Hadithi: Bruno the Fisherman

Hadithi: Bruno the Fisherman

Bruno The Fishman

Episode 5

Mtunzi.Nyemo


“Kwa nini tena jamani? Tatizo nini Sharifa!”
“Hapana! Umeniuliza, nimekwambia hapana! Kuna swali tena katika hilo?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Rahman.
Moyo wa Rahman ukanyong’onyea, hakuamini alichokuwa amekisikia. Mategemeo yake yalikuwa tofauti na jinsi alivyodhani hapo kabla, alihisi kwamba baba yake alimaliza kila kitu na ni yeye tu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa msichana huyo.
Hilo lilimuuma lakini hakutaka kukata tamaa, alijua kwamba huyo alikuwa msichana na kama angeendelea na msisitizo wake basi kuna siku angekubaliana naye.
Mpaka wazazi wanarudi mahali hapo, hakukuwa na kitu kilichobadilika lakini Rahman aliona ni muda wake kupambana.
Maisha yaliendelea, hakuacha kwenda Guolduvai, mara kwa mara alikuwa akienda huko na kuonana na Sharifa, alimuonyeshea kwamba alimpenda kupita kawaida, kila alipokuwa akienda alibeba zawadi kwa ajili ya msichana huyo.
Bado hakuweza kuubadilisha moyo wa Sharifa, msisitizo wake ulikuwa uleule kwamba hakutaka kuwa na mwanaume huyo. Mwezi mmoja ulipokatika, ndipo kidogo moyo wa Sharifa ukaanza kulegea na hatimaye akaanza kumkubali Rahman kwani alionekana kuwa mwanaume mpole na mwenye uvumilivu mkubwa mno.
Tabasamu likaanza kuonekana usoni mwake na hatimaye kumwambia kwamba alikubali kuolewa na yeye lakini kwa sharti moja tu, kama lingeshindikana basi amuache na kufa akiwa hajaolewa.
“Nipo tayari kwa sharti lolote lile,” alisema Rahman.
“Ni kwamba nilikuwa na mpenzi!”
“Niliambiwa. Si huyo Bruno?”
“Ndiyo! Inasemekana alikufa baharini. Ila mimi siamini hilo hata kidogo. Najua atakuwa hai sehemu fulani,” alisema Shakira.
“Labda! Hakuna ajuaye.”
“Sasa basi. Kama kuna siku atarudi tena na kugundulika hakufa! Huo ndiyo utakuwa mwisho wangu mimi na wewe hata kama utakuwa umenioa na kukuzalia watoto,” alisema Shakira.
“Haina shida.”
“Unahisi utaweza kuniacha nikaendelea na maisha yangu na mpenzi wangu?”
“Nitakuruhusu! Nakuahidi kukuruhusu endapo atarudi.”
“Sawa. Kama ni hivyo hakuna tatizo!”
Wakakubaliana na maisha kuendelea. Walikuwa wakifanya kila kitu isipokuwa mapenzi tu. Waliahidiana kwamba wangefanya mapenzi siku ambayo wangeoana na kuwa mume na mke. Kwa Rahman hilo halikuwa tatizo hata kidogo, alichokuwa akikiangalia ni kuwa na msichana huyo tu.
Siku zikaendelea kukatika, wazazi wakafurahia na hatimaye tarehe ya kufunga ndoa ikapangwa na wawili hao kujiandaa. Kwa mzee Jumanne ilikuwa ni furaha tele, hakuamini kama hatimaye alifanikiwa kumlaghai mtoto wake na hatimaye alikuwa akiolewa na kijana kutoka katika familia ya kitajiri.
“Hakika umenifanya nijisikie baba! Nakupenda sana binti yangu! Naomba usahau yote yaliyopita,” alisema mzee Jumanne.
“Asante baba! Nimekusamehe!” alisema Sharifa.
Siku zikakatika na hatimaye siku ya harusi kufikia. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele. Sharifa alichukuliwa na kupelekwa Nairobi, akafanyiwa shopping ya maana huku ikiwa tayari imepita miezi sita tangu alipopewa taarifa ya kifo cha mpenzi wake.
Akarudi Guolduvai akiwa Sharifa mwingine, alibadilika, alikuwa mrembo. Chakula kikapikwa, watu wakajiandaa kusherehekea sherehe hiyo. Simu ikapigwa na kuambiwa kwamba msafara wa bwana harusi ulikuwa njiani kuja kuchukua mke.
Wanawake walikuwa wakicheza ngoma, siku hiyo hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kijijini hapo zaidi ya kusherehekea harusi hiyo kubwa.
Bwana harusi alipofika tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kupelekwa katika uwanja maalumu wa kucheza ngoma za kitamaduni na kuanza kucheza. Madrasa ikaanza kazi yake, ikapiga madufu na dua ya maana kupigwa.
Wakati bwana harusi akijiandaa kufunga ndoa huku mzee Jumanne akiwa amekwishakaa kwenye mkeka tayari kwa kufungishwa ndoa hiyo, kwa mbali alionekana Abdul akiwa anakimbia kwa kasi, shati lilikuwa mkononi mwake, watu walimshangaa, hakuwa akikimbia kimya kimya, alikuwa akipiga kelele kwa nguvu huku akiliita jina la Sharifa.
Shekhe aliyetaka kufungisha ndoa ikabidi anyamaze na kumwangalia kijana huyo ambaye alipitiliza mpaka katika chumba alichokuwamo Sharifa kitu kilichomfanya kila mtu kupigwa na butwaa.
“Sharifa...Sharifaaa...Sharifaaa...” aliita Abdul huku akiwa ameingia, Sharifa aliyekuwa kitandani na shela lake akashtuka baada ya kuona mlango umefunguliwa.
“Kuna nini?”
“Bruno yupo hai! Bruno yupo hai Sharifa....” alisema Abdul huku akimwangalia Sharifa aliyeonekana kushtuka.
“Yupo wapi?”
“Sijui! Ila yupo hai! Tuondoke! Bruno yupo hai,” alisema Abdul huku akimshika Sharifa mkono na kumvuta.
Kitendo cha kusikia Bruno yupo hai, Sharifa alichanganyikiwa. Hakukuwa na ndoa tena, huyo ndiye alikuwa mwanaume wa maisha yake, alikubaliana na Rahman kwamba kama mwanaume wake angerudi tena kusingekuwa na ndoa.
Wakatoka ndani, wakapita katika umati wa watu waliokuwa nje ambapo ndoa ilitaka kufungwa. Mzee Jumanne alibaki akishangaa, akasimama na kumuita binti yake aliyekuwa akikimbia na Abdul.
“Sharifa...Sharifa kuja hapa...” alisema mzee huyo.
“Siwezi! Siwezi baba! Bruno yupo hai...” alisema Sharifa huku akikimbia, maneno hayo yalimfanya kila mtu kushtuka, iliwezekanaje mwanaume huyo awe hai na wakati alikufa baharini tena miezi sita iliyopita.
Hata kuwakimbiza wakashindwa kwani watu hao walikuwa wakikimbia kwa kasi huku shela likiwa mwilini mwa Sharifa. Ni ndani ya dakika moja tu, wakapotea machoni mwao. Ubwabwa ukawa mchungu. Pale Rahman alipokuwa, alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani.
***
Hawakuchukua muda mrefu baharini wakafanikiwa kufika nchi kavu ambapo moja kwa moja wakaanza kuondoka huku eneo zima likiwa halina mtu kutokana na milio ya risasi iliyokuwa ikisikika mahali hapo.
Wakaondoka mpaka katika geti namba sita la kuingilia bandarini hapo, hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakaondoka mahali hapo na kwenda barabarani.
Bruno hakujua kitu chochote kile, hakujua ni mahali gani walitakiwa kuelekea, alibaki huku akiangalia huku na kule, kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtoa mzee yule ndani ya meli ile na baada ya hapo basi mzee huyo ndiye angeshikilia usukani kwa kuwa alipafahamu Afrika Kusini tofauti na yeye ambaye ilikuwa ni mara ya kwanza kufika mahali hapo.
“Where to?” (twende wapi?) aliuliza Bruno huku akimwangalia mzee yule.
“Wait?” (subiri)
Akasubiri. Mzee Todd akatulia, alionekana kama mtu aliyekuwa akijifikiria kitu fulani hivi. Baada ya dakika moja, akauinua uso wake na kumwambia Bruno kwamba walitakiwa kwenda sehemu, katika Mtaa wa Kloof ambao ulikuwa na maduka mengi, mtaa pekee ambao ulikuwa ukiongozwa kutembelewa na wakazi wengi wa hapo Cape Town.
Mzee huyo aliendelea kumwambia kwamba huko kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu ambaye angewasiliana naye na kuondoka kurudi nchini Marekani. Wakaanza safari ya kuelekea huko huku kila mmoja akiwa hana kitu kabisa mfukoni mwake.
Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, hakukuwa na mtu aliyeamini kama watu hao walitakiwa kutembea katika jiji hilo la kitalii, jiji lililojaza watu wenye pesa ambapo kila mtu aliyekuwa akionekana barabarani alikuwa na muonekano wa pesa.
Safari ya kwenda Kloof haikuchukua muda mrefu, wakafika. Ulikuwa mtaa uliokuwa na watu wengi waliokuwa wakizunguka huku na kule, wengine walikuwa wakijipiga picha za ukumbusho huku wengine wakifanya manunuzi yao.
Wakaelekea mpaka katika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi za kifahari, mageti makubwa, sauti nyingi za mbwa zilikuwa zikisikika, wakalifuata jengo moja na kuanza kugonga geti, wala hazikupita sekunde nyingi, sauti ya mlinzi ikaanza kusikika kutoka katika kipaza sauti kidogo kilichokuwa kimepachikwa ukutani.
“Wewe nani?” alisikika mlinzi huyo.
“Todd.”
“Nikusaidie nini?”
“Ninataka kuonana na Brown.”
“Una miadi naye?”
“Hapana! Naomba kuonana naye.”
Alichokifanya mlinzi ni kupiga simu ndani ambapo akalisema kama alivyoambiwa. Alimwambia mzee huyo kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuulizia aliyeitwa Todd. Mtu ambaye alikuwa akimfahamu mwenye jina hilo alikuwa mmoja tu, mfanyabiashara maarufu aliyekuwa na utajiri mkubwa.
“Todd! Haiwezekani kuja bila taarifa, hebu subiri,” alisema Brown.
Hapohapo akaelekea katika chumba kilichokuwa na kompyuta mbili na kuanza kuangalia nje kupitia kamera ndogo za CCTV zilizokuwa getini. Aliwaona watu wawili waliokuwa wamesimama, mmoja alimfahamu vilivyo, alikuwa ni mzee Todd lakini kwa jinsi alivyoonekana, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.
Hakutaka kubaki ndani, akaondoka na kuelekea getini, akamwambia mlinzi afungue geti, akafanya hivyo na watu hao kuingia. Alimwangalia Todd, hakiamini kama alikuwa yeye, alibadilika, alionekana mchafu, hakuwa yule Todd aliyekuwa akimfahamu.
“Kuna nini kimetokea?”
“Ni habari ndefu sana. Naomba tuingie ndani kwanza,” alisema Todd.
Hilo halikuwa tatizo, wakaingia ndani na kuanza kumuhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea. Alimwambia kuhusu mpango uliokuwa umesukwa, mpango ambao alikuwa na uhakika kwamba nyuma yake kulikuwa na mtu lakini bahati mbaya hakumgundua mtu aliyekuwa nyuma yake.
“Na huyu?”
“Ni kijana ambaye naye aliletwa ndani ya meli ile,” alijibu Todd kuhusu Bruno.
Brown akanyamaza, akamwangalia Todd, hakuamini alichokuwa amekisikia, alihisi kudanganywa. Akamwambia kwanza asubiri aende chumbani ambapo angempa pesa na kwenda kumfanyia harakati zote za kusafiri na kurudi nchini Marekani.
“Nitashukuru sana,” alisema Todd.
Brown akaondoka. Sebuleni walibaki wawili. Bruno alimwangalia Todd, alikuwa mwanaume mzee, aliyehitaji sana msaada wake, alijua kabisa kwamba kama angemuacha pasipo mtu huyo kufika nchini Marekani basi ingekuwa vigumu sana kufika kwa kuwa tu wale watu ambao waliwatoroka wangemtafuta na kumuua.
Walikuwa wamezungumza na Brown, kwa jinsi alivyoonekana, Bruno alihisi kulikuwa na kitu. Akamwambia Todd kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kwa kuwa moyo wake haukuwa na amani na mwanaume huyo aliyekuwa amewakaribisha.
“Ni rafiki yangu!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
“Unamwamini?”
“Asilimia mia moja. Tusubiri!” alisema Todd ambaye alionekana kutokuwa na hofu hata kidogo.
“Hapana! Simuamini. Nahisi kuna jambo. Tuondoke!” alisema Bruno lakini mzee huyo aliendelea kukataa kwa kumwambia kwamba waendelee kubaki kwa kuwa msaada pekee uliokuwa umebaki ulikuwa ni kwa rafiki yake huyo.
