Hadithi: Bruno the Fisherman

Hadithi: Bruno the Fisherman

Bruno The Fishman

Mtunzi.Nyemo

Episode 7

Safari ya kuelekea katika kituo kikuu cha polisi ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Ndani ya gari lile polisi wote walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kwao, kumpata mzee Todd iliwafurahisha na kujiona wakipata pesa ambazo ziliahidiwa kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mtu huyo.
Bunduki zilikuwa mikononi mwao, walimpa ulinzi wa kutosha kwani walichokijua ni kwamba mwanaume huyo alikuwa hatari sana, kama wasingemlinda kama walivyofanya basi hali ingekuwa ya hatari mno. Mzee huyo alikuwa na Bruno humo, walimwangalia kijana yule, hawakumjua alikuwa ni nani kwa yule mzee lakini kitu walichohisi ni kwamba alikuwa kijana wa mzee Todd ambaye alikuwa akishirikiana naye kuuza madawa ya kulevya barani Afrika.
Wakati wakiwa wamekwishafika katika eneo maarufu kwa kuuza vitanda, Vasco Da Gama wakashtukia wakianza kumiminiwa risasi mfululizo. Hawakujua watu hao walikuwa wakina nani, walipigwa risasi lakini hawakuwaona watu waliokuwa wakiwashambulia.
Mpaka wanainama na kujificha, polisi wanne walikuwa chini, damu zilikuwa zikiwatoka. Watu waliokuwa karibu na eneo hilo, hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaanza kukimbia kuyaokoa maisha yao. Vijana ambao waliwashambulia polisi hao, wakatoka walipokuwa wamejificha, walikuwa vijana saba wenye silaha kali aina ya AK 47, walitembea kwa mwendo wa kujiamini huku wakiendelea kulifuata gari lile.
Walipolifikia, wakalizunguka na mwanaume mmoja kuwatangazia polisi waliokuwa humo kwamba walitakiwa kutupa bunduki zao vinginevyo wangelilipua gari hilo. Polisi walivyosikia hivyo wakaogopa na kufanya kama walichoambiwa.
Walifanya hivyo kwa sababu mbili. Moja ni kwamba walihisi kwamba wangelipuliwa kweli lakini kubwa zaidi ni kwamba hawakuwa wakifahamu watu hao walikuwa wangapi.
Walipozitupa tu, wanaume hao wakalisogelea gari hilo, wakawaangalia polisi wote, walikuwa wamelala huku wakiwa na mzee Todd na Bruno ambao nao walikuwa kimya. Vijana hao hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kuwamiminia risasi polisi wote.
“Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno.
***
Milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika kama kawaida. Baada ya mzee Todd na Bruno kukimbia kwa kuruka ukuta, Onyango akabaki ndani ya jumba lile na wenzake. Alijua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, hakujua ni wakina nani walikuwa wakipiga risasi hizo, alichanganyikiwa ndani ya jumba lile kiasi kwamba wakati mwingine alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie ndani.
Alitamani kwenda kupambana lakini kwa jinsi risasi zile zilivyokuwa zikirushwa, alijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari, kwani risasi zilipigwa kwa malengo na nyingi ziliwapata wenzake.
Hakutaka kuona akifa, alitakiwa kupambana mpaka anashinda, njia pekee ya kuyaokoa maisha yake ilikuwa ni kuingia katika dari ndani ya nyumba hiyo. Hilo ndilo alilolifanya, haraka sana akaufungua mlango wa dari na kuingia ndani kujificha.
Huko juu, kulikuwa na harufu chafu, joto lakini alitakiwa kuvumilia kwa sababu tu alitakiwa kuupambania uhai wake. Baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa na wanaume kuingia ndani ya jumba hilo. Aliwasikia vilivyo, wanaume hao wakaanza kuongea ndani ya jumba hilo kwamba watu wote walikuwa wamekufa.
Kwa jinsi Kiingereza chao walivyoongea, alijua kabisa walikuwa Wamarekani, hawakuwa Wazungu wa Afrika Kusini, hakujua sababu za watu hao kuwa mahali hapo na kuwashambulia kiasi hicho. Baada ya dakika moja tu, wanaume hao wakaondoka baada ya kuhakikisha kwamba kila mtu aliyekuwa ndani ya nyumba ile alikuwa amekufa.
Huku akijiandaa kuteremka, akasikia mlango ukifunguliwa tena, muda huo alikuwa Bruno ambaye alifuata kadi ya ATM. Hakumuona, alichokijua ni kwamba alikuwa mmoja wa Wazungu wale hivyo akajificha kama kawaida. Baada ya sekunde kadhaa, mlango ukafungwa na mwanaume huyo kuondoka.
Baada ya nusu saa, Onyango akateremka kutoka ndani ya dari, kile alichokiona kilimsikitisha kupita kawaida, hakuamini kama marafiki zake wote walikuwa wamekufa ndani ya nyumba hiyo.
Hali iliyokuwa ndani ndiyo iliyokuwa na nje pia, kila kona kulitapakaa miili ya marafiki zake. Siku hiyo hapo Soweto kulikuwa na msiba mzito, watu walilia sana na kuwachukua Wazungu kupita kawaida.
Siku iliyofuata, Onyango akawatafuta watu wengine wa kuunda kundi jingine. Alikuwa na hasira mno na hakutaka kabisa kuona wakiendelea kushambuliwa na Wazungu, ilikuwa ni lazima wahakikishe wanapambana vilivyo.
Kundi jingine likaundwa, ingawa alikuwa Mkenya lakini kila Msauzi alikuwa akimpenda, alikuwa mkorofi sana, alijua kupambana na hata kuwalaghai watu wengine waungane naye.
Kuunda kundi kubwa tena haikuchukua siku moja, ilichukua wiki mbili, vijana ishirini wakajikusanya na kuunda kundi jingine kubwa la wahuni. Walichokuwa wakikihitaji zaidi kilikuwa ni silaha tu.
Walizokuwa nazo, hazikutosha, walitakiwa kujipanga na kutafuta nyingine. Baada ya kundi kutimiza mwezi, wakaamua kuondoka hapo na kwenda nchini Msumbiji.
Walichokuwa wakikihitaji kilikuwa ni bunduki tu. Waliogopa kufanya uhalifu Afrika Kusini kwa kuwa walihofia maisha yao na kutafutwa. Hawakutaka kuharibu huko, walitakiwa kuharibu sehemu nyingine kabisa, hivyo wakaenda huko.
Watu waliokuwa na bunduki walikuwa polisi hivyo kuanza kuchunguza na kugundua kwamba kulikuwa na gari la polisi lililokuwa likitoka katika Mbuga ya Limpopo na kuelekea mjini huku wakiwa na bunduki ndani ya gari hilo.
Hiyo ikawa nafasi yao, wakaelekea mjini na kutafuta sehemu kujificha. Hakukuwa na mtu aliyeonekana kuwa na hofu nao, walivaa kiheshima na walikuwa wakirandaranda mpaka kipindi ambacho gari la polisi lilipoanza kuonekana.
Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kulishambulia, watu waliokuwa mahali hapo wakakimbia kwani walijua kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari. Kwa kuwa mule kulikuwa na polisi nane, waliamini kwamba kungekuwa na bunduki za idadi hiyo ambazo zingewafanya kuwa na idadi kubwa ya bunduki na hivyo kuendelea kufanya uhalifu.
“Na hawa tuwafanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Nao wamalize,” alisema mwingine, wakakoki bunduki zao tayari kwa kuwamaliza mzee Todd na Bruno.
Huku kijana yule akijiandaa kuwafyatulia risasi watu hao, Onyango akaamuru waache kwani alitaka kuwaona kwanza. Hilo halikuwa tatizo, kijana huyo akaacha, Onyango akasogea mpaka kule, watu aliowaona, yeye mwenyewe akashtuka.
“Bruno!” aliita huku akionekana kushtuka.
“Onyango!”
“Vipi tena? Mbona sielewi?” aliuliza Onyango huku akiwaangalia kwa mshangao mkubwa.
Bruno hakujibu kitu, kitendo cha kumuona Onyango tu kilimaanisha kwamba maisha yao yangekuwa salama. Hilo lilikuwa eneo la tukio, hawakutakiwa kukaa sana mahali hapo, walichokifanya ni kuchukua bunduki walizokuwa wakizitaka na kuondoka mahali hapo.
Wakaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea nchini Afrika Kusini kupitia katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo. Walijua njia za panya, walijua njia ambazo hakukuwa na kamera.
Asubuhi ya siku iliyofuata wakafika huko, wakaelekea mpaka Soweto na kupumzika. Huko ndipo Bruno akaanza kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea, kwamba walikuwa na mpango wa kwenda Kenya lakini wakajikuta wakikamatwa.
“Mnataka kurudi Kenya?” aliuliza Onyango.
“Ndiyo!”
“Basi subiri nifanye mpango! Endeleeni kukaa hapa.”
Hawakuwa na jinsi, waliambiwa kwamba walitakiwa kusubiri na hivyo kufanya hivyo. Waliendelea kubaki mahali hapo huku siku zikiendelea kukatika. Alichokuwa akikifanya Onyango ni kuwatafutia watu ambao aliwaamini ambao wangewachukua watu hao mpaka nchini Kenya.
Bruno alikuwa na mawazo tele, kwake, siku moja ilionekana kuwa na saa arobaini na nane kwani alikuwa akisubiri sana lakini hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wakati mwingine Bruno alikuwa akimuuliza kuhusu namba za simu za watu aliokuwa akiwafahamu nchini Kenya. Kwa Onyango, hilo halikuwa tatizo, aliwafahamu watu hao kwani kulikuwa na Wakenya wengi kutoka katika Kijiji cha Guolduvai.
Onyango akawa na kazi mbili, kwanza kuwatafuta vijana ambao wangefanikisha wao kufika nchini Kenya lakini pia vijana ambao walitoka katika kijiji hicho.
Baada ya mwezi kukatika ndipo akafanikiwa na hivyo kuwasiliana na Onyango na kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari.
Hata kabla Onyango hakumpelekea namba ya simu ya Alfred, mwanaume ambaye alimpata Afrika Kusini, akaamua kumpigia simu yeye mwenyewe na kuanza kuzungumza naye.
Alimwambia kwamba Bruno, mwanaume ambaye bila shaka alisadikiwa kufariki dunia nchini Kenya alikuwa hai nchini Afrika Kusini, ila mbali na hilo, alimwambia kwamba inawezekana Bruno akaja kuwa bilionea mkubwa kwa kuwa alikuwa na bilionea mkubwa ambaye alimsaidia kwa kila kitu.
“Bruno namkumbuka! Kijiji kizima kinajua kwamba amekufa,” alisema Alfred.
“Hajafa! Tupo naye huku!”
“Wapi?”
“Afrika Kusini!”
“Inawezekana vipi?”
“Ndiyo hivyo, ni stori ndefu, nafikiri akija huko atakwambia nini kilitokea,” alisema Onyango.
“Kwa hiyo nifanyeje?”
“Amesema mtafute rafiki yake anayeitwa Abdul, umwambie kwamba yupo hai!”
“Na nimwambie kuhusu ubilionea wake?”
“Hilo juu yako sasa!” alisema Onyango na kukata simu.
Baada ya hapo, akarudi nyumbani na kumwambia Bruno kwamba kila kitu kilikuwa tayari hivyo walichotakiwa ni kuanza safari siku inayofuata. Hilo halikuwa tatizo, wakajiandaa, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo kwani walikuwa wamekaa mno huku wakinusurika vifo na vifungo.
Bruno hakutaka kuridhika, alihitaji kuzungumza na huyo mwanaume kutoka nchini Kenya, hilo halikuwa tatizo, akapewa namba ya simu na kumpigia lakini kwa bahati mbaya, siku ya Alfred haikuwa ikipatikana.
Mpaka kesho yake inafika na kuondoka, bado simu ya mwanaume huyo haikuwa hewani. Vijana wanne walikuwa wakiondoka nao kuelekea nchini Kenya, hawakutakiwa kufika huko, walitakiwa kuishia njiani lakini pia hawakutakiwa kupitia Msumbiji, walitakiwa kupitia Botswana, Zambia, Tanzania na kuingia nchini Kenya.
Waliiona hiyo kuwa safari ndefu lakini walikuwa na uhakika kwamba watu hao wangeweza kufika huko salama kabisa. Baada ya kujiandaa kwa kila kitu, wakaanza safari hiyo kwa siri kubwa sana kuelekea nchini Kenya.
Wakati huo, tayari Bruno alikwishachukua kiasi cha dola laki moja benki ambapo dola elfu ishirini alimgawia Onyango kama shukrani huku akimuahidi kumtumia kiasi kingine cha pesa baada ya kufika nchini Kenya.
Safari ikaanza, ilikuwa ni ndefu na yenye kuchosha sana. Waliondoka kwa kujifichaficha sana mpaka wakatoka nje ya Afrika Kusini na kuingia Botswana.
Huko, njiani kote ni pesa tu ndiyo iliyokuwa ikitumika. Walipokuwa wakiona mambo magumu, walitoa kiasi cha pesa na kuwahonga polisi hivyo kuruhusiwa kupita katika sehemu ambazo hawakutakiwa kufika.
Walipoingia huko nchini Botswana, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuchukua hoteli ya kawaida na kutulia. Bruno aliendelea kumpigia simu Alfred lakini hakuwa akipatikana, hilo lilimchanganya, alichokuwa akihitaji ni kuzungumza na mwanaume huyo na kumwambia kuhusu kwenda kule alipokuwa akiishi na kumwambia Abdul kwamba alikuwa hai.
Safari hiyo ilichukua wiki tatu mfululizo na ndipo wakafanikiwa kufika Tunduma nchini Tanzania. Hapo, wakachukua basi Mbeya Mjini ambapo huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa kuelekea nchini Kenya.
Njiani, walichoka mno, walitamani hata Tanzania uwe mwisho wao, hawakutaka kuendelea zaidi lakini hawakuwa na jinsi. Walikuwa na pesa za kutosha, walipofika Mbeya Mjini, wakaelekea katika duka la kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kitanzania kiasi cha shilingi milioni sita na kuendelea na safari yao.
Kidogo kuwepo nchini Tanzania kuliwapa amani. Watu wa huko hawakuwa wakiangalia televisheni sana, walizipata taarifa kuhusu mzee Todd lakini hakukuwa na yeyote yule aliyeonekana kujali kuhusu mzee huyo.
Hapo Mbeya Mjini, walikaa kwa usiku mmoja na asubuhi wakapanda basi na kuanza safari ya kuelekea jijini Tanga. Safari yao ilichukua saa kumi na mbili wakafika jiji humo ambapo wakatulia katika nyumba ya wageni huku wakijiandaa safari ya kuelekea Mombasa.
“Tunaingia Kenya kesho, ila pia tutatakiwa kuingia kwa njia za panya kama tulivyofanya huko nyuma,” alisema Bruno.
“Ila Kenya si kwenu?”
“Ndiyo! Sina hati ya kusafiria, nahisi litakuwa tatizo!”
“Sawa. Basi tutatumia pesa kama kawaida,” alisema mzee Todd.
Hilo ndilo la msingi lililotakiwa kufanywa. Walichokifanya siku iliyofuata ni kuanza safari kwa njia ya basi kuelekea nchini Kenya. Njiani, hawakuonekana kuwa na hofu, waliamini kwamba wangefika nchini humo salama kabisa.
Basi lilitembea kwa mwendo wa kasi kuelekea mpakani mwa Tanzania na Kenya. Japokuwa huko kulikuwa na ulinzi mkubwa lakini walikuwa na uhakika wa kupita pasipo tatizo lolote lile. Ndani ya basi walikuwa wakizungumza mambo mengi, mzee Todd alimshukuru mno Bruno kwa kuwa alimsaidia sana mpaka kipindi hicho kuwa hai.
Hakuwa na familia yake lakini kitendo cha kuwa hai kipindi hicho kilimpa uhakika wa kuendelea kuishi na kujipanga kwa ajili ya maisha yake ya mbele.
Kulikuwa na kesi ya kuuza madawa ya kulevya, hakutaka kufikiria hilo sana kwani alikuwa na uhakika wa kulishinda, kitu pekee na cha umuhimu kabisa kilikuwa ni kuelekea nchini Marekani na kuendelea na maisha yake.
“Nakushukuru sana Bruno, bila wewe nadhani sasa hivi ningekuwa marehemu,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Bruno.
“Tumesaidiana! Hata mimi nakushukuru sana! Naamini kila kitu kilitokea kwa mpango wa Mungu!” alisema Bruno huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
“Unahitaji nini nikufanyie?” aliuliza mzee huyo.
“Unifanyie?”
“Ndiyo!”
“Mimi ni masikini sana, mkwe hanitaki kwa kuwa mimi ni masikini!” alisema Bruno.
“Hilo si tatizo! Kuna jingine ambalo unataka nikufanyie?” aliuliza mzee Todd.
“Labda kukitengeneza Kijiji cha Guolduvai ninapoishi, hakuna zaidi,” alijibu Bruno.
Walikaa na kuzungumza mengi, wakati huo safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Baada ya saa kadhaa, wakakaribia katika mpaka wa Tanzana na Kenya kwa upande wa Tanga ulioitwa Horohoro.
Siku hiyo ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, kulikuwa na idadi kubwa ya magari yaliyokuwa yakisubiri kuingia nchini Kenya. Mbali na magari hayo, pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakitaka kuingia na kutoka.
Kila basi, abiria walitakiwa kuteremka na kuangaliwa hati zao za kusafiria. Kwao, hawakuwa na kitu chochote kile, walichokuwa wakikitegemea kilikuwa ni pesa tu walizokuwanazo.
 
Horohoro border aisee umenikumbusha 2010_2013 nimekaa sana hapo kikazi nimewamis watu wa Zingibari, mwaboza na Duga mafoloni
 
Uuwaai hapa ni Kitunga yako tu unajisomea,kama mtu story ishamalizika kuandikwa si itupiwe yote tu..hadi mtu abembelezwe,bora yule anaesema bado anaandika so akimaliza kipande anakitupia
 
Uuwaai hapa ni Kitunga yako tu unajisomea,kama mtu story ishamalizika kuandikwa si itupiwe yote tu..hadi mtu abembelezwe,bora yule anaesema bado anaandika so akimaliza kipande anakitupia
We jamaa unadhan mda wote ni kwenye mtandao kunamaisha nje ya jf
 
Ngoja nianze kufuatilia hii, kufidia nafasi wazi iliyoachwa na Shunie katika Mkufu wa Malkia wa Gosheni.
 
BRUNO THE FISHERMAN

Mtunzi.Nyemo

Episode 8

Mzee Hamidu alichanganyikiwa, alimwangalia binti yake, Ashura aliyekuwa kitandani ambaye alikuwa akisumbuliwa na kifua kikuu, moyo wake ulimuuma mno. Ugonjwa huo ulikuwa ukimsumbua binti yake kwa kipindi cha mwezi mzima, aliambiwa na daktari hapo Mombasa kwamba alitakiwa kumpeleka Nairobi kwa ajili ya matibabu lakini hakuwa na pesa.
Kumpeleka Ashura huko kulihitaji kiasi kikubwa cha pesa, kilihitajika shilingi elfu hamsini ya Kikenya, kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho hata kama angefanya kazi kwa mwaka mzima bado asingeweza kupata kiasi hicho.
Alimwangalia Ashura, moyo wake ulimuuma kupita kawaida, alihitaji pesa kuliko kitu chochote kile. Japokuwa alikuwa mkuu wa polisi mpakani lakini bado mshahara wake haukuwa ukitosha kwa kuwa alikuwa akikatwa madeni mengi ambayo aliwahi kukopa serikali.
Mke wake alikuwa ni mtu wa kulia tu, moyo wake ulimuuma, kila siku alikuwa akikaa pembeni ya binti yake aliyekuwa akikohoa madonge makubwa ya makohozi, alitumia dawa mbalimbali lakini zote hizo hazikuweza kumtibu Ashura.
Siku zikakatika, mzee Hamidu akawa ni mtu mwenye mawazo tele na hata ufanyaji kazi wake haukuwa kama ule ambao ulitakiwa kuwa kwa kuwa muda mwingi alikuwa akimuwaza binti yake aliyekuwa akiteseka kitandani.
Wakati hali ya binti yake ikiendelea kuwa hivyo huku akiwa anaendelea na kazi yake ndipo akapelekewa watu wawili ofisini kwake, mmoja alikuwa Mzungu na mwingine mtu mweusi aliyejitambulisha kwa jina la Bruno.
Watu hao walichukuliwa kutoka ndani ya gari lililokuwa likiingia nchini Kenya kupitia mpakani hapo. Hawakuwa na kitu chochote kile, walikuwa wakiingia nchini Kenya pasipo kibali na hata huyo aliyekuwa akisema kwamba alikuwa Mkenya, hakuwa na kitu chochote kile ambacho kingemtambulisha kwamba alikuwa raia wa nchi hiyo.
Hamidu aliwaangalia, kichwa chake kilivurugika kabisa, hakuwa na hamu ya kuendelea kufanya kazi, alifikiria sana nyumbani kwake, hali aliyokuwa ameiacha kwa binti yake, ilikuwa mbaya mno.
Bruno na mzee Todd waliogopa, walitamani sana kuingia nchini Kenya lakini kwa jinsi hali ilivyokuwa, waliona kabisa wangerudishwa au kwenda kufungwa gerezani kwa kile kilichotokea.
Walibaki wakimwangalia mzee Hamidu, alikuwa kimya huku akiwaangalia kwa zamu. Kitu ambacho kilikuja kichwani mwa Bruno kilikuwa ni pesa tu.
Walikuwa watu watatu ndani ya ofisi ya mzee huyo, hiyo ilikuwa nafasi ya Bruno kuhakikisha anampa rushwa mzee huyo ili wavuke salama mpakani hapo. Hakuamini kama kungekuwa na Mwafrika ambaye angekataa pesa, kila mtu alihitaji pesa kwa kuwa mishahara ya wafanyakazi wa Afrika haikuwa ikitosha kabisa.
“Mlikuwa mnavuka pasipokuwa na vibali, ni kweli?” aliuliza mzee Hamidu huku akiwaangalia.
“Ni kweli ila...”
“Hakuna cha ila, suala ni kwamba mlikuwa mnavuka bila vibali, tena mkajiamini kwa kuona kuwa polisi hawawezi kuwababaisha, mkaona kabisa kwamba sisi si kitu na ndiyo maana mkajiamini, si ndiyo?” aliuliza mzee Hamidu, alionekana kuwa siriazi kupita kawaida, na kila alipokuwa akizungumza, alionyesha na vitendo kabisa.
Kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa vigumu kwa Bruno kuhisi kama mzee huyo angekubali kupokea rushwa, alionekana mwanaume mkakamavu ambaye aliiheshimu mno kazi yake.
Aliwaambia mambo mengi mno, aliwatisha lakini mwisho wa siku Bruno akamuonyeshea noti ya dola mia moja na kumwambia kwamba awaruhusu kupita mahali hapo. Mzee Hamidu akatulia, aliiangalia dola ile, akasimama na kwenda pembeni kabisa ya ofisi ile, akasimama na kuuangalia ukuta.
Hakukuwa na kitu ambacho alijiahidi kutokukifanya katika kazi yake kama kupokea rushwa, kitendo cha kuiona dola ile, kilimkumbusha mtoto wake aliyekuwa nyumbani ambaye alisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu.
Alikaa katika hali hiyo kwa dakika moja na nusu, akayageuza macho yake kwa Bruno na mzee Todd, alikuwa akilia kitu kilichomfanya kila mmoja kumshangaa.
Hakutaka kuwaficha, aliwaambia kwamba hakuwa na lengo la kupokea rushwa, angewaruhusu kuondoka na kuingia nchini Kenya kwani kwa jinsi walivyoonekana, walionekana kuwa na kiu kubwa ya kuingia nchini humo, ila kutokana na hali aliyokuwanayo binti yake, hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kuichukua pesa hiyo.
“Ninaichukua kwa sababu ya mtoto wangu!” alisema mzee Hamidu.
“Amefanyaje?”
“Ni mgonjwa mno! Leo mnaponiona hapa, sijajua ni kitu gani kitaendelea katika maisha yake,” alisema mzee Hamidu, hakupanga kuwaambia watu hao suala hilo lakini alijikuta akiwashirikisha.
Kwa jinsi alivyozungumza, alitia huruma mno, alionekana kuguswa na kile kilichokuwa kikiendelea. Bruno na mzee Todd wakajikuta wakishikwa na huruma, mioyo yao ikajawa na simanzi.
“Tutakusaidia, atakwenda hospitali, atatibiwa na kupona kabisa,” alisema mzee Todd maneno ambayo yalimshtua sana mzee Hamidu.
“Kweli?” aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Niamini!” alisema.
Mzee Hamidu akasimama, akawasogelea na kuwakumbatia. Kwake, kilichokuwa kikiendelea aliona kama ndoto fulani hivi ambapo baada ya muda angeshtuka kutoka usingizini.
Hakukuwa na kesi tena, wakaondoka na kuelekea nyumbani kwa mzee huyo. Walipoonyeshewa Ashura, wao wenyewe walikiri kwamba msichana huyo alikuwa kwenye matatizo makubwa.
Wakachukua gari na kuondoka kuelekea jijini Nairobi. Walitumia saa tatu, wakaingia jijini humo ambapo Bruno akaenda kubadilisha pesa na kuchukua pesa za Kenya na kumpeleka hospitalini.
Walipofika huko, mzee Todd hakuteremka, alibaki ndani ya gari. Bruno, mzee Hamidu, Ashura na mke wa mzee huyo wakaingia ndani ya hospitali na kuonana na daktari, malipo yakafanyika na msichana huyo kulazwa.
“Hiki kitakusaidia wewe na familia yako,” alisema Bruno na kumpa mzee huyo dola elfu kumi na kuondoka zake.
Mzee Hamidu hakuamini, akamsogelea mke wake na kumkumbatia, kwa kiasi alichopewa kilikuwa kikubwa mno ambacho kama angeamua kumtibu mtoto wake, basi wangempa matibabu yote na hata chenji kubaki, tena nyingi tu.
Upande wa pili, Bruno na mzee Todd wakakodi teksi na kuanza kuelekea Mombasa katika kijiji cha Guolduvai. Njiani, mawazo ya Bruno yalikuwa yakimfikiria mpenzi wake, Sharifa, hakujua ni kitu gani kingetokea huko, moyo wake ulikuwa na furaha tele, alitaka kumuona tena, alitaka kuzungumza na mzee Jumanne na kumwambia kwamba alitaka kumuoa msichana huyo kwa kuwa tu alikuwa na pesa, hakuwa masikini kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.
“Siamini kama ninakwenda kumuona Sharifa, ni kipindi kirefu sana kimepita,” alisema Bruno huku akionekana kutokuamini.
***
Sharifa alibaki akimwangalia Alfred, hakuamini kile alichokisikia kwamba mpenzi wake alikuwa na pesa na alikuwa amemtumia kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya ya matumizi yake.
Dola laki moja kilikuwa kiasi kikubwa sana, angeweza kukitumia mwaka mzima na pesa nyingi zingebaki, kwake, hizo pesa hazikuwa tatizo, hazikuweza kumletea furaha zaidi ya kumuona mpenzi wake huyo.
Alimuuliza zaidi Alfred kuhusu Bruno, angefika lini kwani alikuwa amkataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo hivyo alitaka kufahamu ukweli.
“Atafika tu,” alijibu Alfred.
“Lini?”
“Sijajua ila atafika tu!”
Moyo wa Sharifa ukanyong’onyea, hakutaka kurudi nyumbani kwa kuwa tayari alikataa kuolewa kwa ajili ya mwanaume huyo ambaye moyo wake ulitokea kumpenda kwa kiasi kikubwa mno.
Walichokifanya ni kwenda benki ambapo Sharifa akafunguliwa akaunti na kiasi kile cha pesa kuhamishiwa katika akaunti yake huku akimwachia Alfred kiasi cha dola elfu kumi kama shukrani kwake.
Alikaa nyumbani kwa Alfred mpaka ilipofika usiku ndipo akaondoka na Abdul kurudi nyumbani kwao. Mzee Jumanne alipomuona, akamfuata na kuanza kumpiga vibao mfululizo, kwa kile kilichokuwa kimetokea, kilimdhalilisha na kumfanya kuonekana hana maana.
Watu walitoka jijini Nairobi mpaka kijijini hapo kwa ajili ya kufunga ndoa lakini kilichotokea hapo, msichana huyo akakimbia.
Kwake ilikuwa ni aibu kubwa, hakuamini kama binti yake wa kumzaa angeweza kufanya kitu kama kile. Sharifa alilia mno, akaondoka na kuelekea chumbani kwake. Huku nyuma mzee Jumanne alikuwa mtu wa kulalamika tu, alimwambia mke wake kwamba Sharifa aliwadhalilisha sana.
Mke wake alimpoza lakini hakupozeka, hasira alizokuwanazo hapo zilikuwa ni za kiwango cha juu kabisa.
Kijijini hapo, habari ikawa ni Sharifa tu, kile alichokifanya hakikuonekana kuwa kitu kizuri na watu wengi walimlaumu kwa kuwa alikataa kuolewa na mwanaume mwenye pesa kisa Bruno ambaye mpaka kitu hicho hakukuwa na mtu aliyejua mahali alipokuwa, na hata kama alikuwa hai, kila mmoja alijua kwamba alikuwa masikini wa kutupwa.
Siku zikaendelea kukatika, bado Sharifa alikuwa na hamu ya kumuona mpenzi wake, hakutaka kumwambia baba yake kuhusu pesa alizokuwa nazo kwenye akaunti, kila kitu kiliendelea kuwa siri huku akitamani kumuona Bruno akirudi kijijini hapo na kuanza maisha wote wawili.
“Bruno! Rudi mpenzi, ninakukumbuka mno, sikutaka kuolewa kwa ajili yako, rudi mpenzi, nimekukumbuka,” alisema Sharifa. Hayo ndiyo maneno aliyokuwa akiyazungumza kila siku.
Kiasi kile cha pesa kilichokuwa benki hakutaka kutumia pesa yoyote ile, alitulia nyumbani huku sala yake ikiwa ni kumuona mwanaume huyo.
Siku ziliendelea kukatika, mpaka mwezi unakatika, bado Bruno hakuwa amerudi kitu kilichaonza kumtia wasiwasi moyoni mwake.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane jumatatu
 
SAS mkuu c ungefany na nyingn kufidia cku iloenda bure ya jana?
Ni ombi lakin
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom