiana, James hakujua kama lilisikiwa na yule mtu waliyekuwanaye ama la. Kwa wakati huo hilo hakulijali sana badala yake alimfuta Bibiana zile sehemu walizoweza kugusana. Alifanya hivyo ili kuondoa zile alama za vidole ambazo zingeweza kumuingiza matatani iwapo upelelezi wa kina ungefanyika.

Lakini kwa maisha duni ya marehemu Bibiana huo ulikuwa mwisho wa habari. Hakuna utafiti wa ziada ungeweza kufanyika.

Siri kubwa aliyokuwanayo Bibiana ikampelekea kukumbana na mauti yake. Kizuizi kisichomuhusu kikaitwaa roho yake bila hiari yake.

Bibiana akageuka hayati Bibiana!!!!

Ukurasa wake katika kitabu cha simulizi ya maisha ya duniani kikawa kimefunikwa hapo hapo!!!

*****

Jose B hakuamini kabisa kama kwa maneno yake aliyompatia James yangeweza kuwa na thamani hata ya shilingi elfu kumi sasa alikuwa na shilingi milioni mbili mfuko mmoja na mfuko mwingine alikuwa na shilingi laki moja aliyopewa kwa ajili ya nauli yake kurudi nyumbani na pia kwa ajili ya kulipia taksi watakapohitaji kukutana tena.

Jose B Waukweli, alikuwa akizidi kushangaa kuwa James hakuhitaji hata kujua huyo Bibiana anaishi wapi.

"Yaani majina mawili tu yamenipatia milioni mbili???" alijiuliza Jose huku akiwa makini kabisa na mifuko yake wasije wakatokea vibaka na kumkwapulia mavuno yake. Mavuno ya kutibua siri.

"Au jamaa alikuwa amelewa ametoa bila kujua???" hakuwepo wa kumjibu Jose B. Jose Waukweli. Akapuuzia maswali aliyokuwa anajiuliza, akazidi kukaza mwendo akafika kituoni akataka kupanda daladala lakini dhamira ikamsuta akahofia kukabwa na vibaka.

Akanyata hadi zilipokuwa taksi.

"Hadi Nyakato shilingi ngapi??" Jose akamuuliza dereva wa teksi.

"Elfu sita kaka.." alijibiwa.

Jose B wa ukweli akakumbwa na pepo la ubahili akaiona elfu sita nyingi sana. Akaomba kupunguziwa huku akijiapiza kichwani kuwa kama hatapunguziwa basi anaghairi kupanda teksi. Bahati nzuri akapunguziwa ikawa 5000, Jose akaingia ndani ya teksi, dereva akaondoa kuelekea Nyakato Sokoni.

"Ningejua ningesema elfu nne...huenda angekubali." Jose b aliwaza.

Baada ya dakika kumi, Jose akashuka ndani ya teksi akiwa amemlipa dereva gharama aliyokuwa ameitaja.
Hatua ya kwanza tu iliyokanyaga ardhi, Jose B akajihisi yu tofauti, alijihisi kama amekuwa mwepesi sana na ana uwezo wa kupaa, akajiuliza ni nini kinamfanya kuwa hivyo, upesi akapata jibu kuwa ni pesa.
Jose alijitahidi sana kujiweka katika hali ya kawaida lakini haikuwezekana alitamani sana kumwambia mtu jambo lililomtokea lakini ubinafsi nao ukamkumba akagundua kuwa akimwambia mtu basi huyo mtu lazima atamwomba kiasi cha pesa. Naye hakuwa tayari kutoa chochote kile.

Jose akaamua kubakia na siri yake. Akaingia hadi chumbani mwake akajifungia akafunga na madirisha akazima simu akazitoa pesa.

Zilikuwa pesa halali kabisa!!!

Jose hakumaliza kuzihesabu baada ya kugundua kuwa alikuwa anatetemeka hivyo kila mara kukosea mahesabu. Harakaharaka kama vile kuna mtu alikuwa anakaribia kuingia alizikusanya pesa zake na kuzihifadhi katika begi lake la nguo. Kisha akajinyoosha kitandani akajaribu kusinzia ikashindikana. Hakuwa na amani hata kidogo.

Akiwa katika kugalagala kitandani, mara ghafla akaikumbuka sauti ya mdogo wake wa kiume akiwa anamlalamikia mama yake kuwa amerudishwa nyumbani kwa kuwa hajalipia pesa ya kiti na meza. Akaisikia sauti ya mama yake ikimjibu, "Subiri baba yako akirudi umwambie mimi sina pesa", baba aliporudi Jose hakuwepo lakini siku iliyofuata mdogo wake hakwenda shule na siku ya pili yake pia ikawa hivyo hivyo.
Jose akainuka upesi, akavaa kandambili miguuni mwake.

"Frediiiiii!!!!." Aliita kwa amri kuu. Sauti ikamfikia Fred ambaye ni mdogo wake.
Hakuitika akaja kimya kimya.

"Kwa nini hauendi shule siku hizi?" Akauliza. Fred hakujibu akatabasamu, ni kama hakutegemea swali kama lile ghafla kiasi kile.

"Nadaiwa pesa ya michango shuleni" alijibu kwa sauti isiyo na matumaini.

"Shilingi ngapi?." Aliuliza kama mzazi.

"Elfu ishirini." Alitamka kwa sauti iliyoonyesha kukata tamaa.

Kwa ishara za vidole Jose akamwita mdogo wake naye akamfuata kwa nyuma. Walipokikaribia chumba, Jose akamwambia asubiri kwa nje. Akatii.

"Kesho nataka uende shule sawa!!!" Jose alizungumza huku akimkabidhi mdogo wake shilingi elfu thelathini. Fred alizipokea huku akiwa katika kutoamini maana tangu azaliwe ilikuwa mara ya kwanza kupokea pesa nyingi kama hiyo kutoka kwa kaka yake. Akashukuru mara mbilimbili akaondoka.

"Hiyo shule yenu inafundisha vizuri?." Aliuliza wakati Fred anaanza kuondoka.

"Hivyo hivyo si unajua shule za serikali." Alijibu kwa unyonge.

"Ok! Nitalifanyia kazi." Alijibu kwa ujivuni huku akiwa ameridhika.

Jose alikuwa kama anamiliki milioni mia.

*****

Emmy alishangazwa sana na safari ya ghafla iliyofanywa na mume wake mtarajiwa, lakini hakuwa na malalamiko yoyote kwani hiyo ilikuwa ni mara ya pili tangu wawe katika mahusiano kwa James kusafiri ghafla bila kuaga.

Hali hiyo ya kutokuwepo kwa James ilimtia katika upweke. Kwani walikuwa wameahidiana kwenda ufukweni kujiliwaza katika siku hiyo. Hivyo Emmy hakujisikia kabisa kubakia nyumbani, lakini hakuwa na pahali pa kwenda.

Akiwa katika chumba chake Emmy aliamua kupoteza mawazo kwa kuangalia filamu mbalimbali, nyingi zikiwa zinahusiana na maisha ya mahusiano ya kimapenzi na ndoa kwa ujumla. Kati ya filamu alizokuwa akiangalia nyingi zilikuwa zimeigizwa na wahindi.

Akiwa amezama katika dimbwi la kutafakari filamu hizo, alisikia mlango wake ukigongwa.

"Ingia!!" Aliruhusu.

Aliyekuwa anagonga mlango alipojaribu kufungua haukufunguka, ndipo Emmy akakumbuka kuwa alikifunga kitasa kwa kutumia funguo. Taratibu akaichukua kanga yake akajifunga vyema na kuuendea mlango akaufungua. Alikuwa mama yake.

"Mama nawe!! Ushanikatisha tena filamu yangu." Alianza kudeka Emmy akimlaumu mama yake kuwa amemsumbua.

"Sio mimi mamangu, una mgeni jamani na simu hata hupokei." Alijibu mama yake Emmy huku akimfinyafinya Emmy mashavu yake laini kabisa.

"Nani tena mama sasa hivi….nawe mbona umeng'aa hivyo unaenda wapi tena mama?? unataka kuniacha mwenyewe hivyo"

"Mimi naenda kwenye ‘Vikoba' mwanangu ushasahau?...ni Lameck amekuja" akamnong'oneza. Emmy akashtuka kidogo. Ni kama hakuitegemea taarifa hiyo kutoka kwa mama yake.

"Yupo wapi?."

"Sebuleni amejaa tele anakusubiria."

"Haya nakuja mama…" Aliaga Emmy na kurejea ndani. Akavaa vyema akajipodoa kidogo kisha akajongea sebuleni.

Macho yake yakakutana na macho ya Lameck, wakajikuta wote wanatabasamu. Ilikuwa ni miaka mingi sana imepita tangu wawili hawa watengane.

Lameck alikuwa ni baba yake mdogo na Emmy, lakini kwa umri waliendana kabisa, kwani Lameck alikuwa mtoto wa mwisho katika familia ya baba yake na Emmy mzee John James. Lameck na Emmy walikua pamoja wakicheza wote, ile heshima ya baba mdogo ilisalia katika jina tu lakini kimatendo walikuwa ni walewale.

Katika utoto wao walicheza michezo mingi sana ikiwemo ule wa kibaba na mama huku katika kombolela pia wakikumbuka jinsi walivyokuwa wanajificha pamoja.

Baada ya kumaliza darasa la saba walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza, Emmy akatupwa Maswa shule ya wasichana huku Lameck yeye akipelekwa shule ya kata hapohapo jijini Dar es salaam.
Huo ukawa mwanzo wa wawili hawa kupunguza ukaribu. Lakini kila likizo waliweza kuwa pamoja katika kusoma masomo ya ziada.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, walikutana tena jijini Dar es salaam. Katika kipindi hiki ndipo yalitokea haya yanayowafanya washangaane na kucheka kwa pamoja.
Emmy na baba yake mdogo wakaanza kutamaniana kimapenzi. Walijaribu kuzuizi hisia zao lakini hawakufanikiwa.

Walipokuwa wakipata upenyo wakiwa wawili, walikuwa wanakumbatiana, na kubusiana.
Jambo ambalo hawakufanikiwa kulitenda ni kufanya mapenzi kwani kila mara walipotaka kujaribu Emmy alikuwa analia kuwa anaumia. Lameck hakutaka kulazimisha akawa anaacha. Alikuwa na huruma sana na hakupenda kumuumiza Emmy ambaye kamwe hakuwahi kufanya mapenzi.

Ngoja ngoja ya Lameck, mara matokeo ya kidato cha nne yakatoka, Emmy akarudishwa shule za wasichana Msalato Dodoma. Lameck hakufaulu, akaamua kwenda jeshini.

Inapita miaka, mawasiliano yanapungua na sasa Emmy afisa mikopo katika benki ya serikali NMB anakutanisha macho na Lameck mwanajeshi kamili kambi ya Makambako Mkoani Njombe.
Wanashindwa kujizuia kucheka wanalipuka kwa vicheko weanakimbiliana na kukumbatiana kwa takribani dakika mbili.

"Hayooo!!!!" mama Emmy anawazomea kiutani alipowakuta wamekumbatiana. Wakajishtukia wakaachiana.

"Mi naenda hivyo Emmy…ngoja niwaache baba na mwana mbadilishane mawazo….shemeji baadaye.." aliaga mama Emmy na kuondoka akiwaacha nyuma Lameck na Emmy.

**************

EMMY na LAMECK wamekutana tena, je watataka kukumbushia kamchezo ka zamani?? Kumbuka Lameck alimuacha Emmy akiwa bikra...

JAMES yupo Mwanza, amemuua BIBIANA kwa kutaka kumwekea kizuizi……JE ndo mwisho wa matatizo??
Vipi hatma ya DEO aliyekuwa anashirikiana na BIBIANA??

JOSE B WAUKWELI ana presha ya kumiliki pesa nyingi kwa ghafla, je ni salama pesa hizi????

*******************

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom