Hadith ya punda, DOWANS na Symbion

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Hapo zamani kulikuwa na kijiji na katika hicho kijiji kulikuwa na punda aliekuwa akitumiwa kubeba mizigo ya wanakijiji. Wenye kutaka kwenda kusaga, kuchota maji, kubebea mazao walimkodi kuwafanyia kazi zao. Mwenye punda akataka kumuuza na kuachana na biashara ya punda yule.

Wanakijiji wengi walimponda punda yule kwa nameno ni mzee na ameshatumika sana na hana nguvu mabishano yalikuwa makali sana. Kwa bahati akatokea mtu nje ya kijiji kile akasema yeye anamnunua na atamwacha pale pale kijijini na kuendelea kumkodisha kama awali ila kwa kiwango cha juu kidogo. Wanakijiji waliokuwa wakisema punda ni mkongwe na hana tena nguvu wakabadilisha maneno na kuanza kumsifia kuwa ni punda mwenye nguvu na anahitajika kwa ajili ya kusaidia matatizo ya uchukuzi. Wanakijiji wamegeuka mandumilakwili! Wanakijiji kama hawa ni wanafiki na wazandiki walishindwa kumnunua punda kwa sababu ya mwenye punda ila huyu mmiliki wa sasa wa punda kwa sifa anazopewa akitaka kuuza itakuwa rahisi sana.
 
husomeki kabisa
ebu jaribu kuandika ingalao kama umefika kidato cha pili na sio darasa la saba+veta.
 
husomeki kabisa
ebu jaribu kuandika ingalao kama umefika kidato cha pili na sio darasa la saba+veta.

Wewe huwezi kuelewa kwasababu hujui lugha ya picha na elimu yako ni sunday school
 
Back
Top Bottom