Huku wakiwa wamejiachia kwenye kochi na Kituo cha Televisheni cha SABC kikiendelea na matangazo huku kikiwa kimejiunga na Kituo cha Habari cha CNN cha nchini Marekani, wakaona taarifa ya habari ambayo ilimshtua kila mmoja.
Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusishwa na madawa ya kulevya. Nyumbani kwake kulikutwa na kilo tano za madawa ya kulevya, nakala ambazo zilionyesha kabisa kwamba alikuwa akiifanya biashara hiyo kupeleka Mexico, Cuba na sehemu nyingine.
Polisi waligundua hilo baada ya kwenda kupekua nyumbani kwake na kukuta vitu hivyo vyote. Wote wawili walishangaa kwani mtu huyo aliyekuwa akitafutwa alikuwa Todd.
“Nini?” aliuliza Todd huku akisimama na kuisogelea televisheni.
Hakuamini alichokuwa akikiangalia, alishangaa, ni kweli alikuwa akifanyya biashara ya madawa ya kulevya tena kwa siri kubwa, na hakuwahi kuyapeleka madawa hayo nyumbani na hata familia yake haikuwa ikijua kilichokuwa kikiendelea, sasa iweje mzigo wa madawa hayo yakutwe nyumbani kwake? Nani aliyaweka na wakati hakuwahi kufanya kitu kama hicho?
“Tuondoke,” alisema Bruno, bado hakuwa na amani.
“Hapana! Brown atanisaidia,” alisema mzee huyo huku akianza kutokwa na machozi, alitia huruma.
Bruno hakuwa na imani na Brown, alihisi kabisa kwamba mtu huyo kulikuwa na jambo alilotaka kulifanya. Akayapeleka macho yake katika televisheni ambapo ilitangazwa kwamba kwa yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa ka mzee huyo basi angepewa kiasi cha dola milioni mbili.
“Tuondoke!” alisema Bruno kwa hasira, hakutaka tena kuona mzee huyo akikataa, akamshika na kuanza kumvuta kwenda nje.
Todd alikataa lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana na Bruno na kuondoka naye mahali hapo kwani hakuwa na jinsi, kama kweli mwanaume huyo alikuwa na hofu na Brown, basi hakuwa na jinsi.
***
Bilionea Maxwell alishika simu yake na kuanza kuongea na Innocent, kijana ambaye alikuwa karibu sana na mzee Todd. Alimpigia simu kwa lengo moja tu la kutaka kucheza mchezo fulani ambao aliamini ungeweza kumpoteza kabisa Todd.
Alimwambia kuhusu mpango wake aliokuwa nao, alihitaji mtu wa kumsaidia na hakuona kama kungekuwa na mtu mwingine zaidi ya Innocent. Alimwambia wazi kwamba alitenga kiasi cha dola milioni moja kwa ajili yake kama malipo kwa kazi kubwa aliyoitaka aifanye.
Dola milioni moja kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kiliichanganya mno akili ya kijana huyo. Haraka sana akamuuliza kuhusu kazi hiyo, hakutaka kumficha, alimwambia kwamba alitakiwa kumsaliti mzee Todd.
“Kivipi?”
“Ninataka kuiteka familia yake, si kwa nia mbaya, hapana, ni kwa nia nzuri sana na baadaye nitaiachia,” alisema Maxwell kana kwamba alikuwa mtu mzuri.
“Mmh!”
“Ndiyo! Unaweza kunisaidia katika hilo. Nitakulipa dola milioni moja keshi,” alisikika mzee huyo.
Hilo lilionekana kuwa jambo gumu lakini kiasi cha pesa alichokuwa ametajiwa kilikuwa kikubwa mno, kilimchanganya, hakutaka kuona kiasi hicho cha pesa kikipita mbele yake, kama alitakiwa kumsaliti basi hakukuwa na tatizo lolote lile.
Alikuwa bosi wake, alimfanyia kazi, hakuwa ndugu yake, kama alikuwa bosi wake, aliamini kuna siku mzee huyo angekuwa na uwezo wa kumfukuza na kumuajiri mtu mwingine kwa kuwa tu alihitaji pesa na hata muda mwingine kubana matumizi.
Alijitoa kafara na kumwambia Maxwell kwamba alikubaliana naye hivyo hizo pesa ziandaliwe, hilo halikuwa tatizo. Alichokifanya Maxwell ni kuwasiliana na vijana wake na kuwaambia kwamba alihitaji mzigo wa madawa ya kulevya kilo tano, akapelekewa na kuanza kuwapa maelekezo juu ya nini kilitakiwa kufanyika.
Akapigiwa simu Innocent na kuambiwa kwamba kuna vijana wangekwenda nyumbani hapo na kuingia ndani, walinzi wasingeweza kuwagundua kwa kuwa yeye mwenyewe alitakiwa kusema kwamba alikuwa akiwafahamu kama marafiki wa Todd.
Hilo likafanyika, vijana wakaelekea huko. Innocent mwenyewe hakuona jinsi madawa yalivyokuwa yamebebwa kwani yalibebwa kwa siri sana tena kwa vifurushi vidogo.
Wakati wameingia mpaka sebuleni na vijana wanne, Innocent akaenda kumuita mke wa Todd. Kitendo cha kuondoka sebuleni hapo kilionekana kuwa kosa kubwa, hapohapo vijana wale wakachukua vifurushi vile vya madawa na kuanza kuvificha katika makochi na sehemu nyingine.
Mpaka Innocent na mkewe wa Todd wanafika sebuleni, tayari walikamilisha kila kitu. Wakamwambia mwanamke huyo kwamba walitakiwa kwenda sehemu kuonana na mume wake kwa kuwa alikuwa amejificha kwa kuogopa kutafutwa na wabaya wake.
“Mnasemaje?”
“Mzee yupo! Amejificha, alikwenda nchini Msumbiji. Kuna watu walimteka na kutaka kumuua, alifanikiwa kuwatoroka na kuja huku. Wabaya wake wapo hapahapa jijini New York, ameogopa kuja nyumbani kwani anaamini kwamba wanaweza kuja hapa na kumuua,” alisema kijana mmoja kwa sauti ya unyenyekevu, tena kwa suti aliyokuwa amevaa, ilikuwa vigumu kugundua kama alikuwa mtu mbaya.
“Yupo wapi?”
“Kwenye jumba lake la mafichoni. Mama! Mzee yupo kwenye hatari sana,” alisema kijana huyo, akabadilisha muonekano wa sura yake, akawa na huruma ghafla kama Papa John Paul wa Pili alivyokuwa.
“Jamaniiiiii!”
“Mama hatuna muda,” alisema kijana huyo.
Hakutaka kuchelewa, kwake, mume wake alikuwa kila kitu moyoni mwake, alimpenda kuliko kitu chochote kile. Kwa kuwa aliambiwa kwamba mumewe alikuwa akimsubiri, akamuita na binti yake kwa lengo la kwenda huko kuonana naye.
Wakaondoka kwa kuwa alimwamini kijana yule lakini la zaidi ni kwa sababu alimwamini Innocent. Walinzi hawakujua chochote kile, wakawaruhusu kuondoka, wakaingia ndani ya gari na kuondoka.
Baada ya Maxwell kuambiwa kwamba kila kitu kilikamilika, akapiga simu polisi na kujidai akitoa taarifa ya madawa ya kulevya. Polisi walivyosikia tu, haraka sana wakaelekea huko, walipofika na kufanya upekuzi, wakayakuta madawa hayo ya kulevya na hivyo mtu wa kwanza kushukiwa alikuwa mzee Todd.
Taarifa ikatolewa kwamba mzee huyo alikuwa akitafutwa, na mbaya zaidi ilitoka taarifa iliyosema kwamba alikwenda Afrika kupeleka mzigo mwingine. Kiasi cha dola milioni moja kikawekwa mezani kwa kila mtu ambaye angefanikisha kukamatwa kwake.
***
Mke wa mzee Todd, Juddie na mtoto wake, Martha walipelekwa mpaka katika chumba kilichokuwa na mwanga hafifu na kuambiwa watulie kwenye viti vilivyokuwa ndani ya chumba hicho.
Hawakuelewa mahali walipokuwa, walikuwa wakiangalia huku na kule, chumba hicho kiliwaogopesha kwani mbali na kuwa na viti hivyo pekee, kuta za chumba hicho zilikuwa na michirizi ya damu ambayo ilionyesha kabisa kwamba hakikuwa chumba cha mchezo hata kidogo.
Waliogopa, hawakujisikia amani. Japokuwa waliambiwa kwamba Todd alikuwa huko na ndiye ambaye alikuwa akiwahitaji, hawakuhisi kama kweli hilo jambo lilikuwa hivyo, walihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
Walimwamini Innocent, hawakuwa na hofu naye hata kidogo. Watu waliokuwa wamewachukua hawakuwafahamu lakini kwa kuwa Innocent alihusika katika kila kitu, hawakuhofia kitu chochote kile.
Wanaume wale walikuwa wakiingia kwa zamu, kila walipowauliza, walijibiwa kwamba walitakiwa kutulia kwani kila mtu aliyekuwa ndani ya chumba kile hakutakiwa kupiga kelele kwa kuwa ukimya ndiyo ulikuwa ulinzi wao pekee.
“Tell us, where is Todd?” (tuambie, Todd yupo wapi?) aliuliza Juddie.
“I told you to shout the hell up,” (nimekwambia nyamaza) alisema mwanaume huyo kwa hasira na sauti kubwa iliyomfanya Juddie na mtoto wake, Martha kuogopa.
Wote waliogopa, waliwaona watu hao kuwa mahatili ambao wangewatoa roho yao muda wowote ule kama tu wangeendelea kuongea kitu ambacho hakikutakiwa kufanyika ndani ya chumba hicho.
Waliendelea kukaa mpaka ilipofika usiku wa manane. Hawakulala, bado walikuwa wakiamini kwamba Todd angetokea lakini mpaka inafika alfajiri hakukuwa na dalili za mwanaume huyo na kugundua kwamba kulikuwa na jambo jingine lililokuwa likiendelea.
Asubuhi, wakaletewa chai na kuanza kunywa. Hawakunywa kwa raha, walikunywa huku wakiwa na hofu nzito mioyoni mwao. Ilipofika majira ya saa nne, mwanaume mmoja akaingia na kuanza kuzungumza nao.
Huyo ndiye aliyewaambia kilichokuwa kikiendelea, walikuwa mahali pale kwa kwa sababu Todd alikuwa amewafanya jambo baya ambalo hakutaka kuwaweka wazi. Walishangaa, waliuliza kuhusu jambo hilo baya, hawakuambiwa kitu zaidi ya kuambiwa watulie tu.
Maxwell alipigiwa simu na kuambiwa kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Akaridhika na hivyo kuanza kumtafuta Todd kwenye simu lakini akamkosa.
Hakutaka kujali sana, alichokifanya ni kuwapigia vijana wake na kuwauliza kilichokuwa kikiendelea. Kitu ambacho kilimchosha ni baada ya kusikia kwamba mwanaume huyo alikuwa ametoroka.
“Ametoroka?” aliuliza Maxwell, hakuamini alichokuwa amekisikia.
“Ndiyo mkuu!”
“Inawezekana vipi? Hivi kweli anaweza kutoroka ndani ya meli? Anaweza kuogelea?” aliuliza Maxwell huku akionekana kuchanganyikiwa.
Kijana huyo akaanza kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea bandarini mpaka Todd kutoroka akiwa na kijana waliyemuokota baharini kwa lengo la kumsaidia.
Maxwell alichanganyikiwa, hakuamini alichokisikia, akahisi kabisa alikuwa akidanganywa au kulikuwa na mchezo uliokuwa umechezwa. Si kwamba hakufahamu kuhusu mapigano ya risasi yaliyotokea bandarini huko Cape Town, alifahamu kila kitu lakini kilichomshangaza ni namna ambavyo watu hao walitoroka.
Kwa hasira, akawaambia wawatafute na kukata simu. Kichwa chake kilichanganyikiwa. Kutoroka kwa Todd kilimaanisha kitu kibaya kwake, hakutaka kuona mwanaume huyo akiendelea kuwa hai, kuendelea kuwa hai kungemaanisha mwisho wake kwani kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima kumtafuta na kulipa kisasi.
Wakati huo, taarifa za habari katika vituo mbalimbali vya televisheni vilikuwa vikitangaza kuhusu kutafutwa kwa mwanaume huyo. Kila kona, picha yake ilionekana.
Dunia ilipigwa na butwaa, kile kilichokuwa kikionekana kilimshangaza kila mmoja. Wengi hawakuamini kama utajiri wa mzee huyo ulitokana na biashara ya madawa ya kulevya aliyokuwa akiifanya.
Wema wake, ukasahaulika, chuki za Wamarekani dhidi yake zikaanza kutawala katika mioyo yao. Kila kona watu walikuwa wakiongea kuhusu jambo hilo tu, waliandika mabango, kwenye mitandao walitoa maoni yao huku wakiitaka dunia iseme mahali alipokuwa mwanaume huyo aliyekuwa akiwapoteza vijana wengi kwa kuwauzia madawa ya kulevya.
Maofisa wa FBI (Federal Bureau Of Investigation) wakaanza kumtafuta nchini Marekani huku wale wa CIA (Central Interlligence Agency)wakiondoka kwenda barani Afrika ambapo waliambiwa mtu huyo alikuwepo kwa lengo la kumtafuta.
“We have one week! We have to arrest this dude,” (tuna wiki moja! Inapaswa tumkamate huyu mshikaji) alisema ofisa mmoja.
“Did you find out where he is by now?” (ulikwishajua mahali alipokuwa sasa hivi?)
“Nope! But we have to,” (hapana ila inabidi tumkamate)
Wakati picha zake zilipokuwa zikitoka katika vyombo mbalimbali vya habari ndipo kipindi hichohicho ambacho Brown aliona kwenye televisheni. Alichoamini ni kwamba Todd alikuwa nchini Marekani lakini baada ya kuambiwa na mlinzi kwamba alikuwa akihitajika na mwanaume huyo getini, hakuamini.
Kiasi cha pesa kilichokuwa kimewekwa kilikuwa kikubwa mno, hakutaka kuona akikikosa, kwake, pesa zilikuwa muhimu kuliko hata urafiki. Alikwishawahi kuua watu wengi kwa sababu ya pesa, aliwasaliti watu wengine kwa sababu ya pesa, sasa kumsaliti Todd na kumchoma kwa polisi hakukuwa na tatizo lolote lile.
Kule chumbani alipoelekea, akachukua simu yake na kuwapigia polisi. Aliwaambia kwamba alimuona Todd yule aliyekuwa akitafutwa na muda huo aliokuwa akizungumza nao alikuwa ndani ya nyumba yake, hivyo walitakiwa kufika haraka sana kumkamata.
“Una uhakika ni yeye?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa polisi aliyekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu.
“Acha ushamba! Sasa kama sina uhakika ningewapigia?” aliuliza Brown, swali alilokuwa ameulizwa lilimkasirisha kupita kawaida.
Simu ilipokatika, akaondoka na kurudi sebuleni, alitaka kupiga stori na watu hao mpaka pale ambapo polisi wangefika na kumkamata. Alipokwenda sebuleni, kilichomshangaza ni kwamba mwanaume huyo hakuwepo. Alichanganyikiwa, akatoka na kwenda kwa mlinzi, akamuuliza na kumwambia kwamba watu hao wawili waliondoka.
“Kwa nini uliwaruhusu?”
“Hukuniambia niwazuie mkuu! Nilidhani umemalizana nao,” alijitetea mlinzi.
Hilo lilimchanganya mno, aliona kabisa mamilioni ya dola yakiondoka mikononi mwake katika hatua ya mwisho kabisa. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alitoka mpaka nje ya nyumba ile na kuangalia huku na kule, si Todd wala Bruno aliyekuwa akionekana.
Njiani, Todd na Bruno walipishana na gari mbili za polisi zikienda kule walipokuwa wametoka. Hapo, ndipo Todd akaamini kwamba Brown hakuwa mtu mzuri, alikuwa amewachongea kwa polisi kwa kuwa kukamatwa kwake kungemfanya kupata kitita cha dola milioni moja.
***
Rahman alihisi kuchanganyikiwa, pale alipokuwa hakukukalika hata kidogo, alimwangalia mzee Jumanne ambaye naye kwa kumwangalia tu alionekana kuchanganyikiwa kama alivyokuwa.
Alimpoteza mwanamke aliyekuwa akimpenda, tena katika hatua ya mwisho kabisa kabla ya kufunga ndoa. Alinyong’onyesa, pale alipokuwa alihisi kabisa akipigwa na baridi kali na kuanza kutetemeka,
Uso wake ukajawa na aibu, kila mtu aliyemwangalia, akamuonea huruma kwani hakuvumilia, ni ndani ya sekunde chache machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake.
Alimpenda mno Sharifa, kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu. Alimuahidi mambo mengi mno, na kweli angeyatimiza kwa kuwa alikuwa akimpenda lakini cha kushangaza, msichana huyo akakimbia huku akipiga kelele kwamba hataki kuolewa kwa kuwa Bruno alikuwa hai.
“Who is this man?” (huyu ni nani?) alimuuliza baba yake huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Bruno! The poorest fella in the village,” (Bruno! Mwanaume masikini kabisa hapa kijijini) alijibu baba yake kwani aliambiwa na mzee Jumanne kwamba Bruno alikuwa masikini mno.
Mzee Jumanne alihisi miguu ikimtetemeka, alihisi kama angeanguka muda wowote ule kwani kile kilichokuwa kimetokea, hakukiamini hata mara moja.
Hakutaka hata kumwangalia Rahman, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alikuwa amechanganyikiwa, mtu muhimu kabisa ambaye alitakiwa kuzungumza naye alikuwa James, yeye ndiye aliyemuagiza kwenda kumuua Bruno, kama hakufa, nini kilitokea.
James alikuwa kwenye harusi hiyo, yeye mwenyewe alikuwa amepigwa butwaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka Abdul kufika mahali hapo na kusema kwamba Bruno alikuwa hai.
“James! Nini kimetokea?” aliuliza mzee Jumanne.
“Sijui ni kitu gani kimetokea.”
“Wewe si ulisema ulimuua?”
“Hapana! Nilisema tulimtupa baharini!”
“Ikawaje?”
“Bila shaka alikufa kwani mawimbi yalikuwa yakipiga makubwa mno, bahari ilichafuka,” alisema James huku akimwangalia mzee huyo.
“Niambie kitu kiimoja. Bruno alikufa au hakufa?” aliuliza mzee Jumanne.
“Nahisi alikufa!”
“Sikiliza. Sitaki uhisi. Niambie alikufa au hakufa?”
“Kwa kweli ni ngumu kujibu ila kwa jinsi mawimbi yalivyokuwa, alikufa,” alijibu James, yeye mwenye hakuonekana kujiamini hata kidogo.
Hilo likawa gumzo kijijini hapo, kila mtu alikuwa akiliongelea suala hilo kwamba iliwezekanaje Bruno yule waliyeambiwa kwamba alikufa baharini miezi sita iliyopita awe hai?
Kila mmoja akashikwa na hamu ya kumuona, walitaka kuamini baada ya kumuona lakini si kusikia kama walivyokuwa wamesikia. Alipokimbia Sharifa na Abdul, hakukuwa na mtu aliyepafahamu, wote walikuwa wakisikilizia kumuona mtu huyo, je, ni kweli alikuwa hai au mchezo tu uliokuwa umepangwa?
***
Bruno na mzee Todd walikuwa wakitembea kwa kasi kuelekea Upande wa Kaskazini, vichwa vyao vilikuwa vikifikiria maisha yao yangekuwaje nchini Afrika Kusini huku yeye, Todd akitafutwa dunia nzima kwa makosa ambayo hakuwahi kuyafanya.
Kichwa chake kilimfikiria mke wake na mtoto wake, aliwakumbuka, alitamani kuungana nao tena lakini kwa kipindi hicho haikuwezekana kabisa. Ukiachana na yeye, Bruno kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mpenzi wake, Shakira tu.
Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea huko, alitamani kurudi haraka nchini Kenya ili kwenda kuonana naye kwa mara nyingine lakini hilo halikuwezekana kabisa. Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kurudi nchini humo na wakati mfukoni mwake hakuwa na pesa yoyote ile.
Hapo Cape Town walitembea kwa kujificha sana mpaka walipofika katika kituo cha treni za umeme cha Bellstar Junction. Hapo walitaka kupanda treni na kuondoka jijini Cape Town na kuelekea Johannesburg ambapo huko waliamini kwamba wangepata msaada wa kuondoka nchini humo.
Hawakuwa na pesa mfukoni lakini mzee Todd alikuwa na pesa nyingi katika akaunti yake. Aliogopa kwenda benki na kuchukua pesa kwani sura yake ilikuwa dili kila sehemu na watu walimtafuta kwa nguvu kubwa.
“Ninataka kuelekea benki kuchukua pesa, ila nahisi nitakamatwa. Unadhani unaweza kwenda kwa ajili yangu?” aliuliza Todd huku akimwangalia Bruno.
“Kwenda benki?”
“Ndiyo!”
“Sawa. Benki gani?” aliuliza.
“Barclays!”
“Haina shida.”
Alichomwambia ni kwamba alitakiwa kwanza kwenda huko kwa lengo la kuchukua karatasi ya kuandikia hundi (cheque) na yeye kuipeleka benki. Hilo halikuwa tatizo, akaelekea benki ambapo huko akakutana na dada mmoja wa Kizulu na kuanza kuongea naye.
Alizungumza naye huku akionekana kuwa mchangamfu mkubwa, alijua kumteka mtu kupitia mazungumzo yake kiasi kwamba msichana huyo aliyeitwa kwa jina la Susan akabaki akikenuua tu kwani kila neno alilolizungumza Bruno kwake liliukuna moyo wake.
“Umetoka wapi?” aliuliza Susan, hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa akiongea kama Bruno.
“Kenya!”
“Ooh! Kumbe Afrika Mashariki. Nawapenda watu wa huko, wanaongea sana, ni wachangamfu mno. Si ndiyo ilipo Tanzania?” aliuliza msichana huyo.
“Ndiyo!”
“Ninawapenda sana Afrika Mashariki!”
Hilo likampa uhakika wa kukamilisha kile alichokitaka. Akamwambia kwamba lengo la kufika mahali hapo lilikuwa ni kuchukua kitabu cha hundi. Hilo halikuwa tatizo, Susan akampa kitabu hicho na Bruno kuondoka mahali hapo.
Huko alipokwenda, alimfuatan mzee Todd na kumpa kile kitabu. Mzee huyo akakichukua na kuandika kiasi cha dola milioni moja apewe mkononi. Bruno alipokichukua kitabu hicho na kuangalia, hakuamini, alimwangalia vizuri mzee Todd, alihisi kama kiasi kile cha pesa alichoandikiwa kilikuwa ni uongo.
“Dola milioni moja?”
“Ndiyo! Hakikisha unakwenda na kufungua akaunti yako. Utazichukua hizi pesa na kuziingiza kwenye akautnti yako, tutakuwa tunazitumia kupitia akaunti yako,” alisema mzee huyo.
Bruno alichanganyikiwa mno, hakuamini alichokuwa akikisoma kwenye cheki ile. Kiasi kile, kwa pesa za shilingi ya Kenya kilikuwa ni sawa na bilioni moja, milioni mia mbili na senti kadhaa huku kwa shilingi ya Kitanzania ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Akaondoka mahali hapo na kumuacha mzee huyo akiwa sehemu amekaa kwa kujificha sana. Alipofika, kama kawaida yake akamfuata Susan na kuanza kuongea naye. Kitu cha kwanza alichohitaji kilikuwa ni kufungua akaunti.
“Una randi elfu ishirini?” aliuliza Susan.
“Ya nini?”
“Kufungulia akaunti!”
“Sina! Ila nitakuwa nazo baada ya kufungua akaunti!”
“Kivipi?”
Alichokifanya Bruno ni kumuonyeshea Susan ile hundi aliyokuwa ameandikiwa. Msichana huyo hakuamini, kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kilitakiwa kuingia mara baada ya kufunguliwa kwa akaunti hiyo.
Haraka sana Susan akampeleka sehemu ya kupiga picha, akafanya hivyo na kufuata taratibu zote na kiasi hicho cha pesa kumlipia yeye mwenyewe kwani aliamini kwamba angelipwa kwa fadhilla alizokuwa ameonyesha.
Mchakato ulipokamilika, hundi ile ikachukuliwa na pesa kutolewa katika akaunti ya mzee huyo na kuingizwa katika akauti ya Bruno, akatoa kiasi cha dola elfu ishirini na dola elfu moja na kumpa Susan kisha kuondoka zake.
Hilo likamfurahisha mzee Todd na kuona kwamba walikuwa wakienda kufanikiwa kile walichokuwa wakikitaka. Wakawa na pesa, walichokifanya ni kukata tiketi na safari ya kuelekea Johannesburg kuanza.
Njiani, mzee Todd alikuwa na kofia, hakutaka kugundulika na mtu yeyote yule kwani aliamini kwamba dunia nzima ilikuwa ikifahamu kama alikuwa akitafutwa. Treni hiyo ilichukua saa moja mpaka kufika katika Jiji la Johannesburg ambapo wakateremka na kufikiria kwenda kupumzika hotelini.
Kitu walichokifanya ni kununua simu. Kila mmoja akanunua yake pamoja na laini ambazo zilisajiliwa kwa jina la Bruno. Kila kitu kilipokamilika, kwa kuwa namba ya mke wake aliifahamu, akaanza kumpigia.
Simu haikuita muda mrefu ikapokelewa na mkewe. Sauti yake haikuwa ya kawaida, alikuwa akizungumza huku akilia. Alihitaji msaada kwani pale alipokuwa hakukuonekana kuwa salama kabisa.
Wakati akizungumza naye, mara simu akapokonywa na sauti ya mwanaume kusikika kutoka upande wa pili. Iliongea kibabe, sauti ambayo haikuonekana kuwa na mchezo hata kidogo.
“Tunakuhitaji ndani ya saa arobaini na nane. Mbali na hilo, utaziona maiti za familia yako ufukweni. Una saa arobaini na nane kujisalimisha kwetu,” alisema mwanaume huyo kwa sauti yenye utetemeshi.
“Wewe nani?”
“Si lazima unifahamu. Fanya kama nilivyokwambia,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.
Mzee Todd akabaki akitetemeka, hakujua mwanaume huyo aliyekuwa akizungumza upande wa pili alikuwa nani. Akachoka, akatulia kwenye kiti huku akitetemeka kupita kawaida.
Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Maneno aliyozungumza mwanaume huyo yalionyesha kabisa kwamba familia yake haikuwa salama huko ilipokuwa.
“Halo...halo...” aliita lakini hakukuwa na sauti iliyosikika upande wa pili.
Bruno alibaki akimwangalia mzee huyo, alikuwa akilia, machozi yalitiririka mashavuni mwake. Alionekana kuumizwa na kile kilichokuwa kimetokea. Aliipenda familia yake na mara kadhaa alikuwa akiizungumzia kwamba aliikumbuka na alitamani sana kuonana nayo.
Akamuuliza kilichokuwa kimetokea, akamwambia kwamba familia yake ilitekwa na mtu asiyemfahamu na alimuhitaji ndani ya saa arobaini na nane kitu ambacho kilikuwa ni vigumu kufanyika.
“Kwa hiyo?” aliuliza Bruno kwa sauti ya upole.
“Sijajua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika. Familia yangu itauawa! Familia yangu itauawa!” alisema mzee Todd huku akilia kama mtoto.
***
Hakukuwa na mtu aliyekuwa muhumu kwa kipindi hicho kama mzee Todd. Maofisa wa CIA walikuwa wakimtafuta kila kona, walimtaka mzee huyo kwa udi na uvumba.
Walihangaika kila kona kumtafuta lakini hawakujua mahali alipokuwa. Wakati mwingine waliambiwa kwamba alikuwa nchini Msumbiji, walisafiri na kwenda huko lakini hawakufanikiwa kumpata.
Mzee huyo aliwasumbua kichwa kupita kawaida. Dunia ilikuwa kimya, kila mmoja alitaka kuiona nguvu ya Marekani kwamba kama ingeweza kumpata mwanaume huyo au la.
Walihangaika, kwenye simu hakuwa akipatakana na hata walipojaribu kuitraki simu yake hawakuambulia kitu chochote kile. Walisumbuka kwa muda wa wiki nzima ndipo siku moja wakafanikiwa kuiona simu ya mke wake ikiita, ilikuwa ikipigiwa na simu kutoka nchini Afrika Kusini.
Waliifuatilia simu ya mkewe bila yeye mwenye kugundua. Walijua kwamba ilikuwa ni lazima kwa mzee huyo kuwasiliana na familia yake na ndiyo maana walikuwa makini sana kuhakikisha wanakamata mawasiliano kutoka kwa watu hao.
Simu iliyopigwa katika simu ya mwanamke huyo ilitoka Afrika Kusini walichokifanya ni kuiunganisha na kuanza kusikiliza mazungumzo ya watu hao. Maneno waliyoyasikia yaliwashangaza, Juddie alisikika akilia huku akiomba msaada kuonyesha kwamba alikuwa kwenye hatari na baada ya hapo wakasikia sauti ya mwanaume ikimwambia kwamba alimpa saa arobaini na nane tu awe amejisalimisha.
Maofisa wa CIA hawakujua kilichokuwa kikiendelea, hawakujua ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia. Ili kujua kile kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni lazima kumkamata Todd na kumuuliza kuhusu hayo yote yaliyotokea na huku wakiwa wameandaa kesi kwa lengo la kumpeleka mahakamani.
“Simu imetoka Afrika Kusini karibu na kituo cha treni cha Johannesburg Park. Waambie vijana waende huko, wamuwahi mzee huyo na kumtia mikononi mwao,” alisema mwanaume mmoja, haraka sana simu ikapigwa Afrika Kusini, maofisa wa CIA waliokuwa huko, wakawataarifu kwamba mahali walipokuwa hakukuwa mbali na kituo hicho, hivyo walikuwa wakienda haraka sana kuhakikisha mzee huyo anatiwa mikononi.
***
Johannesburg haikuonekana kuwa sehemu salama kwa maisha yao, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo huko Bruno akimwambia mzee Todd kwamba walitakiwa kuelekea nchini Kenya kwani alikuwa akizijua sehemu nyingi za kujificha ikiwemo kijijini kwake.
Hilo halikuwa tatizo, lakini kabla ya kuondoka kuelekea nchini humo ilikuwa ni lazima wapate mtu ambaye angewaunganishia na meli yoyote ile ili waondoke kuelekea Kenya. Kwa Bruno, kwake lilionekana kuwa suala kubwa na gumu kwani humo Afrika Kusini, hakuwa na ndugu, rafiki au mtu yeyote yule.
Walitamani kukutana na mtu yeyote ambaye angewaambia mahali pa kwenda kwani kwa jinsi mzee Todd alivyokuwa akitafutwa, walijua kabisa kwamba wasingeweza kupanda ndege, ilikuwa ni lazima kuondoka nchini humo kwa kutumia gari au meli.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza mzee Todd.
“Let’s go to Soweto. I’m sure there are people who can help us out,” (Au twende Soweto, naamini huko kuna vijana wengi ambao wataweza kutusaidia,” alisema Bruno.
Hakuwahi kufika Soweto lakini alisikia tu kwamba huko kulikuwa ni uswahilini mno, kulikuwa na wahuni wengi ambao walikuwa wakipanga madili yao ya kuvamia benki na hata kufanya uchafu wa kila aina. Ilikuwa ni lazima kwenda huko kama tu walikuwa wakihitaji msaada wa kuondoka nchini humo.
Soweto ilikuwa ndani ya Johannesburg hivyo haikuwa vigumu kwao kufika huko. Kwa kuwa walikuwa na kofia, miwani hawakuhofia kumuuliza mtu yeyote mahali ilipokuwa Soweto. Walipouliza kwa mtu mmoja tu, akawaambia mahali kulipokuwa na kuanza kwenda huko.
Walikuwa na hofu, waliijua Soweto, kulikuwa na fujo za kila aina, watu walikuwa wakiuawa kila siku, haikuwa sehemu salama ya kuishi kwani watu wote waliokuwa wakiishi humo walikuwa waswahilini ambao waliamini zaidi katika fujo.
Baada ya dakika kadhaa, wakaingia Soweto. Sehemu hiyo haikutofautiana na sehemu nyingine za uswahilini. Kulikuwa na nyumba mbovu, barabara za vumbo na kitu pekee ambacho kilipendezesha mtaa huo ni uwanja wa timu ya Orlando Pirates.
Kila mtu alikuwa akiwaangalia jinsi walivyokuwa wakitembea mtaani. Walikuwa wakiangalia huku na kule, kwa kuwaangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua kwamba watu hao walikuwa wageni. Walitembea kwa kujishtukia huku muda mwingi wakiangalia huku na kule.
Walitembea mpaka walipokuta sehemu iliyokuwa imefungwa kamba kwa mbele. Hiyo ilikuwa ni kuingia ndani kabisa ya mtaa huo wa Soweto. Watu waliokuwa wakipita hapo walikuwa wale wa kitambo au wahuni ambao kutoa roho za watu ilikuwa ni sawa na kuua mbu.
Magari yote yaliyokuwa yakiibwa mjini, yalipitia hapo na kamba ile kufungwa. Hao ndiyo walikuwa chanzo cha mashirika ya umeme kuanzia mfumo wa luku kwa kuwa hawakuwa wakilipa na kila siku watu wa umeme waliokuwa wakienda huko walikuwa wakipigwa na wengine kuuawa.
Walisimama pale barabarani huku wakijifikiria kama iliwezekana kuvuka mahali pale au la. Kwa kupaangalia, palionekana kuwa pa kawaida, hakukuwa na mtu yeyote, barabara ya vumbi haikuwa hata na gari moja.
“Kuna kamba! Hii inamaanisha haturuhusiwi kuingia?” aliuliza Bruno, hakujua maana ya kamba ile.
“Nahisi kwa magari! Sisi tuingie,” alisema mzee Todd.
Hicho ndicho walichokifanya, wakaingia kwa kuivuka kamba ile, wakateembea kwa mwendo wa kawaida kusonga mbele huku kila mmoja akionekana kuogopa mno. Walipopiga kama hatua mia moja, mbele wakamuona mwanaume akijitokeza na kusimama barabarani.
Mkono wa kulia alishika panga huku wa kushoto akiwa na bunduki aina ya AK-47. Mwanaume huyo alivalia usongo kichwani kama Rambo huku akiwa na kaoshi na kipenzi kilichokuwa kimechanikachanika.
Wakasimama na kuanza kuangaliana na mwanaume yule. Kabla hawajachukua hatua yoyote ya kufanya, wakageuka nyuma, wanaume wengine waliokuwa na muonekano kama wa mwanaume yule aliyekuwa mbele yake wakatokea, walikuwa zaidi ya wanne.
Mpaka kufikia hapo, wakajua maana ya Mtaa wa Soweto. Walisikia tu kwamba ndani ya mtaa huo mauaji yalikuwa waziwazi, halikuwa jambo la kushangaza kuwaona watu wakipigwa au miili yao kutupwa barabarani kama mizoga.
“Hey! White! What are doing here?” (Hey! Mzungu! Unafanya nini hapa?) lilikuwa swali la kwanza alilouliza mmoja wa wanaume waliokuwa nyuma yao.
Hakukuwa na Mzungu aliyejaribu kwenda Soweto. Watu hao hawakupendwa huko kwa kuwa weusi waliamini kwamba walikuwa katili na ndiyo waliokuwa wakiwatesa watu weusi wengi nchini humo.
Kulikuwa na mapigano ya chini kwa chini baina ya Wazungu na watu weusi. Walitafutana kimya kimya, Wazungu walikuwa wakiokotwa wakiwa wamekufa na hata wakati mwingine nao watu weusi waliokotwa wakiwa wamekufa.
Hakukuwa na mtu aliyemaliza uhasama huu, ulikuwa ukiendelea huku kila mmoja akijiona kuwa sahihi na kusingekuwa na mtu yeyote wa kumbabaisha.
Soweto haikuwa na maendeleo makubwa na watu hao waliamini kwamba Wazungu ndiyo waliokuwa wakiinyima maendeleo kwani pamoja na kuwa katika jiji la biashara la Johannesburg lakini uswahilini bado kuliendelea kuwa Soweto.
Wazungu wengi waliwahusisha wanawake weusi katika biashara ya ngono. Walikuwa wakiwachukua na kuwapeleka katika madanguro ya Kizungu na hata cassino na kuanza kuwafanya walivyotaka.
Wanawake hao walitafuta pesa, walijua kwamba walikuwa wakijidhalilisha lakini hawakuwa na jinsi, kwa kuwa walikuwa wakaiingiza pesa, kwao
Kitendo cha mzee Todd kuonekana humo ilikuwa ni hatari kwa maisha yake, aliulizwa swali lakini hakuwa na jibu lolote lile. Wakawasogelea na kuanza kuwaangalia vizuri, waliporidhika, wakawachukua, wakawafunga kamba na kuanza kuondoka nao.
Wote wakajua huo ndiyo ulikuwa mwisho wao, walikuwa na hofu na kuona kwamba huo ungekuwa mwisho wao. Walipitishwa mitaani, kila mtu aliyekuwa akiwaangalia, alishangaa na zaidi kuliko yote walikuwa wkaimshangaa mzee Todd, ilikuwaje ajiamini aende Soweto na wakati Wazungu wote walikuwa wakiogopa kwenda huko?
Ni mwendo wa dakika tano tu wakafika katika jumba moja bovu na kuingizwa humo na kuamriwa watulie kwani kulikuwa na kiongozi wao aliyetakiwa kuwaona na kuwauliza maswali machache kabla ya kutoa uamuzi kwamba baada ya kuuawa huyo Mzungu, naye Bruno alitakiwa kuuawa au la.
“Do they want to kill us?” (wanataka kutuua?) aliuliza mzee Todd huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Yeah! They really want to kill us. Let’s get prepared,” (Ndiyo! Wanataka kutuua hasa. Tujiandae tu) alisema Bruno kwani kwa jinsi watu wale walivyokuwa wakionekana, walionyesha kila dalili za kutaka kuwamaliza watu hao.
Kitu walichokifanya ni kuwapokonya simu zao na kwenda kuzifungia ndani. Wakawapekua na kuwakuta na pesa, dola aambazo napo wakazichukua na kadi ya benki ambayo kwao ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile.
“How much do you have?” (mna kiasi gani?) aliuliza mwanaume mmoja huku akiwa ameshika kadi ya ATM.
“We have nothing...” (hatuna kitu) alijibuu Bruno.
“You must be kidding me,” (utakuwa unanitania)
“Serious brother, we have nothing,” (siriazi kaka, hatuna kitu) alijibu Bruno, hakutaka kumuacha mzee Todd aongee kwani kwa hofu aliyokuwanayo ingekuwa rahisi kusema kiasi chote kilichokuwa kwenye akaunti na wakati yeye mwenyewe alikuwa akikitaka.
“Give me the password,” (nipeni namba ya siri) alisema mwanaume huyo.
 
mbona umerudia kupost episode ambayo tayari tumeshaipita mkuu??
 
Bruno The Fishman

Mtunzi. Nyemo

Episode 5

Mwendelezo wa episode ya NNE

Bruno na mzee Todd hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa mwezi mwingine wa pili. Hawakupenda kukaa nchini humo, kila mmoja alihitaji kuondoka kuelekea nchini mwao lakini hawakuwa na jinsi, waliendelea kubaki nchini humo nyumbani kwa Jonathan huku mzee Todd akiendelea kupatiwa matibabu.
Siku ziliendelea kukatika, Bruno hakutakiwa kutoka ndani, alikuwa na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba bado watu hao walikuwa wakimtafuta kila kona hivyo angeweza kuuawa.
Alikuwa kama mwali, kila siku ilikuwa ni kuamka ndani na kubaki humohumo mpaka jioni. Yalikuwa ni maisha ya shida, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuwasiliana na Abdul aliyekuwa nchini Kenya kwa lengo la kumwambia kuwa hakufa, ili taarifa hiyo ampe Sharifa ambaye bila shaka alikuwa na wasiwasi mkubwa huko alipokuwa.
Kupata simu halikuwa tatizo ila tatizo kubwa lilikuwa ni kupata simu ya mtu mmoja aliyekuwa nchini Kenya ambaye angemuunganishia kuzungumza na msichana huyo.
Kila siku alizungumza na mzee Todd ambaye alimwambia jinsi alivyokuwa akiumia kuona akiwa mbali na familia yake. Hao ndiyo walikuwa watu aliokuwa akiwategemea, hakuwa na ndugu, maisha yake tangu alipokuwa kijana mpaka alipopata utajiri, mkewe na mtoto wake ndiyo walikuwa watu pekee.
“Unahisi tutaweza kuondoka hapa salama?” aliuliza mzee Todd.
“Ninatumaini hilo mzee! Cha msingi ni kumuomba Mungu katika hili, ila ni lazima tuondoke salama hapa,” alisema Bruno, alimwambia mzee huyo maneno ya kumfariji kiasi kwamba akahisi kwamba Bruno alikuwa malaika aliyetumwa kwa lengo la kumtia moyo pale alipokuwa akimevunjika moyo.
Wakati akiendelea kuugua kitandani pale ndipo alipopewa taarifa juu ya kifo cha familia yake ambapo maiti zao zilikutwa ufukweni.
Ilikuwa taarifa mbaya iliyouumiza moyo wake, hakuamini kile alichokuwa akikiona, moyo wake ulimwambia kwamba ni Maxwell ndiye aliyefanya hivyo.
Lawama zake zilikuwa kwa mwanaume huyo, aliuumiza moyo wake na kuhisi kabisa kwamba alifanya hivyo kwa kuwa alihitaji mali zake, aliutaka utajiri wake na hata kushikilia biashara nyingi alizokuwa akizifanya.
Hakulia sana, hakuhuzunika sana kwani mahali walipokuwa hakutaka wenyeji wao wagundue kwa kuamini kwamba kama ingetokea hivyo basi ilikuwa ni lazima wakatoe taarifa katika kituo cha polisi na kukamatwa.
Siku ziliendelea kukatika huku mawazo juu ya familia yake yakimuumiza moyoni mwake. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, hakuwa na watu wengine wa karibu sana kwani tangu alipokuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya hakuwa anajiamini kuwa na watu wa karibu zaidi ya familia yake, yaani hata walinzi wake hakuwa akiwaamini.
Waliendelea kuwa hapo mpaka mwezi ulipokatika ambapo wakakubaliana kwamba ni lazima waondoke kuelekea nchini Kenya kwa kupitia njia za panya mpaka kufika huko.
Hilo halikuonekana kuwa tatizo, alichokifanya Bruno ni kuzungumza na Jonathan na kumwambia kile walichokuwa wakikitaka.
Jonathan akawaambia kwamba halikuwa jambo zuri kupitia njia za panya, kwa kuwa walikuwa na pesa na hati zao za kusafiria zilipotea basi lingekuwa jambo jema kama wangekwenda uhamiaji kwa lengo la kukabidhiwa nyingine.
“Hapana! Nadhani kwa njia za panya ni vizuri zaidi,” alisema Bruno.
“Hapana! Njia hizo si salama, mnaweza kuuawa,” alisema Jonathan.
Walimwambia Jonathan kwamba walitaka kuondoka nchini humo kwa njia za panya lakini mwanaume huyo aliendelea kuwasisitizia kwamba hizo hazikuwa njia nzuri kwenda nazo kwani watu wengi ambao walikuwa wakitumia njia hizo walisafiri kwa hofu kubwa kitu ambacho hakutaka kuoana watu hao wakikutana nacho njiani.
Wakaambiwa wasubiri wakati Jonathan akifuatilia hati zao za kusafiria uhamiaji. Hilo likaonekana kama kwa kosa kubwa, hawakutaka kuendelea kubaki nyumbani hapo, katika kipindi ambacho Jonathan alikuwa ameondoka kuelekea huko, huku nyuma nao wakatoroka nyumbani hapo.
Sehemu ya kwanza kabisa ambayo walitaka kwenda ilikuwa ni katika Jiji la Pretoria ambapo waliamini kwamba safari yao ya kuelekea nchini Kenya ingeanzia hapo.
Walipoondoka, wakaelekea mpaka katika Kituo cha Treni cha Sandton ambapo hapo wakapanda treni na kuanza safari ya kuelekea Pretoria.
Ndani ya treni hakukuwa na mtu aliyewagundua, walivalia kofia na miwani kiasi kwamba ilikuwa vigumu sana kwa nyuso zao kuonekana.
Ndani ya treni walikuwa kimya kabisa, hawakutaka kuzungumza jambo lololote lile. Walijifanya kufuatilia safari huku wakiwa wameviinamisha vichwa vyao.
Kutoka hapo Johannesburg mpaka Pretoria walitumia saa mbili na dakika kadhaa, wakafika ambapo hawakutaka kukaa sana, ilikuwa ni lazima waunganishe safari mpaka Polokwane.
Hapo hakukuwa na treni ya kwenda huko, walitakiwa kuchukua basi ambalo lingewapeleka mpaka huko. Bado hilo halikuwa tatizo, wakakata tiketi na kuanza kuelekea Polokwane.
Ndani ya basi hilo kulikuwa zaidi ya abiria hamsini, kila mmoja alionekana kuwa na jambo lake, wote walikuwa bize huku wengine wakiwa na mizigo mikubwa, hakukuwa na mtu aliyemfuatilia mwenzake, kila mmoja alikuwa bize na mambo yake.
Walichukua saa nne ndio wakaingia huko. Giza tayari lilianza kuingia na kulikuwa na baridi kali, wakatafuta vyumba na kwenda kulala. Huko, kila mtu aliendelea kuwa na mawazo juu ya watu wake.
Mzee Todd alikuwa kwenye maumivu makali, bado hakuamini kama kwelii familia yake ilikuwa imeuawa kinyama, alikuwa na hasira mno na hakuona kama kweli Maxwell alistahili kuishi, kwa kuwa aliimaliza familia yake, naye ilikuwa ni lazima ammalize kwa gharama yoyote ile.
Upande wa pili na Bruno alikuwa na mawazo yake kuhusu mpenzi wake, Sharifa. Moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona kwa mara nyingine tena na kumwambia kile kilichotokea na kwamba hakufa.
Kwa kiindi hicho, kwa esa ambazo zilikuwa katika akaunti yake aliyokuwa ameifungua hao Afrika Kusini zilikuwa nyingi mno ambazo angeweza kuzitumia kwa kufungua biashara nyingi nchini Kenya.
Wakati mwingine alitamani hata kumkimbia mzee Todd na kupotea zake lakini kila aliofikiria hali ya mzee huyo, hatua alizokuwa akipitia katika maisha yake, hakuona kama lilikuwa jambo jema kufanya kile kilichokuwa kikimjia kichwani mwake.
Asubuhi iliofika, wwakajiandaa kwa ajili ya kuendelea na safari yao kama kawaida. Hapo Polokwane Mjini walitakiwa kuanda basi mpaka sehemu iitwayo Mankweng ambao hao wangeunganisha mpaka Tzaneen, Nkowankowa hadi Phalaborwa ambao hao wangekutana na vijana waliokuwa wakifanya shughuli ya kuwaitisha watu miakani kwa njia za anya kuelekea nchini Msumbiji.
Hawakutaka kuoteza muda, baada ya kula na kuchukua kiasi cha esa kilichoonekana kuwatosha, wakaondoka kuendelea na safari yao. Ilikuwa ndefu mno, waliondoka asubuhi lakini mpala inafika majira ya saa kumi na mbili jioni bado hawakuwa wameingia Phalaborwa ambao wangetakiwa kulala.
Kila mtu ndani ya gari alichoka kuita kawaida, waliofika Nkowankowa, kama kilometa mia nne mpaka Phalaborwa wakaamua kulala hao.
Hakukuwa na abiria aliyeruhusiwa kutoka ndani ya gari, walitakiwa kubaki humohuko kwani sehemu za vijiji kama hizo hazikuwa nzuri kwa usalama wao.
Abiria wakalala usingizi wa mang’amung’amu hadi asubuhi ambao safari ikaendelea kama kawaida. Hapo, kutokana na ubovu mkubwa wa barabara walitumia saa sita kufika Phalaborwa.
“Nyie mnataka kwenda wapi?” aliuliza kijana mmoja.
“Msumbiji!” alijibu Bruno.
“Msumbiji! Kwa njia za halali au?”
“Kama ingekuwa kwa njia ya halali unahisi tungekuja huku?” aliuliza Bruno, alichoka, hakuhitaji maswali yoyote yale.
Kijana yule akawachukua na kuwapeleka katika jumba moja chakavu ambapo huko wakakutana na vijana watatu ambapo yule kijana mmoja akawaelezea shida yao na kupewa maelekezo kwamba walitakiwa kuyafuata kama walitaka kufika nchini Msumbiji salama kabisa.
“Yapi hayo?” aliuliza Bruno.
“Kwanza mna randi elfu tano?” aliuliza kijana mmoja huku akiwa ameshika kipande cha bangi.
“Pesa si tatizo,” alisema Bruno na kutoa kiasi cha pesa kilichokuwa kikihitajika na kumpa.
Kijana yule akaanza kuwaambia kuhusu safari yao ambayo wangewaelekea mpaka katika msitu wa Kruger na wao kuunganisha mpaka nchini Msumbuji.
Kruger ulikuwa moja ya misitu hatari sana iliyokuwa na wanyama wakali. Waliwaambia kwamba wao wangewapeleka mpaka mwanzo wa msitu huo na safari ya mbele walitakiwa kwenda peke yao ila wangewaambia njia nzuri na salama mpaka kufika nchini humo.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mchana huohuo wakaanza safari ya kuelekea katika msitu huo ambao ulikuwa ni kama kilometa kumi kutoka hao waliokuwa.
Njiani walikuwa wakipiga stori na Bruno kuwaambia kwamba wao walikuwa maharamia ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuteka meli Afrika Kusini na kukomba mizigo yote lakini kwa kipindi hicho walitakiwa kurudi Msumbiji kwa kuwa kule Cape Town hakukuonekana kuwa salama kabisa.
“Na kama mimi nikitaka kuwa mharamia?” aliuliza jamaa mmoja.
“Kwanza ni lazima ujue kuigana, uwe japo na mkanda mmoja wa karate, ujue kuua kwa kumpiga mtu sehemu hatari mwilini mwake lakini la zaidi ni lazima ujue kuambana na watu hata sita waliokuwa na bunduki,” alisema Bruno huku akionekana kuwa makini sana.
“Wewe umefuzu?”
“Ndiyo! Nakumbuka mtu wa kwanza kabisa kumuua alikuwa The Ruler! Mnamfahamu?” aliuliza Bruno.
“Haana! Ndiye nani?”
“Eeeh! Hamumfahamu mtu aliyekuwa akitisha sana kwa mauaji Somalia, yule ambaye alimteka mpaka mtoto wa rais?” aliuliza Bruno.
“Hapana!”
“Fuatilieni, mtajua mtu huyo alikuwa ni hatari kiasi gani. Ndiye mtu wa kwanza kumuua,” alisema Bruno.
Kila kitu alichokuwa akiongea mahali hao kilikuwa ni uongo asilimia mia moja. Aliwaangalia vijana hao, hawakuwa wakieleweka, kwa jinsi walivyoonekana, alihisi kabisa kama wangeweza kuwageukia baada ya kuona pesa.
Aliliona hilo na ndiyo maana alikuwa akiwaambia stori za uongo zilizowafanya vijana hao kuanza kuogoa na kuhisi kwamba walikuwa na watu hatari sana ambao wangeweza kuwapiga ndani ya dakika kadhaa tu.
“Na huyo Mzungu?” aliuliza jamaa mmoja kwa sauti ya chini.
“Huyo ndiye mafia mwenyewe. Muitalia, hana maneno mengi lakini ana roho ya kinyama zaidi ya Musolini,” alisema Bruno, wote wakashtuka.
“Mmh!”
“Huyo ni mtu hatari sana, unamuona anachechemea, alipigwa risasi tano mguuni, lakini mpaka leo bado anatembea, huyo ni mtu hatari sana,” alisema Bruno, vijana wale wakawa na hofu zaidi na kuona kwamba muda wowote ule wangeweza kugeuziwa kibao.
Wakaona safari ikiwa mbali mno, hawakutaka kuwaamini tena watu hao, walionekana kuwa hatari na hawakuwa na mchezo hata kidogo. Baada ya saa moja, wakafika waliokuwa wakielekea na kuwapa maelekezo kuhusu njia walizotakiwa kupita.
“Ila kumbukeni kwamba kuna wanyama wakali sana,” alisema jamaa mmoja, Bruno akaanza kucheka.
“Wanyama wakali? Hahaha! Hawana nafasi, tuna uwezo wa kupambana na simba zaidi ya watano, usijali,” alisema Bruno maneno ambayo yaliwafanya vijana wale kuhisi kwamba mtu huyo alikuwa jasiri sana.
“Basi sawa. Safari njema,” alisema mmojawao.
“Sawa,” aliitikia Bruno na kuanza safari ya kuelekea katika mbuga ya wanyama ya Kruger iliyokuwa ikisifika kuwa na wanyama wakali.
***
Hawakutakiwa kuogopa kuingia msituni, ilikuwa ni lazima wavuke na kusonga mbele mpaka nchini Msumbiji. Mbuga ya Kruger ilitisha mno, kila walipokuwa wakipiga hatua ni sauti za ndege na wanyama tu ndizo zilizokuwa zikisikika kila kona.
Waliendelea kusonga mbele, walikuwa makini, mioyo yao ilikuwa ikimuomba Mungu wasiweze kuingia mikononi mwa wanyama wakali kama simba, chui na wengineo.
Ndani ya saa tatu walikuwa wakitembea tu, walichoka lakini hawakutaka kupumzika. Njiani walikutana na wanyama wa kawaida kama nyumbu, swala, tembo na wanyama wengi wanaokula majani.
Baada ya kutembea kwa umbali wa kilometa kama thelathini ndipo wakabahatika kuiona hoteli moja kubwa na ya kitalii iliyoandikwa King Lion kwa juu ambayo ilikuwa maalumu kwa watalii waliokuwa wakitembelea mbuga hiyo.
Wakaanza kuifuata, walipoifikia, getini wakasimamishwa na walinzi walioonekana kuwashangaa mno. Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka watu hao kutembea katika mbuga hiyo ambayo ilikuwa ikitisha kupita kawaida.
“Nyie mmetoka wapi?” aliuliza mlinzi mmoja huku akiwashangaa.
“Huko mbugani!”
“Mmewezaji kutembea katika mbuga hii?” aliuliza mlinzi mwingine.
Kulikuwa na matukio kadhaa yaliyokuwa yakitokea huko, watalii walikuwa wakiuawa hovyo kila walipokuwa wakitembea, katika hoteli hiyo, kulizungushwa nyavu ngumu kwani hapo kabla simba walikuwa wakiingia na kuwashambulia watalii.
Kitendo cha wao kutembea mbugani na kuonekana kuwa salama kabisa kilionekana kama muujiza fulani kwa walinzi wale.
“Tumekuja kupanga vyumba,” alisema Bruno, aliamua kuwakatisha kwani walichokuwa wakikizungumza kilikuwa ni usalama wao tu wakati walipokuwa wakipita mbugani.
Hilo halikuwa tatizo, wakachukuliwa na kupelekwa ndani mpaka mapokezi ambapo hapo wakachukua vyumba na kutulia.
Kabla ya kwenda kila mtu chumbani kwake, mzee Todd akataka kukaa na Bruno kwa lengo la kuzungumza naye mambo mengi, hilo halikuwa tatizo, Bruno akakubaliana naye na hivyo kuanza kuzungumza.
Kitu kikubwa kabisa alichokisema mzee huyo ni kumshukuru Bruno kwa kile alichokuwa amemfanyia, alipambana naye, alimsaidia pasipo kuangalia kama walikuwa wakifahamiana kabla au la.
Walikutana kwenye meli lakini kwa jinsi alivyokuwa akimsaidia ilikuwa ni kama ndugu yake wa karibu au rafiki ambaye walikutana tangu miaka mingi nyuma.
“Ni upendo tu! Nitahakikisha unafika nyumbani kwako salama,” alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo.
“Nitashukuru sana. Sina familia, unalijua hilo?” aliuliza mzee Todd.
“Nalijua, sitaki kukumbuka, inaniuma sana kila nikikumbuka kile nilichokuwa nikikiona kwenye televisheni,” alisema Bruno huku uso wake ukionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na huzuni moyoni mwake.
“Kuna jambo jingine muhimu nitakwambia siku nyingine, labda baada ya kufika nchini Kenya,” alisema mzee huyo na kumruhusu Bruno kuondoka.
Bruno hakujua ni kitu gani mzee Todd alitaka kumwambia, hakutaka kufikiria sana, kichwa chake kikaanza kumfikiria mpenzi wake, Sharifa ambaye alikuwa nchini Kenya huku akijua kwamba alikuwa marehemu.
Alitamani sana kumpigia simu lakini hilo lilishindikana kwa kuwa hakuwa na namba ya mtu yeyote kutoka nchini Kenya.
Hapo, wakakaa siku ya kwanza, wakakaa siku ya pili mpaka ya kumi, hawakutaka kuondoka haraka kwani waliona kuwa hiyo ilikuwa sehemu salama na ya kujificha ambapo kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angebaini kwamba walikuwa mahali hapo.
***
Watalii waliendelea kumiminika ndani ya hoteli hiyo, kila siku kulikuwa kunaingia idadi kubwa ya watalii waliofika nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuangalia wanyama waliokuwa katika mbuga hiyo.
Wakati hao wakiendelea kuingia humo, wengine walikuwa wakiondoka huku wakiwa wamelipa kiasi kikubwa cha dola kilichoifanya nchi hiyo kupiga hatua kubwa kwenye sekta ya utalii.
Wazungu hao hao waliokuwa wakiingia ndiyo walioweza kumbaini mzee Todd. Siku ya kwanza kumuona tu, hawakutaka kujiuliza, walimfahamu mzee huyo, walikuwa wakifuatilia sana kwenye televisheni kuliko Waafrika ambao mtu huyo alikuwa barani kwao.
Hawakutaka kuchelewa, haraka sana simu ikapigwa mpaka jijini Johannesburg ambao wao wakawasiliana na polisi waliokuwa katika mbuga hiyo na kuanza kufanya harakati za kumtia mzee huyo mikononi mwao.
Walikijua chumba alichokuwa amepanga, wateja walisema walimuona mzee huyo akiingia chumbani kwake lakini hakukuwa na mtu aliyejua kama mwanaume huyo alikuwa mzee Todd aliyekuwa akitafutwa dunia nzima.
Polisi hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakaelekea katika chumba alichokuwa amepanga na kuanza kugonga huku wakihitaji kufunguliwa mlango.
Hakukuwa na mtu aliyefika kuufungua kitu kilichowapa uhakika kwamba inawezekana mzee huyo alikuwa amelala au alikuwa bafuni akioga. Kwa kutumia kadi ya kuingilia ambayo waliichukua kwa mhudumu, wakaufungua mlango na kuingia ndani.
Humo, hawakukutana na mtu yeyote yule, kitanda kilikuwa kimetandikwa huku juu ya meza kukiwa na kikombe kilichokuwa na kahawa, walipokwenda kukiangalia, kwa jinsi mule ndani kulivyokuwa ilionyesha kabisa kwamba mtumiaji wa kikombe kile hakuwa ameondoka muda mrefu uliopita, hivyo wakazidi kumtafuta.
Walimtafuta kila kona lakini hawakuweza kumpa. Wakatoka ndani na kuelekea nje, huko, wakaliona gari moja la watalii likitaka kuondoka mahali hapo kuelekea mbugani zaidi kwa lengo la kuangalia wanyama.
Wakahisi kwamba mzee huyo alikuwa humo, wakalifuata na kuanza kuwaangalia watalii wote waliokuwa wamesimama na wengine kukaa kwa nyuma, waliangalia kwa makini sana lakini mwanaume huyo hakuonekana.
Wakajua kabisa kwamba hakuwa humo, wakaondoka kurudi hotelini na kuanza kumtafuta tena. Walitumia nguvu nyingi sana lakini hawakuwa wamefanikiwa hivyo kuwauliza tena wale Wazungu kujua kama kweli mtu waliyekuwa wamemuona ndani ya chumba kile alikuwa mzee Todd au walimchanganya.
“He was the one!” ( alikuwa yeye?)
“Madam, we have tried to look for him i every corner but we didn’t find him,” (mama, tumejaribu kumtafuta kila kona lakini hatukumpata) alisema polisi mmoja.
“But I saw him, he was the one,” (lakini nilimuona, alikuwa mwenyewe) alisema mwanamke huyo huku akionekana kuwa na uhakika wa kile alichokuwa akikizungumza.
Walimwamini, wakaelekea tena na kuanza kumtafuta lakini hawakufanikiwa kumpata. Hilo liliwashangaza sana, wakatoka na kuanza kuangalia mpaka nje ya hoteli ile, walipomkosa, wakaamua kwenda kuangalia kwenye orodha ya magari yaliyoondoka na watalii kwenda kuangalia wanyama.
“Yameondoka magari mawili tangu saa moja,” alisema mwanaume aliyekuwa akitoa ruhusa ya kuyaondoka magari hapo kuelekea ndani kabisa ya mbuga hiyo.
“Sawa.Ila ninachokijua mimi ni kwamba magari huwa yanakwenda upande wa Magharibi, si ndiyo?” aliuliza polisi.
“Ndiyo! Huenda huko kwa kuwa ndiyo kulipokuwa na wanyama.”
“Sasa mbona kuna moja limekwenda Mashariki?” aliuliza.
“Mashariki?”
“Ndiyo!”
“Haiwezekani!”
“Kwani wewe unaporuhusu magari yaondoke, huwa huyaangalii?”
“Nayaangalia. Dereva alivyopiga simu kuhitaji gari nilimwambia aende ofisini kwangu kuchukua ufunguo kwani nilikuwa nimebanwa na haja hivyo nilikwenda chooni,” alijibu.
“Basi habari ndiyo hiyo! Kuna moja limekwenda upande wa Mashariki,” alisema polisi huyo, mwenzake akaingilia:
“Ila si tumeangalia kwenye lile gari lililokwenda Mashariki na tukamkosa?”
“Ndiyo! Ila kwa nini lielekee Mashariki? Nahisi kuna kitu! Hebu tulifuatilieni,” alisema polisi huyo, wakatoka kwa kasi, wakachukua gari lao na kuanza kulifuatilia gari hilo katika upande ule wa Mashariki huku kila mmoja akihisi kwamba ndani ya gari lile alikuwepo mzee Todd, ila kila walipokuwa wakikumbuka kuwa walipokwenda kuwaangalia watu waliokuwemo mule hawakuweza kumuona, walichanganyikiwa, kwa hiyo safari yao ilikuwa ni kama kwenda kubahatisha tu.
***
Tangu walipoanza kukaa katika Hotel ya King Lion hawakuwa na amani kabisa, walikuwa na hofu kwa kuhisi kwamba watu waliokuwa hapo wangeweza kuwagundua.
Hawakuwa na wasiwasi na watu weusi, waliwajua kwamba hawakuwa wafuatiliaji, hata kama wangeonyeshewa picha sasa hivi kwamba mtu huyu anatafutwa basi ndani ya dakika ishirini kama wangekutana naye ingekuwa vigumu sana kumkumbuka.
Walichokuwa wakikiogopa ni hao Wazungu waliokuwa wakiingia na kutoka katika hoteli hiyo. Ni kweli mzee Todd alikuwa akivaa kofia na wakati mwingine miwani lakini hilo halikumfanya kuwa na amani moyoni mwake, alihisi kabisa kwamba kuna siku tatizo fulani lingeweza kutokea.
Walikaa hapo kwa siku kadhaa, baada ya hapo, kuna mtu alionekana kumtilia shaka kwani kila alipokuwa akimwangalia, hakuwa akiyahamisha macho yake kwa haraka, ilikuwa ni kama alikuwa akimfahamu au waliwahi kukutana naye kwa siku chache zilizopita.
Hiyo haikuwa mara ya kwanza, ilikuwa ni mara nyingi Mzungu huyo alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi naye. Walichokifanya ni kuanza kusuka mipango ya kutoroka kwani wasingeweza tena kuendelea kubaki mahali hapo.
Hiyo ilikuwa ni mbuga kubwa ya wanyama, kwa ile iliyokuwa upande wa Afrika Kusini iliitwa Kruger ila kwa upande wa Msumbiji iliitwa Limpopo.
Kutoka Kruger mpaka Limpopo kulikuwa na umbali wa kilometa zaidi ya hamsini, ilikuwa ni mbali mno hivyo walihitaji usafiri wa kuondoka nao kuelekea katika mbuga hiyo.
Alichokifanya Bruno ni kuanza kufuatilia, alitaka kujua jinsi madereva wa magari yale ya kuwatembeza watalii mbugani walikuwa wakipata vipi ufunguo.
Kwenye kufuatilia kwake akagundua kwamba kulikuwa na ofisi maalumu waliyokuwa wakienda na kuchukua ufunguo huko.
Humo kulikuwa na meneja wao, hakuishia hapo, aliendelea kufuatilia na kugundua kwamba meneja huyo hakuwa na choo ndani ya ofisi yake, alipokuwa akitaka kujisaidia, alikwenda katika choo cha wafanyakazi na kujisaidia.
Mbali na hayo yote, alihitaji nguo. Akapeleleza na kugundua mahali ambapo nguo za madereva zilipokuwa zikikaa. Akaanza kufuatilia ratiba za madereva hao na kugundua kwamba kwa siku kati ya magari nane yaliyokuwa mahali hapo yalikuwa yakiondoka magari sita na mawili kubaki.
Akajipanga na mzee Todd, siku ambayo walitakiwa kuondoka, Bruno alikuwa akiangalia saa yake tu huku akiwa amemwambia mzee Todd ajiandae.
Alikaa katika kiti kilichokuwa karibu na ofisi ya meneja wa hoteli hiyo, watu walikuwa wakiingia na kutoka ndani ya ofisi hiyo.
Hakuwa na haraka, alichokuwa akikiangalia ni idadi ya magari yaliyokuwa kule nje, alikuwa akiyafuatilia kwa karibu kabisa.
Baada ya saa nne kukaa katika kiti kile, mlango wa ofisi ile ukafunguliwa na meneja kutoka. Akamsalimia na kuelekea chooni kujisaidia.
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake, haraka sana akasimama, akachungulia dirishani, gari iliyokuwa imebaki ni Jeep moja na Toyota 110 tatu.
Akaingia ndani ya ofisi ile, akaangalia huku na kule, funguo zilikuwa zimewekwa kwenye ubao uliopigiliwa ukutani. Akaangalia ufunguo wa Jeep, akauchukua, akaelekea katika chumba kidogo ambacho kilikuwa kikitumika kuhifadhia nguo za wafanyakazi, akachukua shati moja na kutoka harakahara.
Alipofika nje, akamuita mzee Todd, akamfuata, Wazungu wengine walipomuona mzee Todd akielekea kule kulipokuwa na gari, wakahisi kwamba zamu yao ilikuwa imefika hivyo kuifuata gari ile na kupanda huku mzee Todd akiwa mbele na Bruno.
“Tutafanyaje kama hawa wamepanda?” aliuliza mzee Todd huku akionekana kuwa na hofu.
“Tunaondoka nao!”
“Mbugani?”
“Hapana! Mjini,” alisema Bruno.
Hakutaka kuchelewa, hapohapo akaliwasha gari hilo, alipotaka kuliondoa tu, akashtukia akisimamishwa na polisi waliokuwa wakija kule kwa kasi, akatulia na kuwasikilizia huku akionekana kuwa na hofu nzito.
Polisi wale walifika mahali pale na kuanza kuwaangalia Wazungu wale waliokuwa nyuma, walimwangalia mmoja baada ya mwingine, waliporidhika wakaliruhusu pasipo kuangalia mbele kwani walijua watu waliokuwa wakikaa mbele walikuwa muongozaji na dereva tu.
Bruno akapiga gia na kuanza kuondoka mahali hapo. Hakuendesha kwa mwendo wa kasi kwa kuwa hakujua kuendesha gari vizuri, pale mbele alikuwa akipewa maelekezo na mzee Todd ambapo kila alipokuwa akiyafuatisha, gari lilikuwa likiondoka mpaka alipozoea.
Wakaondoka mahali hapo, Wazungu wale nyuma hawakujua mahali walipokuwa wakielekea, walionekana kuwa na wasiwasi kwani walizoea kuona wakiondokea upande wa Magharibi lakini siku hiyo walikuwa wakienda upande mwingine kabisa, upande wa Mashariki.
Hawakuuliza, gari lilikuwa kwenye kasi, njiani walikuwa wakipishana na wanyama, waliamini kwamba gari lingesimama na wao kuwaangalia wanyama hao na hata kuwapiga picha lakini haikuwa hivyo.
Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, gari liliendeshwa kwa kasi mpaka lilipofika katika eneo lililokuwa na kibao kilichoandikwa “Welcome Limpopo” yaani wakikaribishwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo.
Ulikuwa ni mwendo mrefu mno, walitumia saa moja na nusu ndani ya hilo gari huku likiwa kwenye mwendo wa kasi. Walipofika sehemu ambayo waliamini kwamba ingekuwa salama, wakateremka na Bruno kuwafuata wale watu kule nyuma.
“Nisikilizeni,” alisema, kila mtu akawa kimya huku akiogopa.
“Kana kuna mtu anajua kuendesha gari, aende mbele aendeshe mrudi hotelini, sisi tushafika,” alisema Bruno.
Hawakutaka kubaki mahali hapo, wakaondoka kusenga mbele ambapo waliamini kwamba kungekuwa salama kabisa.
Mtalii mmoja akaelekea mbele ya gari lile na kuanza kuliendesha kurudi hotelini huku kila mmoja akishangaa juu ya watu wale, walikuwa wakina nani? Na kama walikuwa wabaya kwa nini hawakuwajeruhi? Kila walichojiuliza walikosa majibu.
Polisi wale waliokuwa wakielekea kule lilipokwenda gari lile, baada ya nusu saa wakakutana na gari la watalii likirudi hotelini kwa mwendo wa kawaida.
Wakalisimamisha na kuwauliza kuhusu watu hao, wakawaambia kila kitu kilichotokea na kusisitiza kuwa watu wale hawakuwa hatari kwa sababu kama wangekuwa hatari ilikuwa ni lazima wawafanyizie au hata kuwaibia kila kitu walichokuwanacho.
“Ni watu wema sana, sidhani kama walikuwa na malengo mabaya, ila ni watu wazuri mno, hawakutujeruhi wala kutuibia,” alisema jamaa mmoja huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikizungumza.
***
“Ni wakina nani hao?”
“Sifahamu.”
“Hebu vuta kamera kwa karibu zaidi. Hapohapo, hebu waangalie vizuri!’ alisema mwanaume mmoja.
Watu wanne walikuwa ndani ya chumba kilichokuwa na kompyuta kadhaa ambazo ziliunganishwa na baadhi ya kamera zilizokuwa zimefungwa katika Mbuga ya Wanyama ya Limpopo.
Walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kupitia katika kompyuta zao. Waliweza kumuona Bruno na mzee Todd wakipiga hatua katika mbuga hiyo.
Walipowaangalia, kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwao ni kwamba watu hao walikuwa majangili. Mikononi hawakuwa na bunduki yoyote ile lakini walihisi kwamba inawezekana walikuwa wamezificha sehemu kwa kuwa tu hawakutaka kuonekana nazo.
Haraka sana simu ikapigwa kuelekea katika kitengo maalumu cha ulinzi na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea. Taarifa iliyotolewa ni kwamba watu hao walikuwa majangili na hivyo walitakiwa kufuatiliwa haraka sana.
Hilo halikuwa tatizo, vijana waliokuwa na bunduki nzito wakaanza kuelekea huko, upande wa Magharibi ambapo kila mmoja aliamini kuwa walipewa taarifa ya watu hao kwa kuwa walikuwa majangili.
 
Bruno The Fishman

Mtunzi. Nyemo

Episode 6

Bruno na mzee Todd hawakuwa na habari, walikuwa wakiendelea kusonga mbele huku wakiwa makini kuangalia kila kona. Walimuomba Mungu awalinde kwani mbuga hiyo ilikuwa na wanyama wakali na wakati mwingine walikuwa na sifa ya kuwashambulia watalii waliokuwa wakienda huko.
Walitembea kwa mwendo wa haraka uliojaa umakini, kila walipokuwa wakiwaona wanyama wanaokula majani, waliongeza umakini zaidi kwani waliamini kwamba pembeni yao kulikuwa na wanyama wala nyama kama simba, chui na wengine wengi.
Hawakuwa wakiongea, kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, walihisi kabisa kwamba wangesikiwa na wanyama ambao kuna uwezekano walikuwa wamejificha mahali fulani. Waliendelea kupiga hatua na baada ya kufika katika mto Mturuma, wakasimama na kuanza kujadiliana kama ilikuwa ni sahihi kuvuka mto huo au la.
“Ila unahisi kutakuwa na mamba?” aliuliza Bruno.
Mzee Todd akauangalia kwa makini zaidi, maji yake yalikuwa yamesimama, aina ya mito hiyo huwa hatari kwa sababu mamba hupendelea kukaa humo. Hawakutaka kuuvuka kwanza, ilikuwa ni lazima kuufanyia upekuzi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuuvuka.
Wakati wakiwa wanajadiliana ndiyo kilikuwa kipindi ambacho askari pori walikuwa wakija kule walipokuwa kwa kasi kubwa. Walikuwa ndani ya magari yao, walishikilia bunduki na kuona kabisa huo ulikuwa muda wa kuwakamata watu hao na kuondoka nao kwani miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikipigwa marufuku na ambavyo kesi yake ilikuwa kubwa ilikuwa ni ujangili.
Wakati wamekaa hapo, wakasikia mlio wa magari kutoka nyuma yao, waliogopa, walijua tu kwamba walikuwa maaskari, wakabaki wakiwa wamesimama, walikuwa na uwezo wa kuingia ndani ya mto ule lakini mioyo yao ilikuwa migumu kabisa kuchukua uamuzi huo.
Wakabaki wakiwa wamesimama, magari hayo mawili yakafika, maaskaro watano waliokuwa na bunduki wanateremka na kuanza kuwafuata, walipowafikia, hawakutaka kuzungumza nao jambo lolote lile, wakawachukua na kuondoka nao.
“Mna bahati sana, yaani mngeingia ndani ya ule mto, tungeipata mifupa yenu tu,” alisema askari mmoja huku akiwaangalia watu hao.
Ndani ya gari ndipo wakaambiwa kwamba walikuwa chini ya ulinzi kwa kuwa iligundulika kwamba walikuwa majangili. Walishangaa, walijitetea kwamba hawakuwa majangili lakini hakukuwa na mtu aliyewaelewa.
Walifungwa pingu na kupelekwa mpaka katika kituo cha polisi cha hapo mbugani na kuambiwa kusubiri. Humo, hawakunyamaza, waliendelea kusisitiza kwamba hawakuwa majangili na hivyo walitakiwa kuachwa na kuondoka lakini askari hawakutaka kuwaacha.
Ilipofika mchana, mlango wa mahabusu ukafunguliwa na kuambiwa kutoka ndani ya mahabusu ile. Wakachukuliwa na kuelekwa katika ofisi ya mkuu wa kituo kwa lengo la kuhojiwa maswali kadhaa.
Mkuu huyo aliwaangalia, alijua kabisa kwamba watu hao hawakuwa majangili kwa kuwa walipokuwa wamewafuatilia hawakuwakuta na silaha yoyote ile ambayo ingewaonyesha kwamba walikuwa majangili.
Aliwaweka ofisini kwake na kuanza kuzungumza nao, kitu pekee alichotaka kufahamu ni sababu ya watu wale kuwa mule mbugani, walikuwa wakitafuta nini na walikuwa wakielekea mahali gani.
“Tulipotea njia,” alisema mzee Todd, alimwambia Bruno kwamba hakutakiwa kuzungumza kitu chochote kile.
“Kutoka wapi?”
Wakaanza kumwambia stori nyingine kabisa ambayo ilikuwa ni uongo mtupu, walimwambia kwamba walikuwa na wenzao kutoka nchini Afrika Kusini ambao walikuwa wakitembea katika mbuga ya wanyama kwa lengo la kutafuta dawa za mitishamba lakini wakati wakiwa huko, walikimbizwa na wanyama wakali na kupotea na hata pale walipokuwa hawakujua walikuwa mahali gani mpaka walipofikishwa kituoni.
Kwa sababu aliongea mzee Todd, aliaminika kwa asilimia mia moja na hiyo kuambiwa kwamba warudi kwanza mahabusu kabla ya kutolea ambapo moja kwa moja wangechukuliwa na kurudishwa Afrika Kusini.
“Ila sisi siyo Waafrika Kusini!” alisema Bruno.
“Nyie mmetoka wapi?”
“Kenya!”
“Kwa hiyo mnataka mrudishwe Kenya?”
“Ikiwezekana mkuu kwani tulikwenda Afrika Kusini kwa ajili ya hizo dawa za mitishamba tu!” alisema Bruno.
“Basi sawa!”
Wakati wakiwa ofisini kwa mkuu wa kituo, polisi wengine walikuwa katika chumba kingine wakiangalia televisheni. Huko ndipo walipoweza kuiona picha ya mzee Todd akiwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake.
Polisi wakabaki wakiangalia, mwanaume aliyekuwa akionyeshwa walimfahamu sana, alikuwa yuleyule ambaye walikuwa naye katika kituo hicho. Haraka sana wakainuka na kuelekea ofisini kwa mkuu wao na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea.
Haraka sana naye akafungua televisheni na kuangalia kile alichoambiwa, ni kweli alikuwa mzee Todd, mwanaume aliyekuwa akitafutwa na CIA kwa udi na uvumba.
Wakafurahi, kiasi kilichokuwa kimetolewa kilikuwa kikubwa mno, lingekuwa kosa kubwa kama wangemuachana mwanaume huyo aondoke mikononi mwao.
Mkuu akawaambia vijana wake kwamba hawakutakiwa kuwashtua, ili waweze kumpata vizuri na kuondoka naye mpaka mjini ambapo huko wangempeleka mpaka katika kituo kikuu cha polisi kilichokuwa Limpopo.
Ndani ya saa moja, wakawatoa katika mahabusu kirafiki kabisa, waliwaambia kwamba walitakiwa kusafirishwa haraka sana kuelekea nchini Kenya waliokuwa wakitaka kuelekea.
Kwa jinsi mkuu wa kituo alivyokuwa akiongea, alionekana kumaanisha alichokuwa akiwaambia na hakutaka kuwaonyeshea dalili zozote za kuonekana walikuwa na la jambo.
Njiani, walikuwa wakizungumza, waligongesheana mikono lakini mioyoni mwao walijua kile ambacho kingekwenda kutokea mbele ya safari.
Walipanga kupita nao mjini, kwenda sehemu fulani ambao huko wangewaweka chini ya ulinzi na kuwachukua kuwaeleka katika kituo kikuu cha polisi.
Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kawaida kabisa, walikuwa wakipiga mahesabu jinsi ya kuwaweka watu hao chini ya ulinzi kwani kwa jinsi mabosi wa madawa ya kulevya walivyokuwa watu hatari, walihisi kabisa kwamba kama wangefanya mchezo wangeweza kuuawa wao.
Gari lilibakiza umbali kama wa mita elfu moja kufika katika kituo hicho cha polisi, polisi hao wakaanza kuandaa bunduki zao kitendo kilichowashtua Bruno na mzee Todd na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotakiwa kutokea.
“Mmh!” aligunda Bruno, polisi hao wakawanyooshea bunduki zao na kuwaambia kwamba walikuwa chini ya ulinzi.
“Jamani! Tumefanya nini?” aliuliza Bruno huku akiambiwa alale chini haraka sana.
“Todd! Kila mtu anakujua kama wewe ni mtu hatari sana. Upo chini ya ulinzi, ulidhani ungeisumbua dunia kwa kipindi kirefu? Ni muda wako kwenda kuhukumiwa kwa kile kilichotokea, ila pole sana kwa vifo vya familia yako, sikuwa nimekugundua mpaka nilipoambiwa kwamba ni wewe,” alisema mkuu wa kituo huku akitabasamu, polisi wote nane waliokuwa ndani ya gari hilo waliwanyooshea bunduki.
Simu ikapigwa makao makuu ya polisi na kuambiwa kwamba yule muuza madawa ya kulevya aliyekuwa akisumbua alikamatwa na hivyo walikuwa njiani kuelekea katika kituo kikuu cha polisi hapo Limpopo.
Polisi wa makao makuu hawakuamini kile walichoambiwa kwamba muuza madawa huyo alikuwa amekamatwa, taarifa zikaanza kusambazwa katika kituo hicho kwamba kila polisi alitakiwa kujiandaa kumuweka chini ya ulinzi mwanaume huyo kwa kuwa alikuwa mtu hatari sana.
“Wapo wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Vasco Da Gama,” alijibu polisi mmoja sehemu ambayo haikuwa mbali sana kutoka katika kituo hicho. Polisi wote wakaweka bunduki zao tayari na walichokuwa wakikisubiria ni mwanaume huyo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom